Inawezekana CHADEMA hawajui wanachokitaka

Inawezekana CHADEMA hawajui wanachokitaka

Utakuwa labeled kama Lumumba ukikubali kwa mfano kuwa bunge la sasa ambalo 99.999% ni CCM (walioingia kwa kuteuliwa na magufuli) lisimamie kupiga kura na kujadili rasimu ya Mkandara. Msikilize Mnyika katika press conference yake, mwenye akili na utashi wa demokrasi ataungana naye!
Kwani kuna Bunge sasa hivi au kikundi cha watu walioitana Bungeni?
 
Kwani kuna Bunge sasa hivi au kikundi cha watu walioitana Bungeni?
Pendekezo moja wapo ni hilo sasa, eti maoni ya Mkandara na some few individuals yapelekwe "bungeni", 99.999% ni CCM, yapitiwe then yaende kupigiwa kura na wanachi. Rubbish! Mwenye akili hawezi kukubali ujinga huo....
 
Makala hii imeandikwa katika gazeti la Raia Mwema (25/10/2022).

HESABU za kisiasa za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) mara zote ni kama zinakosa uhalisia, hali ambayo inasababisha wao kukwama katika kutimiza malengo yao ya kisiasa!...

Ndugu yangu,
Ulichoandika wewe na hiyo makala ni NYIMBO zile zile za akina Ndugai, Kabudi etc walipokuwa wanahanjahanja kusaka na kulinda kula zao. Kwao maisha ni kufaidi na "Ukitaka kufaidi jipendekeze" Ndio Tanzania ilipofikia,na ndio LEGACY ya mwndazake. Nchi inapokwenda kombo ukanyamazia ni aibu. Katiba mpya ndio dawa.
 
Salute Mkuu umejibia hii hoja vema, maana hoja ni lazima ijibiwe na hoja iliyo bora zaidi, chama dola kama kinaamini kwa dhati kuwa CDM imefilisika kisiasa why mpaka leo kivuli cha CDM wanakiogopa?,viongozi wa ccm wamekua wana zunguka nchi nzima kwa kutumia kodi yangu bila kikwazo chochote, ILA pale Mh.Mnyika alipoamua kutembea hapo Morogoro tayari policeccm hao na defenders zangu wanamzuia wakati hajavunja sheria yeyote, why wasimwache kama CDM ni mfu?,common guy's hii sio rocket science why uhangaike na mtu mfu (maiti)haiwezi kufanya chochote hata ukiipiga vibao!,ccm bila vyombo vya dola ni karatasi please prove me wrong
Amina
 
Ujinga ni kujitoa kushirki kutoa maoni alafu ripoti ikifika unakuwa wa kwanza kutoa maoni juu ya maoni waliyotoa wengine, kwa neno moja huo unaitwa upuuzi
Hata uundaji wa hicho kikosi kazi ulikuwa feki, vichekesho, ungekuwa mkweli tungekusikia. Hebu tuache basi kuchezea taifa letu.
 
Tatizo la CDM mtu yoyote atakae kua na mawazo tofauti na nyie aidha awe ndani ya Chama au nje ya Chama kitu cha kwanza mnamuita Lumumba.

Ingekua ni Cult au kikundi cha dini tungewaelewa ila kam ni Chama cha kidemokrasia lazima mawazo yapishane. Hoja hazijaisha ila haina maana kujadili hoja ambazo hazipata muafaka.
Tunaangalia na dhamira za hoja zenu siyo za kujenga ni upuuzi mtupu kwa
Nakuelewa katika hilo but unfortunately ukianza kuuliza kitu tofauti na msimamo wa CDM hasahasa vijana immediately unakua labeled ni Lumumba.
Kama mawazo yako, maneno yako ni ya kilumumba kwa nini unaogopa kutambuliwa kwa matendo yako?
Hivi huoni jinsi ambavyo CCM inatumia dola kunyanyasa na kuzuia wenye mawazo mbadala kufanya siasa nchini?
 
CHADEMA CHADEMA, haipo bungeni Wala kwenye Halmashauri lakini inajadiliwa utadhani chama tawala. Big up CHADEMA
 
Nadhani Demokrasia unayoipambania ni pamoja na kuwa na TOLERANCE ili upokee mawazo mbadala na ya kwako

Tolerance kwa CHADEMA tu?. Yani CHADEMA ndio wafanyiwe mabaya wao wavumilie?. Wapotezwe. Wauawe, wapigwe risasi, waibiwe kura, waibiwe wabunge viti maalum, wafunguliwe kesi za ugaidi?. Tupunguze unafiki.
 
Mwandishi chawa anadhani kuandika hivyo ndio atakaubalika na mama Samiah.
 
Kitu Chadema wanachokijua wanamchukia Zitto Kabwe hayo mengine tuwasamehe tu.

Mbona Zitto na CHADEMA hawachukiani? Ni CCM inachochea chuki baina yao. Ndio maana Zitto amesema wazi kuwa baba yake kwenye siasa ni Mbowe na kwenye uchaguzi wa 2020 walimuunga mkono mgombea urais wa CDM.
 
Mbona Zitto na CHADEMA hawachukiani? Ni CCM inachochea chuki baina yao. Ndio maana Zitto amesema wazi kuwa baba yake kwenye siasa ni Mbowe na kwenye uchaguzi wa 2020 walimuunga mkono mgombea urais wa CDM.
Zitto na CDM hahahaha labda huwajui vijana wa CDM. Mtu ambae anaweza kukaa meza moja na Zitto kutoka CDM ni Mwenyekiti tu.
 
Ujinga ni kujitoa kushirki kutoa maoni alafu ripoti ikifika unakuwa wa kwanza kutoa maoni juu ya maoni waliyotoa wengine, kwa neno moja huo unaitwa upuuzi

Upuuzi ni Rais kuunda kikozi kazi na kukilipa pesa za walipa Kodi halafu kwenye kupokea mapendekezo ya kikosi kazi, rais kila pendekezo analikrush kana kwamba kile kikosi kazi kimejiteua chenyewe.
 
Nakubaliana na andiko, chadema ni hakuna wanachojua.

Ilaa mwandishi namsahihisha, kikosi kazi hakipo juu ya katiba. Kusema wana mapendekezo mazuri ikiwemo matokeo ya uraisi kupingwa mahakamani ni ujinga, kwa kuwa katiba hairuhusu.

Chadema kinajadiliwa Kama vile ni chama tawala. Mtu anajipinda kurasa mbili za gazeti kuisema CHADEMA, ila mambo ya tozo , mhawo wa umeme na maji, mfumuko wa Bei amepiga kimya.
 
Nakuelewa katika hilo but unfortunately ukianza kuuliza kitu tofauti na msimamo wa CDM hasahasa vijana immediately unakua labeled ni Lumumba.

Ndio practice huwezi ukawa tofauti na msimamo wa chama na ukawa mwanchama wa chama hicho. Muulize Ndugai alipoenda tofauti na Mwenyekiti wake wa chama alishambuliwa mpaka akaomba radhi na bado hakusamehewa Hadi kujiuzjlu.

Huwezi kuwa mwanachadema ukawa na msimamo tofauti na CHADEMA. Vyama vipo vingi tafuta chama chenye msimamao au mawazo Kama yako.
 
Zitto na CDM hahahaha labda huwajui vijana wa CDM. Mtu ambae anaweza kukaa meza moja na Zitto kutoka CDM ni Mwenyekiti tu.

Ni madhaifu ya Zitto ya kihistoria ndio bado yamejenga perception mbaya kwa vijana wa CHADEMA, ila tukifika kwenye common ground CHADEMA haina chuki na Zitto.
 
Ujinga ni kujitoa kushirki kutoa maoni alafu ripoti ikifika unakuwa wa kwanza kutoa maoni juu ya maoni waliyotoa wengine, kwa neno moja huo unaitwa upuuzi

Mkuu ulikuwa mjumbe wa kikosi kazi nini? CDM hawajatoa maoni kuhusu hicho kikosi kazi, wao wameonyesha shaka yao juu ya nia ya hicho kikosi kazi. Nadhani ndio demokrasia yenyewe, au?

Na kwa taarifa yako, CDM wanapoponda hayo mapendekezo ya kikosi kazi, wanatengeneza mazingira wa hayo mapendekezo mengi kutekelezwa kama sehemu ya kuwaprove wrong, kitu ambacho kisingeweza kutekelezwa iwapo vyama vyote vingeunga mkono.
 
Tunachokitaka Chadema ni kushika hatamu, CCM haina jipya Mafuvu yale yale.
skeleton-head-less.gif

icon_mrgreen.gif
 
Back
Top Bottom