Inawezekanaje nchi ndogo ya Denmark kuipa misaada nchi kuubwa Tanzania?

Mkuu nikuulize, kukaa kwao kikabila kumewasaidiaje na kukaa kwetu pamoja makabila mseto kumetukwamishaje? Chukulia baadhi ya makabila yanayokaa pamoja mpaka sasa kama Wamasai, Wasandawe, Wabarbaig n.k., kumekuwa na msaada wowote kwao tofauti na makabila mengine?
 
Nini? Soko la Kariakoo lilijengwa na Mjerumani? Ni kweli mkuu?

Sikuwa nafahamu hilo. Kama ndivyo, Mjerumani alikuwa ni mkoloni mzuri japo inasemekana alikuwa mkali sana na mbabe mno.
Someni historia zipo wandugu.

Wakati wa utawala wa wajerumani walijenga hilo jengo na likawa ni ofisi zao, walitaka wawe watumia kwa shughuli kama ghafla na sherehe.

Baadae walipokuja waingereza wakapageuza kuwa ni soko kwa wakazi wa Dar-es-Salaam.
 
Bora umezitaja hizo nchi tatu, maana ni mataifa ambayo idadi ya raia ni chache sana ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika, lakini pia hizo nchi zina makabila machache. hapo ndiyo utaona sababu mambo yao yanaenda vizuri relatively speaking.
 
🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏
Ingelikuwa ni maamuzi yangu, hayo mawazo yangeingia kwenye utekelezaji haraka sana.
Suala na kodi na maendeleo huwa haya mijadala hata kama huna fedha za kulipa kodi itatafutwa namna ulipe.

Ndo maana kwa wenzetu kila mtoto anezaliwa tayari data huingizwa kwenye mfumo. Akifika miaka 16 waanze kumwambia awez akupiga kura na akifika 18 huambiwa ajiandae kulipa kodi maana tayari anakuwa amepewa ile namba ya bima.
 
Kitaifa mshikamano unakuwa siyo harmonious sababu tofauti zinakuwa kubwa zaidi ya umoja kwa huu utaifa feki wa kubuni wa Utanzania ukilinganisha na nchi za Ulaya ambapo utaifa unaendana na ukabila.
 
Someni historia zipo wandugu.

Wakati wa utawala wa wajerumani walijenga hilo jengo na likawa ni ofisi zao, walitaka wawe watumia kwa shughuli kama ghafla na sherehe.

Baadae walipokuja waingereza wakapageuza kuwa ni soko kwa wakazi wa Dar-es-Salaam.
🙏🙏🙏
 
Bora umezitaja hizo nchi tatu, maana ni mataifa ambayo idadi ya raia ni chache sana ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika, lakini pia hizo nchi zina makabila machache. hapo ndiyo utaona sababu mambo yao yanaenda vizuri relatively speaking.
Ni kweli, lakini kama nilivyosema hapo juu ukiamua kwamba mikoa ijitegemee kama "pilot project" na uangalie "progress" utaona kwamba waweza kufanikiwa.

Tunaweza sema Mtwara iimarishwe ili isaidie Lindi, au Mbeya, Rukwa, Ruvuma na Katavi isaidie mikoa yote ya kusini kimandeleo.

Ukiangalia nchi yetu mikoa mingi ina fursa kubwa ya kiuchumi ila tatizo lipo kwenye usimamizi wa uchumi na vyanzo vya mapato.
 
Kwa hilo, nakubaliana nawe mkuu.
 
Nakubaliana na wewe. Mikoa ya Tanzania kwa kiasi kikubwa ndiyo kigezo kikubwa cha kutofautisha mipaka ya makabila nchini. Mikoa ingepewa hadhi ya majimbo yajitawale kiuchumi na kisiasa kama ilivyo Nigeria na USA. Hizi ni nchi mbili zenye very diverse population kama Tanzania.
 
Usije ujatamka hayo mbele ya Trump. Alishawahi kutoa kejeli mbaya sana ya kibaguzi dhidi ya Bara la Afrika.

1. Aliziita nchi za Kiafrika "Shithole countries"

2. Alizitukana nchi za Kiafrika kwa kusema "Afrika inatakiwa itawaliwe tena"
Olay, we unaonaje kwa upande, alikuwa right or wrong
 
Naked truth
Yaani itokee tuhamishwe waafrika tupelekwe ulaya na marekani halafu wazungu wake Africa, wakati wa kuhama hamna unachochukua zaidi ya nguo ulizovaa
Baada ya miaka mitano,ni sisi ambalo tutaomba viza na kulia ubarozini ili tukubaliwe kuingia tena Afrika
 
Shida ni kwamba walio kwenye nafasi za maamuzi asilimia 98 wapo kwa ajili ya matumbo yao, na baada ya wao kutoka wana tengeneza watu watakao kuja kuendelea kulinda maslahi yao, ndio mfumo walio uweka, ukija ukataka kuwapinga na kufuata haki na kua muadilifu na muwajibikaji utaondoka bila kupenda
 
Denmark ni nchi kubwa na kongwe kuliko Tanzania- cheki history na facts.

Leo ki eneo Tanzania ni kubwa kuliko, Uingereza lakini miaka 70 iliyopita, Uingereza ilikuwa I atawalaye 25% ya nchi za uliwengu.

Hivyo Ukubwa na ukuu wa nchi hauko katika eneo/ardhi.
 
Baadhi ya Viongozi wa Bara la Afrika ni mafisadi wala rushwa wezi Majambazi na wezi Unafikiri kweli tutaendelea kichumi?
 
kupora mali za watu nakuua hakuwezi kuleta maendeleo
 
Mkiacha wizi, kudai Rushwa kama za mama zao, kuwa na moyo wa kujituma na kufanya kazi bila kusubiri hongo ama kweli mtawapita hao mnaowaita kanchi

Siku hela zote zitatumika zote kwenye sehemu zilikoelekezwa bila kuiba basi mjue mmekaribia pepo

Majizi lini yakafika mbali?
 
Sifa ulizonimwagia ni mtego mkuu🤣.
Anyways nina akili za kutosha kuvukia barabara ila hazifikii za wazungu🤣.
Ningekua nina akili kama.za wazungu ningefanya jambo nchi yangu iwe kama Denmark.
Asante kwa pongezi lakini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…