INEC yamjibu Polepole, yasisitiza uhuru wa mifumo yake ya uchaguzi

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
838
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (INEC) imekanusha vikali madai yaliyotolewa naaliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, ambaye pia ni kada Chama Cha Mapinduzi (CCM), aliyejitokeza hivi karibuni kukosoa mamlaka.

Polepole, katika mazungumzo yake yaliyofanyika usiku wa kuamkia jana, alidai kuwa mifumo ya CCM, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Tume ya Uchaguzi imeunganishwa, kauli ambayo alidai inakiwezesha chama chake kupata ushindi hata kabla ya siku ya uchaguzi.

Madai haya yalizua gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii na kulazimisha INEC kutoa taarifa rasmi kupitia kurasa zake.

Katika taarifa hiyo, Tume imekanusha madai hayo, ikiyataja kuwa ni ya upotoshaji na kutokana na ukosefu wa uelewa. Taarifa hiyo, iliyotiwa saini na Mkurugenzi wa Uchaguzi, imefafanua kuwa daftari la kudumu la wapiga kura halijaunganishwa na mfumo wowote wa serikali au wa kisiasa.
Mfumo wa upigaji kura, kuhesabu, na kutangaza matokeo hautumii mfumo wa aina yoyote ya kielektroniki," ilisema taarifa hiyo. "Badala yake, mfumo unatumia taratibu za kawaida (manual) kama ilivyozoeleka."
INEC pia imefafanua kuwa kitambulisho cha taifa hakitumiki kupigia kura, badala yake kinachotumika ni kadi ya mpiga kura inayotolewa na Tume yenyewe. Aidha, imebainisha kuwa vyama vya siasa hupewa nakala ya daftari inayoonesha idadi ya walioandikishwa katika vituo husika baada ya uboreshaji kukamilika.

Tume imetoa wito kwa wananchi kupuuza taarifa za upotoshaji zenye lengo la kuzua taharuki na kuharibu sifa ya mfumo wa uchaguzi. Kulingana na INEC, kauli za aina hiyo zinatolewa na watu wasio na uelewa wa kutosha.
 
Watanzania sio wajinga tena.

Wanawaona mnavyotembea uchi ila wanavunga kama hawaoni tupu zenu.
 
Screenshot_20250824-113512~2.png
 
Mtuhumiwa anapinga tuhuma dhidi yake, halafu anataka tumwamini...

After all, Mtenda kitendo mwenyewe Humphrey Polepole na wenzake walioshiriki kuunganisha mifumo hii ndiye anayesema na kukiri waziwazi. Na tunajua kuwa huyu Polepole alikuwa ni mmoja wa viongozi wenye nyadhifa za juu kabisa za utendaji ndani ya CCM...

Nyie watuhumiwa NEC (Ramadhani Kailima na mwenyekiti wako Jaji Mwambegele) mnaweza vipi kuushawishi umma usimwamini mtenda kitendo Humphrey Polepole wakati huo akiwa katibu wa itikadi, sera na uenezi wa CCM na msaidizi wa karibu wa Rais Magufuli..??

Nyie wakati huo (Kailima na Jaji Mwambegele) hamkuwepo. Nani mwenye akili timamu anaweza kuuamini utetezi wenu butu huo?

Before, kulikuwa na shahidi za kimazingira tu. Mfano uropkaji wa Nape Nauye, Anna Makinda na wana CCM wengine akiwemo Samia mwenyewe. Lakini sasa uropokaji wao umethibitishwa na Polepole mshiriki wa moja kwa moja wa hujuma hizo...!!

Need we say more..??
 
Back
Top Bottom