Ingekuwa wewe...

Ingekuwa wewe...

...aaah, hiyo najua mamie. Hata mamsap akiniita 'Mbu!' najua mnhh... leo kunakuhesabu boriti wakati wa kutafuta majibu ya kina...!

nataka yale majina kwenye salooni na kitchen party ambazo 'hazijatulia', am sure baba nanihii, sio kabisa...kwani nishasikia mwiko kumremba remba mumeo huko... kuhofia kusaidiwa au kuchorwa unavosaidiwa!

All in all, mimi na kilongalonga changu, naye ana chake,...presha za nini?

Mr. au Mzee.
 
dada Belinda,
Ukitaka ndoa yako idumu kwa muda mrefu usipende kufuatilia fuatilia mambo kuhusu mmeo mwache huru mwache free tu atafanya mpaka atachoka....


hapa umenigusa utamu kweli! yani ukikaa useme unamchunguza mwanaume hutakuwa na amani, wachaa afanye weee akichoka/akiona ametoka sana nje ya mstari na bila kuulizwa/kuhijiwa atajirudi mwenyewe na kwa adabu tele! mana umeuliza/umehoji mpaka umechoka! inilinisaidia sana hii njia looo na pia inahitaji moyo coz utaona cmu inaita wanaongea wajuavyo ile ki juu juu tu mwaname huyoo anatoka, naenda kumuona fulani! walaa huhoji ki undani, unamwacha aende arudi muda atakao! atacheza rafu sana but kuna cku atajirudi tu.
 
Khaa! fidel yaani achoke wakati kanizeekea?! No way,atatulia tu na utibaigana tunaoapply kwenye ndoa. Pia kumbuka mwanaume ukimwachia anakuona zuzu sometimez bora uwe na msimamo mara kadhaa ajue hapa inawezekana au hapa no! Halafu mwanamme ni rahisi kumjua anachofanya,huhitaji kutumia muda kumchunguza maana vidumu kazi kushindana umahiri na mama mwenye nyumba..



unaweza ukaongea naee weee mpaka ukachoka ukaona hana muelekeo wa kubadilika kwa wakati huo sasa hapo ndipo unapompa nafac amalize atakayo! ni ngumu jamani! BJ unaweza kujua anachofanya na asijali kwa lolote kushtuka ni baadae atakapokuwa kazinduka na anataka kutulia, na akitulia kwa style hi na adabu/heshima ni mbele kuliko kitu kingine!
 
Mmenikumbusha rafiki yangu mmoja alipigiwa simu akiwa na mke wake akawa hapokei simu, halafu kaweka mlio tofauti mke akimwambia pokea hataki anasema simjui ananisumbua mke mbabe kidogo akapoke amaana alihisi kitu iweje abadilishe mlio ili akipiga amjue ni nani , akaweka loud speaker akamwambia pokea , msichana kaanza nimeshafika stand muda mrefu hupokei simu na unajua mi huku ni mgeni njo unipokee, jamaaa akajibu sawa kwa maelekezo ya mke akamwambia kampokee umlete hapa nyumbani jamaa akaenda kumpokea mke nyuma kwenye tax akamwambia ukileta ujanja nimekwambia mpeleke nyumbani wakafik msichana akaanza huyu ni nani jamaa anababaika, sasa inaonyesha huyo msichana alihaidiwa mambo mengi kwa hiyo akawa anajiamini akaanza kumpaka shost wangu, mwanaume hakupendi unajipendekeza walikuwa hawajafunga ndoa bado, amesema atakuacha anioe,shost akamchukua yule mwanaume akamfungia kwenye chumba akaanza kupambana na yule msichana akamtandika na mkanda akamaliza akachomeka pasi akampasi mapaja, akamfungulia mwanaume akamwambia mmsaidie wewe si ulimwahidi akija utanifukuza, yule msicha na akasema dada nisamehe hutakaa unione tena wala unisike katika maisha yako, tangu siku hiyo mwanaume huyo ameshika adabu na ndoa kafunga sidhani kama ana vimeo tena ( lakini kufanya haya yahitaji koyo uwe na unajiamini na uwe strong)



kubwa kuliko! huyo binti hatataka maishani kwake kuckia mume/mchumba wa mtu.
 
...ama wanawake ni wasiri, yaani hamtaki kutaja majina mengine mnayotuita huko saloon na kwenye kitchen party? tajeni tu yale mabaya mabaya hasa mnapofundwa chungu hakikai kwenye figa moja, au ukikerwa nk...🙂

Mbu, jina mojawapo baya ni ZOBA.
Jina zuri ni MAHABUBA.
 
Shetani huwa hapendi kuona watu wanafurahia maisha ya ndoa. Hufanya kila liwezekanalo kuingiza chuki na mifarakano. Chakufanya ni kudumu katika sala, muuombe Mungu pamoja kwa kusali ama kuswali pamoja katika hali zote, kila siku iendayo kwa mola. Kusameheana na kuvumiliana ni silaha muhimu. Kupeana uhuru, ndoa isiwe ni kifungo. Na kufanya mapenzi kwa bidii na kujituma ni kiungo muhimu.

Masa
Kufanya mapenzi kwa bidii yakiambatana na sala shekhe.
Kwani tendo la ndoa ni ibada ati.

Mwasali pamoja kabla ya kuanza mchezo.Mnyezi MUNGU hufurahi sana pale mtu anapomwingilia mkewe shekhe.
 
Nimekupata Belinda ila huoni sie tunawaita majina matamu tukiwa na wenzetu ila wao wanatuita ya ajabu?

Ila kwa wale wenye vidumu nasikia huwezakumwita mumewe hili bwege au **** sina hakika kama ni kweli

In most cases sisi wanawake tupo romantic na caring kwenye mazingira ya kimahaba,mpaka mwanamke akuite jina lako halisi au ahifadhi kwenye simu ujue ameudhiwa/amekerwa sana. Tumezoea mume wangu,husband na mengine mazuri.

Sasa kwa hao wanawake wenye vidumu ambao wengi wao sababu ya waume zao kuwa na vidumu pia, lazima heshima inapungua kwa wanandoa. Kwahiyo mume ataitwa jina kama bwege,zoba,ngumbaro, lakini hawezi save kwenye simu ni wakati wa storiz na wanawake wenzake.
 
unaweza ukaongea naee weee mpaka ukachoka ukaona hana muelekeo wa kubadilika kwa wakati huo sasa hapo ndipo unapompa nafac amalize atakayo! ni ngumu jamani! BJ unaweza kujua anachofanya na asijali kwa lolote kushtuka ni baadae atakapokuwa kazinduka na anataka kutulia, na akitulia kwa style hi na adabu/heshima ni mbele kuliko kitu kingine!

Mwisho wa siku hatuwezi kushindana na wanaume katika mambo yao. Pia kimya kinamuumiza mtu anaona hujali wala nini,kumbe wewe unaumia tu moyoni na vijimambo vyake. Japokuwa kuna matatizo yanayofanana fanana kati ya wanandoa mbalimbali ila utakayempata kuwa mwenzi wako wa maisha ndo utajua jinsi ya kuhandle matatizo kwenye ndoa.
 
Back
Top Bottom