kibobori mahoro
JF-Expert Member
- Dec 12, 2022
- 7,452
- 10,785
Professor Lumumba of Kenya gave the answer "Africa tends to elect foools to the office ". Akili kubwa kuongozwa na akili ndogo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ukisikia kubwa jinga ndo haya sasaDenmark inatarajia kuufunga ubalozi wake nchini Tanzania ifikapo 2024. Ni kati ya nchi ambazo zimekuwa zikiipa Tanzania misaada, tokea ikiitwa Tanganyika hadi sasa ikiwa inajulikana kwa jina adhimu, Tanzania.
Lakini Denmark ni nchi ya namna gani?
Ukifanya ulinganisho, Tanzania imeizidi kwa mambo mengi isipokuwa ujinga na umaskini. Ina rasilimali nyingi sana kuizidi, na hata idadi ya watu tumeipita mbali sana.
Denmark, ni kanchi kadoogo, kenye ukubwa wa kilomita za mraba 42,920 lakini inaizidi kiuchumi Tanzania, nchi Kuubwa kieneo, yenye kilomita za mraba 945,087.
Denmark, ni kanchi kadoogo kenye watu milioni tano lakini inaipa misaada nchi kuubwa, Tanzania, yenye watu milioni sitini na moja.
Ni nini siri ya kanchi kadogo kuizidi nchi kubwa kama Tanzania? Imekuwa ikiisadia Tanzania tokea 1963, enzi hizo ikiitwa Tanganyika, lakini hakuna taarifa ya Tanzania ambayo ni nchi kubwa kuisaidia Denmark kanchi kadogo.
Imewezekanaje kwao lakini kwetu ikashindikana?
Mwingine anaweza kusema ni kwa sababu ya ukoloni, lakini hilo halina mashiko. Hata Korea Kusini ilishawahi kuwa koloni la Japan, lakini kwa sasa wanatukimbiza kiuchumi.
Ni nini walichogundua hao watu weupe ambao weusi wa Tanganyika na Zanzibar hawajagundua?
Angalia, hata eneo la Korea Kusini ni dogo sana ukililinganisha na ukubwa wa Tanzania. Ina kilomita za mraba 100,210 na watu milioni hamsini na moja.
Inawezekanaje kanchi kadoogo, Denmark, kuipa misaada nchi kuubwa, Tanzania?
Korea Kusini ina miaka mingapi?Nchi Ina miaka 60 ila mnataka maajabu ya kiuchumi?