Sio bilioni moja tu. Unafahamu mishahara ya wachezaji na benchi zima la ufundi? Hao wachezaji na makocha wa nje wengi wanalipwa 10M+ kwa mwezi? Bado hao kina Boko wa milioni 5, 6 hadi 7!
Hapo bado kambi, usafiri wa ndege, basi n.k
Kwa mwezi malipo ya wafanyakazi wote zinafikia Milioni Mia Nne, hapo Simba
Wacha usafiri, ghalama za timu, usafiri, dhalula, hoteli, matibabu nk.
Wastani pesa ya uendeshaji inafikia million mia Sita Kwa Mwezi hapo Simba.
Piga hesabu msimu nzima
Ndio maana timu zikifulia hao wote wanao ongea ongea wanakuwa kimya.
Vilabu vya Simba na Yanga vinawekezwa Kwa mapenzi Tu ya wawekezaji.
Ndio maana wawekezaji wao ni wapenzi WA hizo timu.
Manji, Rostam, GSM ni wapenzi WA Yanga.
Ndio maana wanafadhiri timu Yao hata wapate hasara wapo Tu.
Hatusemi hawapati faida flani Ila haikidhi matumizi Yao hadi sasa hivi.
Labda hapo baadae kidogo.
Ukitaka kuhakikisha subiri wajitoe njaa itanza siku hiyo hiyo.
Na hawa waongeaji hutawasikia wakiongea ongea.
Kumbuka Manji alivyo liliwa kurudi Yanga.
Lazima tuwaheshimu wawekezaji wa timu zetu. Na kuwasikiliza wanacho ongea.
Wameleta mabadiliko makubwa kwenye Soka letu Kwa ghalama zao binafsi kabisa.