Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Katika nchi yetu na pengine duniani kote,hesabu ndio somo linalotajwa kuwa gumu(wengi wanashindwa kulielewa) kuliko masomo mengine mengi, ila binafsi naona kwa nchi yetu siasa za nchi hii ndio somo gumu zaidi kueleweka kwa watanzania walio wengi.
Inawezekana kabisa hata wale ambao ni "magwiji"wa hesabu, baadhi yao ndio wakawa vilaza wakubwa katika kuelewa siasa za nchi hiii.
Hali hii ya watu kushindwa kuelewa siasa za nchi yetu,ndio msingi wa wanasiasa kuwarubuni watu na kuwafanya kama wajinga kiasi kwamba hata wakifanya mambo ya kijinga na kipuuzi, bado kuna watu watawatetea na hata wakitimiza wajibu wao, kuna watu watawatukuza kama miungu watu.
Kwa mfano,hivi sasa kuna mwanasiasa mmoja mwenye madaraka makubwa tu kaamua kufanya mambo yasiyofaa yenye muelekeo wa chuki,ubaguzi,uonevu,n.k, ila kuna watu kutokana na siasa kwao kuwa ni somo gumu, haya yote hawayaelewi ingawa wanayoana kisa tu Bwana yule anafanya baadhi ya mambo mengine yanayoonekana kuwa ni mazuri lakini ambayo ndio wajibu wake kwa nafasi yake.
Kutokana na uelewa mdogo wa watu katika kuwapima wanasiasa kwa matendo na kauli zao,watu wanashindwa kuelewa kuwa huyu bwana ndio chanzo kikuu cha yote haya na badala yake utawasikia baadhi ya wenzetu wakilaumu wasaidizi wake eti ndio wanamshauri vibaya na kwamba hao ndio wanampotosha!!!
Mfano mwingine ni mwanasiasa mmoja machachari aliewahii sema kuwa kuna kiongozi fulani aliwahi ishi kwa "uongouongo" jambo ambalo ukilichunguza utagundua ni kweli kwa baadhi ya mambo(mfano lile swala la kuunganisha nchi "A" na nchi "B") ila mwanasiasa huyo alishambuliwa sana kwa kauli yake hiyo na ukichunguza utagundua hii ni kutokana na siasa kuwa ni somo gumu sana kueleweka kwa walio wengi na ndio maana watu wanadanganyika sana na wanasiasa.
Uzuri mzee wa watu kwa heshima na busara zake, aliwahi kukiri hadharani kuwa katika zama zake, kuna mambo ya kijinga yalifanyika, ila watu wanashindwa kuelewa kuwa hili la kuunganish nchi "A" na nchi "B" ni moja ya hayo makosa aliyoyafanya enzi zake(mchakato mzima ulivyofanyika).
Na bahati mbaya sana kwa sasa amepatikana yule anaetumia uelewa mdogo wa watu katika mambo ya siasa kutaka kufanya karibu kila mtu ni kilaza wa siasa za nchi hii ila msishangae akawapata wengi maana siasa limekuwa somo gumu sana katika Taifa hili na wengi wataendelea kufeli hili somo mpaka kwenye vyumba vya kupigia kura na kutugharimu tusiohusika na ujinga huu.