Ni vizuri mwanaume akamzidi mwanamke ila isiwe sana, muwe na umri tofauti lakini rika moja, mkiwa na umri tofauti sana mtatofautiana interest harafu mnakuwa na life experience tofauti kitu kinachoweza kuleta migogoro, mfano mwanaume miaka 40 mwanamke miaka 23, mwanaume mambo ya 23 yrs anakuwa ashayaacha muda mrefu, anakuwa na interest tofauti anawaza kujenga, maendeleo, wakati binti wa miaka 23 anawaza shopping, kuchart fb, bbm, n.k so anajikuta anamiss sana kushare mambo fulani fulanitna wanaume wa rika lake, sasa hapo ndipo kuchapiwa kunapoanza, ni ngumu sana kuwakuta wanandoa waliopishana sana kiumri wakicheza beach kimahaba mahaba kwani mwanaume anakuwa hana interest na mambo yale, yeye ni kuzaa, kulea na kutafuta hela, hakuna cha baby baby, honey..Pia idadi ya miaka ya kuzidiana inategemea umri wa mwanamme kwa wakati huo, either kawahi kuoa au kachelewa, mfano kijana anayeoa akiwa na miaka 20, mara nyingi anaoa mwanamke wa umri wake kabisa kama sio kumzidi miaka 2 au 1, lakini mtu wa miaka 50 ni ngumu kuona kaoa mwanamke wa miaka 45 hadi 50, ataoa kuanzia 30 hadi 40.