benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Makala hii imeandikwa katika gazeti la Raia Mwema (25/10/2022).
HESABU za kisiasa za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) mara zote ni kama zinakosa uhalisia, hali ambayo inasababisha wao kukwama katika kutimiza malengo yao ya kisiasa!
CHADEMA ni kama hawana malengo ya muda mrefu na hawana malengo pia ya muda mfupi, ni kama wanatembea gizani!
CHADEMA mpaka sasa hawajatambua kuwa hawana kitu mkononi mwao na kwamba wanaanza sifuri kabisa! Jinsi ya kuanza sifuri ni tofauti na kuanza kwa mtu ambaye tayari ana kitu mkononi! Chama hiki mpaka dakika hi wana Mbunge mmoja tu wa jimbo katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wabunge 19 wa viti maalum ambao pia hawawatambui.
Hawana ushawishi wala majukwaa ya maana za kisiasa,
Hawana ushawishi kwa Watanzania wengi kwa sasa, tofauti na miaka sita iliyopita!
Mara zote nawaambia CHADEMA wajifunze kufanya kitu kinaitwa kukubaliana na hali ya siasa ya wakati huo. Wanajeshi kabla ya kuingia kwenye uwanja wa medani makamanda huwa wanafanya kitu kinaitwa kukubaliana na hali"!
'Appreciation' kwa kifupi ni hali au tendo la kufanya tathimini ya kina na ya haraka kuhusu mambo fulani fulani kabla ya kuingiiza vikosi vyako katika uwanja wa medani! Appreciation ufanyika ili kuweza kukubali mapungufu yako na ubora wako na kupima vikwazo ambavyo unaweza kukutana navyo kwenye uwanja wa medani na kutokea hapo ndio unajua jinsi ya kupanga mipango yako na ajenda zako za kivita!
Mipango ya kisiasa ni sawa na mipango ya kivita!CHADEMA a hawajiulizi kwa nini Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kumshikilia Mzee wangu Kanali mstaafu wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Abdulrahman Kinana, Mzee Kanali mstaafu Ngemela Lubinga?!
Wakati Chadema wanaangaika kupata makomando wa kumlinda kaka yangu Freeman Mbowe, wenzao CCM wanaangaika kutengeneza wanasiasa wa kimkakati kama Mzee Kinana!
CHADEMA ni kama hawana mkakati wa kisiasa wa kuwashauri vizuri, chama chao kinatembea na hoja nzito "Katiba Mpya" lakini wakiwa gizani. Mpaka unajiuliza, hawa watu wapo makini? Kwanini wanafanya makosa haya ya wazi kabisa?mpaka unashangaa!
Una ushawishi sifuri, jukwaa la kisiasa sifuri halafu unataka Katiba Mpya sasa, utaipataje kirahisi ajenda hii nzito na kubwa?, hauna hata wabunge kumi angalau bungeni, hautaki hata ruzuku, hauna jukwaa la kufanya siasa ili angalau upate ushawishi kwanza!
Katibu Mkuu wa CHADEMA , John Mnyika katoka hadharani na kutangaza kupinga ripoti ya kikosi kazi cha Rais Samia Suluhu Hassan, ambacho kiliundwa kwa ajili ya kuleta maoni ya jinsi gani ya kuendesha siasa Nchini! Uhitaji wa kikosi hiki ulikuja baada ya kuwepo kwa kitu kinaitwa "kifungo cha kisiasa"
Kwa zaidi ya miaka mitano kwa wapinzani nchini! Hongera nyingi kwa Mama Samia angalau anataka kuweka grisi kwenye vyuma vyenye kutu za kisiasa kupitia siasa za maridhiano lakini Chadema hawataki! Kha! Kikosi kimekuja na mapendekezo 18 mazito ikiwemo ajenda ya kufanya mikutano ya kisiasa, matokeo ya Urais ya Tume ya Uchaguzi yahojiwe mahakamani na mengine mengi mazuri.
Kwanza CHADEMA ya Mnyika iliwapasa washangilie maoni ya kikosi kazi hiki! Walipaswa kwanza wangekomaa na Mama Samia angalau mapendekezo hayo 18 ya kikosi kazi angalau yapite! Wakati mwingine ni jambo zuri kuliko kupata sifuri! Wangeweka malengo yao angalau wapate mambo 10 ya msingi ndani ya ripoti halafu nane wamwachie Mama Samia kwani Mheshimiwa Rais kashasema kwamba maoni yale hayaifungi Serikali.
Wakati Katibu wa CHADEMA , Mnyika akipinga ripoti ya kikosi kazi, vyama zaidi ya sita vya upinzani kesho yake vikatoka na kuipongeza Serikali kwa ripoti ile ya kikosi kazi! Hawa sasa wanajua kwamba hawana kitu mkononi afadhali wachukue angalau kidogo kwa sasa sababu hawajui kesho itakuwaje kwao!
Sioni ramani ya CHADEMA ni ya wapi, lini na nini wanataka kwa sasa! Ishu sio kutaka, ishu ni je utakipata? ni suala la kufanya "kukubaliana kisiasa" halafu unaseti mitambo yako kulingana na upepo ulivyo, Mama Samia sio mwepesi kihivyooo!