johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Nimesikiliza kauli moja tu ya mtumishi wa Mungu Mchungaji Msigwa akikiri kuwa ana undugu na Rais Magufuli.
Na zaidi Mchungaji Msigwa akasema kama wanafamilia "wao" wana namna wanavyoshughulikia mambo yao.
Nilichojiuliza ni kwanini Mchungaji Msigwa hajawahi " Kujimwambafy" kwamba yeye ana uhusiano na Rais Magufuli?
Pale Chimala na Matamba wanajua kuwa Mchungaji Msigwa ana uhusiano na Rais Magufuli lakini jimboni Iringa wengi wamejua juzi.
Siyasemi haya kwa sababu ya Msigwa kulipiwa faini kwani hata mstaafu Kikwete aliwahi kumlipia " mahali" mwanaharakati huru na hakuna aliyehoji.
Ninachotaka kusema hapa ni ushupavu wa Dr Magufuli na Mchungaji Msigwa walivyouhifadhi uhusiano wao bila walio wengi kufahamu.
Hata juzi kama Mnikulu ndiye angeenda Segerea kumtoa Mchungaji bila shaka Msigwa angepanda gari ya serikali kurudi nyumbani tatizo ni zile sare za kijani ndio zilizoiletea shida familia hii.
Cha muhimu tumepata somo kuwa bado kuna " turufu" zimebaki pale Ufipa na huenda hawa waliohamia CCM ni magarasa matupu.
Maendeleo hayana vyama!