GE2025 INEC tutamtangaza mshindi wa kiti cha Urais ndani saa 72

GE2025 INEC tutamtangaza mshindi wa kiti cha Urais ndani saa 72

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Uchaguzi Jumatano 29 October
Matokeo ya Udiwani Jumatano hiyo hiyo
Matokeo ya Ubunge, Alhamisi 30 October
Matokeo ya urais Ijumaa November most
Jumapili November 3 Kuapishwa kwa Rais
Jumanne November 5 Wabunge Dodoma kumchagua Spika, na Naibu Spika, na kuapishwa mpaka Ijumaa
Ijumaa November 8 jina la Waziri Mkuu linatangazwa
Jumamosi November 9 Waziri Mkuu ataapishwa Dodoma

Wiki inayofuata, ni Rais Samia anateua wabunge wa kumsaidia ikiwemo yule mwanae wa Kigoma, kisha anatangaza baraza la mawaziri, Konda Boy mambo ya ndani!.

Maisha Yanaendelea ...

P
"Ubagazaji unaendelea"
 
Ni kigezo gani kinachotumika kufanya hiyo tallying ya Uraisi tofauti na Tallying ya udiwani ? Hapo ndipo kwenye kupindua meza. Ingefaa mambo yote yafanyike hapo hapo kwenye kata na nyie waandishi mujiganawe katika kata zote nchini na mulete matokeo yote, mutupe mahesabu, hizi habari za kwenda Dodoma kwa sasa zimechuja
Vituoni ni kuhesabu tuu kura na kubandika matokeo yote ubaoni, tallying huwezi kufanyia kituoni, hufanyikia kwenye tallying centers baada ya kupokea matokeo ya vituo vyote vya udiwani mshindi anatangazwa siku hiyo hiyo ya uchaguzi, Ubunge ni baada ya kupokea matokeo yote ya jimbo zima na kwa Rais ni baada ya kupokea matokeo yote nchi nzima.
Huwezi kufanyia tallying kituoni!
P
 
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imesema itamtangaza mshindi wa kiti cha Urais ndani ya muda usiozidi saa 72, baada ya zoezi la upigaji wa kura kumalizika Oktoba 29 mwaka huu, na washindi wa nafasi ya Ubunge na Udiwani, wakitarajiwa kutangazwa wakati wowote baada ya kujumlisha idadi ya kura katika maeneo husika.



HIYO SI TUME HURU YA UCHAGUZI ; NI TUME HURU YA UCHAFUZI

Tanganyika na Zanzibar hakujafanyikapo uchaguzi huru tokea kupatikana kwa uhuru
 
Vituoni ni kuhesabu tuu kura na kubandika matokeo yote ubaoni, tallying huwezi kufanyia kituoni, hufanyikia kwenye tallying centers baada ya kupokea matokeo ya vituo vyote vya udiwani mshindi anatangazwa siku hiyo hiyo ya uchaguzi, Ubunge ni baada ya kupokea matokeo yote ya jimbo zima na kwa Rais ni baada ya kupokea matokeo yote nchi nzima.
Huwezi kufanyia tallying kituoni!
P
Poti, hebu ngoja nitofautisne na wewe kwa mara ya kwanza leo. Nafikiri jibu lako ni la kiupotoshaji wa makusudi unaolenga kuficha mianya ya wizi wa kura!

“kuhesabu kura” na “kutally” ni mambo mawili yanayohusiana moja kwa moja. Tallying ni kujumlisha kura zote kutoka vituo vya kupigia kura, na kama hatua hiyo haitanguliwi na uwazi katika kila kituo, ndipo wizi wa kura unaanza! Nafikiri mpako hapo tuko Pamoja.

Pili, kama matokeo yanabandikwa tu ubaoni bila uthibitisho wa pamoja na nakala kusainiwa na mawakala wote wa vyama, kisha matokeo hayo yanapelekwa “tallying center” bila ulinzi wa kweli (kumbuka maneno ya yule mkuu wa wilaya aliyesema mambo yanayofanyika mapolini, kumbuka vibegi vya polisi vinavyolalamikiwa) au uwazi wa kidijitali, ni rahisi sana kubadilishwa njiani. Hapo ndipo wizi wa kura unafanyika.

Kwa hiyo, ili tuondokane na wizi wa kura, inafaa na inatakiwa iwe kwamba, tallying lazima ianze kituoni, kwa maana ya kwamba kila kituo kinapaswa kuwa na fomu rasmi (mfano: fomu ya matokeo ya kituo – Form 16A kama ilivyo kule kwa majirani Kenya) ambayo inasainiwa na mawakala wote, nakala yake inatolewa kwa kila chama, na matokeo hayo yanachapishwa hadharani na kupakiwa kwenye mfumo wa kitaifa wa kidijitali papo hapo. Hapo ndipo uwazi unapoanza.

Sasa tufanyeje, labda tutumie jjia mbadala za kuzuia wizi wa kura mfano hapa chini:
  1. Tutumie mfumo wa kidijitali wa kutuma matokeo moja kwa moja kutoka kituoni hadi kituo cha taifa (iNEC central server) bila kupitia mikono ya watu katikati.
  2. Tuweke matokeo ya kila kituo mtandaoni kwa wakati halisi (real-time), wananchi waweze kuona fomu na kura halisi.
  3. Mawakala wa vyama na waangalizi wa ndani na nje wawepo wakati wote wa kuhesabu na kusaini matokeo.
  4. Long term, sheria zibadilishwe ili matokeo ya kila kituo (polling station) yawe ndiyo ya mwisho na ya lazima, yaani hakuna mtu au chombo chochote kinachoweza kuyabadilisha baadaye.
Kwa hiyo, mtu yeyote ukiwemo wewe poti wangu, akija hapa akasema kwamba “huwezi kufanya tallying kituoni” anamaanisha hawataki uwazi, kwa sababu tallying inaanza pale kura zinapohesabiwa kituoni na matokeo yakisainiwa na kuthibitishwa.
Kituo ndicho msingi wa matokeo halali, si “tallying center” ambayo mara nyingi hutumika kuhalalisha matokeo yaliyochezewa.

Kama hii haitafanyika, uchaguzi utakuwa ni kiini macho na hauna maana tena, wapiga kura tunachezewa chezewa tuna na kodi zetu zinaharibiwa bila sababu ya msingi na ndio maana wale jamaa wanasema bila mageuzi ni kama uchaguzi haupo, yaani kwa maneno mengine, uchaguzi ni mazingaombwe tu, michezo ya udanganyifu na kiini macho. Nani anataka hayo mambo ya karata tatu, tatu mzuka? Ni wanufaika pekee tu wanayataka. Period.
 
Uchaguzi Jumatano 29 October
Matokeo ya Udiwani Jumatano hiyo hiyo
Matokeo ya Ubunge, Alhamisi 30 October
Matokeo ya urais Ijumaa November most
Jumapili November 3 Kuapishwa kwa Rais
Jumanne November 5 Wabunge Dodoma kumchagua Spika, na Naibu Spika, na kuapishwa mpaka Ijumaa
Ijumaa November 8 jina la Waziri Mkuu linatangazwa
Jumamosi November 9 Waziri Mkuu ataapishwa Dodoma

Wiki inayofuata, ni Rais Samia anateua wabunge wa kumsaidia ikiwemo yule mwanae wa Kigoma, kisha anatangaza baraza la mawaziri, Konda Boy mambo ya ndani!.

Maisha Yanaendelea ...

P
Mkuu ina maana mwanae hawezi kutoboa kule mpaka asubiri nafasi za uteuzi? Vip Mwamba kwenye hizo 10 na yeye ataachwa kweli?
 
TOKA MAKTABA :

Hivi ndivyo itakuwa mahojiano na vyombo vya kimataifa na rais mtarajiwa Samia Hassan baada ya kushinda uchaguzi



View: https://m.youtube.com/watch?v=5Br3QYqvRFo
Mwanasiasa mkongwe na waziri wa zamani wa maswala ya kigeni Netumbo Nandi-Ndaitwah alikuwa naibu wa rais, na sasa ameshinda uchaguzi uliokuwa huru wa nchini Namibia
 
Mtanzania ambaye mpaka sasa bado hajui nani atatangazwa kuwa mshindi wa Urais, mshindi wa ubunge kwenye jimbo lake na mshindi wa udiwani kwenye kata yake, akatafute msaada wa kitabibu Mirembe Hospital. I can wager any sum of money on the outcome, knowing I won’t lose a penny!
Kama yupo namimi nitatoa gharama zoote za matibabu!
 
Uchaguzi Jumatano 29 October
Matokeo ya Udiwani Jumatano hiyo hiyo
Matokeo ya Ubunge, Alhamisi 30 October
Matokeo ya urais Ijumaa November most
Jumapili November 3 Kuapishwa kwa Rais
Jumanne November 5 Wabunge Dodoma kumchagua Spika, na Naibu Spika, na kuapishwa mpaka Ijumaa
Ijumaa November 8 jina la Waziri Mkuu linatangazwa
Jumamosi November 9 Waziri Mkuu ataapishwa Dodoma

Wiki inayofuata, ni Rais Samia anateua wabunge wa kumsaidia ikiwemo yule mwanae wa Kigoma, kisha anatangaza baraza la mawaziri, Konda Boy mambo ya ndani!.

Maisha Yanaendelea ...

P
HATOGOMBEA 2V3
 
Back
Top Bottom