Shida kubwa ya vijana wengi tunasahau kuwekeza ni starehe na makundi tunayokutana nayo kazini. Mbaya kuliko yote kutokufanya kazi kwa uwaminifu, kupenda rushwa, dhuluma kupitia viti tuna vikalia vimegeuka kuwa laana badala ya Baraka. Watu wanalipwa vizuri na mapato mengi ya ziada wanapata ila Mungu hajawabariki una bambikiza watu Kodi, una umiza watu kwa kiti umekikalia lazima hata wakulipe pension ya 500m utarudi kwenye ufukara maana pesa yako ni ya laana ndio maana kule Kongo makamo wa Rais nyakati za Mobutu yupo mtaani anaokota makopo hata hapa Tz Kuna watu walikuwa na nafasi ila ni fukara utadhani hakuwahi kuwa kiongozi ktk Taifa hili.
Dharau na majigambo pia yamewaacha wengi kwenye dimbwi la umasikini unapata pesa unaona watu ni kama panya na wewe ndio mwewe Mungu anakusubiri uzeeni uwe panya na ulio waona panya wawe mwewe.
Haijalishi leo una Tshs ngapi au unaiba huko serikalini kiasi gani as long as mapato yako ni ya dhuluma jiandae kwa ufukara, kifo au magonjwa ya ajabu uzeeni.
Ofisi ulio Kaa leo Kuna mtu alikaa vizuri na anaishi vizuri leo ila same kiti Kuna mtu alikaa akaharibu na anahaha mtaani hivyo jifunze kwa Hilo.
Palikuwa na mkurugenzi mmoja huko miaka ya nyuma alisumbua sana alitumia nafasi yake vibaya wafanyakazi wa serikali walio ajiriwa wakapita hiyo wilaya walikiona cha mtemakune, alikuwa akitafuna kila mwanamke mbele yake mpaka wake za watu ila kilio cha mama mmoja alie kuwa akitaka uwamisho na kudhulumiwa uwamisho wake kama mke wa mtu hakikumuacha salama. Leo ukimuona hutoamini kama aliwahi kuwa mkurugenzi akiendeshwa na magari ya serikali.
Anaomba omba na anajutia ubaya alifanyia watu yaani amechoka.
Nawaandikia huu Uzi kuwatahadharisha wale mnadhani vyeo na nafasi mnazo nifimbo kwa watu heshimu watu na wapende watu utastaafi kama mti wa Mwerezi kandokando ya maji. Nina story nyingi hazitoshi hapa kuandika ila nisomo kwetu vijana 🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿