Uchaguzi 2020 Inauma sana, nasikiliza matokeo hapa nahisi kama roho inataka kutoka

Uchaguzi 2020 Inauma sana, nasikiliza matokeo hapa nahisi kama roho inataka kutoka

Hawana adabu hawa wapinzani wametutukana sana hawa, acha waisome namba.

Sasaivi ndio tutajua maana ya Ile kauli mbiu ya HAPA KAZI TUU

Wabunge, madiwani, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa na wakurugenzi wao waliokua wanashindwa kutekeleza ilani na kufikia wananchi kwa sababu za tofauti za kisiasa inabidi wafanye kazi kwelikweli

Sipati picha siku rais apite wananchi wamwambie tuna shida na hatujawahi kumwona mbunge miezi12 au miaka2😁😁😁
 
Sasaivi ndio tutajua maana ya Ile kauli mbiu ya HAPA KAZI TUU

Wabunge, madiwani, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa na wakurugenzi wao waliokua wanashindwa kutekeleza ilani na kufikia wananchi kwa sababu za tofauti za kisiasa inabidi wafanye kazi kwelikweli

Sipati picha siku rais apite wananchi wamwambie tuna shida na hatujawahi kumwona mbunge miezi12 au miaka2😁😁😁
Yani sasa hivi hakuna uzembe wala hakuna kutegea ni kazi, kazi, kazi, kazi.
 
Heri angegombea mbowe mwenyewe maana alichokifanya Tundu ni sawa alikuta chama kinapumulia mashine yeye akakikatia kabisa na kukiingiza kaburini
Nadhani hili litakua fundisho kwa wapinzani wa vizazi vijavyo
Hata mimi Tundu aliporudi na kuanza kutema nyongo binafsi, niliwaza ni bora Mbowe angesimama mwenyewe, maana mengi yalimkuta awamu hii angeweza kuyaunganisha na sera.
Shida Lissu alishatangaza tangu ile enzi ya HARDTALK BBC kuwa atarudi kugombea uraisi.
Chadema nadhani walijua sio mtu sahihi ila hawakuwa na uthubutu wakumwambia sababu ya:
(1.) ubabe wake,
(2.) Kwakuwa ilikuwa mara ya kwanza anarudi tangu Lissu ale shaba, walidhani watu watakuwa na huruma naye (kumbe watu wanapambana na hali zao,
(3.) ACT-WAZALENDO walikuwa hawana mgombea kipindi hicho, na Zitto amekuwa akijifanya BFF wa TL tangu shaba, hivyo walihofia TL kujiunga naye na kuiua CHADEMA.

Ukiangalia kampeni za TL mwanzoni akiwa na Mwamba, utaona Mwamba alikuwa hana amani. Na kibaya zaidi TL alitumia kampeni zile kumwaga nyongo binafsi badala ya kuuza chama au sera.

Ila wasivunjike moyo.
Mwamba arudi to basics. Atafute damu mpya, yenye akili zilizotulia kama akina Dr. Slaa waisuke Chadema upya. Waachane na siasa za kiki, zimepitwa na wakati. Aachane na baadhi ya wakongwe wanaofanya siasa kwa mazoea na hawataki kubadilika. Aone Magu alivyoibadilisha CCM, nayeye anaweza kuibadilisha Chadema.
 
Kufikia 2020 upinzani wote utakuwa umefutika. Nadhani sasa mnajua maana halisi ya kufutika.
Upinzani siyo vyama, hata ndani ya CCM kuna upinzani / wapinzani.
Upinzani upo mioyoni mwa watu
 
Baada ya nchi kumfurusha mkoloni mwaka 1961, 2020 tumemkataa tena mkoloni.

Hongereni watanzania, mkoloni na beberu ametujua sisi ni watu wa namna gani
 
Upinzani walishauriwa vizuri, wasiingie kwenye uchaguzi kwa hii tume ya uchaguzi. Kikwete aliwabeba mnoo.

Wamefanya vizuri sana kuingia kwenye uchaguzi na hapo walipofikia ni pazuri sana wametufanya watanzania wengi tuelewe kuwa kumbe kinyume na katiba kuwa mamlaka ya nchi inatoka kwa wananchi kwenye hili mamlaka inatoka kwa Rais
 
Pole mkuu,

Nakushauri uingie barabarani kama Lissu alivyodai.

Hili siyo la upinzani ni la watanzania wote sababu faida ya demokrasia ni kwa watanzania wote sasa inatoweka na watanzania wenzetu wanatumika kuondoa mfumo wa vyama vingi na kuingiza mfumo wa chama kimoja kibabe
 
Yaani nasikiliza matokeo hapa nahisi kama roho inataka kutoka.

Chama chochote cha upinzani kupata hata kiti kimoja bungeni ni ndoto labda iwe kwa kuridhisha tu wanananchi kuwa kuna demokrasia😡😡😡

Tuendelee tu kukamilisha ratiba.
acha uongo ww kijana
Roho kutaka kutoka unajua au unajichatua tu...!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom