Pasco kwa hiyo unataka kutuaminisha kuwa wa zanzibar wana onewa? Wanabaguliwa? Wana nyanyaswa?
Leo hii matokeo mabovu unayo yaona yametoka na serikali yako na ndiyo ya kubeba lawama!
Hivi kama wanafunzi wanao jiunga na form one wana pelekwa wakiwa na maksi chini ya mia(100) kati ya miambili hamsini na bado unategemea miujiza ya ufahulu?
Serikali yako haikutosheka ikaona ifute mtihani wa form two ambao ulikuwa kipimo kizuri cha wanafunzi, nia yao kupata sifa kisiasa kuwa wamefanikiwa kusomesha wanafunzi wengi na walio maliza kidato cha nne.
Serikali yako hikasahau kupeleka vitabu mashuleni, walimu wa kutosha hakuna, shule hazina maabara alaf unategemea miujiza ya kufaulu!
Serikali yako imekataa kusikiliza vilio vya walimu kuboresha mazingira ya kufundishia, walimu wamekuwa kama watumwa alaf unategemea wafundishe kwa moyo wakati wana njaa?
Kwa nini tumsingizie Ndalichako makosa ya serikali yako? Necta hawapati faida yeyote kumflisha mtu, watoto wamevuna walicho pandiwa na serikali yako!
Pasco haya ni matokeo ya elimu kuchanganywa na siasa sasa bomu limelipuka tuna msingizia Ndalichako na necta!
Ccm walikuwa wamejenga hizi shule za kata kutafuta umaarufu kisiasa wala si kuboresha elimu ndio maana walikuwa wana tafuta kila njia wanafunzi wamalize kidato channe bila kujali watamaliza vipi ndio maana walishusha marks za kujiunga kidato cha kwanza na kuondoa mtihani wa kidato cha pili, wameshituka wakati kumekucha na wamesha tengeza zero zaidi ya miambili elfu.
Pasco kufail kwa wanao au kutopata marks za kulizisha wala si sababu za kuonewa na necta, nani anajua walikuwa na hali gani kwenye chumba cha mtihani? Tuache visingizio kabisa!
Najua tume ya waziri mkuu inataka kuhalalisha kumuondoa ndalichako kwa makosa ya serikali maana hakuna jipya kwenye tume hiyo zaidi ya kutaka kuonesha umma kuwa wanafunzi wameonewa na necta wakati tunajua serikali ni chanzo na ni kawamba na mlugo ndio walitakiwa kuwajibika!
Serikali ya ccm imeshindwa kwenye mradi wao washule za kata sasa wanaona wamtafute mchawi na kutaka kuwadanganya wanchi kuwa watoto hawakupata zero kupiti hiyo tume ya"janjajanja".
Ni wazi sababu za kumfukuza ndalichako zinatafutwa ili kutimiza matakwa ya kina "
Pasco"