Ha ha ha ha una matatizo wewe yaani ulinganishe hizo timu hapo na hiki kigumu cha machakani hakina hata uwanja, timu yake ya vijana kambi ni wanalala njaa na kulala chini!? Ndio yaleyale ya kusema sisi level zetu ni kugombania wachezaji na Al ahly, Mazembe, Kaizer chiefs halafu Bwalya tu mmekosa hela za kumpata. Hizo timu ulizotolea mfano hapo ni bahari na ardhi kwa simba. Tafuta bajeti yao kwa msimu na miundo mbinu walonayo halafu uje udanganye wenzako tena. Asee usiilinganishe simba na hizo timu tena! Simba ni klabu masikini kwa kila kitu yaani Management, Kifedha,Kiwango, ligi mbovu inayocheza n.k. Wanasimba hebu jitahidini kujitegemea katika kufikiri basi kuliko kuliko kumtegemea Haji Manara afikirie kwa niaba yenu eboo!