Influencer na rafiki wa Davido afariki wakati akifanyiwa upasuaji wa kuongeza ukubwa wa uume

TheCrocodile

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2021
Posts
1,864
Reaction score
5,254
Mfanyabiashara raia wa Uingereza na Nigeria, pamoja na influencer wa mitandao ya kijamii ambaye pia ni rafiki wa Davido, Igho Tiny Ubiribo, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 43 baada ya kufanyiwa utaratibu wa kuongeza ukubwa wa uume akiwa nchini Thailand.

Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na TMZ, Ubiribo, ambaye pia alikuwa akifahamika kwa majina ya Denisi au Ego, alifanyiwa utaratibu huo katika kliniki moja jijini Bangkok, ambapo madaktari walitumia mililita 40 za mchanganyiko wa hyaluronic acid na lidocaine.
Baada ya kufanyiwa utaratibu huo, Ubiribo alikwenda kupata massage akiwa pamoja na mke wake, Danielle Simba Allen. Hata hivyo, akiwa katika shughuli hiyo alianza kupata maumivu makali ya kifua na baadaye alizimia mara mbili.

Alikimbizwa katika Hospitali ya Sukhumvit, ambako madaktari walifanya zoezi la kumrejesha katika hali ya kawaida (CPR) kwa zaidi ya dakika 100. Pamoja na juhudi hizo, Ubiribo alitangazwa kuwa amefariki dunia.
Taarifa za kitabibu zinaeleza kuwa chanzo cha kifo chake kilikuwa pulmonary embolism, hali inayotokea pale ambapo donge la damu linapoziba mshipa wa damu unaoelekea kwenye mapafu.

Uchunguzi wa mwili wake baada ya kifo ulibaini kuwa kemikali ya Hyaluronic acid iliyotumika kwenye sindano hizo iliingia kwenye mishipa ya damu na kufika kwenye mapafu. Hali hiyo ilisababisha kuziba kwa mishipa ya damu kwenye mapafu, tatizo linalojulikana kama pulmonary embolism, ambalo lilisababisha kifo chake.

Kifo hicho kimetokea wakati Ubiribo akiwa likizo nchini Thailand pamoja na mke wake.

Pumzika Kwa Amani.

Screenshot_20260905-194849.jpg
FB_IMG_1788646280343.jpg
 
Influencer na mfanyabiashara Kutoka Uingereza mwenye asili ya Nigeria, Igho Ubiribo (43), amefariki nchini Thailand baada ya kuchomwa sindano za kuongeza ukubwa wa uume.

Baada ya kufanyiwa matibabu hayo, Ubiribo alianza kupata maumivu makali ya kifua na baadaye akazimia. Alikimbizwa hospitalini, lakini alifariki licha ya juhudi za madaktari kumuokoa.

Uchunguzi wa mwili wake baada ya kifo ulibaini kuwa kemikali ya Hyaluronic acid iliyotumika kwenye sindano hizo iliingia kwenye mishipa ya damu na kufika kwenye mapafu. Hali hiyo ilisababisha kuziba kwa mishipa ya damu kwenye mapafu, tatizo linalojulikana kama pulmonary embolism, ambalo lilisababisha kifo chake.

Kifo hicho kimetokea wakati Ubiribo akiwa likizo nchini Thailand pamoja na mke wake.

Pumzika Kwa Amani.
Jinga KABISA KABISA KABISA
 
Jinga kabisa 43 ndiyo unakuja kujua kwamba una Kibamia? Miaka yote hiyo mbona alivumilia na kibamia iweje uje kustuka at 43? Binadamu turidhike na tulivyopewa wa mbili havai moja.
 
Back
Top Bottom