Inauma sana na haivumiliki

Inauma sana na haivumiliki

Kwa nini unataka kulazimisha mapenzi?

Kwa nini unataka kumdhuru mtu kwa sababu kaamua hakupendi tena?

Wewe ni mbaya hivyo kwamba huwezi kupata mwingine?

Yani huyo peke yake ndiye alikuwa mwokozi wako dunia nzima?
Mkuu Kiranga sikuhizi mee wana wa roga keee ili wadumu nao sasa inapotokea kee kakorogwa na mee, na Mee kavurugwa na mwingine ndo utasikia na kuona kee anahangaika hadi mitandaoni .
Lakini kwa kawaida ya kee ukimuumiza sehemu 1 yeye ata kuumiza sehemu zote hadi ahakikishe unalala vilabuni
Hahahaaa !
Hivyo ukiona kee kaja mitandaoni kulalamika ujue ndumbaa isha take place
 
Ndoa ni nini? ndoa ni mkataba wa hiyari baina ya watu wawili( hapo inaweza kuwa zaidi ya) wenye lengo malaamu, kama kuishi pamoja ama vinginevyo inategemeana na hao watu wenyewe, sasa kama Ndoa tu ni mkataba wa hiyari ambao unaweza kuvunjika ama kuingia kwenye migogoro muda wowote, itakuwa mahusiano Mkuu? Mahusiano ni sehemu ya Maisha, ni hatua, ni mapito ni kujifunza, ni changamoto, ni vita, ni visasi, ni sehemu ya Maisha, je Maisha yakikupiga utayashusha Busha? kwa kuwa yamekusaliti, vipi kama ndugu walishaona tangu mwanzo huyo mtu uliyenaye si sahihi kwako tangu awali na walishajaribu kukwambia hukuliona hilo kwa wakati huo, si ulikuwa unafaidi penzi? kila kitu kina matokeo mawili, hasi na chanya, si mahusiano tu, hata biashara, unaweza fanya biashara fulani, kwa miaka kadhaa, isikupe kile unachotaraji, ukaamua kuachana nayo na kuanzisha biashara ingine na huko ukapata mafanikio, je ni kweli ile biashara ya mwanzo ni mbaya kiasi hicho? ama ni namna ile ambayo wewe ulikuwa ukiiendesha ile biashara ya awali? hatutakiwi kujuta kwa lolote ikiwa bado tunaishi, pangusa makalio anza upya.
 
Hamjifunzi kutoka story za watu??
Mwanaume maskini hakupendi anatafuta huruma tu....siku akipata hakuna rangi hutaacha kuiona
 
Unakuwa na mahusiano na mtu kipato cha chini

umeamua kumpenda na kumvumilia jinsi hali yake yamaisha ilivyo mnavuka mabonde vichaka na milima kwa pamoja dharau kejeli na maneno ya hovyo kutoka kwa ndugu kisa uliyenae hohehae.

hata zile salamu kutoka kwa ndugu hakuna unaamua kuziba masikio ukiamini ipo siku mungu atafungua milango kwa huyo ulie nae shida inakuja mwanaume akisha jipata nyumban hapakaliki kutwa kiguu na njia na wanawake wengine mwisho wa siku anakuja kuoa mwanamke mwingine.

Je, mwanaume wa namna hii utamfanya nini kumshusha busha kumtafutia wahuni wafanye yao au utamwacha aiende ukiangalia kakupotezea muda?

Inauma kwakweli
The game does not run on gratitude. Mwache aende zake.
 
Wahenga wanasema Kila mwanaume mwenye mafanikio ujue nyuma yake Kuna mwanamke.

Shida ni kujua je ni mwanamke gani yupo nyuma ya ayo mafanikio anyway pole sana Mkuu uwende umefanyika daraja ivyo kazi yako imeisha tafuta mwingine ambaye atakuwa daraja kwako
Hii methali ilikuwa zamani
 
Mkuu Kiranga sikuhizi mee wana wa roga keee ili wadumu nao sasa inapotokea kee kakorogwa na mee, na Mee kavurugwa na mwingine ndo utasikia na kuona kee anahangaika hadi mitandaoni .
Lakini kwa kawaida ya kee ukimuumiza sehemu 1 yeye ata kuumiza sehemu zote hadi ahakikishe unalala vilabuni
Hahahaaa !
Hivyo ukiona kee kaja mitandaoni kulalamika ujue ndumbaa isha take place
Hayo yote hayajibu swali langu la kwa nini ulazimishe mapenzi?
 
Marriage requires patience, understanding, ability to bow out in argument and love.

Love marriage fad has blinded people to assume that dating and small term relationship lead to marriage. In reality it doesn’t.

A person good with sex, doesn’t mean he’s going to be good with finances. A person good with money may not be good with sex. And you can guess the rest of scenarios.

Nobody is perfect. But people want perfection for their own life. So they pick and choose their comfort zone in marriage, which doesn’t stand for many in relationship.

That’s why some women have love affair till they find financially secure and decent guy, then they dump their current lover. Many men have love affair with progressive modern woman but they want stability in relationship so they marry conservative woman. Some people just want time pass and intimacy exploration before marriage too.
Aya tafsiri sasa[emoji1783]
 
Kwamba wakati unampenda yupo hoe hae na yeye anakupa penzi na wewe unamjali kwa hali haikuwa quid pro quo.... ?

Ukiishi kwa leo na sio kwa kesho (enjoy the moment) na ukigundua kwamba huwezi kumiliki kiumbe (binadamu) na huwa wanabadilika, basi mambo haya hayatakusumbua kabisa..., badala ya kukumbuka visa alivyokupa utakumbuka good times mlizo enjoy...

Yesterday is a memory today is a gift and tomorrow a mystery
 
Ukiachwa hilo ni kosa lako.

Ama umemkubali mtu ambaye si sahihi tangu mwanzo. Kosa lako.

Ama mtu alikuwa sahihi mwanzo akabadilika, ukashindwa kumuacha wewe kwanza. Kosa lako.

Ama mtu sahihi, ila kakuchoka tu. Kosa lako.

Vyovyote vile hutakiwi kuachwa.

Ukiachwa usilalamike. Tafuta mwingine tu.

Kwa sababu, kuachwa ni kosa lako.

Bila kujali wewe ni mwanamke au mwanamme. Bila kujali unahudumia au unahudumiwa.

Unatakiwa kuwa na mvuto mkali sana kiasi kwamba wewe tatizo lako liwe ukiingia kwenye mahusiano watu hawataki kuachana nawe.

Yani wao ndio wawe wanalazimisha mahusiano na wewe, sio wewe unalazimisha mahusiano na wao.

Ukiachwa ujue ushazembea sehemu hapo.

Jitafute ujiongeze mwenyewe bila kutaka kumdhuru mtu.

We jamaa uko vizuri sana kwenye kujenga hoja, ndo maana hapa JF unawasumbua sana watu
 
Hamjifunzi kutoka story za watu??
Mwanaume maskini hakupendi anatafuta huruma tu....siku akipata hakuna rangi hutaacha kuiona
Acha kupotosha watu - hii ni sumu mbaya sana unayoipandikiza kwa hawa watoto wa 2000 ambao wengi engine zao hazina Kilometer nyingi na hazijawahi kufanyiwa overhaul
 
Back
Top Bottom