Ingelikuwa siasa ni mpira wa miguu

Ingelikuwa siasa ni mpira wa miguu

Mbahili

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
281
Reaction score
525
Niwasalimu tena kwa jina la Jamhuri ya Muungano. "Kazi iendelee😅😅 (japo kuwa hamna kazi..)

Nimekaa na kuwaza hivi siasa ingekuwa mpira wa miguu; CCM hutumia mfumo gani na Chadema mfumo gani (tuseme vyama vingine wakae upande wa mashabiki)

Mimi nimewaza hivi; CCM hutumia mfumo wa 541 yaani mabeki watano viungo wanne na mshambuliaji mmoja wakati CHADEMA ni 343... yaani mabeki watatu viuongo wanne na washambuliaji watatu..

Ukiangalia mifumo hizi kwa makini, CCM wanapossess mpira na kupiga counter Attack.. yaani mchezo wa CCM ni wakushtukiza.. wanakuacha uchezee mpira kisha wakupige counter.

Upande wa pili CHADEMA huposess pia, hucheza na mpira lakini wanashindwa kufika langoni.. yaani wana mpira mzuri, pasi kama zote ila hukutana na viungo 4 na mabeki 5.. hakupitiki... kwa walioshindwa elewa hapa angalia game ya simba na raja simba aliepigwa tatu kwa mkapa😅. Hapo simba chadema raja ccm.

Kiuhalisia mambo yako hivi...
Chadema huenjoy sana kujiona wana watu.. wanapenda kuona wafuasi wengi kwenye mikutano yao. Swali la msingi ( Je hawa watakupigia kura?)

Ccm wamemstukia mpinzani wao.. ukiwapa uwanja wa kucheza hawana ujanja wa kufunga (Huu ni mchezo hatari lakini salama).

Viongozi chadema bado hutumia siasa za kale kufikia lengo. Kwa mwenendo huu, bado Ccm ndio chama tawala na pia ndio chama pinzani kuu. Chadema ni kikundi cha watu waliojiwekea imani kwa wananchi, na kuomba chama tawala misaada ya kuendesha chama.

Fikiria......
Uwanja ni wa Morocco (Raja), Refa ni wa Raja, kanuni za mchezo kasuka raja.. hapa simba anamashabiki tu tena waliosafiri kwa tabu kidogo.. swali fikirishi...... Je Simba atapata hata goli?😂
unnamed.jpg
 
Uko sahihi

Bila ya Katiba Mpya,hakuna la maana litakalofanyika
 
  1. Kwamba CCM kushinda kwa kuengua wagombea wa upinzani ni mfumo wa 541.
  2. Kwamba CCM kushinda kwa kuzuia mawakala wa upinzani ni mfumo wa 541.
  3. Kwamba CCM kutengeneza kura fake na kuziingiza kwenye masanduku ya kura ni mfumo wa 541.
  4. Kwamba kuzuia mawakala wa upinzani ni mfumo wa 541.
  5. Kwamba kutangaza matokeo fake ni mfumo wa 541.
Only an insane person would believe this ridiculous argument.
 
Last paragraph please, "kiwanja cha kwako, waamuzi wako, mpira wako washabiki nusu wako... utashindwaje kushinda?

"Technically inaitwa COUNTER ATTACK" ndio maana mara nyingi wako offside, sababu hapo awali tumesema hadi VAR ni yao basi "CCM has scored a very tactical goal" In Peter drury's voice
 
Kiuhalisia mambo yako hivi...
Chadema huenjoy sana kujiona wana watu.. wanapenda kuona wafuasi wengi kwenye mikutano yao. Swali la msingi ( Je hawa watakupigia kura?)
Acha utoto kwamba tatizo la Chadema ni kutopigiwa kura au ni mchakato mzima wa uchaguzi. Mfano uchaguzi wa TAMISEMI more than 90% ya wagombea wa upinzani walienguliwa Sasa hapo hata ukipiga kura Kuna faida Gani?

Tuache kujazana uongo, mfumo wa uchaguzi una matatizo na ndio maana Samia kakubali issue ya katiba mpya na tume huru. Anajua zaidi Yako jinsi wanavyoiba kura.
 
Back
Top Bottom