Inawezekana Vipi Zanzibar Kuna Div I, Div II, na Div III Chache, Ila Div IV na Div Zero Nyingi?!.

Hahahaaa punguzeni madrasa nendeni na shule mpate ufaulu mzuri
Hata ivo msijali hakuna elimu kubwa kuzidi elimu ya Allah
Ila huu uzi wa kitambo sana 2013!!
Mnisamehe kwa kutonesha kidonda
 
 
 
Jee kuna uwezekano matokeo mabaya ya Zanzibar na shule za dini fulani yanahusiana na imfluence ya dini hiyo kwenye akili za waumini?!, au ni imfluence ya Waarabu?!.

Pasco

Dini ku-influence matokeo ya darasani ni swali muhimu.
Lakini tujiulize, vipi Irani, Egypt, Algeria, Saudi Arabia na maeneo mengine duniani ambako wakazi wengi ni wa 'dini' hiyo, hali ya elimu ya kimagharibi ikoje?

Kuhusu Zanzibar, maoni yangu ni kwamba kuna mgongano mkubwa kati ya imani za kitamaduni za wazanzibari na imani za 'dini'. Mgongano huu wa imani hizi ni kama umepea zaidi kwenye imani potofu zinazofifisha ustawi wa jamii badala ya kuzamia kwenye imani chanya zinazohanikiza maendeleo.

Ni jukumu la 'scholars' wa dini na scholars wa sayansi ya ustawi wa jamii kuwakwamua Wazanzibari hapa walipokwama.
 
Sometimes tusiwe tuanjiuliza na hali ipo wazi tuu, kuna MTU kacoment why shule za kikristo zinafaurisha, ebu nenda katika izo shule ukajionee elimu inavotiliwa mkazo then wakati huo huo nenda Muslim seminary ukaone kinachotiliwa mkazo ni mafunzo ya dini au ya elimu then uje useme unategemea shule zipi zitafaurisha zaid, ingawa zipi shule za kiristo ambazo nazo wanakazia zaid mafunzo ya kidin ambapo matokeo take mfano wake ni iyo shule ya kisabto ya arusha ilyo top ten za mwisho. Point ni kwamba usitegemee kupanda majani ukavuna mahind, kama unawafundisha watoto dini mtiani ukaja wakatolewa elimu dunia unategema watafaulu?
 
Iyo shule ya wasabato arusha nasikia jamaa hata majani ya chai hawatumii wala soda,wapo busy na dini sana! Wanatakiwa wabalance kati ya mafundisho ya dini na elimu za humu dunia pia.Likewise shule za unguja la sivyo wasubirie jecha afute matokeo
 
Wanafunzi wako vizuri ila SMZ iangalie jinsi ya kuboresha maslahi ya walimu Zenji au ikiwezekana Wizara ya elimu iwe ya muungano, wafanyakazi wa SMZ wanalipwa mishajara midogo mno ukilinganisha na wale walio katika taasisi za Muungano
 
Iyo shule ya wasabato arusha nasikia jamaa hata majani ya chai hawatumii wala soda,wapo busy na dini sana! Wanatakiwa wabalance kati ya mafundisho ya dini na elimu za humu dunia pia.Likewise shule za unguja la sivyo wasubirie jecha afute matokeo
Wanakunywa mtundula...
 
mkuu umenena
 
Mimi ni mwl wa chuo kikuu nchini zaidi ya miaka 20. Nimewafundisha wanafunzi kutoka zanzibar. Wengi ni dhaifu sana kwenye masomo. Usiombe upate mwanafunzi wa ku supervise dissertation, hapo ndipo utakapojua uzito wa kazi hiyo. Tuseme kweli wengi ni wadhaifu hata wale waliomaliza na GPA nzuri ktka degree ha kwanza.
 
Duuuh shida kweli kweli, kipi kifanyike ili hawa watu wanyanyuke kielimu
 
Kwanza umepotosha kutokana na kichwa cha habari hapo juu,then znz kuna div 1 na 2 nyingi tu tena za science,pia znz kuna shule znz zina matokeo mazuri mara 10 kuliko ya bara..fanya research kwanza ndio uandike sio unakurupuka tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…