Wakuu habari,
Tume huru ya uchaguzi Tanzania (INEC) imewakabidhi wagombea urais uchaguzi mkuu 2025 magari mapya aina ya LandCruise GX VXR Mpya ya 2025 zero kilometer.
Haitakua busara Mgombea wa CCM kupewa gari maana wanajitosheleza wale, kwanza msafara wa kuchukua tu fomu ilidhihirisha tayari wana magari ya kutosha na harambee walipata mabilioni inawatosha itakua uharibifu wa rasilimali za umma
----------------------------
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) itamkabidhi kila mgombea atakaetimiza vigezo na kutangazwa kuwa mgombea Urais wa chama cha siasa kitakacho shiriki Uchaguzi Mkuu 2025, gari hili aina ya LandCruise GX VXR Mpya ya 2025 zero kilometer
Magari haya yanatolewa kwa wagombea Urais pekee, pamoja na Dereva kwa ajili ya kumuwezesha Mgombea Urais kusafiri na kufika popote pale atakapohitaji kufika kwa ajili ya kurahisisha shuguli zake za kufanya Kampeni na kuomba kura kwa wananchi
----------------
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) leo Jumatano Agosti 27, 2025, imewateua rasmi wagombea wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.
Katika hafla iliyofanyika katika ofisi za INEC jijini Dodoma, wagombea wote wa urais waliotimiza masharti ya kikatiba na kisheria wamethibitishwa rasmi kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya juu zaidi ya uongozi nchini
Hata hivyo, upekee wa mwaka huu ni hatua ya INEC ya kuwapatia wagombea magari mapya sambamba na dereva na mlinzi, baada ya kuteuliwa
Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhan Kailima amewakabidhi wagombea magari aina ya Land Cruiser GXR mapya, akibainisha kuwa utaratibu huo umewekwa kisheria ili kuhakikisha wagombea wanaendesha kampeni zao katika mazingira salama na yenye usawa.
“Utaratibu huu ni wa kisheria. Mgombea akitimiza vigezo, INEC inamkabidhi gari jipya, dereva na mlinzi kwa ajili ya shughuli za kampeni,” amesema Kailima
Chanzo: Mwananchi_official