MKEHA
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 716
- 1,143
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wabunge wengi waliochangia kamati ndogo ya sheria na ajira kuna kubebana sana kwenye SECRETARIAT ya ajira. Wabunge wamesema siku hizi kuna kanda watu wake hawaajiriwi kabisa.
Kuna vimemo vinawataka wabunge watie mkono ili ajira zitoke. Je NEPOTISM inatokea ndani ya secretariat yenyewe ama mfumo ndo unaamua yupi apate ajira.
Mbunge wa Simanjiro bwana Ole Sendeka ameenda mbali sana kwa kutoa taarifa kuwa suala la ajira limegawa nchi katika vipande. Kuna ukanda unapata ajira sana huku wengine wakiishia kwenye usaili tu
Amesema hapo zamani serikali ililiona hilo chini ya Mwalimu Nyerere na kuamua kila mkoa kuwa na pass mark zake ili kuweka usawa katika nchi.
Wengine wamesema serikali iige jinsi majeshi yetu yanavyo ajiri kwani kila wilaya huwa na nafasi zake maalum na hivyo kuwa na uwoano mzuri kwenye ajira zaajeshi japo wamesema askari wengi huingiza watoto wao, ndugu zao na.marafiki zao kwenye ajira hizi.