Inawezekana kuishi bila kufanya dhambi

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Dhambi kila mtu anazijua.ni kuenenda kinyume na anavyopenda MFALME MUNGU JEHOVA.mimi Binafsi nilivokuwa mdogo nilijiwekea lengo kwamba ninatamani niishi maisha ya kitakatifu bila kufanya dhambi Ili nije kurithi ile ahadi ya kuonana na MUNGU. nilijipa matumaini kwamba inawezekana kabisa baada ya kusoma katika maandiko jinsi mitume na manabii walivyookolewa na mkono wa MUNGU baada ya kuamua kuwa wakamilifu.baada ya kukua na kuwa mkubwa nikasikia maneno ya walimwengu walionitangulia kwamba kila mwanaadamu kaumbwa na mapungufu kwa hiyo kukosea Ni LAZIMA hata uamue kufanya Nini Ni lazima tu utende dhambi huku wakisisitiza kuwa msamaha na Toba upo.kama unavyojua ujana huu na makuzi ya mtaa nikajikuta nimekuwa mtenda dhambi Kama nyie.kwa sasa natamani Sana niishi bila dhambi maana zinanila Sana zinanitesa.nimejitahid Sana kusali,kusoma neno la MUNGU, kubadilisha marafiki,kuombewa na viongozi wa dini lakini bado najikuta naanguka dhambini.naombeni msaada wenu ndugu zangu Kama Kuna yoyote ambaye amefanikiwa kuishi muda mrefu bila kufanya dhambi anisaidie ushauri anipe dondoo za kuwashinda haya mapepo ya dhambi.kiukweli Nina Hali mbaya Sana maana nikisema nimeokoka najikuta nasahau na nikiangukia tu mtegoni Basi majini yanarudi Kama yote yananiingiza hukumuni naanza kujilaumu.lakini nikifikiria naona kabisa Kama inawezekana kuishi bila uasherati,bila uongo bila kiburi bila tamaa bila ulevi .niko serious ndugu zangu naogopa Sana kifo na Moto uliohaidiwa watenda maovu.nahitaji kampan ya marafiki wema ambao hawatendi dhambi tubadilishane mawazo waweze kunisaidia kiroho njia rahisi wanazotumia kumshinda yule baba wa uwongo ibilisi.nisije kuangamia natambua yesu masiha ndiye njia kweli na uzima lakini tangu nianze kumsikia na kujifunza kuhusu yeye kwenye biblia bado sijapona kiimani.labda kwa sababu hayupo katika ulimwengu huu wa macho alishaenda mbinguni ndo maana nasadiki Kisha narudi dhambini baada ya kujaribiwa.nisiongee mengi nachohitaji kwa Sasa Ni kuacha dhambi kabisa nijaribu na maisha ya Upande wa pili ya watakatifu mliopo duniani.kama unaweza kunisaidia kwa namna yoyote please unaweza kuni PM.asanteni nategemea kupata msaada sio TU wenye kutia moyo ila wenye mbinu za kiufundi za kujinasua dhambini utumwani
 
Labda ufe ndio utakuwa mwisho wa kutenda dhambi ila kama upo hai haiwezekani(kuna vitu kuvishinda kazi sna kuna kitu kitaalam kinaitwa "PUSSY" hauwezi kukikimbia....
 
as long as unaishi huwezi kwepa dhambi

mfano kwa sisi waislam kuacha miba au chupa njiani tu ni dhambi sasa jiulize mwenyewe utaokota chupa ngapi kwa siku imagine upo dsm sasa

nimejibu kichwa cha uzi tu content nimeshindwa kusoma hujaweka paragraph halafu ni ndefu najiona naishiwa pumzi tu 😉
 
Labda ufe ndio utakuwa mwisho wa kutenda dhambi ila kama upo hai haiwezekani(kuna vitu kuvishinda kazi sna kuna kitu kitaalam kinaitwa "PUSSY" hauwezi kukikimbia....
Kwa hiyo mkuu hiko kitu kimewashinda mababu na mababu zetu,sema nn kwa mfano ukaamua kuoa ili ukile kile KIDONDA kwa Uhuru na kwa haki.si inawezekana?yaani usichepuke nje
 
Duh Sasa mkuu tutapataje kupona Ina maana tukubaliane tu kwamba yaishe tukachomwe Moto .unavyounguza vile
 
Duh Sasa mkuu tutapataje kupona Ina maana tukubaliane tu kwamba yaishe tukachomwe Moto .unavyounguza vile
kwa imani yangu..yale mema unayofanya yanamalipo makubwa kuliko dhambi unazofanya

mfano:-
baya 1 utalipwa dhambi 1
zuri 1 utalipwa swahabu 10

kazi ni kwako
 
na sitamani iwezekane mana dhambi raha sana.
 
Manabii wenyewe walitenda zambi sembuse wewe wanaoweza kuishi bila kutenda zambi ni watoto wadogo tu
 
Hii ni vigum tena sana
Huenda hata dhambi tumeumbiwa kama yalivyo magonjwa
Biblia inasema hata kumtazama tyu mwanamke tayari umekwisha zini naye kwa macho!
Je kwa siku unatazama wangap????
 
Kwa hiyo mkuu hiko kitu kimewashinda mababu na mababu zetu,sema nn kwa mfano ukaamua kuoa ili ukile kile KIDONDA kwa Uhuru na kwa haki.si inawezekana?yaani usichepuke nje
hakuna mwanaume anayependa mwanamke mmoja.... na ukitamani tu mwanamke asiye mke wako tayari ni dhambi...

kwa hyo huwezi ishi bila kutenda dhambi
 
Dhambi zikipotea bas misikiti na makanisa yatapotea piA
 
Lile ninalo lipenda kulitenda silitendi, ila lile nisilo lipenda ndio nalitenda.... By Apostle Paul...... Tukisema hatuna dhambi, tunajidanganya wenyewe... By apostle John
 
Inawezekana,kwasababu dhambi ni vile vitendo vya makusudi,yaan unajua kuwa unakosea kila kwa jeuri/kiburi chako wewe unafanya tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…