Ingekuwaje kama Josephine Myrtle Corbin angezaliwa Afrika kipindi hicho?

Ingekuwaje kama Josephine Myrtle Corbin angezaliwa Afrika kipindi hicho?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Jina lake ni Josephine Myrtle Corbin. Alizaliwa Marekani 12/05/1868.

Maumbile yake hayakuwa ya kawaida. Alizaliwa akiwa na miguu minne, na pea ya viungo vya uzazi uzazi. Madaktari mbalimbali waliomfanyia uchunguzi walibainisha kuwa Josephine alikuwa na afya njema na anaweza kuishi kama binadamu mwingine yeyote.

Kutokana na upekee wa mwonekano wake, watu walikuwa na kawaida ya kumtembelea kumwona. Baba yake kuona hivyo, alifanya hiyo hali fursa. Aliamua awe anawatoza "kiingilio".

Pamoja na ulemavu aliokuwa nao, Josephine hakuruhusu kutawaliwa na mitazamo hasi
Aliyaishi maisha yake kikamilifu.

Alipotimiza miaka 19, alifunga ndoa na Daktari aliyeitwa James Clinton Bicknell. Walijaliwa watoto watano, wa kiume mmoja na wa kike wanne.

Kuna madai kuwa aliwazaa watoto watatu kwa kutumia viungo vya uzazi vya upande mmoja na watoto wawili kwa kutumia viungo vya uzazi vya upande mwingine.

Josephine alifariki 06/05/1920 akiwa na miaka 59 baada ya kuugua.

Wenzetu wameelimika tokea zamani. Ndiyo maana walimchukulia Josephine kama mtu wa kawaida.

Sijui yapi yangemkuta Josephine kama angezaliwa Afrika tarehe hiyo, 12/05/1868

 
Dahhh.....
Kuna wanaume wana bahati mazee...😋
Huyo Dr alikua anauhakika wa sehem mbili...😜
 
Kama mapacha na zetu zeru walikuwa wakitupwa, sidhani kama huyo angenusurika.
Kijijini kwetu kuna water falls, ambako ndio watoto wote waliozaliwa na matatizo yoyote walikuwa wanatupwa. Siku hizi ni kivutio cha utalii, lakini babu zetu walikuwa hawakatizi yale maeneo
 
Back
Top Bottom