Uchaguzi 2020 Ingekuwa katika Nchi za wenzetu, Nyalandu na wenzake wangejitoa na kumuachia Lissu

Uchaguzi 2020 Ingekuwa katika Nchi za wenzetu, Nyalandu na wenzake wangejitoa na kumuachia Lissu

Membe mwenzake ameshaonyesha dalili za kumuunga mkono Lissu ila yeye kakomaa.

Hii sio soka ambayo umapaswa kukomaa hata kama bao moja unalotafuta katika mechi ya fainali kwenye dakika za majeruhi , haliwezi badili matokeo pale mpinzani wako anapokuwa na anaongoza kwa magoli mengi.
kazi aliyo tumwa na ccm inaweza kuigarimu cha dema kwa kuungana na membe

Bora cdm wakasimama kama walivyo maana tayar jamii ina imani nao kuliko kuungana na watu ambao kwa jicho la tatu wana timiza walicho tumwa
 
Kumbe mnapenda mambo ya ccm ya fomu moja ya kugombea eeeh

Tuwe makini na maneno yetu tusije jikuta tunasahau tulicho sema jana

Kuingia kwenye ulingo ni ushujaa kujitoa ni kushindwa kabla ya pambano

Hapo neno demokrasia itumike kama ilivyo kwa jina la chama
Kujitoa ni tofauti na kuzuia watu kugombea ili mtu fulani apite kimezengwe.
 
Unaogopa nini kusubiri mechi iishe?
Membe mwenzake ameshaonyesha dalili za kumuunga mkono Lissu ila yeye kakomaa.

Hii sio soka ambayo umapaswa kukomaa hata kama bao moja unalotafuta katika mechi ya fainali kwenye dakika za majeruhi , haliwezi badili matokeo pale mpinzani wako anapokuwa na anaongoza kwa magoli mengi.
 
Asimame Nyalandu,Lissu au mgombea yoyote sisi tunasema kipigo kipo pale pale safari hatutaki wapinzani wapate hata Jimbo moja la uchaguzi.

Yaani tutawatembezea kipigo cha pakashume yaani turuhusu mapusi kwenda kunajisi Ikulu kweli ????hilo jambo haliwezekani hata kidogo
 
Mpaka muda huu, nashindwa kuwaelewa Nyalandu na wenzake kwani nyakati zinambeba Lissu kwa asilimia 100.

Kwa hali ilivyo, ingekuwa ni katika nchi za wenzetu,mfano US, mtu kama Nyalandu naamini angetangaza kujitoa na kumuunga mkono Lissu bila kusubiri kupigwa kura na wajumbe.

Anyway, wacha tusubiri lakini huku ni kushindwa tu kusoma alama za nyakati kwa kisingizio cha demokrasia, demokrasia ambayo haimpi nafasi yeye na wenzake.

Hata hivyo,hii itakuwa ni fursa ya Lissu kuonyesha kukubalika kwake ndani ya chama kulinganisha na wagombea wenzake.

Wacha tusubiri labda kuna wanaopanga kujitoa siku ya kupiga kura kupitisha mgombea na kumuunga mkono Lissu maana siasa ndio zilivyo.
Sasa mkuu ikitokea Nyalandu akashinda itakuaje?
 
Ingelikuwa ninchi za Wenzetu
Mwenyekiti wa Kudumu Chadema Asingeweza Kuzuia wengine Kugombea kiti hicho na kuwa yeye miaka nenda Rudi
Ingelikuwa ni kwenye nchi za wenzetu, CCM isingetumia muda na rasilimali nyingine nyingi kumhujumu Mwenyekiti wa CHADEMA aliyeko madarakani kwa mujibu wa katiba.
 
Asimame Nyalandu,Lissu au mgombea yoyote sisi tunasema kipigo kipo pale pale safari hatutaki wapinzani wapate hata Jimbo moja la uchaguzi.

Yaani tutawatembezea kipigo cha pakashume yaani turuhusu mapusi kwenda kunajisi Ikulu kweli ????hilo jambo haliwezekani hata kidogo
Utakuwa unakunwa ww sio bure ..
 
Kwa kifupi sana ni kwamba Nyalandu alichkua form kimkakati zaidi (km backup tu) hasa iwapo lolote lingetokea kwa Tundu Lissu....

Kwa sasa wanatimiza tu mchakato wa kidemokrasia lkn Rais ni Lissu haina ubishi
 
Kujitoa ni tofauti na kuzuia watu kugombea ili mtu fulani apite kimezengwe.
Mkuu neno demkrasia inapaswa kutekelezwa kwa kiwango cha juu ili kuionyesha dunia chama kinautofaut na vyama vingne

Ukisha dhubutu hupaswi kurud nyuma kwa kigezo cha kusema fulan atanishinda

Ukishinda je
 
Kwa kifupi sana ni kwamba Nyalandu alichkua form kimkakati zaidi (km backup tu) hasa iwapo lolote lingetokea kwa Tundu Lissu....

Kwa sasa wanatimiza tu mchakato wa kidemokrasia lkn Rais ni Lissu haina ubishi
Je akipita mwingne itakuwaje?
 
Kwanini unaogopa taratibu zisifuatwe? wacha mambo ya ajabu, muhimu kura zipigwe mshindi apatikane.
 
Tena afadhali mara elfu Mbowe aliendelea kuwa m/kiti . Kwa Mwambe sijui chama kingeuzwa mazima huko Lumumba na mwenyekiti (Mwambe).
Mwambe aliishaandaa safu yake ya uongozi iliyosheheni mamluki watupu, ambao kazi yao ya kwanza ingekuwa kuwafukuza kutoka CHADEMA, wale wote wenye msimamo imara wa kupambana CCM, kama alivyofanya Lipumba.
Sasa hivi huko aliko kama mamluki wengine kawa (kama) muhogo mchungu, Binadamu hawauli, hata ngiri na nguruwe pori pia hawautaki.
 
Sikubaliani na mtoa mada, namkubali lissu lakini sikubaliani na lissu kupita Vila kupingwa, jambo LA msingi haki itendeke.watu wapige kura kwa haki, kura zihesabiwe wazi atakayeshinda aungwe mkono
 
Back
Top Bottom