ministrant
JF-Expert Member
- Jan 17, 2014
- 1,400
- 2,623
Sasa Mkuu si ndiyo maana yametolewa magari yenye uwezo hata wa kupita kwenye hizo njia mbovu bila kumwacha mgombea akiwa anaumwa mgongo ili aje kuwaahidi kuwa mkimpatia ridhaa atazitengeneza na kuwajengea vituo vya afya vya kutosha na kuwawezesha wananchi kiuchumi na nyie mmiliki 'Mavieite' yenu mpunguze wivuKuna mambo yanaumiza sana akili. Wakati wanachezea pesa za walipa kodi, kuna barabara kibao tu nchini ni za vumbi huku zikiwa hazipitiki wakati wa masika! Ukienda kwenye shule za serikali za msingi na sekondari; kuna upungufu mkubwa wa miundombinu! Ukija kwenye huduma za afya, hali bado hairidhishi! Vipato vya wananchi walio wengi vipo kwenye hali duni!
Halafu wananunua magari ya kifahari kwa ajili ya wanasiasa kupigia misele!! Aisee kuzaliwa Afrika ni laana tosha.
