Likitugusa tunalalamika, ila likitupa favor tunalitetea.
Mleta mada anasema Haji angelalamika sana kama ingekuwa Yanga ndiyo wenye viporo.
Kwa hiyo nilitegemea D10 alalamike kwa sababu Simba ana viporo, ila kwa vile halalamiki ina maana anaona ni sahihi.
Msimu huu wakati ligi unaanza Yanga kacheza 11 straight games Dar, was that right? Jibu ni hapana.
Tunachotakiwa ni kuhakikisha tunalilia haki sawa na sheria sawa bila kujali kwamba zinatubeba au la, maana kuna leo na kesho. Swala la viporo siyo geni, hata Yanga huwa anakuwa navyo. Tupambane kulifuta kwa pamoja.