Injini ya ndege ya United Airlines yalipuka angani

Naona watu wanaishambulia Boeing wakati tatizo lililotokea ni la hizo engines Pratt & Whitney PW4077 ambazo zimetengenezwa na kampuni nyengine kabisa
Kwanini hizo matatizo zinatokea kwenye kampuni hii ya Boeing tu ..kila ndege zao basi ni matatizo tu

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
yeah yapo matatizo yanatokea kwenye ndege zao hao Boeing na hata Airbus nao yanatokea huko sema Boeing ndio kuzidi na zidhani kama kuna kampuni la ndege ambalo halijapta hivi vimikasa vya hapa na pale, ila kwa hili msiwatwishe mzigo wa lawama Boeing mana hilo tatizo ni la zile engines sio wao Boeing
 
Hebu fafanua mkuu fly by wire
Katika ndege yoyote kuna vitu vinaitwa flight controls surfaces, hivi ni vifaa ambavyo vinawekwa katika pembe mbalimbali za ndege ambazo hutumika kucontrol uelekeo wa ndege kam vile pitch roll na yaw. Mfano wake ni Rudder, hii utaikuta katika mkia wa ndege kwenye lile bawa liliosimama kitaalamu huitwa vertical stabilizer, hii rudder inatumika kucontrol yaw movement. Elevators, hizi utazikuta katika mkia wa ndege kwenye mabawa mawili yaliyolala kulia na kushoto kitaalamu huitwa horizontal stabilizers, elevators hukontrol pitch movement. Aelerons, hizi utazikuta katika mabawa ya ndege yote mawili la kulia na kushoto ,hizi hutumika kukontrol roll movement.

Kwakua hizi flight control surfaces zinakontroliwa na marubani kupitia pedals na control wheel (usukani) kwa hiyo inabidi kuwe na muunganiko kutoka kule kwenye hizo controls surfaces mpaka kwenye pedals na control wheel ambavyo hupatikana kwenye chumba cha marubani (cockpit) , sasa kwa hapo zamani huo muunganiko ulikuwa ni link ya machumachuma yani kuna links za mechanical components kama vile cables,pulleys, rods,gears,crank na chains kutoka huko kweny control surfaces mpka kufikia kwenye cockpit ambapo zitaenda kulink kwenye pedals na usukuani wa ndege. Kwa mfano pilot akikanyaga pedeli hiyo movement ya hiyo pedeli itasafirishwa kupitia huo muunganiko wa pulleys,cables,rods etc mpaka kufikia kwenye control surface husika. Huu mfumo pia hutumiwa mpaka sasa kwenye hizi ndege ndogondogo ambazo huwa hazizalish aerodynamic forces kubwa kivile ukilinganisha na aerodynamic forces zinazozalishwa kwenye heavy aircrafts.

Katika modern aircrafts hizo mechanical components hazipo yani siku hizi utakutana na wires,sensors,actuators and computers na hapo ndipo tunapopata neno "Fly by wire" ikimaanisha tunaruka kwa msaada wa wires na sio machumachuma tena. Hapo sa hv ni mwendo wa input and output signals tu .
Hemu ngoja nikupe basic kidogo ya namna hii sysytem inavyofnya kazi.
Katika fly by wire sysytem inputs za pilot ambazo hutokana na kiasi gani pilot atakavyokanyaga pedeli au kiasi gani pilot atavyozungusha usukani ambapo humo kwenye usukani na pedeli kuna sensors mbalimbali zitakazobadilisha hayo matendo ya pilot kuwa electric signals, then hizi inputs zitatumwa kwenye computers kupitia wires kisha hutafsiriwa na computer then computer itazichakata hizi inputs kwa kukotoa factors mbalimbali za ndege ambazo zinahusiana na kazi husika anayoitaka pilot ili kutambua ni njia gani bora ya kuzimove hizo flight control surfaces kulingana na condition ya ndege kwa wakati huo kwa weledi mkubwa sana ili kutiii matakwa ya pilot kiufasaha na kiurahisi zaidi, kisha hizo taarifa zinazotoka hapo (output signals) zitapelekwa kwenye pump na solenoid valves ili kuweza kuruhusu hydraulic oil iweze kutoka katika pressure na njia sahihi kabisa ili kwenda kuziactuate hizo control surfaces kwa ufanisi mkubwa. Kwa lugha rahisi katika fly by wire system Actuators zinapata maelekezo kutoka kwenye computers ili kujua ni nini cha kufanya ili kukamilisha matakwa ya pilot lakin katika system ya mechanical, actuators zinapokea maelekezo moja kwa moja kutoka kwa pilot kupitia muunganiko wa component mbalimbali kama cables na pulleys . Kwahiyo kwa kutumia hii system ya fly by wire tutapata faida kedekede kama kupunguza uzito wa ndege, ndege kuweza kuvumilia kasoro mbalimbali,kupunguza ulaji wa mafuta,kurahisisha uendashaji wa ndege yani pilot atajiona kama anacheza game vile, kupunguza gharama za ukarabati wa ndege etc.......

Sasa tuje kwenye kesi yetu ya Boeing 777 ambayo injin yake moja ilifeli lakin ndege ikaweza kufanya emergency landing bila ya shida.
Injini moja inapofeli mana yake nguvu ya ndege (Thrust) itazalishwa upande mmoja na upande mwengine haitakuwepo na hii itasababisha balance ya ndege kupotea na kuhatarisha kabisa usalama wa ndege.Chukulia mfano injini ya kulia imefeli hapa utabakiwa na injini ya kushoto ambayo itakuwa inakupeleka uelekeo wa kulia bila ya wewe kupenda na hapo ndege ndipo inapokuwa katika very tricky aerodynamics , so ili kuweza kurudisha balance ili ndege ipate kwenda straight hapo sasa ndio fly by wire system itakuwa uwanja wa nyumbani, computers zitapiga mahesabu ya kufa mtu ili kujua ni jinsi gani ya kucheza na hizo flight control surfaces ili ndege iweze kuzalisha nguvu kinzani (counter torque) katika ule upande ambao injini imefeli, hiyo nguvu kinzani itayozalishwa itasaidia kurudisha ile balance iliyopotea na kuifanya ndege iwe katika msawazo wake wa kawaida ili ipate kwenda in a straight velocity.
View attachment 1713841
images(78).jpg
View attachment 1713843
 
View attachment 1713841View attachment 1713842View attachment 1713843
Respect... Advanced Avionics
 
Back
Top Bottom