Inawezekana Rais Magufuli amesaini ule mkataba wa ushirikiano na mataifa ya Ulaya (EPA)?

jmushi1

Platinum Member
Joined
Nov 2, 2007
Posts
26,329
Reaction score
25,263
Wanajamvi,

Kuna habari zimekuwepo kuhusu nchi za EU kuanza kutoa misaada mara baada ya nchi hizo kusimamisha misaada hiyo kwasababu ya ukosekanaji wa demokrasia nchini. Lakini kuna makala moja nimekutana nayo ambapo inaonyesha Mh. Rais ameshaanza kubadili msimamo kuhusiana na mkataba huo wa ushirikiano wa kibiashara na mataifa ya Ulaya, ama “Economic Partnership Agreement”(EPA). Mkataba ambao mwanzoni rais alisema ni wa kinyonyaji na kikoloni. Na ukapingwa vikali hadi bungeni.

Mkataba huu ulipoletwa mwanzoni, Magufuli aliuita kuwa ni “mkataba wa kikoloni”, kwasababu unaenda tofauti na malengo ya serikali yake ya viwanda. Na bunge lilifuatia kwa kuupigia kura ya “Hapana”. Point yao ikiwa ni kwamba hatuwaweza kufanikisha sera ya viwanda kwasababu hatuwezi kushindana nao, na pia tunategemea kodi za mapato kutokana na bidhaa zinazoingizwa kutoka kwenye mataifa hayo.

Rais Magufuli aliuponda sana mkataba huo mbele ya rais Museveni wa Uganda. Mkataba huo ni wa kuondoa ushuru kwenye bidhaa baina ya mataifa hayo ya Africa na Europe.

Hadi kufikia mwaka jana, Rwanda na Kenya tayari walikwisha usaini mkataba huo. Mkataba huu ulitakiwa usainiwe na mataifa yote ya EAC. Baadhi walisaini na baadhi hawakusaini tukiwemo sisi, Uganda na Burundi.

Kwenye makala hii, mwandishi anaonesha kuwepo na uhusiano kati ya serikali kuonyesha dalili za kubadili msimamo kwenye mkataba be serikali kunyimwa msaada na mataifa hayo kwa kukandamiza demokrasia.

Sasa nilikuwa nikijiuliza ni kipi kimefanyika wakabadili mawazo? Ndipo nikakutana na hii.

Kwa kifupi, mwandishi anaonyesha uwezekano wa “quid pro quo”, yani mkataba unasainiwa na vikwazo vinaondolewa bila kujali kama sababu zilizofanya vikwazo hivyo vikawekwa zimekwisha kufanyiwa kazi!

Je, hapa tunajifunza nini? Je, kuna kingine ambacho Magufuli akiwapa basi watafumbia macho yote waliyokuwa wakiyakodolea mimacho hapo mwanzoni? Mfano uminywaji wa demokrasia?
 
Mwandishi anadai maofisa wa EU walishtushwa na uamuzi wa Maghufuli kubadili mawazo na kutaka kuusaini huo mkataba. Mwanzoni nilijiuliza nini kimebadilika kwenye mkataba huo? Kwasababu Maghufuli aliwahi kuuita ni “mkataba wa kikoloni”

 
Gazeti la Business Daily nalo linasema kuwa serikali inachukuwa hatua za kutaka kusaini mkataba huu a kikoloni ili kujaribu kukarabati mahusiano yaliyokuwa yameharibiwa na matendo yasiyo ya kidemokrasia. Serikali ilikuwa imeharibu mahusiano na EU hadi balozi wao kurudishwa kwasababu ya ukosekanaji wa demokrasia Tanzania.

Fresh review
 
Yaan wewe jibu ushatoa kuwa sababu ni kuondelewa vikwazo

Alafu hapo hapo bado tena unatuuliza tena sisi sababu

Hakuna mbabe mbele ya mbeberu hayo majamaa yana uwezo wa kukushushia wahyi ukabaki unashangaa tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani nimeuliza sababu? Wapi hapo?
 
Yaan wewe jibu ushatoa kuwa sababu ni kuondelewa vikwazo

Alafu hapo hapo bado tena unatuuliza tena sisi sababu
Hakuna mbabe mbele ya mbeberu hayo majamaa yana uwezo wa kukushushia wahyi ukabaki unashangaa tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hapa umemix madesa. Nitasema sababu ni kuondolewa vikwazo kama atakuwa ameshaini huo mkataba.

Sababu zilizotolewa na waandishi hao zinahusishwa na serikali kuonyesha nia ya kutaka kusaini mkataba huo.

Nimeuliza tu kama umeshasainiwa maana kina MsemajiUkweli, Pascal Mayalla na YEHODAYA walileta habari za misaada kutolewa. Unachokiwa ni maoni mkuu na si maneno ya kwenye kanga!
 
Maana naona hata beberu la Economist inasemekana linaisifia ccm na serikali yake!😂 Kabendera naye ni a victim of circumstances.
 
Mwandishi anadai maofisa wa EU walishtushwa na uamuzi wa Maghufuli kubadili mawazo na kutaka kuusaini huo mkataba. Mwanzoni nilijiuliza nini kimebadilika kwenye mkataba huo? Kwasababu Maghufuli aliwahi kuuita ni “mkataba wa kikoloni”
Hizo setenso za kiingereza zinamaanisha ulivyoandika kiswahili?
 
Mkuu elewa kuwa tajiri hadhihakiwi na hakuna siku mkate utakuwa mgumu mbele ya chai jmushi1,

In God we Trust
 
Hakuna mwenye njaa anayeweza kushindana na mwenye shibe
Mwandishi anadai maofisa wa EU walishtushwa na uamuzi wa Maghufuli kubadili mawazo na kutaka kuusaini huo mkataba. Mwanzoni nilijiuliza nini kimebadilika kwenye mkataba huo? Kwasababu Maghufuli aliwahi kuuita ni “mkataba wa kikoloni”


In God we Trust
 
Kwanza habari quoted ni ya march mwaka jana.

So the hypothesis enumerated above could safely be nullified. In relation to EPA agreement, will surely be signed be it sooner or later.

Swala la EU ku-release mshiko, nafikiri EU wako kwenye competition na UK/US.
 
Hizo setenso za kiingereza zinamaanisha ulivyoandika kiswahili?
Ndiyo, zinamaanisha hivyo.

“Taken aback” ni kushtushwa na kushangazwa.

“to be taken aback. phrase. If you are taken aback by something, you are surprised or shocked by it and you cannot respond at once. Roland was taken aback by our strength of feeling.”-Collins Dictionary
 
Sasa ndo umeandika kitu gani?
 
Kwa hiyo akisaini mkataba wa EPA hata hoja za demokrasia zitaisha!

Maelezo yako yanaonyesha kumbe tatizo halikuwa suala la demokrasia bali Mkataba wa EPA!

Tukisema hizi kelele za EU na USA kudai demokrasia ni kibwagizo tu kwa sababu maslahi yao yamezibwa tutakuwa tunakosea!


Sent from my iPhone
 
Dah! Ndugu kumbe nilikukwaza tena?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa mkuu. Maslahi ya Taifa yamezingatiwa? Au unazungumzia kukaa madarakani kwa gharama yoyote? Vipi kuhusu viwanda?
 
Na aliyeita mkataba wa kikoloni kisha akaja kuusaini tusemeje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…