Inawezekana kweli Barbara Gonzalez ni tatizo Simba

Na alichowanyoosha zaidi Barbara ofisi za Simba kahamishia Masaki, pale kariakoo kawaacha kina Abunuwasi wapige porojo tu, kwahiyo hata wazee wa kupiga mizinga hawana access na CEO na hajawahi kukanyaga makao mkuu ya Simba Msimbazi hata siku moja.

Ofisi zipo Masaki, press na waandishi zinafanyika Serena hotel, kina Abunuwasi kazi yao wanatakiwa kwenda uwanjani tu kushangilia, lazima apigwe vita sana, na alivyoingia tu alianza na huyu tapeli tapeli Haji Manara.
 
Unayajua mengi kuhusu kariakoo hongera sana mtani
 
Tatizo mpira wetu ni upigaji mwingi, Babra namkubali binafsi kwa misimamo yake. Tumezoea unafiki sasa mdada kawakazia hakuna upigaji. Nyie mchezaji wa Mil 100 mnamwambia M 300 bado mnataka asajili tu. Mimi namuelewa anasubiri wakati muafaka na mchezaji sahihi.
 
Tatizo la Simba ni kuanza kutoa Posho za kila mechi ambayo wachezaji hufunga.
Kitu ambacho sio sawa, wale ni waajiriwa watapaswa fanya kazi zao.

Barbra akiondoka Simba itateseka kifedha na kuna wadhamini huenda wakajiondoa
 
Mtani umeongea vizuri..ukweli mtupu.
 
Barbra amesimama kwenye misingi ya uendeshaji wa kampuni(Simba) kwa kuzingatia kanuni za Fedha na Kiutawala hivyo kwa watu waliozoe kufanya vitu kienyeji inakuwa shida kukuelewa.
 
Barbra amesimama kwenye misingi ya uendeshaji wa kampuni(Simba) kwa kuzingatia kanuni za Fedha na Kiutawala hivyo kwa watu waliozoe kufanya vitu kienyeji inakuwa shida kukuelewa.
Kwanza hata muda wa kumboom Barbara hakuna, ofisi zipo Masaki, hakuna Abunuwasi yeyote anayefika Masaki.
 
Ahsante sana.
 
Umepiga penyewe mkuu
 
Umenichekesha hapo lwa makomandoo kwamba jamaa wakatimba mwanza wakijua wanaenda kuzuia getini.. sema popote pale ukiziba mianya ya upigaji lazima upogwe vita ishu ni kucheza nao kwa akili tu usiwabanie sana, upogaji mdogo mdogo ambao hauleti hasara kubwa unapotezea tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…