Mtoa mada una akilia nyingi Sana,wanaokubeza na kukupinga wana akilia mgando.
Kwanza kuumiza kichwa TU na kuja na wazo lako Ni mwanzo wa utafiti(research) Tosha.
Na kuanzia Hapo wengine wanaweza kuongeza kwa kwenda deep zaidi
Tatizo la Wachangiaaji wengi humu na husussani Watanzania huwa tunaviamini Sana vitu vikivyokwisha kamilika na hasa vilivyokamililishwa na wazungu.
Bila kujali hata hao wazungu inawezekana walipata wazo kutoka kwa Mtu mmoja great thinker kama wewe.Ndipo hao mabingwa wakaendeleza alipoishia mtoa wazo.
Kitu kingine Cha kushangaza kwa wachangiaaji wengi,badala ya kujadili mada wanajadili kosa la herufi.spelling wakati tayari wameshajua au walishaelewa kuwa ulitaka kusema Nini au ulimaanisha Nini,lakini ukakosea herufi TU.
Kosa la herufi bila kujua pengine ulikua umekusudia kuandika meno Fulani ukakosea kubonyeza herufi husika.
Hata hivyo mada yako inafikiriaha.
Iweje Nchi jirani na baadhi ya Nchi watu wanakufa kama kuku wa kideri lakini sisi so hivyo?