'Injinia' Hersi Said wa Yanga SC na GSM yako ni lini utaacha 'Uwongo' wako na kupenda 'Kuwadanganya' mno wana Yanga?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
'Injinia' Hersi Said acha kudhani kuwa Watanzania hawafatilii mambo ya Michezo kama hao wana Yanga SC wako ambao kila mara unapenda 'Kuwadanganya' na sijui umewapa 'Sumu' gani ambayo aliyekuwa 'Mfadhili' wako Kipenzi kabisa Yusuph Mehboob Manji hakuwapa.

Ulianza kuwaongopea wana Yanga SC kuhusu wale Wachezaji wenu wa Kikongo ukisema kuwa walikuwa ni Mali ya AS Vita na kwamba Umewanunua ila tunaojua 'Kufuatilia' mambo na 'Kuchimba' tukaenda mbele zaidi na Kugundua ya kwamba kuna Mmoja hapo hakuwa Mali kabisa ya AS Vita na mwingine aliachwa na kuwa 'Free Agent' na hata Yule Mama 'Boss' alikuambia hivyo.

Nikadhani utakuwa 'umekoma' na Kuacha 'Uwongo' wako ambapo tena muda si mrefu tu katika hali ya Kushangaza na Kusikitisha ukiwa Wasafi FM katika Kipindi chao cha Sports Arena umetoka Kuulizwa na Mtangazaji 'Mnafiki' na mwana Yanga SC mwenzio Yusuph Mkule kuwa Kocha wenu huyu mpya 'Myugoslavia' Zlatko Krmpotic anatokea Klabu gani umejibu kuwa anaokea Klabu ya Polokwane City ya Afrika Kusini wakati si kweli na kwamba 'alishafukuzwa' huko tangia tarehe 8 Novemba 2019 baada ya 'Kufungwa' Mechi tano mfululizo tokea 'Aajiriwe' tarehe 18 July 2019.

Nakutahadharisha mapema tu 'Injinia' Hersi Said nadhani huwajui vizuri wana Yanga SC ila Wewe endelea tu 'Kuwadanyanya' utawajua vyema.
 
Siku ambayo kigogo ataacha kuwadanganya matahira kama wewe ndiyo siku huyo tapeli wa Kihabeshi ataacha kuwadanganya wananchi.
 

Nyie mbumbumbu sc
Bichwa sc
Mikia sc
Mahirixi Sc
Kanjibay sc
Matopen sc
Inaonekana ingeneer Heris anawakosesha ucingiz!!! Tulieni hivyo hivyo msumar uingie

@@@ kwa hisani
Fundi Wa mpira
Kjsheti
Carlinhos
 
Kweni akidanganya shida iko wapi?
Ni utaratibu wa Tz kudanganya
Kama kadanganya hebu tupe uthibitisho kua tuisila na mukoko ni free agent.
 
Hata ile timu ya Burundi inatwa .....Noir wanadanganywa ni bingwa wa Burundi wakati amemaliza ligi nafasi ya 3. Ubingwa alitwaa msimu wa 2018/2019.
 
Nyie mbumbumbu sc
Bichwa sc
Mikia sc
Mahirixi Sc
Kanjibay sc
Matopen sc
Inaonekana ingeneer Heris anawakosesha ucingiz!!! Tulieni hivyo hivyo msumar uingie

@@@ kwa hisani
Fundi Wa mpira
Kjsheti
Carlinhos
Ila wakati mwingine uache kutetea ujinga, me mwenyewe leo nimemsikia akisema wamemtoa Polokwane na wa Maurid akauliza kwa kukazia kwamba wamevunja mkataba na jamaa akaitikia, jamaa amekuwa muongo muongo siku hizi
 
Gahrib yeye amemtuma Engineer kwenda Wasafi FM kuongea.

Bakhresa alimtuma Popat kwenda Clouds kuongea.

Mwamedi yeye alichukua kikundi cha uchambaji kikiongozwa na manara akabeba matarumbeta na wasanii akaenda nao Wasafi FM wakacheza vidole juu😂🤣
 

Siku zote Matajiri wanaotambulika Duniani kupitia Jarida maarufu kabisa la Forbes wote hawana Makuu wala mbwembwe wanachangamana na watu! Mtazame Bill Gate utaona kwa Nini Mo hana shida kuchangamana na watu!

Tukirudi kwa Matajiri Uchwala, mbwembwe huwa nyingii kama hao kina Gharib.Una jingine?
 
Huyu jamaa ni 'Muongo' sana anasema huyu kocha amewahi kuitumukia timu yake ya Taifa kwa kucheza match 400 [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Duniani haijawahi kutokea na wala haitatokea mchezaji kucheza match 400 katika timu ya Taifa. Kwenye vilabu sawa. Kwa ujumla huyu akiwa mchezaji alicheza match 8 tu katika timu ya Taifa lake.
Uongo mbaya sana.
Angalia hapa[emoji116]
 
Hata yule mlimbwende wa Angola alikuwa mchezaji huru baada ya kutokuongezewa mkataba na club yake.
 
Ila wakati mwingine uache kutetea ujinga, me mwenyewe leo nimemsikia akisema wamemtoa Polokwane na wa Maurid akauliza kwa kukazia kwamba wamevunja mkataba na jamaa akaitikia, jamaa amekuwa muongo muongo siku hizi
Ni rahisi sana kuwaongopea manyani ukiwarushia ndizi wanalegea.
 
Wahuni wakwepa kodi wa HSC hawa.
 

GENTAMYCINE nikiwa 'ninawasema' Yanga SC hapa Jamvini ( JamiiForums ) si huwa mnaniona 'Mzushi' na 'Nawachukia' tu? Sasa wanaumbuka!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…