Unahalalisha wizi wa kura? Kwahiyo uongozi unapewa na viongozi wa serikali sio wananchi?
Nakuonaga ww ni great thinker kuliko Pro-CCM wenzio, ssa argument ya aina gani hii?
Sijabadili maudhui ya ushiriki wangu kwenye jukwaa letu hili la JF. Kamwe mimi katu sitomjadili mtu wala matukio. Ni hoja, hoja, hoja kwa kwenda mbele na mwanzo mwisho.
Nasimama katika hoja zangu za awali kuwa Viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao kabla, wakati na sasa baada ya uchaguzi walikuwa wamechimba kaburi lao na sasa wanajizika wenyewe humo.
Kaburi lao ni la kuamini Tume ya Uchaguzi siyo huru na CCM itatumia vyombo vyao Dola. Hawakuelewa na kama walielewa maana ya matumizi ya vyombo vya Dola, walidharau. Viongozi wa CCM, ngazi zote, waliisimamia Serikali (kwa maana ya vyombo vyake) kutimiza wajibu wake kama ilivyoainishwa kwenye Ilani ya Uchaguzi, 2015. Serikali imefanya ilichoagizwa na wapiga kura walisikia na wameona.
Upande wa vyama vya upinzani, viongozi walipumbazwa na ruzuku na malipo wa ubunge wakasahau wajibu wao kama wawakilishi.
Wagombea Urais, hasa wa CHADEMA na ACT-Wazalendo (Serikali ya Mapinduzi Zanzibar) kwenye kampeni wakajita kuwatuhumu viongozi wa Serikali za CCM pasipo kuwaeleza wapiga kura wataitoa Tanzania hapa ilipofikishwa na kuipeleka wapi. Ati "Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu (bila ufafanuzi), na Kazi na Bata". Walishindwa kueleza watafanya nini kuhusu miradi ya "vitu" inayoendelea nchini (SGR, Maji, Umeme, Afya, Elimu).
Kwa hoja hizo, ni ubishi na madai ya kitoto kuwa Uchaguzi haukuwa Huru na Haki. Ukirudiwa tena, na kusimamiwa na Tume ya Kimataifa, upinzani utaambulia sifuri.