Watajwa hapo juu katika Headline yangu acheni Kutumia Uyanga wenu uliopitiliza kwa Kuihujumu Simba SC kwa kupitia Madaraka yenu ya Kiserikali mliyonayo kwani msipoangalia mtaleta Chuki, Mgawanyiko na kumfanya Rais Samia achukiwe na wana Simba SC kisha imgharimu pia Kisiasa.
Tunajua kuwa mpo katika Kikosi Kazi Maalum cha wana Yanga SC walioko Serikalini na wenye Nyadhifa Kubwa kutumika Kuihujumu Simba SC kwa kila namna kwa Maagizo ya Mstaafu Mmoja mwana Yanga SC lia lia mwenye Ushawishi mkubwa katika Serikali hii ya Rais Samia ( Bi. Hangaya )
Waziri Dk. Nchemba unajulikana hujawahi kuipenda Simba SC na kuna Kipindi ulipokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ulitumia Nguvu kubwa sana Kuihujumu Simba SC pale ilipocheza na Prisons FC ya Mbeya ila wana Simba SC tulikunyamazia kwakuwa tumetawaliwa na Uungwana Uliotutukuka.
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Abbas Wewe ndiyo hata huwa hufichi Chuki zako za Wazi kwa Klabu ya Simba na ndiyo maana ulipokuwa Msemaji wa Serikali hukupenda kabisa Umaarufu mkubwa wa aliyekuwa Msemaji wa Simba SC Haji Manara uendelee na ulimkalia sana Vikao vya Kumchukulia Hatua ila Busara za Wakubwa wako zilitawala na ukatulia japo hukumpenda kwa alikuwa akikufunika Kiumaarufu Tanzania.
Waziri Dk. Nchemba na Katibu Mkuu Dk. Abbas msidhani wana Simba SC tulio na Akili nyingi na kubwa ( za Kuzaliwa nazo ) tena za Kuwazidi japo mna Doctorates zenu akina Mightier hatujui nini mnakifanya katika Kuihujumu Simba SC kwa Kushirikiana na Watu wa Data akina N-CARD ili Klabu ya Simba ikose Mapato na katika Siku ya Simba Day Jumapili tarehe 19 Septemba, 2021 Uwanja usijae ili nyie Wana Yanga SC Waandamizi na Yanga SC wengine muicheke Simba SC kuwa haikujaza katika Tamasha lao kama lenu.
Mwisho namalizia tu kwa Kuwataarifu Waziri Dk. Nchemba na Katibu Mkuu Dk. Abbas kuwa Klabu ya Simba leo kupitia Matawi yake yote inafanya DUA ya Kuiombea Baraka Klabu na ya Kuwaombea MABAYA wale wote wenye Hila, Husuda na Roho Mbaya dhidi ya Simba SC na Wanatumika kwa kila namna katika Kuihujumu.
Msije tu kusema Mightier sikuwaonyeni.