MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Kuna mshkaji mtaani tulikua tunajadili changamoto iliyopo kwenye zogo la mahindi baina ya Kenya na Tanzania, akanipa uwezekano wa wazo fulani, naifahamu sana Serikali yangu ya Kenya ikitaka kuficha kitu kwanza huwa na mazoea ya kuibua jambo lingine litakalosababisha migongano ya baina yetu kwenye mitandao ya kijamii, tukianza kulumbana hapo fursa inapatikana ya kufanya walichotaka kufanya au kuficha hadi tunapomaliza kulumbana walishafanya yao.
Nimewaza hili la mahindi na kujiongeza, mahindi yaliyopakiwa kwenye malori ya kutokea Tanzania, haya mahindi tunayakula kila siku, mbona ghafla ndani ya wiki hizi mbili ndio pameibuka hili, na kusababisha migongano baina ya Wakenya na Watanzania kwenye mitandao ya kijamii, kipi hicho tunafichwa kinachohusu hizi nchi mbili.
Maana hili la mahindi limeibua mapovu kote, kuanzia Youtube, Twitter, Facebook, mpaka huku JF tunalumbana kwa kwenda mbele, na uwezekano mkubwa upo zikiisha siku 14 au 20 tutaambiwa wamesuluhisha palikua na sintofahamu fulani tu lakini wameweka sawa.
Haya bana sitahoji zaidi, ila kama ni kweli basi wakuu mngetafuta kingine cha kutumia, hili la mahindi mlikosa ubunifu maana mtasababishia watu hasara. Uzuri wa kwetu hapa tuna uhuru wa maoni.
Wana Afrika mashariki bado natoa tahadhari, corona ipo na inapukutisha, vaa barakoa muda wote ukiwa nje, nawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, epuka misongamano, ukihisi dalili zinazofahamika, nenda kwenye kituo cha afya mara moja, acheni hayo mambo ya sijui matangawizi na malimau, hayo yafanye wakati uko mzima ili kuendelea kujichimbia na kuongeza kinga, ila ukihisi kimepenya, kimbilia kwenye kituo cha afya, kunazo dawa za kawaida ambazo zinakipiga vita hiki kirusi.