GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Wazo hili limezaliwa kutokana na michango ya wazoefu waliomo humu JF wa kilimo cha zao tajwa. Kwa kuwa wazo limezaliwa humu, nimeamua kulirejesha humu ili lipate ukosoaji wenye tija.
Kwa mujibu wa wazoefu, inaonekana ngwara ni zao lisilohitaji maji mengi. Hulimwa
mwishoni mwa msimu wa mvua.
Ikiwa ndivyo, haiwezekani kulilima kipindi cha kiangazi?
Maadam linahitaji unyevunyevu tu utakaosaidia kuchipua, kwa nini lisimwagiliziwe kwa maji ya kisima, mto, n.k.?
Kwamba, labda mkulima anaamua kuandaa utaratibu wa kusomba maji kutoka mtoni kwa kichwa, gari, n.k. kwa ajili ya kuloanisha ardhi wakati wa kupanda, kisha baada ya hapo, anamwagilizia mara moja kwa wiki mpaka mazao yake yatakapokomaa.
1. Utaratibu huo utafaa?
2. Kwa wastani, shina moja la ngwara linahitaji maji kiasi gani kwa siku?
3. Kama mtu ataamua kufanya kilimo cha ngwara kipindi cha kiangazi, atapaswa kumwagilizia mara ngapi kwa wiki?
🙏🙏🙏