Mmenikumbusha rafiki yangu mmoja alipigiwa simu akiwa na mke wake akawa hapokei simu, halafu kaweka mlio tofauti mke akimwambia pokea hataki anasema simjui ananisumbua mke mbabe kidogo akapoke amaana alihisi kitu iweje abadilishe mlio ili akipiga amjue ni nani , akaweka loud speaker akamwambia pokea , msichana kaanza nimeshafika stand muda mrefu hupokei simu na unajua mi huku ni mgeni njo unipokee, jamaaa akajibu sawa kwa maelekezo ya mke akamwambia kampokee umlete hapa nyumbani jamaa akaenda kumpokea mke nyuma kwenye tax akamwambia ukileta ujanja nimekwambia mpeleke nyumbani wakafik msichana akaanza huyu ni nani jamaa anababaika, sasa inaonyesha huyo msichana alihaidiwa mambo mengi kwa hiyo akawa anajiamini akaanza kumpaka shost wangu, mwanaume hakupendi unajipendekeza walikuwa hawajafunga ndoa bado, amesema atakuacha anioe,shost akamchukua yule mwanaume akamfungia kwenye chumba akaanza kupambana na yule msichana akamtandika na mkanda akamaliza akachomeka pasi akampasi mapaja, akamfungulia mwanaume akamwambia mmsaidie wewe si ulimwahidi akija utanifukuza, yule msicha na akasema dada nisamehe hutakaa unione tena wala unisike katika maisha yako, tangu siku hiyo mwanaume huyo ameshika adabu na ndoa kafunga sidhani kama ana vimeo tena ( lakini kufanya haya yahitaji koyo uwe na unajiamini na uwe strong)