ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,643
- 51,642
Dhambi kila mtu anazijua.ni kuenenda kinyume na anavyopenda MFALME MUNGU JEHOVA.mimi Binafsi nilivokuwa mdogo nilijiwekea lengo kwamba ninatamani niishi maisha ya kitakatifu bila kufanya dhambi Ili nije kurithi ile ahadi ya kuonana na MUNGU. nilijipa matumaini kwamba inawezekana kabisa baada ya kusoma katika maandiko jinsi mitume na manabii walivyookolewa na mkono wa MUNGU baada ya kuamua kuwa wakamilifu.baada ya kukua na kuwa mkubwa nikasikia maneno ya walimwengu walionitangulia kwamba kila mwanaadamu kaumbwa na mapungufu kwa hiyo kukosea Ni LAZIMA hata uamue kufanya Nini Ni lazima tu utende dhambi huku wakisisitiza kuwa msamaha na Toba upo.kama unavyojua ujana huu na makuzi ya mtaa nikajikuta nimekuwa mtenda dhambi Kama nyie.kwa sasa natamani Sana niishi bila dhambi maana zinanila Sana zinanitesa.nimejitahid Sana kusali,kusoma neno la MUNGU, kubadilisha marafiki,kuombewa na viongozi wa dini lakini bado najikuta naanguka dhambini.naombeni msaada wenu ndugu zangu Kama Kuna yoyote ambaye amefanikiwa kuishi muda mrefu bila kufanya dhambi anisaidie ushauri anipe dondoo za kuwashinda haya mapepo ya dhambi.kiukweli Nina Hali mbaya Sana maana nikisema nimeokoka najikuta nasahau na nikiangukia tu mtegoni Basi majini yanarudi Kama yote yananiingiza hukumuni naanza kujilaumu.lakini nikifikiria naona kabisa Kama inawezekana kuishi bila uasherati,bila uongo bila kiburi bila tamaa bila ulevi .niko serious ndugu zangu naogopa Sana kifo na Moto uliohaidiwa watenda maovu.nahitaji kampan ya marafiki wema ambao hawatendi dhambi tubadilishane mawazo waweze kunisaidia kiroho njia rahisi wanazotumia kumshinda yule baba wa uwongo ibilisi.nisije kuangamia natambua yesu masiha ndiye njia kweli na uzima lakini tangu nianze kumsikia na kujifunza kuhusu yeye kwenye biblia bado sijapona kiimani.labda kwa sababu hayupo katika ulimwengu huu wa macho alishaenda mbinguni ndo maana nasadiki Kisha narudi dhambini baada ya kujaribiwa.nisiongee mengi nachohitaji kwa Sasa Ni kuacha dhambi kabisa nijaribu na maisha ya Upande wa pili ya watakatifu mliopo duniani.kama unaweza kunisaidia kwa namna yoyote please unaweza kuni PM.asanteni nategemea kupata msaada sio TU wenye kutia moyo ila wenye mbinu za kiufundi za kujinasua dhambini utumwani