JOHNGERVAS
JF-Expert Member
- Mar 22, 2016
- 1,487
- 2,599
Inawezekanaje TCRA na JAB kuruhusu Diwani wa CCM Kata ya Kariakoo Haji Sunday Manara kufanya kazi za utangazaji wakati bado ni mwanasiasa active mwenye nafasi ya uongozi?
Je, sheria inaruhusu hali hiyo? Je, kweli anaweza kuwa fair mbele ya hadhira?
Tumeshuhudia interview mbili alizofanya kwa viongozi wa upinzani, akiwemo John Heche Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA pamoja na Ado Shaibu wa ACT. Katika mahojiano hayo, baadhi ya maswali yalionekana kuulizwa zaidi kwa mtazamo wa mwanasiasa na mwana-CCM kuliko kwa misingi ya taaluma ya utangazaji na uandishi wa habari.
Swali la msingi ni hili: mtu akiwa mwanasiasa active, tena kiongozi aliye madarakani, akipewa jukwaa la media bado tunaweza kutegemea neutrality, balance na fairness ya kweli? Au hii ni conflict of interest inayopaswa kuangaliwa upya?
Wakongwe wa sheria, wanahabari na wadau wa media, hili limekaaje kisheria, kitaaluma na kimadili? Pascal Mayalla