Injinia Hersi Said: Timu za Simba na Yanga zinaendeshwa kwa hasara miaka mingi

Uwezo wako umeishia hapo.🤣🤣🤣
 
Hivi vilabu vinataka sifa za kijinga tu kwa sababu matumizi yao ni makubwa kuliko mapato na hawana mali zozote za maana.

Tusubiri miaka miwili au mitatu ijayo hivi vilabu vitakuwa vimefirisika kwa sababu havina mapato ya kustahimili mahitaji yao.
 
Jabri Shikamkono kafirisika yupo Morogoro anacheza bao tu. Kuna mhaya mmoja Dkt. Ruta Nelson alijua vyema hizi timu.
 
Kawajaza Wakongo atajuta amuulize mmiliki wa FM ACADEMIA wakongo hawana tofauti na wanawake kujipura.
 
Timu zikiwa Hoi Kipesa watu mpo Kimyaaa.
Wawekezaji Kwa mapenzi Yao wakiweka pesa zao mnaanza kushangilia Pira Biliani, ooo sijui Mayele fundi, na misemo mingii
The return of Champions.
Huku mkiwadhihaki hao walio waleta Akina Mayele.
Mnataka waseme neno moja tu Faida Faida Faida basi.
Kwanini msiwafukuze hao wawekezaji mchukue hizo Faida wenyewe.
Muwasajiri na hao Akina Mayele tuone Hilo Pira Biliani.
Mawazo yenu ni ya upande mmoja Tu.
 
Sio bilioni moja tu. Unafahamu mishahara ya wachezaji na benchi zima la ufundi? Hao wachezaji na makocha wa nje wengi wanalipwa 10M+ kwa mwezi? Bado hao kina Boko wa milioni 5, 6 hadi 7!
Hapo bado kambi, usafiri wa ndege, basi n.k
 
Sio bilioni moja tu. Unafahamu mishahara ya wachezaji na benchi zima la ufundi? Hao wachezaji na makocha wa nje wengi wanalipwa 10M+ kwa mwezi? Bado hao kina Boko wa milioni 5, 6 hadi 7!
Hapo bado kambi, usafiri wa ndege, basi n.k
Kwa mwezi malipo ya wafanyakazi wote zinafikia Milioni Mia Nne, hapo Simba
Wacha usafiri, ghalama za timu, usafiri, dhalula, hoteli, matibabu nk.
Wastani pesa ya uendeshaji inafikia million mia Sita Kwa Mwezi hapo Simba.
Piga hesabu msimu nzima

Ndio maana timu zikifulia hao wote wanao ongea ongea wanakuwa kimya.

Vilabu vya Simba na Yanga vinawekezwa Kwa mapenzi Tu ya wawekezaji.
Ndio maana wawekezaji wao ni wapenzi WA hizo timu.
Manji, Rostam, GSM ni wapenzi WA Yanga.
Ndio maana wanafadhiri timu Yao hata wapate hasara wapo Tu.
Hatusemi hawapati faida flani Ila haikidhi matumizi Yao hadi sasa hivi.
Labda hapo baadae kidogo.

Ukitaka kuhakikisha subiri wajitoe njaa itanza siku hiyo hiyo.
Na hawa waongeaji hutawasikia wakiongea ongea.
Kumbuka Manji alivyo liliwa kurudi Yanga.

Lazima tuwaheshimu wawekezaji wa timu zetu. Na kuwasikiliza wanacho ongea.
Wameleta mabadiliko makubwa kwenye Soka letu Kwa ghalama zao binafsi kabisa.
 
Kweli kabisa. Umeongea ukweli mtupu. Bila pesa hakuna timu hapo. Kumbuka wenzetu wakenya timu zao baada ya kufulia zilipotea na umaarufu wote ule mfano AFC Leopard na GorMahia kuna kipindi zilipotea kabisa. Kidogo Congo kina AS VITA na TP Mazembe ndio wamewekeza. Mpira ni pesa.
 
Tatizo wanasajili wachezaji na makocha wa kigeni kwa bei ghali na kuwalipa mishahara mikubwa wakati uwezo wao wa kawaida tu.
Hii ligi siyo ya kulipa mshahara wa milioni 10. Haina thamani hiyo
Hata kununua mchezaji kwa 20m ni upuuzi, wakina boko wanarukaruka tu uwanjani
 
Ukiwaambia pisha mdhamini mwingine hawataki
Acheni uzushi nyie, simba na yanga wapo tayari kufanya kazi na yeyote ili mradi wapate pesa, toa mfano wa mdhamini aliye tayari kufanya kazi na hizi timu kwa dau nono akakataliwa
 
Hiyo 35k unaiona ndogo sio
 
Acheni uzushi nyie, simba na yanga wapo tayari kufanya kazi na yeyote ili mradi wapate pesa, toa mfano wa mdhamini aliye tayari kufanya kazi na hizi timu kwa dau nono akakataliwa

Bakhresa alikuwa tayari kununua hisa Simba..
 
Angeandika hivi MO Dewji,
Comments za kumpinga zingefika elfu Kumi na ushee.
Tofautisheni kati ya kile ambacho Mwamedi amekuwa akilalamika mara kwa mara, na hiki kilichosemwa na Hersi

Hoja ya Mwamedi imekuwa "...yeye Mwamedi amekuwa akipata hasara" wakati hoja ya Hersi ni "...timu kupata/kujiendesha kwa hasara"!

Mwamedi anapingwa kwa sababu huwezi kulalamika kwamba unapata hasara wakati Jezi ya Makolo imejaa makolokolo ya METL kila pembe!!

Mwamedi analilia kwamba anapata hasara wakati Simba ina udhamini lakini anaongea kwa namna kana kwamba Makolo yana-depend kila kitu kutoka kwa Mwamedi!
 
Manndugu:

Timu ipo ligi kuu na inatangaza matangazo ya kampuni (Mdhamini) cha ajabu kwenye account hakuna hela yoyote.
 
Watu wao ndio mabinhwa wa kuendesha kampeni dhidi ya MO kuwa anadanganya angemkemea manara anayewaaminidha uongo yanga dhidi ya MO kuweka katangazo tu apate faida
 
Wafusi kama wewe?!!..
 
Hiyo 35k unaiona ndogo sio
Kwangu naweza sema ni pesa ndogo japo sina uhakika kama kila mtu ataiona ndogo.Lakini kutoa elfu 35 kununua jezi ambayo klabu itatumia kwa season moja sidhani kama ni kiwango kikubwa.OK,labda ni kiwango kikubwa ,lakini sasa hapo ujue kwamba ata pale timu zinapokosa matokeo mazuri inabidi tupunguze malalamiko sasa, kwa maana tutakuwa hatuna msaada kwa timu zetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…