FEBIANI BABUYA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 1,916
- 3,850
- Thread starter
-
- #221
Shukrani sana mkuu[emoji120]Ebwana hii story ni ya kimataifa na kama umeitunga wewe mwenyewe kwa akili zako basi wewe ni nyoko wa kimataifa katika utunzi, ukimpata mtu kama Jason Statham akakaa mbele ya kamera ikachezwa....[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]ebwanaeee[emoji119][emoji119] ni noma
Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
Gusa hapo chini chief[emoji116] kuna 46Sana, tupe vitu jomba
Shukrani mkuu[emoji120].....mwendelezo lini?STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 47
SONGA NAYO............
“Ule mpango siku ile ulipangwa kitoto sana Kwenda kutelekeleza lile tukio na naona dharau zinaweza kutufikisha sehemu mbaya sana, kwa sababu tulikuwa tunajua hii nchi wako nyuma sana kwenye suala la ulinzi lakini mwisho wa siku naona kama mambo yanaenda kuwa magumu sana kwa upande wetu sisi, nina imani ambaye alikuwa anarekodi siku ile alikuwa anajua mpango wetu kwa asilimia zote miamoja kwamba muda fulani tungekuwa pale sasa kwanini hakuweza kuzuia kama alijua hilo? Kumbuka wewe ulikuwa upo mbali sana na lile eneo maana yake kama alifanikiwa kuidaka sura yako basi alikuwa anakufuatilia kwa muda mrefu sana na huenda tangu tunaanza ule mpango wetu basi alikuwa anajua. Ule mchezo ambao tuliucheza pale na kumkamatisha yule bwana mdogo tukidhani kwamba ule mchezo ulikuwa umeishia pale bado haukufanya kitu cha maana chochote kile kwani kwani ukweli sio muda utawekwa hadharani” John Mwituka alikuwa akimpa maelekezo kijana wake huyo ndani ya hizo kuta kumi na tano
“Huyo binti ambaye unasema ni mwanasheria baada ya kumkamata yeye amesema amezipata wapi hizo video?”
“Sijaongea naye bado amehifadhiwa sehemu kwa sababu nilitingwa sana na ratiba za kanisani na sitakiwi kuweza kutiliwa mashaka na mtu yeyote yule kwenye mambo yangu yote ambayo nakuwa nayafanya hivyo pia nafanya mambo kwa tahadhari kubwa sana, vijana waliwahi Kwenda kumchukua na bahati nzuri hakukuwa na askari yeyote ambaye alikuwa amefika mpaka muda ule, wamepata frash na laptop ambayo ina hiyo video ambayo unaonekana wewe ukiwa na hiyo silaha kwa maana fupi video inathibitisha kwamba wewe ndiye muuaji mwenyewe na hilo kama lingefika kwenye vyombo vya usalama lingekuwa ni tatizo lingine kwa maana wangeanza kudadisi sana kwamba kama muuaji ni mtu mwingine na yule ambaye alinyongwa mahakamani ni nani? hilo lingekuwa tatizo kubwa sana kwa upande wetu kwa sasa hautakiwi kukaa huku tena maana haina umuhimu wowote ule wa kuendelea kukuficha kwa sasa unatakiwa uingie mtaani mwenyewe ndiye ukaifanye hii kazi kwa sababu siwaamini sana hawa vijana ambao tunawapa kazi”
“Kiongozi nadhani uliniambia kwamba kuna watu ambao umewapenyeza ndani ya idara ya usalama wa taifa wa nchi hii sasa inakuwaje mambo yanaendelea kuwa magumu na vijana wapo?”
“Hakuna kikubwa kinacho endelea huko mpaka inafika hatua mimi mwenyewe naanza kuwa na wasiwasi sana, huko hakuna tamko lolote wala hakuna kikao chochote kilicho kaliwa, vijana wapo huko lakini hata kiongozi wao hawamjui ila kila mtu anaingiziwa mshahara wake vizuri tu hata majukumu ya kazi hawapewi nadhani ni moja ya ishara mbaya sana ambayo tunapaswa kuwa nayo makini isivyo kawaida”
“Ni lini ninatakiwa kuingia mtaani na kazi yangu ya kwanza kuifanya itakuwa ni ipi?” aliuliza mwanaume huyo akiwa yupo tayari kupokea amri yoyote ile kutoka kwa kiongozi wake.
“Jina lako unaitwa Seven japo siyo jina lako kabisa la kuzaliwa, Patrick ndilo jina lako kabisa la kwenye vyeti vyako vya kuzaliwa, kuna sababu kubwa sana ya wewe kuitwa hilo jina la Seven tena kiubwa sana nakukumbusha ili unavyo enda kuyatenda haya mambo ukumbuke kwamba wewe ni nani na unapaswa kufanya nini maana sitegemei kuona makosa yoyote yale kutoka kwako hilo ulikumbuke vizuri sana”
“Baada ya vita kuu ya pili ya dunia inchi ya Marekani ilikuwa imepiga hatua kubwa sana ya kiuchumi na kusimikwa rasmi kama taifa lenye uchumi na nguvu kubwa zaidi duniani kwa sababu tu haikuathirika na janga la anguko la uchumi maana lilikuwa likiyakopesha mataifa mengine mikopo ya gharama kubwa sana na wakati wa kuilipa Marekani ilijikuta kwamba inajikusanyia akiba kubwa ambayo hakuna taifa lolote lile lingeweza kushindani nalo hapa duniani. Lakini taifa letu pendwa halikuweza kubweteka kwa sababu viongozi wa wakati ule walielewa kwamba kuna mataifa yataanza kuutamani ule uchumi hivyo fitina zitakuwa nyingi sana na kwani kila mtu atakuwa anataka atumie mgongo wa Marekani ili angalau kurudisha uchumi wake na hilo jambo lingekuwa ni la hatari sana kwa Marekani yenyewe kwa sababu kama kungekuwa na uzembe hata kidogo tu uchumi ungeenda kwa watu wengine na hapo ndipo taifa letu lilianza kujiimarisha sana kwenye mambo ya ulinzi na kutengeneza makomando na watu ambao walikuwa wana uwezo wa juu sana ili kuweza kulisaidia taifa kukusanya taarifa za siri za nchi mbali mbali kubwa duniani na kujua mipango mizima ya nchi hizo hususani kuihusu Marekani na ndipo hapo ulipo anzishwa mpango wa kila mwaka kumtengeneza the invisible man of the year kwa siri, huyu mtu alikuwa ni rasmi kwa ajili ya kutetea maslahi ya nchi kwa mtu yeyote yule ambaye angeonyesha nia ya kuweza kutaka kuzitolea macho mali zozote za Marekani”
“Walianza kutengenezwa watu tangu enzi hizo mpaka miaka ilivyokuwa inazidi kwenda na ukuaji wa teknolojia ukasaidia pakubwa sana kuzidi kutengeneza watu ambao waliokuwa wapo makini zaidi muda mwingine bora kuliko hata wale ambao walikuwa wapo mwanzo. Ilipofika mwaka 1991 lilitokea anguko kubwa sana la nchi za kisovieti na kuwafanya wayumbe sana kwa sababu umoja huo ndio ulikuwa tishio kubwa sana kwa nchi yetu, sasa kabla ya umoja huo kuvunjika ulitengenezwa mpango wa THE SEVEN PROCEDURES TO REACH MOSCOW, huo mpango ulianzishwa na serikali kwa ajili ya hatua saba ambazo zilitakiwa kufuatwa ili kuifikia Moscow sasa huko Moscow kulikuwa na kipi hasa mpaka utengenezwe mpango kama huo wa pesa nyingi sana?” mzee huyo aliuliza swali ambalo alitakiwa kulijibu yeye mwenyewe alipumzika kidogo akajiweka sawa na kuendelea kumpatia maelekezo kijana wake huyo ambaye alikuwa anataka kumfungulia ndani aingie huko uraiani akayatende yanayo takiwa kutendeka na yeye mwenyewe kwa mkono wake lakini kabla ya Kwenda huko alitaka kwanza kumpa somo ili kumkumbusha kwamba yeye alikuwa ni nani na mgongoni kwake alikuwa ameibeba bendera ya nchi ya Marekani ambayo pia alitakiwa sana kuiwakilisha vyema.
“Hizo hatua sita zilikuwa ni njia za kiusalama za kuweza kusambaza propaganda kuhusu umoja huo ili uvunjike maana ulikuwa una nguvu ya ushawishi kubwa sana duniani na kama ungeendelea kuwepo basi nchi yetu huenda ingepoteza ile nguvu yake ya kuwa taifa lenye nguvu zaidi ulimwenguni, sasa mpango wa hatua sita za propaganda hizo kama ungefeli iliwekwa opsheni ya mwisho ambayo alikuwa ni mtu aliyekuwa ameandaliwa ukiwa ni mwendelezo wa wale watu ambao walikuwa wanaandaliwa tangu vita ya pili ya dunia na mtu huyo ndiye alipewa namba 7 kwenye hayo machaguo hivyo akaitwa SEVEN sasa kwanini Seven?”
“Kuna namba kumi tu duniani japo kuna wengine huwa wanasema zipo tisa kwa sababu sifuri hawaihesabii ila sifuri ni namba kamili kabisa ubaya wake ikiwa nyuma ya namba nyingine haina madhara yoyote yale lakini pale inapokuwa mbele ya namba nyezake huongeza thamani kubwa sana nenda benki mtumie mtu pesa zidisha sifuri moja mbele utalia nakwambia, sasa kwenye hizo namba zote kumi namba ya bahati ni namba 7 hayo ndiyo maisha ya kweli namba saba siku zote ni namba ya bahati sana huenda ndiyo sababu hata mcheza mpira maarufu sana Cristiano Ronaldo amekuwa mtu mwenye hamasa kubwa zaidi duniani kwa sababu ya hiyo namba, sasa hiyo namba ndiyo alipewa mtu huyo akiwa kama ni chaguo la mwisho kama hizo hatua sita zitafeli. Zilianza kusambazwa propaganda nyingi sana kuhusu hayo mataifa na kitu ambacho nchi yetu ilikisambaza sana ni kuhusu kitu kinaitwa UTAIFA (nationalism) kwamba kila taifa ni huru na linapaswa kujitawala lenyewe maana kwa ule wakati walikuwa wanaishi kama taifa moja na walikuwa ndani ya chama kimoja cha Communist Party ambacho kilikuwepo huko Moscow na ndo hapo uliingia ule mpango wa SEVEN PROCEDURES TO REACH MOSCOW, huko ndiko kulikuwa na mizizi ya umoja huo hivyo tulitakiwa kusambaza propaganda hizo ili huko Moscow kusiwe na maelewano kila dola ianze kuhitaji uhuru wa kujitawala wenyewe, hizo njia sita zilifuatwa vizuri tu lakini hata SEVEN mwenyewe aliingizwa huko akiwa kama Mkimbizi kutoka ndani ya nchi ya Msumbiji na kwa sababu alikuwa ni mtu mweusi haikuwa tatizo sana baadae alionekana kama mkimbizi na kuanza kuishi huko huyo ndiye aliye ifanikisha hii oparesheni kwa asilimia 90 zile asilimia kumi tulizitumia kwenye propaganda”
“Aliweza kuvuna siri nyingi sana za wale watu, tulijua mipango yao kwamba wataanzia wapi na wataishia wapi hivyo sisi tulikuwa tunaingilia katikati na kuharibu kila kitu na hatimaye mnamo mwaka 1988 Estonia lilikuwa taifa la kwanza kujitoa kwenye umoja huo na kujitangaza kama taifa lililo huru, nchi moja moja kama Russia, Ukraine, Baltic republics na Georgia zikawa nazo zinahitaji kujitawala kwa kaulimbiu ya UTAIFA, rasmi mnamo mwaka 1991 umoja huo ukawa umevunjika na kila taifa likawa linajitawala lenyewe, hapo ukawa umebaki mchezo mdogo sana kuhakikisha kwamba Ukraine inaingizwa kwenye umoja wa nchi za Magharibi maana tungekuwa tumemuweka mfukoni Russia asingekuwa na jeuri hata kidogo na jambo hilo limezua utata sana mpaka leo. Miaka 12 baadae yule SEVEN mwenyewe baada ya kukamilisha jambo hilo alikuwa anajiandaa kutoroka kule lakini alikamatwa akiwa anakaribia kufika mpakani aliuawa kwa kunyongwa kule kule. Lile lilikuwa pigo kubwa sana kwa taifa kwa sababu ni mtu ambaye alikuwa amefanya kazi moja kubwa sana kuhakikisha taifa letu linapiga hatua kubwa kwenye kufanikisha jambo hilo”
“Kutokana na heshima yake ikaamuliwa kwamba vijana wengine ambao watakuwa wanatengenezwa hao ambao ni special kwa ajili ya hizo misheni basi watakuwa wanaitwa hilo jina lake ndiyo sababu baada ya wewe kukidhi hivyo vigezo ulipewa hilo jina la SEVEN kama kumuenzi mwenzako ambaye alikuwa amekutangulia sijajua kwanini role model wako ni mtu mwingine kabisa ambaye taifa lilikuwa linamtafuta sana, huo ni mwendelezo hata wewe siku ukifa basi atakuja SEVEN mwingine ni kama unavyo angalia zile movie za James Bond, akiondoka huyu basi anakuja mwingine sasa hiyo ni sawa na kwenu ninyi hapo. Nilikuwa nakukumbusha ili uelewe kwamba unacho enda kukifanya unatakiwa kukifanya kwa moyo wako wote kwa ajili ya kulilinda taifa lako ambalo wenzako hawakulala kwa ajili ya kuhakikisha kwamba lipo salama muda wote, kama utahitaji msaada wa aina yoyote ile vijana wapo wa kutosha kwahiyo muda wowote unaweza ukawatumia kwa namna yoyote ile mimi muda mwingi nitakuwa kanisani na kule hautakiwi kabisa kufika labda kama kutakuwa na jambo ambalo linakuwa nje ya uwezo wako na hauna msaada wowote ule mwingine" mzee huyo alimpa historia ya jina lake na kumkumbusha majukumu yake ya mhimu ambayo inatakiwa hata afe akiwa anayapigania alitakiwa kuiheshimu sana bendera ya taifa lake popote pale alipo maana ndiyo ilikuwa inatakiwa ailinde maisha yake yote mpaka siku anakufa.
“Nimekuelewa kiongozi, nasubiri amri yako” alisikiliza kwa umakini maelezo ya bosi wake na alikuwa yupo tayari kupokea amari ya bosi wake, alikuwa kama vile mashine ambayo ilikuwa imetengenezwa kwa ajili ya kazi maalumu na kwake kazi hiyo alikuwa tayari kuitumikia.
“Go and clear the city (Nenda na ukasafishe mji)” hilo ndilo neno ambalo lilitoka kwenye kinywa cha kiongozi wake, sasa rasmi alikuwa anaachiwa akalisafishe jiji la Dar
“As you ordered boss (Kama ulivyo amuru bosi)” alipewa amri na aliipokea kwa moyo wote sasa alikuwa anazama mtaani kwenda kudili na kila kilichokuwa kinaenda vibaya.
Mtaa unaenda kuwaje huyu mwanaume anatakiwa kulisafisha jiji kwa viashiria vyote ambavyo vingewafanya waingie sehemu mbaya na huko mtaani pia ameingia Jason, unahisi kunatokea nini huko?......47 sina la ziada inafika tamati naomba tukutane ndani ya sehemu ijayo.
Wasalaam
Bux the storyteller.
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Kesho mkuuShukrani mkuu[emoji120].....mwendelezo lini?
Kesho ndo leo ama kesho?[emoji851][emoji851]
Duh Jason keshaanza timbwili zake[emoji23][emoji23] mkuu FEBIANI BABUYA tuletee uhondo tena kwa heshima ya vyura na MAKOLO [emoji1787][emoji1787]STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 49
SONGA NAYO............
“Huyu mtoto umesema ni nani?” John Mwituka aliuliza akiwa anaiangalia vizuri hiyo picha ambayo ilikuwa kwenye simu, Jason akiwa anaonekana kwenye sura ya bashasha sana.
“Huyo ndiye ambaye anasemekana kuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa, vipi kiongozi mbona kama umeshtushwa sana na hiyo picha vipi unamjua huyo mtoto?” aliona kama mzee huyo hiyo picha anaifahamu ndiyo maana alikuwa anaingalia kwa umakini sana kana kwamba alikuwa anamjua mtu huyo vizuri sana.
“Hapana simjui ila nimeshangaa sana bwana mdogo sana kama huyu kupewa nafasi kubwa sana namna hii mbona kama hainiingilii akilini hata kidogo” alijibu ili kumzuga mkuu wa majeshi ila alikuwa ana uhakika kwamba huyo mtu haikuwa mara ya kwanza kumuona kwenye maisha yake japo siku ile wakati mwanae anamuonyesha hiyo picha kuna taarifa kwenye kichwa chake zilikuwa zinaonyesha kwamba aliwahi kumuona kama sio kukutana naye hapo nyuma kidogo. Alifikiria sana ilikuwa wapi mpaka akamuona kijana huyo, siku ambayo alikuwa amealikwa Ikulu kwa ajili ya kupongezwa kwa kazi nzuri sana ya uchungaji ambayo imetukuka kwa namna alivyokuwa amesaidia sana kuweza kutokomeza tabia za ajabu mtaani kwani watu walimwamini sana kiasi kwamba kuna watu walikuwa wapo tayari kuacha mambo ya ajabu na kuanza kusali kwenye kanisa lake.
Hiyo ndiyo siku ambayo alipishana na Jason akiwa anatoka ndani ya chumba cha mkutano ambacho mheshimiwa raisi alikuwa anaongea na kijana huyo, hapo sasa kumbukumbu zake aliamini kwamba hicho kitu kilikuwa sawa sawa na alivyokuwa anhisi japo kuhusu kijana huyo kuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa hio nalo lilikuwa geni sana kwa upande wake.
“Hata mimi nilikuwa najiuliza swali hilo hilo kama wewe kwa sababu mimi nilikuwa rafiki mkubwa sana wa Mark, raisi, IGP pamoja na mwenzetu mmoja ambaye alikuwa ameshakufa tayari sasa kutokuwa na taarifa za haya mambo zinaanza kunipa taarifa kwamba huenda hawa watu walisha nijua kama sio kutujua mapema sana na huenda wanatuwekea mtego ili tuzame moja kwa moja kisha ndipo waje wajitokeze hadharani”
“Achana na hayo mambo nipe taarifa za huyo kijana pamoja na kile kilichofanya mpaka leo ukataka kukutana namimi hapa” aliongea kwa sauti yake nzito ambayo ilimfanya mkuu wa majeshi aiweke sauti yake sawa ili amuelekeze alicho jia ikiwa ni pamoja na kumpa taarifa chache za Jason.
“IGP moja kwa moja amefanikiwa kujua kwamba mimi sipo upande wao yaani ni kwamba nawasaliti, siku ile nilituma meseji kumsisitiza Mark asifanye kile kitu ile simu IGP aliipata mapema na zile meseji zangu akazifuta kama kujaribu kunisaidia lakini hata hivyo inasemekana kwamba Jason anajua kwamba kuna meseji zilifutwa kwa sababu hata mimi alinitafuta na kunisihi kama nahusika basi niseme mapema ila mimi niligoma kabisa kuhusiana na tuhuma hizo”
“Yule bwana mdogo amekua na kuishi nikiwa namuona kuambiwa kwamba ni usalama wa taifa kwangu haikuniingia akilini ila baada ya kuona IGP anasisitiza sana niliamua kulichukulia hili jambo kwenye uzito wa hali ya juu sana”
“Kitu cha kwanza ambacho niliambiwa na sikutaka kukichukuliwa poa japo IGP kuna namna alinipa stori za uongo ni baada ya kuambiwa kwamba huyo bwana mdogo ana kundi lake moja la watu watano la hatari sana na mmoja wao alikuwa yupo pale NIT. Niliamua kulichukulia uzito na kuwatuma watu pale mchana wake walimkosa ila majira ya usiku walienda na kuuawa vibaya sana alipona mmoja ambaye alileta miili ya wenzake naye sikuona umuhimu wake wa kuendelea kuishi hivyo nikamuua”
“Kuja kwako leo naona kabisa mambo yameanza kuharibika nadhani kuna umuhimu kwanza wa kumjua huyu bwana mdogo ni nani kwenye upande wake wa pili ndipo tuweze kuangalia namna ya kuweza kumkamata, kwa sababu hatuwezi kumfuata mtu bila kujua kwamba yupoje na ni mtu gani ambaye anampa kiburi nyuma yake” alitulia na kuhema kwa nguvu sana baada ya kutoa hayo maelezo mbele ya John Mwituka.
“Mhhhhhh kwahiyo unataka nini kifanyike?”
“Najua mheshimiwa raisi wa sasa na IGP wana taarifa za yule mtu na wanaonekana wazi kwamba kuna mambo mengi sana ambayo wananificha, hivyo nahitaji kwanza tumpate IGP huyu lazima atatupatia taarifa zote ambazo zipo nyuma ya huyu mtoto” aliongea akiwa anasubiri mchungaji huyo aweze kuchangia chochote kuhusu hicho alichokuwa amekiongea.
“Huyo ni rafiki yako wewe kwanini unakuja kuniambia kwamba nimkamate wakati majibu ya nini kinatakiwa kufanyika unayo? kwanini usilifanye wewe mwenyewe hilo jukumu?” mkuu wa majeshi aliulizwa swali ambalo alikuwa na majibu yake kabisa.
“Mimi sitakiwi kabisa kujulikana kama nahusika na hayo mambo mapema sana namna hii, mimi nahitaji kwanza kuwa karibu na wale watu ili niendelee kujua kile ambacho kimepangwa ni kipi, kwahiyo nahitaji nyie ndo mmkamate huyu mtu kisha mmhoji”
“Utakuwa tayari kwa madhara ambayo yatatokea?”
“Ndiyo”
“Nipe kete ya mkono wake wa kulia”
“Ana watoto wawili ila ana binti yake mdogo huyu ndiye udhaifu wake mkubwa, anampenda sana huyu mtoto na yupo tayari kufanya chochote kwa ajili yake. Anasoma pale St Joseph hivyo mkimpata huyu basi mtu huyu atakuwa tayari kuwasikiliza kwa lolote lile na huyu ndiye ambaye anatakiwa kuja kuelezea historia nzima ya huyu kijana ili tujue kwamba tunadili na mtu wa aina gani”
Maelezo yake yalikuwa yamekamilisha mazungumzo yao
“Usinisumbue tena nitakutafuta mwenyewe nitakapo maliza kazi, unaweza Kwenda” John Mwituka alimjibu mtu huyo na kumhitaji aondoke maana hakutakiwa kukaa sana hilo eneo kitu ambacho kingeleta taharuki sana kama watu wangemuona.
Cosmas Laurien ndilo lilikuwa jina la mwanaume mmoja ambaye naye alizua taharuki kubwa sana ndani ya jiji la Dar es salaam. Huyu alikuwa ni miongoni mwa watu ambao walikuwa na biashara kubwa sana ndani ya jiji la Dar na utajiri wake ulikuwa umewafikia karibia watu wengi sana ndani ya hili jiji maana yake alikuwa akifahamika sana kwa biashara zake ambazo alikuwa anaziendesha ndani ya jiji hili. Kilichokuwa kimeleta taharuki kubwa sana siku hiyo majira ya jioni ikiwa ni siku moja tu tangu yasambazwe matangazo ya kuwapa wahusika wa mauaji ya jaji mkuu na raisi muda wa kuweza kujitokeza hadharani na kuomba msamaha, tajiri huyo alionekana akikimbilia kwenye midia moja kubwa sana kwa ajili ya kuomba msaada.
Midia hiyo ilikuwa inaendelea na matangazo yake ya moja kwa moja ndipo walipovamiwa na ugeni wa tajiri huyo ambaye getini alidai kwamba alikuwa amealikwa humo ndani na kwa vile walinzi walikuwa wakimjua vizuri hawakuwa na shaka naye sana walimruhusu japokuwa walikuwa na walakini sana kutokana na hali yake ilivyokuwa. Alikuwa amechakaa sana siku hiyo, nguo zake zilionekana kuu kuu sana huku akiwa amelowa damu kwenye maeneo ya mwili wake na miguuni akiwa peku anaendelea kutoa damu. Alikimbilia humo ndani na Kwenda kukaa kwenye sakafu akiwa anawaomba watu hao wasikatishe matangazo kwani alihitaji kuomba msaada na msamaha kwa ujumla maisha yake yalikuwa kwenye hatari kubwa sana hata kufika tu hapo ilikuwa ni bahati kubwa sana yeye kupona.
Watu wote ambao walikuwa wanaendesha matukio ya kipindi cha muda huo ambacho kilikuwa moja ya vipindi pendwa na vikubwa sana nchini kwa kutoa taarifa za uhakika walibaki wanamshangaa sana ikiwa ni pamoja na watazamaji ambao walikuwa wanatazama tukio hilo moja kwa moja.
“Mr Laurien umeingia hapa kwa namna ambayo siyo yenyewe na hata sisi huwa hatuingii tukiwa namna hiyo, kuna tatizo gani mpaka umesema kwamba unataka kuomba msamaha pamoja na kuomba msaada?" aliongea mama mmoja ambaye alikuwa ndiye kiongozi wa kipindi hicho huku akiwa anampatia mtu huyo maji ya baridi hapo chini ya sakafu alipokuwa amekaa. Aliyapokea maji hayo na kuyabugia kwa nguvu kiasi kwamba alikuwa na siku kadhaa ndani ya jangwa na alikuwa hajui kama atatoka salama kwenye hilo eneo.
“Ananiua,ananiua” aliongea na kuachia kikombe hicho huku akitazama nyuma yake sehemu ambayo ilikuwa na mlango.
“Nani anakuua?” mama huyo alitamka huku akiwa anawaangalia wenzake kwa mshangao na wote walikuwa kwenye mshangao mkubwa hivyo walibaki wanatazamana tu kila mtu akitamani kutoa neno lakini hawakujua ni neno gani sahihi la kulitoa kwa muda huo.
“Funga mlango, funga mlango tafadhali” alitamka akiwa ananyanyuka na kusogea mbele zaidi ambako kulikuwa ni mbali na mlango, hapo ndipo walipo shuhudia damu ya kutosha kwenye lile eneo ambalo alikuwa amekaa, walimtazama kwenye mwili wake na kugundua kwamba kwenye miguu yake yote vidole vyake vilikuwa vimekatwa kabisa na hakubahatika kubakishwa na kidole hata kimoja. Kila mmoja humo ndani alishtushwa sana na jambo hilo kwa sababu lilikuwa ni jambo la usalama hali ya mtu huyo haikuonekana kuwa nzuri ila alisisitiza sana wasiufungue mlango huo na mwisho akaangua kilio kikali sana.
“Kaka yangu naomba unisamehe sana, nimekukosea sana wewe na familia yako. Ni tamaa za mali zimeniponza ndugu yangu ila mimi sikuwahi kuwaza kuwa hivi, nipo tayari kurudisha kila kitu naomba uruhusu niishi kaka yule mtu ataniua kama nikiendelea kushikilia hizi mali zako kwa nguvu” aliongea akiwa analia sana huku wasiwasi mkali ukiwa ni sehemu ya mwili wake. Kwa maelezo yake huyu alikuwa ni moja kati ya ndugu wa baba yake na Nayrah au waweza kumwita Nurryat Hashim na hawa ndio wale ambao waliweza kumtapeli baba yake mali zake zote bila kujali kwamba mzee huyo aliwatoa mbali sana na kujitolea kuwasaidia kwa kila hali na kila alichokuwa nacho hakuwa mchoyo kuwachotea kiasi kikubwa ndugu zake lakini ndio hao hao ambao walikuwa wamemfanya kuwa na ulemavu wa akili mwanaume huyo, msaada wake mwenyewe ulimponza.
Kuna kipi kimemkuta mpaka anakuja yeye mwenyewe kuomba msaada kwenye vyombo vya habari na kumfanya aombe msamaha hadharani kwa kudai kwamba alihusika moja kwa moja kuwatapeli mali familia hiyo? Hata mimi sijui sana mgoja tuendelee kugusa taratibu.
49 naachia kalamu hapa tukutane wakati ujao.
Wasalaam
Bux the storyteller.View attachment 2696703
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
[emoji28][emoji28] mkuu huko mbele kunatisha sana [emoji91]. Baadae kidogo naileta hapa [emoji996]Duh Jason keshaanza timbwili zake[emoji23][emoji23] mkuu FEBIANI BABUYA tuletee uhondo tena kwa heshima ya vyura na MAKOLO [emoji1787][emoji1787]
Sent using Jamii Forums mobile app