India: Wananchi waendelea kuandamana wakitaka Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ajiuzulu

India: Wananchi waendelea kuandamana wakitaka Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ajiuzulu

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Vyama vya upinzani nchini India vimeendelea kutoa wito wa kutaka Mkuu wa Tume ya Uchaguzi wa nchi hiyo ajiuzulu, baada ya kuandaa maandamano mapya siku ya Jumapili Novemba 1, 2026. Maandamano hayo ni sehemu ya kuonyesha kutoridhishwa na serikali ya Waziri Mkuu Narendra Modi.

Maandamano hayo yaliyoitishwa na muungano wa vyama vya upinzani unaojulikana kama INDIA, yalivutia makumi ya maelfu ya waandamanaji. Baadhi yao walikuwa na vyombo vya muziki na bendera mbalimbali huku wakiimba nyimbo na kupiga kelele za kupinga sera za serikali kuu. Vyama kadhaa vya muungano huo, ulioanzishwa mwaka 2023 kwa lengo la kumng'oa Modi madarakani, vilihamasisha wafuasi wao kutoka majimbo mbalimbali kushiriki maandamano hayo.

Maandamano hayo yaliongozwa na Rahul Gandhi, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Congress, akiungwa mkono na vuguvugu la vijana linaloitwa “Cockroach”. Yalifanyika katika uwanja wa Ramlila Maidan, eneo kubwa la wazi lililopo New Delhi, wiki chache baada ya polisi kutumia nguvu kuwatawanya waandamanaji.

Waandamanaji walitoa wito wa kulinda demokrasia ya India, huku wakitaka Mkuu wa Tume ya Uchaguzi, Gyanesh Kumar, ajiuzulu kutokana na mzozo unaohusu zoezi la kupitia upya daftari la wapiga kura.

Hata hivyo, Tume ya Uchaguzi pamoja na serikali ya Modi wamekanusha tuhuma hizo, wakieleza kuwa zoezi hilo linalenga kuondoa majina yaliyojirudia na ya watu wasiostahili kuwa kwenye daftari la wapiga
kura.

1793628247359.png
 
CCM ni shida Dunia nzima.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom