Sawa, mimi nimeandika utumbo, najiuliza kama hayo maswali na hoja vinatoka kwa mtu mzima, kijana, mtoto au kichaa!!!
Unasahau kuwa Mgombea wa Urais kupitia CCM aliwekewa pingamizi kwa kutokutimiza vigezo wakati alikwisha kuwa mbunge mzoefu na kisha kuteuliwa na kuchaguliwa kuwa Rais wa nchi kwa sasa, itakuwa huyo uliyemtaja!
Huwa mnadai utawala wa sheria, iweje leo utetee kupitishwa tu kwa wagombea wasiokidhi vigezo, kwa mujibu wa sheria, ati ili waupe mchakato mzima legitimacy? Kumbuka kuwa wagombea ni wawakilishi wetu, kwenye vyombo (Halmashauri na Bunge) vyenye maamuzi juu ya maisha yetu, hivyo basi, wanapaswa kuwa watu wenye umakini wa hali ya juu kabisa.
Unapenda kutoa mifano ya nchi za nje, kutetea hoja zako mufu na zenye mwelekeo na hisia za siasa potofu na uchwara km hiyo IEBC ya Kenya, wakati ni dhahiri huko kunatokota (hakuko shwari kisiasa) hata sasa, wanapoelekea Uchaguzi Mkuu wao.
Ifike mahala tukubaliane kuwa viongozi wa upinzani, miaka 5 ya utawala wa Magufuli, hawakujifunza kubadilika kisiasa, ili waondokane na siasa za ulaghai majukwaani. Wakati wagombea wote wa CCM (Madiwani, Wabunge na Urais) walieleza kwa ufasaha na mifano, walichowafanyia wapiga kura (kwa maana ya kutimiza ahadi) kwa miaka 5, ili waaminike, wagombea wa upinzani walikebehi hayo. Wakati wagombea wa CCM, wakirejea historia ya nyuma kueleza ya kesho itakuwaje, wale wa upinzani walibaki kubwabwaja kwa hadithi zisizoeleweka. Katika hali hiyo, ya kisiasa, ni wazi wagombea wa CCM walijitokeza kuaminika zaidi kwa wapiga kura.