Injinia Soma hiyoo: Simba yasajili striker kutoka Brazil

Injinia Soma hiyoo: Simba yasajili striker kutoka Brazil

Mkuu shukran kwa upekuzi, tumepigwa,, nadhani hata Moe hajafurai hii kitu
Huyo jamaa labda hujamuona vizuri, yupo confortable on the ball, ana nguvu ana kasi, very skillful player na ana uwezo mkubwa sana wa kupunguza wachezaji. Mchezaji kama huyu atasaidia sana kuisumbua defense ya wapinzani kwa kasi yake. Akipartner na Kagere na Boko patakuwa patamu sana. He is an excellent player kama mtu anaujua mpira.
 

Huyu mchezaji ni mzuri sana tuvumilie tu
Wala huhitaji kumvumilia ni bonge la mchezaji, nitajie mchezaji Simba mwenye kasi kama yule na ambae yupo confortable anapokokota mpira kama huyu. Ana nguvu, anapunguza watu ile mbaya!! Very good player in my book, hongera Simba.
 
Watu wanacomplain tu,timu aliyotoka ndo ya kwanza kwenye msimamo,jamaa ukimwangilia YouTube anapiga magoli hata ya kichwa na mashuti
Sio mchezaji wa kikosi kinachoanza na 2018/19 kamaliza msimu Hana goli hata moja
Kazi ya straika Ni kufunga
 
KLABU ALIYOTOKA MCHEZAJI MPYA WA SIMBA
Mabingwa wa Tanzania na wanarobofainali wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC, kama kawaida wameshusha silaha nyingine muda ule ule wa siku zote.
Huyu ni Wilker Henrique da Silva kutoka Brazil. Lakini watu wengi wamechanganya kuhusu klabu anayotoka. Hapa chini ni ufafanuzi wake.
Da Silva ni mzaliwa wa mji wa Franca kwenye jimbo la Sao Paulo nchini Brazil. Alizaliwa Oktoba 26, 1995.
Amekuja Simba akitokea klabu Bragantino do Para, iliyopo kwenye mji wa Braganca ndani ya jimbo la Para, lililopo Kaskazini mwa Brazil, likipitiwa na mto maarufu wa Amazon.
Kwenye mji huu kuna timu mbili zinazotumia jina la mji wenyewe. Kuna Bragantino Clube do Pará ambayo ndiyo aliyotoka Da Silva. Kwa kifupi huitwa Bragantino PA.
Halafu kuna Clube Atletico Bragantino ambayo kwa kifupi huitwa C.A Bragantino.
BRAGANTINO YA DA SILVA
Klabu ya Da Silva, Bragantino Clube do Pará, inashiriki ligi daraja la nne ya Brazil ambayo hufahamika kama Campeonato Brasileiro Série D.
Pia inashiriki ligi kuu ya jimbo la Para inayoitwa Campeonato Paraense na katika msimu wa 2018 ilimaliza katika nafasi ya 3.
BRAGANTINO NYINGINE
Ile timu nyingine inayoitwa Clube Atletico Bragantino au kwa kifupi C.A Bragantino, inashiriki ligi daraja la pili inayoitwa Campeonato Brasileiro Série B.
Ilipanda mwaka 2018 kutoka ligi daraja la tatu inayoitwa Campeonato Brasileiro Série C ambako ilimaliza katika nafasi ya 4.
Hii ndiyo tofauti ya vilabu hivi viwili ambavyo vinatoka mji mmoja wa Braganca kwenye jimbo la Para nchini Brazil.
 
Nipo uwanjani naangalia mechi kati ya simba na Gwambina,kituko nnachokiona hapa kwamba wachezaji Wa simba wanaachiana shin guards. Yaani anayetoka anavua shin guards anampa anayeingia. Hivi hii si ni moja ya indicator ya umasikini?
 
Naskia brazil nzima imesimama kwa usajili wa huyu jamaa

Hongeren watan

Pogba atawafaa sana , naskia man u hawamtaki
 
Kule brazili mtoto wa kiume akizaliwa tu zawadi yake ya kwanza kupewa na baba ake ni njumu football boots.

Kule kila mtu anakipaji wote hawewezi kusajiliwa ulaya. Yani brazili kila kona mpira kama ilivyo bongo kila kona umbea.

Hongera simba kwa kujiongeza bila uwoga kwenda kusajili mpira ulipozaliwa
Jaja Square
 
Huyu mjinga ni hatari nanaona nafasi ya okwi imepata fundi
Kweli kabisa statistics zinajieleza
tapatalk_1561131664389.jpeg
 
View attachment 1133335

Jokes: Jamaa inasemekana ana uwezo wa kupiga chenga uwanja mzima
Umenikumbusha M-Brazil wa Yanga, aliyeitwa Jaja. Aliondoka bila kuaga.

Hakuna mchezaji wa Kibrazil anayeweza kupambania namba hapa Bongo. Kuwaacha Kotei na Niyonzima kwa Mbrazil ni sawa na kubeti kuwa Stars itabeba kombe la Afrika kule Misri.

Vv
 
Naona vyura. A.k.a wazee wa propaganda wako kimya maana simba ina wa washa washa sana.
 
Back
Top Bottom