Injinia Hersi Said: Timu za Simba na Yanga zinaendeshwa kwa hasara miaka mingi

Injinia Hersi Said: Timu za Simba na Yanga zinaendeshwa kwa hasara miaka mingi

We na akili kubwa yote hiyo bado hufahamu hatua za mahitaji.
Mwanadamu kila anapozidi kupata pesa mahitaji yake yana adilika.
Kasome, Manslow Hierachrchy of Needs ya Abraham Manslow 1943 utaelewa.
Mfanya biashara tajiri inafikia wakati anatumia pesa yake nyingi kutaka fahari tu, na furaha ya moyo wake.
MO alishasema hili
"mi naifadhiri Simba napenda furaha tu"
Matajiri wanaanzisha baadhi miradi ambayo hawapati faida hata chembe, ukiwafuatilia Akina Bill gates, Bezos, Dangote utaelewa vizuri.
Nadharia za Kisomi zinalikubali hili Jambo ndio maana Manslow anaheshimika kitaaluma.
Wewe mwenzetu sijui unatokea wapi

wewe mwenye akili kubwa Sana.
Uwezo wako umeishia hapo.🤣🤣🤣
 
Hivi vilabu vinataka sifa za kijinga tu kwa sababu matumizi yao ni makubwa kuliko mapato na hawana mali zozote za maana.

Tusubiri miaka miwili au mitatu ijayo hivi vilabu vitakuwa vimefirisika kwa sababu havina mapato ya kustahimili mahitaji yao.
 
Kwakuwa ameongea Eng. wala hutawasikia wakibweka.

Watu tusichokijua ni kuwa hizi timu zetu sometimes zinatia hasara tupu.Mzee Jabir Kingamkono (kama sijakosea jina lake),aliyekuwa Mfadhili wa Simba aliishia kufirisika.Mzee Hassan Dalali alijitoa kwa hali na mali, leo hata pa kulaza kichwa chake tu ni taabu.Halafu Mo Dewji akiongea kuhusu hasara anazopata kama mwekezaji watu wanamzomea.
Jabri Shikamkono kafirisika yupo Morogoro anacheza bao tu. Kuna mhaya mmoja Dkt. Ruta Nelson alijua vyema hizi timu.
 
''Timu hizi zinajiendesha kwa hasara kwa miaka mingi ndio maana zimekwama. Ukisema hivi mtu anaweza asikuelewe lakini ukitazama mapato ya klabu na matumizi ndio utajua kwanini zinajiendesha kwa hasara'' - Eng. Hersi Said Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM.

#KipengaXtra
Kawajaza Wakongo atajuta amuulize mmiliki wa FM ACADEMIA wakongo hawana tofauti na wanawake kujipura.
 
Timu zikiwa Hoi Kipesa watu mpo Kimyaaa.
Wawekezaji Kwa mapenzi Yao wakiweka pesa zao mnaanza kushangilia Pira Biliani, ooo sijui Mayele fundi, na misemo mingii
The return of Champions.
Huku mkiwadhihaki hao walio waleta Akina Mayele.
Mnataka waseme neno moja tu Faida Faida Faida basi.
Kwanini msiwafukuze hao wawekezaji mchukue hizo Faida wenyewe.
Muwasajiri na hao Akina Mayele tuone Hilo Pira Biliani.
Mawazo yenu ni ya upande mmoja Tu.
 
Kwani home boy klabu ya simba kwa mwaka inatumia kiasi gani katika bajeti yake? Hivi unaposema sijui kuna matangazo kwenye jezi ,unajua thamani ya kila tangazo kwenye jezi.Nakupa mfano,msimu uliopita Simba na mdhamini wa timu ambaye ni Mo walisaini mkataba wa kutangaza sabuni ya Mo poa.Mkataba ulikuwa na thamani ya shilingi milioni mia mbili as it was reported.I am not sure whether this was true or not.Sasa tufanye leo hii kila tangazo liwe na hii thamani maana yake ni kwamba matangazo yote, umesema matano yata count kama bilioni moja.Swali langu ni hivi ni kweli klabu kama simba inaendeshwa kwa bajeti ya bilioni moja kwa msimu?
Sio bilioni moja tu. Unafahamu mishahara ya wachezaji na benchi zima la ufundi? Hao wachezaji na makocha wa nje wengi wanalipwa 10M+ kwa mwezi? Bado hao kina Boko wa milioni 5, 6 hadi 7!
Hapo bado kambi, usafiri wa ndege, basi n.k
 
Kwa mwezi malipo ya wafanyakazi wote zinafikia Milioni Mia Nne, hapo Simba
Wacha usafiri, ghalama za timu, usafiri, dhalula, hoteli, matibabu nk.
Wastani pesa ya uendeshaji inafikia million mia Sita Kwa Mwezi hapo Simba.
Piga hesabu msimu nzima

Ndio maana timu zikifulia hao wote wanao ongea ongea wanakuwa kimya.

Vilabu vya Simba na Yanga vinawekezwa Kwa mapenzi Tu ya wawekezaji.
Ndio maana wawekezaji wao ni wapenzi WA hizo timu.
Manji, Rostam, GSM ni wapenzi WA Yanga.
Ndio maana wanafadhiri timu Yao hata wapate hasara wapo Tu.
Hatusemi hawapati faida flani Ila haikidhi matumizi Yao hadi sasa hivi.
Labda hapo baadae kidogo.

Ukitaka kuhakikisha subiri wajitoe njaa itanza siku hiyo hiyo.
Na hawa waongeaji hutawasikia wakiongea ongea.
Kumbuka Manji alivyo liliwa kurudi Yanga.

Lazima tuwaheshimu wawekezaji wa timu zetu. Na kuwasikiliza wanacho ongea.
Wameleta mabadiliko makubwa kwenye Soka letu Kwa ghalama zao binafsi kabisa.
 
Kweli kabisa. Umeongea ukweli mtupu. Bila pesa hakuna timu hapo. Kumbuka wenzetu wakenya timu zao baada ya kufulia zilipotea na umaarufu wote ule mfano AFC Leopard na GorMahia kuna kipindi zilipotea kabisa. Kidogo Congo kina AS VITA na TP Mazembe ndio wamewekeza. Mpira ni pesa.
 
Tatizo wanasajili wachezaji na makocha wa kigeni kwa bei ghali na kuwalipa mishahara mikubwa wakati uwezo wao wa kawaida tu.
Hii ligi siyo ya kulipa mshahara wa milioni 10. Haina thamani hiyo
Hata kununua mchezaji kwa 20m ni upuuzi, wakina boko wanarukaruka tu uwanjani
 
Ukiwaambia pisha mdhamini mwingine hawataki
Acheni uzushi nyie, simba na yanga wapo tayari kufanya kazi na yeyote ili mradi wapate pesa, toa mfano wa mdhamini aliye tayari kufanya kazi na hizi timu kwa dau nono akakataliwa
 
Huu ndo ukweri na ukweri lazima usemwe tu.Juzi tu hapa AZAM walitia mipunga yao kwenye ligi watu wakadai ni ndogo sijui ligi yetu kubwa,kelele zikawa nyingi lakini ukweli ni kwamba mpira wetu bado mchanga sana mtu kuwekeza pesa yake akapata faida.GSM na UTO yake wamejitahidi kutoa jezi waone kama watapata faida huko lakini sasa wadau wanachofanya,wanaacha kununua jezi original wanaenda kununua jezi ya buku tano tano.Then,timu zinapokosa matokeo utasikia sisi ni brand kubwa mara haya matokeo si yetu.Sasa hizo brand ukubwa wake uko wapi kama wanachama wake kununua jezi ya elfu 35 msala.
Hiyo 35k unaiona ndogo sio
 
Acheni uzushi nyie, simba na yanga wapo tayari kufanya kazi na yeyote ili mradi wapate pesa, toa mfano wa mdhamini aliye tayari kufanya kazi na hizi timu kwa dau nono akakataliwa

Bakhresa alikuwa tayari kununua hisa Simba..
 
Kwakuwa ameongea Eng. wala hutawasikia wakibweka.

Watu tusichokijua ni kuwa hizi timu zetu sometimes zinatia hasara tupu.Mzee Jabir Kingamkono (kama sijakosea jina lake),aliyekuwa Mfadhili wa Simba aliishia kufirisika.Mzee Hassan Dalali alijitoa kwa hali na mali, leo hata pa kulaza kichwa chake tu ni taabu.Halafu Mo Dewji akiongea kuhusu hasara anazopata kama mwekezaji watu wanamzomea.
Angeandika hivi MO Dewji,
Comments za kumpinga zingefika elfu Kumi na ushee.
Tofautisheni kati ya kile ambacho Mwamedi amekuwa akilalamika mara kwa mara, na hiki kilichosemwa na Hersi

Hoja ya Mwamedi imekuwa "...yeye Mwamedi amekuwa akipata hasara" wakati hoja ya Hersi ni "...timu kupata/kujiendesha kwa hasara"!

Mwamedi anapingwa kwa sababu huwezi kulalamika kwamba unapata hasara wakati Jezi ya Makolo imejaa makolokolo ya METL kila pembe!!

Mwamedi analilia kwamba anapata hasara wakati Simba ina udhamini lakini anaongea kwa namna kana kwamba Makolo yana-depend kila kitu kutoka kwa Mwamedi!
 
''Timu hizi zinajiendesha kwa hasara kwa miaka mingi ndio maana zimekwama. Ukisema hivi mtu anaweza asikuelewe lakini ukitazama mapato ya klabu na matumizi ndio utajua kwanini zinajiendesha kwa hasara'' - Eng. Hersi Said Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM.

#KipengaXtra
Manndugu:

Timu ipo ligi kuu na inatangaza matangazo ya kampuni (Mdhamini) cha ajabu kwenye account hakuna hela yoyote.
 
''Timu hizi zinajiendesha kwa hasara kwa miaka mingi ndio maana zimekwama. Ukisema hivi mtu anaweza asikuelewe lakini ukitazama mapato ya klabu na matumizi ndio utajua kwanini zinajiendesha kwa hasara'' - Eng. Hersi Said Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM.

#KipengaXtra
Watu wao ndio mabinhwa wa kuendesha kampeni dhidi ya MO kuwa anadanganya angemkemea manara anayewaaminidha uongo yanga dhidi ya MO kuweka katangazo tu apate faida
 
Kwa mpaka sasa sidhani kama kuna anayepiga hayo ila kwa upande mwingine tunaamini hao Wawekezaji nao ni greathinkers au wamezungukwa na Greathinkers watumie huo Mtaji wa Mashabiki kupata faida.

Hizo timu mitaji yao ni Wafuasi, kila kona ya nchi kuna mashabiki wa hizi timu, na zimebeba roho za Watu jiongezeni Wazee.
Wafusi kama wewe?!!..
 
Hiyo 35k unaiona ndogo sio
Kwangu naweza sema ni pesa ndogo japo sina uhakika kama kila mtu ataiona ndogo.Lakini kutoa elfu 35 kununua jezi ambayo klabu itatumia kwa season moja sidhani kama ni kiwango kikubwa.OK,labda ni kiwango kikubwa ,lakini sasa hapo ujue kwamba ata pale timu zinapokosa matokeo mazuri inabidi tupunguze malalamiko sasa, kwa maana tutakuwa hatuna msaada kwa timu zetu.
 
Back
Top Bottom