Uchaguzi 2020 Inawezekanaje miundo mbinu iliyojengwa na pesa za watanzania wote, ionekane kuwa imejengwa na CCM pekee?

Turufu kubwa inayotumiwa na wanaCCM, ili Rais Magufuli apewe tena miaka mingine 5 ya kutawala nchi hii, ni kuwa Rais huyo amejenga reli ya SGR, amejenga mafly overs, amejenga mabarabara ya lami, anajenga bwawa la umeme katika mto wa Rufiji

Nimekuwa nikijiuliza ni kwanini juhudi zinazofanywa na watanzania wote, bila kujali itikadi zetu za kisiasa, sifa zote achukue mtu mmoja, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, ambaye pia ndiye Rais wetu Magufuli?

Kwa kuwa siyo siri tena, kuwa turufu kubwa wanayotumia wanaccm kuelekea uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu, ni ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali inayoendelea nchini, utadhani kuwa pesa ya kugharimia miundo mbinu hiyo, anatoa toka mifukoni mwake, yeye Rais Magufuli!

Hata serikali ya makaburu wa Afrika Kusini, walijenga miundo mbinu ambayo ndiyo inayongoza kwa ubora wake humu barani Afrika. Hata hivyo wananchi wa nchi hiyo, waliamua kumchagua mzalendo mweusi, Shujaa Nelson Mandela kuwa Rais wao na kuwapiga chini makaburu weupe ambao ndiyo waliokuwa wakijidai kuwa miundo mbinu hiyo imejengwa na wao.

Vile vile inajulikana kuwa pesa yote ya walipa kodi wa nchi hii, ya wanaccm na wanaChadema, zinakusanywa kwa pamoja na kuwekwa kwenye Hazina ya Taifa na ndiyo hizo zinazojenga, hiyo miundo mbinu, ambayo wanaccm "wanajimwambafai" kuwa wamejenga wao!

Wakati tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu ni lazima watanzania tusikubali kulaghaiwa kwa hizo propaganda nyepesi kuwa eti miundo mbinu yote nchi hii imejengwa na wanaccm!

Hebu tusikilize sera za kila mgombea na wananchi tuchague kiongozi ambaye tunaamini ndiye atakayetuvusha kama Taifa, katika umoja wetu na kudumisha utulivu wa nchi hii.

Tusichague kiongozi ambaye tunamuona dhahiri kuwa analibomoa kwa kasi kubwa Taifa hili umoja wetu na kuleta chuki ndani ya jamii ya watanzania.

Mungu ibariki Tanzania.
Naona watu wanafunguka taratibu na wanaanza kuujua ukweli wa mambo kwamba propaganda za ccm zilikuwa zimetawala na ukweli ni kwamba hakuna jipya lililofanywa na ccm tangu 2015 ambalo hasingefanya rais mwingine yeyote kutoka vyama vya upinzani tena kwa ubora zaidi.
 
CCM mjifunze kujenga hoja na sio kufanya mambo kwa jazba kama mwenyekiti wenu.
Turufu kubwa inayotumiwa na wanaCCM, ili Rais Magufuli apewe tena miaka mingine 5 ya kutawala nchi hii, ni kuwa Rais huyo amejenga reli ya SGR, amejenga mafly overs, amejenga mabarabara ya lami, anajenga bwawa la umeme katika mto wa Rufiji

Nimekuwa nikijiuliza ni kwanini juhudi zinazofanywa na watanzania wote, bila kujali itikadi zetu za kisiasa, sifa zote achukue mtu mmoja, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, ambaye pia ndiye Rais wetu Magufuli?

Kwa kuwa siyo siri tena, kuwa turufu kubwa wanayotumia wanaccm kuelekea uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu, ni ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali inayoendelea nchini, utadhani kuwa pesa ya kugharimia miundo mbinu hiyo, anatoa toka mifukoni mwake, yeye Rais Magufuli!

Hata serikali ya makaburu wa Afrika Kusini, walijenga miundo mbinu ambayo ndiyo inayongoza kwa ubora wake humu barani Afrika. Hata hivyo wananchi wa nchi hiyo, waliamua kumchagua mzalendo mweusi, Shujaa Nelson Mandela kuwa Rais wao na kuwapiga chini makaburu weupe ambao ndiyo waliokuwa wakijidai kuwa miundo mbinu hiyo imejengwa na wao.

Vile vile inajulikana kuwa pesa yote ya walipa kodi wa nchi hii, ya wanaccm na wanaChadema, zinakusanywa kwa pamoja na kuwekwa kwenye Hazina ya Taifa na ndiyo hizo zinazojenga, hiyo miundo mbinu, ambayo wanaccm "wanajimwambafai" kuwa wamejenga wao!

Wakati tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu ni lazima watanzania tusikubali kulaghaiwa kwa hizo propaganda nyepesi kuwa eti miundo mbinu yote nchi hii imejengwa na wanaccm!

Hebu tusikilize sera za kila mgombea na wananchi tuchague kiongozi ambaye tunaamini ndiye atakayetuvusha kama Taifa, katika umoja wetu na kudumisha utulivu wa nchi hii.

Tusichague kiongozi ambaye tunamuona dhahiri kuwa analibomoa kwa kasi kubwa Taifa hili umoja wetu na kuleta chuki ndani ya jamii ya watanzania.

Mungu ibariki Tanzania.
Tatizo ni kukosa mme ndio maana unakuwa na hoja za kipuuzi. Ina maana hujui nini maana ya chama tawala?
 
Mleta mada jiulize kwanini unapata huduma mbovu hospitari unaenda kumlaumu raisi? Mtaani kwenu mvua zimeharibu miundombinu nawewe unaangalia huchukui hata mda kurekebisha.unaisubili serikali
 
Maana ya chama tawala si kuzungumzia yaliyopita kwani hayo ni madogo kuliko aliyoyafanya mkoloni. Mkoloni alipoingia alitukuta hatuna barabara, reli, ndege, hosipitali, shule na kadhalika. Tulimuondoa na hakupiga porojo ya alivyovijenga kwani alijua alijenga kwa kutumia raslimali za wananchi na yeye skiwa msimamizi tu, aliondoka bila kudai aongezewe miaka mingine.
 
Tumeikabidhi serikali pesa zetu izitumie kwenye matatizo yatakayotukabili.
 
Maana ya chama tawala si kuzungumzia yaliyopita kwani hayo ni madogo kuliko aliyoyafanya mkoloni. Mkoloni alipoingia alitukuta hatuna barabara, reli, ndege, hosipitali, shule na kadhalika. Tulimuondoa na hakupiga porojo ya alivyovijenga kwani alijua alijenga kwa kutumia raslimali za wananchi na yeye skiwa msimamizi tu, aliondoka bila kudai aongezewe miaka mingine.
Mtu mpumbavu hudhani upumbavu ni ushajaa. Mtu mwenye akili timamu huwezi kumsifia mkoloni kisa alijenga shule. Huna tofauti na binti anayepigwa mimba kisa ananunuliwa chips.
 
mbona hoja zako za matusi ndugu , mjibu mtu kwa hoja kama alivyokujibu , hakuna hasiyejua kutukana lakini kutukana inaonesha jinsi mtu alivyo katika upeo wake .
 
Upumbavu ni hali ya kutotumia common sense kug'amua kitu sahihi.
Mtu mwenye akili timamu huwezi kumsifia mkoloni aliyejenga reli ili ainyonye nchi yako.
 
sasa mjibu mwenzako kwa hoja hakuna sababu ya kumwita mtu mpumbavu au mjinga , hatuna sababu ya kutoa tafsiri ya neno mjinga au mpumbavu tubishane kwa mitazamo na si maneno yasiopendeza
 
Upumbavu ni tusi?
 
lebabu11
Tunachoona hakijakaa sawa, ni kwa huyu Rais tuliyenaye kujiona kuwa apewe sifa yeye pekee, kwa kutengeneza miundo mbinu hiyo, wakati ni kodi za wananchi wote, bila kujali itikadi zetu za kisiasa, ndiyo tuliotengeneza miundo mbinu hiyo

Kilichopo ni matokeo ya ujinga wa wananchi, siasa za ghiliba na udanganyifu wa wapambe.
Hata hivyo, inahitajika elimu na uelewa kwamba maendeleo yote katika nchi, hufanywa na wananchi wenyewe. Viongozi wamepewa dhamana tu ya kuonesha njia na wanaweza kuondolewa wakati wowote, na maendeleo yatakuwepo ila kwa kasi tofauti (kubwa zaidi au ndogo).
 
pong
Hoja nyingine aisee zinashangaza Sana. Unashangaa hilo eti Tanzania sifa anapewa rais mbona huko nchi nyingine husemi mana nchi zote duniani Marais wanao fanya vizuri ndio husifiwa kwa kuleta maendeleo Ila akisifiwa wa Tanzania tu inakuwa nongwa.
Eti ni katumia kodi za wananchi kwani katika hizo nchi nyingine huko hao Marais wanajenga kwa pesa zao mfukoni? Mbona awamu nyingine zilishindwa kujenga hiyo miundombinu au walikuwa hawakusanyi kodi?

Kwa mfano ikitokea Lissu kashinda uchaguzi na kuwa Rais kisha akanunu meli za masafa marefu Cargo na kuzidi kuimarisha bandari, akajenga SGR hadi Mpakani na Zambia, mahospital, mashule n.k je hapo tutamsifia nani kwa hiyo kazi?

Mtu kapewa dhamana ya kuongoza taifa kakaa ofisini kwa miaka mitano akijenga nchi kwa mipango yake pamoja na Ilani ya chama chake sasa eti leo hutaki asifiwe yeye Kama sio Chuki binafsi kumbe ni nini sasa?

Halafu ccm ndio chama kilicho madarakani kwasasa hivyo Ilani inayo tumika kujenga nchi ni ya ccm sasa ni ajabu kushangaa kwanini ccm isifiwe au kuwa na nguvu.

Mbona ikifanya madudu huwa tunaisema ni serikali ya ccm ndio imeharibu Ila ikifanya mazuri hutaki tuseme ni serikali ya ccm.

Mana chama chochote kitakacho ingia madarakani kitakuwa hivo hivo, hoja Kama hizi mkienda nazo kwenye uchaguzi alafu mkawaambie wananchi wa Kigoma walio jengewa barabara nzuri kabisa ya lami Kigoma- Nyakanazi mjue kabisa mnakwenda kushindwa vibaya Sana.
pongezi zinakwenda kwa serikali na sio kwa mtu binafsi. mara nyingi tumemsikia akijidai kuwa ametoa hela kujenga mabarabara, ndege nk. hizi kauli zake sio kabisa
 
Turufu kubwa inayotumiwa na wanaCCM, ili Rais Magufuli apewe tena miaka mingine 5 ya kutawala nchi hii, ni kuwa Rais huyo amejenga reli ya SGR, amejenga mafly overs, amejenga mabarabara ya lami, anajenga bwawa la umeme katika mto wa Rufiji

Nimekuwa nikijiuliza ni kwanini juhudi zinazofanywa na watanzania wote, bila kujali itikadi zetu za kisiasa, sifa zote achukue mtu mmoja, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, ambaye pia ndiye Rais wetu Magufuli?

Kwa kuwa siyo siri tena, kuwa turufu kubwa wanayotumia wanaccm kuelekea uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu, ni ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali inayoendelea nchini, utadhani kuwa pesa ya kugharimia miundo mbinu hiyo, anatoa toka mifukoni mwake, yeye Rais Magufuli!

Hata serikali ya makaburu wa Afrika Kusini, walijenga miundo mbinu ambayo ndiyo inayongoza kwa ubora wake humu barani Afrika. Hata hivyo wananchi wa nchi hiyo, waliamua kumchagua mzalendo mweusi, Shujaa Nelson Mandela kuwa Rais wao na kuwapiga chini makaburu weupe ambao ndiyo waliokuwa wakijidai kuwa miundo mbinu hiyo imejengwa na wao.

Vile vile inajulikana kuwa pesa yote ya walipa kodi wa nchi hii, ya wanaccm na wanaChadema, zinakusanywa kwa pamoja na kuwekwa kwenye Hazina ya Taifa na ndiyo hizo zinazojenga, hiyo miundo mbinu, ambayo wanaccm "wanajimwambafai" kuwa wamejenga wao!

Wakati tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu ni lazima watanzania tusikubali kulaghaiwa kwa hizo propaganda nyepesi kuwa eti miundo mbinu yote nchi hii imejengwa na wanaccm!

Hebu tusikilize sera za kila mgombea na wananchi tuchague kiongozi ambaye tunaamini ndiye atakayetuvusha kama Taifa, katika umoja wetu na kudumisha utulivu wa nchi hii.

Tusichague kiongozi ambaye tunamuona dhahiri kuwa analibomoa kwa kasi kubwa Taifa hili umoja wetu na kuleta chuki ndani ya jamii ya watanzania.

Mungu ibariki Tanzania.
Magufuli anapenda sifa mno ambazo hata hastahili
 
TUKIACHA USHABIKI WA KISIASA
Kiongozi wa juu wa Chama aliyeko madarakani kipindi flani, NDIYE anaweza kusukuma mambo yatendeke na kwa kiasi gani
Mf: China miaka yoote iliongozwa na maraisi wazuri tu ILA alipo ingia Mao Tse Tung (mwaka 1945) ndiye aliyeleta mabadiliko makubwa ya Uchumi yanayoifanya china itishie Dunia Nzima
Tanzania kwa mfano imewaliwa na Maraisi wengi; ila Alipo ingia huyu amesukuma maendeleo kwa kiasi kikubwa naweza kusema zaidi ya mara mbili ya walio pita.
Sisemi kuwa waliopita hawajafanya kitu: Iko hivi, Raisi mmoja anaweza kujenga shule 35, mwingine ajenge 200. au mwingine anaweza kujenga Hospitali (vituo vya afya 50: Mwingine ajengine aingie ajenge 250; na miundo mbinu nk
Hivyo yule aliyeweza kusimamia na kupunguza ubadhirifu hivyo kutekeleza miradi mingi kwa kipindi chake; ndio hujivunia chama chake na sio hapa TZ ni utaratibu wa DUNIA NZIMA

Kasome vizuri historia ya China. Mao ndiye aliyeirudisha nyuma kwa kung’ang’ania itikadi ya kikomunisti ya dola kumiliki nguzo kuu za uchumi na yeye kutukuzwa kwa kila jambo. Yeye ndiye anajenga barabara, reli, madaraja. Operesheni kubwa kama za moyo, ubongo zinafanyika kwa maelekezo yake! Na ujinga mwingi wa aina hiyo.

Mkombozi mkuu aliyeharakisha maendeleo ya kisasa China ni Deng Xiaoping. Huyu ndiye aliyeleta mageuzi makuu ya kiuchumi na kuondoa ukiritimba wa dola na watawala. Bila huyo usingesikia huawei, techno, xiaomi, alibaba, ccecc, nk. Ingekuwa kama North Korea ambako kutwa kucha TV inaimba sifa za kiongozi mpendwa! China walishatoka huko. Sasa wanaendesha udikteta wenye akili zaidi.
 
Kawaida yao hio hata viwanja vya mipira nchini vilijengwa na wananchi wote lkn vikabinafsishwa kwa CCM,utasikia tu Ccm kirumba.
 
Hamueleweki nyie juzi hapa mmeanzisha nyuzi lukuki mkimsifia JK na mkapa kwa maendeleo waliyoyafanya hamkukumbuka ni kodi zenu?
Hao madamis ata usihangaike nao wako na hasara kubwa na wanatia hasara nyingi kwenye taifa hili la JMT.
Magufuli na CCM yake ndio wamepewa ridhaa ya kukusanya kodi na kusimamia rasili mali zetu nyie makapuku kauzeni chai na mkileta ubishi tunawatundu lissu.
 
Back
Top Bottom