Innocent Killer (The Revenge)

Innocent Killer (The Revenge)

Ebwana hii story ni ya kimataifa na kama umeitunga wewe mwenyewe kwa akili zako basi wewe ni nyoko wa kimataifa katika utunzi, ukimpata mtu kama Jason Statham akakaa mbele ya kamera ikachezwa....[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]ebwanaeee[emoji119][emoji119] ni noma

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
Shukrani sana mkuu[emoji120]

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 46

SONGA NAYO............
Monalisa baada ya kufika eneo ambalo alikuwa ana uhakika kwamba palikuwa ni kwa baba yake kama walivyokuwa wametambulishana, alijinyoosha wakati huo mlango huo ulifunguliwa na bodguard wa baba yake ndiye ambaye alikuwa amekuja kumpotea, Slyvester ndiye alikuwa hapo huyu alikuwa bodguard wa John Mwituka ambaye alikuwa mchungaji wa kanisa la WITH GOD YES, WE CAN. Makazi ya mheshimiwa mchungaji yalikuwa umbali wa kilomita tano tu kutoka eneo ambalo lilikuwepo hiko kanisa lake. Alikuwa amejenga majumba ya kifahari ambayo yalikuwa yamepangana ndani ya kuta moja nzito na gharama kubwa sana hapo ndipo ambapo Monalisa alikuwepo kwa huo muda.

Alishuka kwenye gari na kutabasamu baada ya kumuona Slyvester, wakakumbatiana kwa furaha sana, walionekana walikuwa wanajuana vizuri sana

“Welcome back the Queen of US, Tanzania is yours now”
“My pleasure baby boy” alitamka kwa mapozi huku akitembea kwa maringo kuelekea eneo ambalo ulikuwepo mlango wa kuingilia ndani ya geti hilo, Slyvester alitikisa kichwa kwa tabasamu, alikuwa akimpenda sana huyo mwanamke kuwa naye karibu alikuwa anajisikia amani sana, basi alichomoka kwa kasi na Kwenda kumfungulia geti malkia wao huyo na kuingia naye moja kwa moja ndani ya geti. John Mwituka alikuwa amenyoosha mikono yake akiwa anamsubiri mwanae huyo akamkumbatie

“Daddy, aliita kwa furaha sana akiwa anamkimbilia mzee huyo ambaye alikuwa kwenye suti safi sana, walikumbatiana kwa muda mrefu kidogo kisha wakaachiana”

“Enhe unazidi kukua tu unatakiwa uniletee mkwe kwa sasa nianze kucheza na wajukuu maana umri wangu unakimbia sana” mzee huyo aliongea kwa utani na kuwafanya wote wacheke sana huku wakiwa wanaelekea ndani, Slyvester aliishia hapo hapo aliishia kula kwa macho tu maana alikuwa akiteseka sana na hatu ambazo alikuwa anazipiga mwanamke huyo wakati anaingia ndani, suruali ambayo ilikuwa imembana sana ilimfanya sehemu zake za nyuma ambazo zilikuwa zimetuna sana kuruka ruka huku na huku na kumfanya kuonekana kama yule Cleopatra wa Misri mwanamke mrembo zaidi kuwahi kuumbwa kwenye huu ulimwengu kama sio kuzaliwa

“Mkweo amenikimbia kule kaja huku Tanzania bila hata kuniaga hivyo nataka nimtafute ili nikuletee wajukuu mpaka ukimbie mwenyewe” Monalisa aliongea kwa furaha sana akiwa anamaanisha Jason, aliongea uso wake ukionyesha furaha sana akiwa analitaja jina la mwanaume huyo ambayo halmashauri yote ya mwili wake ilikiri kwamba alikuwa akimpenda isivyo kawaida huyo mwanaume na kumfanya kuwa mwanaume halisi kabisa ambaye alizaliwa kwa ajili yake kwenye haya maisha ya hapa duniani na hakutamani kukutana na mtu mwingine kwenye maisha yake zaidi ya huyo Jason ambaye hakuwahi kumjua kiundani sana

“Huyo mwanaume hujawahi kuniambia ni nani?” mchungaji huyo aliongea huku akielekea kwenye friji na kutoa wine wakati huo mwanae akiwa amejibwaga kwenye sofa

“Utamuona tu hata usiwe na haraka dady”
“Mhhhhh una uhakika na huyo kijana na unahisi unamjua kiasi kwamba ukajihakikishia kwamba anaweza kuwa na wewe na usiwe kwenye hatari?”

“Daddy i can protect myself please don’t treat me as a poor helpless kid” alimjibu baba yake kwamba anaweza kujisaidia yeye mwenyewe hivyo baba yake asimchukulie kama mtoto ambaye hana uwezo wa kujimudu mwenyewe akiwa anapokea wine kwa mkono wake mmoja, mzee huyo aliishia tu kuguna bila kujibu chochote kile

“Nipe sababu ya kuja Tanzania ghafla hivi na nitajie huyo kiongozi gani ambaye amekupa ruhusa wewe ya kuja Tanzania” mzee huyo aliuliza akiwa anakaa upande wa pili wa sofa na kutazamana na binti yake.

“Dady hata sijapumzika ushaanza maswali kama kituo cha polisi aaaah” alikuwa akideka sana kwa baba yake hivyo kufuatiliwa sana aliona kama vile anaonewa

“Wewe ni mwanangu jukumu la kuhakikisha usalama wako lipo kwenye mkono wangu hivyo mimi ndiye ninapaswa kuwajibika kwako, unahisi kama kuna tatizo lolote lile likitokea upande wako nitalaumu nani? kwa sasa hali ya hapa haijatulia kwa sasa polisi na majeshi ya nchi pamoja na usalama wa taifa watasambazwa kila sehemu kuhakikisha wahusika wa hili tukio wanapatikana hivyo kosa hata la nukta moja tu unaweza ukakuta mtu anapoteza maisha au kuishia jela na kumwaga siri zote nje unahisi itakuwaje na kama wewe ukiingia kwenye matatizo nitamlaumu nani zaidi ya kujilaumu mimi mwenyewe”

“Baba, mimi ninaweza kujilinda mwenyewe tafadhali nadhani hilo unalijua vizuri”
“Sijasema hauwezi kujilinda ila kumbuka kwamba wewe bado ni wa kike hivyo bado ni dhaifu hata kama una uhatari kiasi gani hivyo nataka nipate majibu ya maswali yangu ili twende sawa”

“Baba hakuna aliye nipa hiyo ruhusa mimi nilifanya vile ili nipate ruhusa yako kuja au haukunimisi?” aliongea kwa kudeka sana ila mzee huyo alikuwa amemkazia sana uso wake

“Nipe hizo sababu zilizo kufanya ukaja ghafla sana ndani ya nchi hii” aliongea kwa sauti nzito akiwa siriasi sana na sura yake ilibadilika
“Nimekuja kumtafuta huyo mtu” mchungaji huyo aliinamisha kichwa chake na kusikitika sana
“Naomba picha yake” Monalisa alisita sana ila alitoa simu yake na kuitafuta picha ambayo yeye alikuwa na Jason, mzee huyo aliitazama picha hiyo kama mtu ambaye anajaribu kufumba macho yake ili kukumbuka jambo, kwake sura hiyo haikuwa ngeni sana ila alijaribu sana kukumbuka juu ya kuwahi kuonana na mtu huyo ila alishindwa kabisa kumkumbuka.

“Anatokea kwenye familia gani na anafanya kazi gani?” aliuliza na kumshtua sana binti yake
“Baba”
“Hakuna cha baba nijibu maswali yangu siwezi kuacha binti yangu akaenda sehemu ambayo siyo lazima nijue mwanangu anaelekea wapi na anaenda kuishi maisha gani lakini pia hilo lisikusahaulishe sana kwamba wewe ni nani na itanisikitisha sana kama utasahau kuhusu nchi yako kwa sababu ya mwanaume na mapenzi, umekula kiapo kwa ajili ya nchi yako na kumbuka hatupo hapa kuuza sura tupo hapa kwa sababu ya kazi maalumu hivyo hilo unatakiwa uliweke kwenye kichwa chako” maneno ya baba yake ni kama yalimuingia vizuri sana yeye kama jasusi wa Marekani hakutakiwa kutanguliza mapenzi mbele kwenye sehemu ambayo anatakiwa kuyatetea maslahi ya taifa lake.

“Mimi sijawahi kumjua sana baba, nilikutana naye ndani ya chuo cha Havard ndipo tukaanza ukaribu na kwa sababu mimi nilikuwa mpweke sana kule nilijikuta naanza kumzoea na kumpenda, nilimfuatilia sana ili japo nipate taarifa zake hata kidogo ilikuwa ni ngumu sana sijawahi kupata chochote zaidi tu ya kuniambia kwamba yeye anatokea ndani ya taifa la Tanzania. kuna siku ambayo nilikuwa naye tukiwa pembezoni mwa bustani ya chuoni iliingia simu kwenye simu yake kutoka Tanzania kaka yake akiwa anahitaji msaada kwamba anauawa na alikuwa anamtaka mdogo wake akamsaidie, hapo niliona amechanganyikiwa sana nilijaribu kumuuliza shida nini aliniambia tu kwamba nyumbani kuna matatizo anatakiwa Kuja haraka sana. hakuweza hata kuniaga maana aliondoka akiwa anakimbia basi nami nikaanza kumfuata taratibu nyuma, safari yake ilienda kuishia kwenye ofisi ya moja ya maprofessor wa pale chuo”

“Nilikaa pale na kusubiri kwa masaa manne lakini sikuona mtu akitoka pale kwenye ile ofisi mpaka baadae sana nilipo muona yule professor anatoka mle ofisini nikahisi wataongozana lakini cha ajabu alipafunga akiwa mwenyewe, ikabidi nimkimbilie ili nimuulize mpenzi wangu yuko wapi alinambia tu kwamba amesafiri kurudi Tanzania sasa nikawa namuuliza alitokaje pake wakati sijamuona akitoka maana yule ni mpenzi wangu hivyo natakiwa kujua usalama wake, jibu alilo nipa ni kwamba alikuwa anawahi nyumbani basi akawa ameondoka”

“Kuanzia pale nilikuwa nina wasiwasi naye sana nikajipa kazi nyingine ya kuanza kumfuatilia yeye ili kama kuna tatizo niweze kujua kwamba kuna kitu gani ambacho nilikuwa ninafichwa pale maana haikuwa hali yan kawaida na ukizingatia mpenzi wangu alikuwa hapatikani kabisa, basi kwenye kuchunguza chunguza kwangu nikaja kujua sehemu ambayo anaishi yule professor nikawa nimejipanga usiku wa kuamkia leo nimfuate ili niweze kumbana aniambie kuna mambo gani ambayo ananificha mimi au alisha muua mpenzi wangu kwani kama angekuwa hai ningempata hewani kama siyo yeye kunitafuta maana tulikuwa tunapendana sana lakini kitu cha ajabu mimi wakati nimevamia pale ambapo nilikuwa nina uhakika kwamba ni nyumbani kwake mmiliki wa ile nyumba nilimkuta akiwa nje ananisubiri na alikuwa akijua kabisa kwamba mimi nipo pale. Nilijaribu kutaka kumpiga ila nilicho kutana nacho kimenitisha sana maana alitokea kijana mmoja ambaye sikubahtika kumuona sura yake alinipiga kama mtoto mdogo na kuniambia kwamba kama asingekuwa ananijua basi angeniua pale pale, niliambiwa niondoke na nisije kurudi tena ile sehemu kwani pale ni nyumbani kwa Dr Morgan na huyo professor hata wao hawamjui”

“Sikutaka kukubali hilo jambo liishe kirahisi sana namna hiyo hivyo nikawatafuta wenzangu na kuwapa maelekezo kwamba waende ile sehemu na wahakikishe kwamba wanamteka yule Dr Morgan huenda kuna jambo nyuma yake lakini kitu cha ajabu wamefika pale pale kwenye nyumba ile ile wakadai kwamba pale ni nyumbani kwa askari wa Marekani na ana familia yake kabisa kwenye lile eneo, nilibisha sana hilo jambo mpaka pale walipo nitumia video ndipo nikaamini ila nimebaki nimechanganyikiwa kwamba haya mambo yanawezekana vipi? Hivyo kwa sababu nilikuwa nina mpango tayari wa kuja Tanzania basi nikaamua kuondoka na kuamua kuachana na hilo jambo kwa muda kisha nitaendelea nalo nitakapo rudi ndani ya Marekani. Sababu za kuja hapa Tanzania kubwa ni mbili, ya kwanza ni kumtafuta huyo mwanaume lakini jambo la pili ni kutoa msaada kwenye hili Sakata linalo endelea kwa sababu nina uwezo wa kuingia popote pale inapo hitajika na hakuna mwanaume anaweza kutoka kwenye mkono wangu hivyo kama kuna mtu tunamhitaji au kuna mambo ya siri tunahitaji kuyapata hususani kwa wakati huu ambao tunatakiwa kuyasaficha mambo yote ambayo yanaweza kuleta shida nitatoa msaada” stori yake ilimuacha baba yake kwenye mshangao mkubwa sana kwani mwanae alikuwa aneonyesha uzembe mkubwa sana agenti wa CIA anaingia kwenye mapenzi kizembe sana na mwanaume ambaye hayajui hata maisha yake ya nyuma yapoje na anatokea kwenye familia ya aina gani, aliona kulikuwa kuna shida kubwa sana.

“Kwa sasa enda kapumzike mimi nitarudi kesho ndipo tutaanza kulifanyia kazi swali lako hilo, naondoka hapa nitarudi keshi jioni kwa sababu baadae nina ibada ndefu nitarudi usiku sana na nitalala saa moja tu kisha kesho mapema sana natakiwa kuwa makao makuu sijaenda muda kidogo sijui namna kazi zinavyokwenda kule lakini pia nataka nikakutane na Seven”

“Whaaaat seven yupo Tanzania?”
“Yeye ndiye ambaye alikuwa amewekwa kwenye mpango wa kukamilisha hii kazi na kumaliza tatizo lolote lile ambalo lingeweza kujitokeza wakati kazi hii inafanyika” alijibu mzee huyo akiwa anasimama kuhitaji kuondoka humo ndani.

“No tutaenda wote baba”
“Wapi?”
“Makao makuu”
“Hapana sio kwa kesho”
“Kwanini”
“Seven nadhani unajua jinsi anavyo kupenda kama akijua wewe upo Tanzania basi tutaharibu kila kitu kwa sababu hataweza kufanya kazi kwa uhuru hivyo inatakiwa ukae naye mbali maana wewe mwenyewe ulishawahi kumwambia unampenda kama rafiki tu na huwezi kuwa naye kama mumeo hivyo hakuna haja ya kukutana naye kwa sasa” maneno ya mzee huyo yalimfanya aondoke hapo sebuleni kwa hasira sana na kuelekea juu ghorofani, kuna maswali mengi sana ambayo alikuwa anahitaji kumuuliza mwanaume huyo kwani ni muda mrefu sana alionekana kuto mtia kwenye macho yake lakini majukumu ya kazi yalikuwa hayamruhusu kabisa mrembo huyo kuweza kumuona mwanaume huyo.

Mchungaji alitoka mpaka nje na kumuita Slyvester karibu yake
“Naomba umfuatilie kwa umakini mwanangu kila hatua anayo ipiga na hakikisha hakuna tatizo lolote lile linalo mkuta, mimi naondoka naenda kanisani lakini sitarudi kabisa hapa japo yeye nimemwambia nitarudi usiku, naweza kurudi kesho jioni hivyo hakikisha anakuwa salama, usimwamini sana kumuacha peke yake yule bado ni mwanamke anaweza kuwa na uwezo sana wa kujilinda lakini bado kuna udhaifu huwa wanawake huwa wanakuwa nao hasa kwa mtu au kitu anacho kipenda na hicho kinaweza kuleta matatizo makubwa sana huyo ndiye niliye naye kwenye huu ulimwengu hivyo ni mara mia upoteze hata mkono wako lakini sio kuruhusu binti yangu kupata tatizo lolote lile” alimaliza kutoa maagizo akiwa anaelekea kwenye gari siku hiyo hakutaka kuongozana na mtu yeyote yule, kijana wake huyo alibaki ameinamisha kichwa kutoa heshima kwa bosi wake mpaka pale alipotoka nje ya geti la nyumba hiyo.

46 naweka nukta hapa.
Wasalaam

Bux the storyteller.
1689346560558.jpg

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Huu mzigo tarehe 20 mwezi huu tutakuwa nao hadi mwisho.

Ipo ukurasa wa 80 kwa sasa kwa vipande vya kawaida hivyo tarehe 20 softcopy yake inakuwa tayari na vipande vyake vitakuwa tayari mpaka mwisho.

Usiikose hii simulizi ni [emoji91]

Na kama ulibahatika kuisoma ULIMWENGU WA WATU WABAYA basi tunaongea lugha moja na unanielewa namaanisha nini kuhusu hili andiko.

Bei yake itakuwa ni shilingi 5000 tu pekee za kitanzania, yaani elfu moja moja tano tu.......

Nitakupatia utangulizi wake uiguse ambapo imehusisha nchi ya Tanzania na Rwanda.

Baada ya watu wasio julikana kulipua bunge la nchi ya Tanzania ambapo watu 198 walikufa na ikasadikika kwamba wahusika walifanikiwa kukimbilia nchini Rwanda kupitia mpango ulio itwa OPERATION REACHING RWANDA.

Anatumwa jasusi mmoja huko na kuyagundua mambo ya kutisha sana ambayo ndiyo yanatufanya tuutumie muda wetu kuisoma DOCUMENT namba 72....

Jasusi huyo wa kike anakamatwa na kubakwa na wanaume kumi huku akiwa ababakwa na wanaume watano kila baada yaa siku mbili.

Kubakwa kwa mwanamke huyo kunatupa nafasi ya kumjua mwanaume ambaye ndiye atatueleza kinaga ubaga kwamba ni nani alimvesha paka kengele.......ni hatari sana.

Kwanini iitwe DOCUMENT namba 72? Ina nini ndani yake? Basi huo ndio unakuwa mwanzo wa wewe kuzifunua kurasa ili kuujua uhalisia wa mengi yaliyo jificha.

WhatsApp yangu ni 0621567672

Haya ndiyo tunaenda kuyafunua

Kalamu ni ya yangu mwenyewe [emoji996]

Langu jina naitwa FEBIANI BABUYA

Wao wanapenda kuniita.......Bux the storyteller.

Chao.View attachment 2689692
FB_IMG_1687153087384.jpg

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 47

SONGA NAYO............

“Ule mpango siku ile ulipangwa kitoto sana Kwenda kutelekeleza lile tukio na naona dharau zinaweza kutufikisha sehemu mbaya sana, kwa sababu tulikuwa tunajua hii nchi wako nyuma sana kwenye suala la ulinzi lakini mwisho wa siku naona kama mambo yanaenda kuwa magumu sana kwa upande wetu sisi, nina imani ambaye alikuwa anarekodi siku ile alikuwa anajua mpango wetu kwa asilimia zote miamoja kwamba muda fulani tungekuwa pale sasa kwanini hakuweza kuzuia kama alijua hilo? Kumbuka wewe ulikuwa upo mbali sana na lile eneo maana yake kama alifanikiwa kuidaka sura yako basi alikuwa anakufuatilia kwa muda mrefu sana na huenda tangu tunaanza ule mpango wetu basi alikuwa anajua. Ule mchezo ambao tuliucheza pale na kumkamatisha yule bwana mdogo tukidhani kwamba ule mchezo ulikuwa umeishia pale bado haukufanya kitu cha maana chochote kile kwani kwani ukweli sio muda utawekwa hadharani” John Mwituka alikuwa akimpa maelekezo kijana wake huyo ndani ya hizo kuta kumi na tano

“Huyo binti ambaye unasema ni mwanasheria baada ya kumkamata yeye amesema amezipata wapi hizo video?”

“Sijaongea naye bado amehifadhiwa sehemu kwa sababu nilitingwa sana na ratiba za kanisani na sitakiwi kuweza kutiliwa mashaka na mtu yeyote yule kwenye mambo yangu yote ambayo nakuwa nayafanya hivyo pia nafanya mambo kwa tahadhari kubwa sana, vijana waliwahi Kwenda kumchukua na bahati nzuri hakukuwa na askari yeyote ambaye alikuwa amefika mpaka muda ule, wamepata frash na laptop ambayo ina hiyo video ambayo unaonekana wewe ukiwa na hiyo silaha kwa maana fupi video inathibitisha kwamba wewe ndiye muuaji mwenyewe na hilo kama lingefika kwenye vyombo vya usalama lingekuwa ni tatizo lingine kwa maana wangeanza kudadisi sana kwamba kama muuaji ni mtu mwingine na yule ambaye alinyongwa mahakamani ni nani? hilo lingekuwa tatizo kubwa sana kwa upande wetu kwa sasa hautakiwi kukaa huku tena maana haina umuhimu wowote ule wa kuendelea kukuficha kwa sasa unatakiwa uingie mtaani mwenyewe ndiye ukaifanye hii kazi kwa sababu siwaamini sana hawa vijana ambao tunawapa kazi”

“Kiongozi nadhani uliniambia kwamba kuna watu ambao umewapenyeza ndani ya idara ya usalama wa taifa wa nchi hii sasa inakuwaje mambo yanaendelea kuwa magumu na vijana wapo?”

“Hakuna kikubwa kinacho endelea huko mpaka inafika hatua mimi mwenyewe naanza kuwa na wasiwasi sana, huko hakuna tamko lolote wala hakuna kikao chochote kilicho kaliwa, vijana wapo huko lakini hata kiongozi wao hawamjui ila kila mtu anaingiziwa mshahara wake vizuri tu hata majukumu ya kazi hawapewi nadhani ni moja ya ishara mbaya sana ambayo tunapaswa kuwa nayo makini isivyo kawaida”

“Ni lini ninatakiwa kuingia mtaani na kazi yangu ya kwanza kuifanya itakuwa ni ipi?” aliuliza mwanaume huyo akiwa yupo tayari kupokea amri yoyote ile kutoka kwa kiongozi wake.

“Jina lako unaitwa Seven japo siyo jina lako kabisa la kuzaliwa, Patrick ndilo jina lako kabisa la kwenye vyeti vyako vya kuzaliwa, kuna sababu kubwa sana ya wewe kuitwa hilo jina la Seven tena kiubwa sana nakukumbusha ili unavyo enda kuyatenda haya mambo ukumbuke kwamba wewe ni nani na unapaswa kufanya nini maana sitegemei kuona makosa yoyote yale kutoka kwako hilo ulikumbuke vizuri sana”

“Baada ya vita kuu ya pili ya dunia inchi ya Marekani ilikuwa imepiga hatua kubwa sana ya kiuchumi na kusimikwa rasmi kama taifa lenye uchumi na nguvu kubwa zaidi duniani kwa sababu tu haikuathirika na janga la anguko la uchumi maana lilikuwa likiyakopesha mataifa mengine mikopo ya gharama kubwa sana na wakati wa kuilipa Marekani ilijikuta kwamba inajikusanyia akiba kubwa ambayo hakuna taifa lolote lile lingeweza kushindani nalo hapa duniani. Lakini taifa letu pendwa halikuweza kubweteka kwa sababu viongozi wa wakati ule walielewa kwamba kuna mataifa yataanza kuutamani ule uchumi hivyo fitina zitakuwa nyingi sana na kwani kila mtu atakuwa anataka atumie mgongo wa Marekani ili angalau kurudisha uchumi wake na hilo jambo lingekuwa ni la hatari sana kwa Marekani yenyewe kwa sababu kama kungekuwa na uzembe hata kidogo tu uchumi ungeenda kwa watu wengine na hapo ndipo taifa letu lilianza kujiimarisha sana kwenye mambo ya ulinzi na kutengeneza makomando na watu ambao walikuwa wana uwezo wa juu sana ili kuweza kulisaidia taifa kukusanya taarifa za siri za nchi mbali mbali kubwa duniani na kujua mipango mizima ya nchi hizo hususani kuihusu Marekani na ndipo hapo ulipo anzishwa mpango wa kila mwaka kumtengeneza the invisible man of the year kwa siri, huyu mtu alikuwa ni rasmi kwa ajili ya kutetea maslahi ya nchi kwa mtu yeyote yule ambaye angeonyesha nia ya kuweza kutaka kuzitolea macho mali zozote za Marekani”

“Walianza kutengenezwa watu tangu enzi hizo mpaka miaka ilivyokuwa inazidi kwenda na ukuaji wa teknolojia ukasaidia pakubwa sana kuzidi kutengeneza watu ambao waliokuwa wapo makini zaidi muda mwingine bora kuliko hata wale ambao walikuwa wapo mwanzo. Ilipofika mwaka 1991 lilitokea anguko kubwa sana la nchi za kisovieti na kuwafanya wayumbe sana kwa sababu umoja huo ndio ulikuwa tishio kubwa sana kwa nchi yetu, sasa kabla ya umoja huo kuvunjika ulitengenezwa mpango wa THE SEVEN PROCEDURES TO REACH MOSCOW, huo mpango ulianzishwa na serikali kwa ajili ya hatua saba ambazo zilitakiwa kufuatwa ili kuifikia Moscow sasa huko Moscow kulikuwa na kipi hasa mpaka utengenezwe mpango kama huo wa pesa nyingi sana?” mzee huyo aliuliza swali ambalo alitakiwa kulijibu yeye mwenyewe alipumzika kidogo akajiweka sawa na kuendelea kumpatia maelekezo kijana wake huyo ambaye alikuwa anataka kumfungulia ndani aingie huko uraiani akayatende yanayo takiwa kutendeka na yeye mwenyewe kwa mkono wake lakini kabla ya Kwenda huko alitaka kwanza kumpa somo ili kumkumbusha kwamba yeye alikuwa ni nani na mgongoni kwake alikuwa ameibeba bendera ya nchi ya Marekani ambayo pia alitakiwa sana kuiwakilisha vyema.

“Hizo hatua sita zilikuwa ni njia za kiusalama za kuweza kusambaza propaganda kuhusu umoja huo ili uvunjike maana ulikuwa una nguvu ya ushawishi kubwa sana duniani na kama ungeendelea kuwepo basi nchi yetu huenda ingepoteza ile nguvu yake ya kuwa taifa lenye nguvu zaidi ulimwenguni, sasa mpango wa hatua sita za propaganda hizo kama ungefeli iliwekwa opsheni ya mwisho ambayo alikuwa ni mtu aliyekuwa ameandaliwa ukiwa ni mwendelezo wa wale watu ambao walikuwa wanaandaliwa tangu vita ya pili ya dunia na mtu huyo ndiye alipewa namba 7 kwenye hayo machaguo hivyo akaitwa SEVEN sasa kwanini Seven?”

“Kuna namba kumi tu duniani japo kuna wengine huwa wanasema zipo tisa kwa sababu sifuri hawaihesabii ila sifuri ni namba kamili kabisa ubaya wake ikiwa nyuma ya namba nyingine haina madhara yoyote yale lakini pale inapokuwa mbele ya namba nyezake huongeza thamani kubwa sana nenda benki mtumie mtu pesa zidisha sifuri moja mbele utalia nakwambia, sasa kwenye hizo namba zote kumi namba ya bahati ni namba 7 hayo ndiyo maisha ya kweli namba saba siku zote ni namba ya bahati sana huenda ndiyo sababu hata mcheza mpira maarufu sana Cristiano Ronaldo amekuwa mtu mwenye hamasa kubwa zaidi duniani kwa sababu ya hiyo namba, sasa hiyo namba ndiyo alipewa mtu huyo akiwa kama ni chaguo la mwisho kama hizo hatua sita zitafeli. Zilianza kusambazwa propaganda nyingi sana kuhusu hayo mataifa na kitu ambacho nchi yetu ilikisambaza sana ni kuhusu kitu kinaitwa UTAIFA (nationalism) kwamba kila taifa ni huru na linapaswa kujitawala lenyewe maana kwa ule wakati walikuwa wanaishi kama taifa moja na walikuwa ndani ya chama kimoja cha Communist Party ambacho kilikuwepo huko Moscow na ndo hapo uliingia ule mpango wa SEVEN PROCEDURES TO REACH MOSCOW, huko ndiko kulikuwa na mizizi ya umoja huo hivyo tulitakiwa kusambaza propaganda hizo ili huko Moscow kusiwe na maelewano kila dola ianze kuhitaji uhuru wa kujitawala wenyewe, hizo njia sita zilifuatwa vizuri tu lakini hata SEVEN mwenyewe aliingizwa huko akiwa kama Mkimbizi kutoka ndani ya nchi ya Msumbiji na kwa sababu alikuwa ni mtu mweusi haikuwa tatizo sana baadae alionekana kama mkimbizi na kuanza kuishi huko huyo ndiye aliye ifanikisha hii oparesheni kwa asilimia 90 zile asilimia kumi tulizitumia kwenye propaganda”

“Aliweza kuvuna siri nyingi sana za wale watu, tulijua mipango yao kwamba wataanzia wapi na wataishia wapi hivyo sisi tulikuwa tunaingilia katikati na kuharibu kila kitu na hatimaye mnamo mwaka 1988 Estonia lilikuwa taifa la kwanza kujitoa kwenye umoja huo na kujitangaza kama taifa lililo huru, nchi moja moja kama Russia, Ukraine, Baltic republics na Georgia zikawa nazo zinahitaji kujitawala kwa kaulimbiu ya UTAIFA, rasmi mnamo mwaka 1991 umoja huo ukawa umevunjika na kila taifa likawa linajitawala lenyewe, hapo ukawa umebaki mchezo mdogo sana kuhakikisha kwamba Ukraine inaingizwa kwenye umoja wa nchi za Magharibi maana tungekuwa tumemuweka mfukoni Russia asingekuwa na jeuri hata kidogo na jambo hilo limezua utata sana mpaka leo. Miaka 12 baadae yule SEVEN mwenyewe baada ya kukamilisha jambo hilo alikuwa anajiandaa kutoroka kule lakini alikamatwa akiwa anakaribia kufika mpakani aliuawa kwa kunyongwa kule kule. Lile lilikuwa pigo kubwa sana kwa taifa kwa sababu ni mtu ambaye alikuwa amefanya kazi moja kubwa sana kuhakikisha taifa letu linapiga hatua kubwa kwenye kufanikisha jambo hilo”

“Kutokana na heshima yake ikaamuliwa kwamba vijana wengine ambao watakuwa wanatengenezwa hao ambao ni special kwa ajili ya hizo misheni basi watakuwa wanaitwa hilo jina lake ndiyo sababu baada ya wewe kukidhi hivyo vigezo ulipewa hilo jina la SEVEN kama kumuenzi mwenzako ambaye alikuwa amekutangulia sijajua kwanini role model wako ni mtu mwingine kabisa ambaye taifa lilikuwa linamtafuta sana, huo ni mwendelezo hata wewe siku ukifa basi atakuja SEVEN mwingine ni kama unavyo angalia zile movie za James Bond, akiondoka huyu basi anakuja mwingine sasa hiyo ni sawa na kwenu ninyi hapo. Nilikuwa nakukumbusha ili uelewe kwamba unacho enda kukifanya unatakiwa kukifanya kwa moyo wako wote kwa ajili ya kulilinda taifa lako ambalo wenzako hawakulala kwa ajili ya kuhakikisha kwamba lipo salama muda wote, kama utahitaji msaada wa aina yoyote ile vijana wapo wa kutosha kwahiyo muda wowote unaweza ukawatumia kwa namna yoyote ile mimi muda mwingi nitakuwa kanisani na kule hautakiwi kabisa kufika labda kama kutakuwa na jambo ambalo linakuwa nje ya uwezo wako na hauna msaada wowote ule mwingine" mzee huyo alimpa historia ya jina lake na kumkumbusha majukumu yake ya mhimu ambayo inatakiwa hata afe akiwa anayapigania alitakiwa kuiheshimu sana bendera ya taifa lake popote pale alipo maana ndiyo ilikuwa inatakiwa ailinde maisha yake yote mpaka siku anakufa.

“Nimekuelewa kiongozi, nasubiri amri yako” alisikiliza kwa umakini maelezo ya bosi wake na alikuwa yupo tayari kupokea amari ya bosi wake, alikuwa kama vile mashine ambayo ilikuwa imetengenezwa kwa ajili ya kazi maalumu na kwake kazi hiyo alikuwa tayari kuitumikia.

“Go and clear the city (Nenda na ukasafishe mji)” hilo ndilo neno ambalo lilitoka kwenye kinywa cha kiongozi wake, sasa rasmi alikuwa anaachiwa akalisafishe jiji la Dar

“As you ordered boss (Kama ulivyo amuru bosi)” alipewa amri na aliipokea kwa moyo wote sasa alikuwa anazama mtaani kwenda kudili na kila kilichokuwa kinaenda vibaya.

Mtaa unaenda kuwaje huyu mwanaume anatakiwa kulisafisha jiji kwa viashiria vyote ambavyo vingewafanya waingie sehemu mbaya na huko mtaani pia ameingia Jason, unahisi kunatokea nini huko?......47 sina la ziada inafika tamati naomba tukutane ndani ya sehemu ijayo.

Shukrani mkuu[emoji120].....mwendelezo lini?
 
Hello,

Habari ya wewe?

Ni matumaini yangu kwamba u mzima wa afya kabisa.

Napenda kukutaarifu kwamba ile simulizi yetu ambayo tumeisubiri kwa hamu sana kwa muda mrefu ya DOCUMENT namba 72 , sasa inapatikana yote mpaka mwisho ambapo unaweza ukachagua kama unahitaji kutumiwa kwa mfumo wa Softcopy yaani pdf au vipande vya kawaida.

Bei yake ni shilingi 5000.

Unaweza kutuma kupitia namba

0621567672. HALOTEL

0745982347. MPESA

jina FEBIANI BABUYA.

Wasalaam.
FB_IMG_1687153087384.jpg

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 49

SONGA NAYO............

“Huyu mtoto umesema ni nani?” John Mwituka aliuliza akiwa anaiangalia vizuri hiyo picha ambayo ilikuwa kwenye simu, Jason akiwa anaonekana kwenye sura ya bashasha sana.
“Huyo ndiye ambaye anasemekana kuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa, vipi kiongozi mbona kama umeshtushwa sana na hiyo picha vipi unamjua huyo mtoto?” aliona kama mzee huyo hiyo picha anaifahamu ndiyo maana alikuwa anaingalia kwa umakini sana kana kwamba alikuwa anamjua mtu huyo vizuri sana.

“Hapana simjui ila nimeshangaa sana bwana mdogo sana kama huyu kupewa nafasi kubwa sana namna hii mbona kama hainiingilii akilini hata kidogo” alijibu ili kumzuga mkuu wa majeshi ila alikuwa ana uhakika kwamba huyo mtu haikuwa mara ya kwanza kumuona kwenye maisha yake japo siku ile wakati mwanae anamuonyesha hiyo picha kuna taarifa kwenye kichwa chake zilikuwa zinaonyesha kwamba aliwahi kumuona kama sio kukutana naye hapo nyuma kidogo. Alifikiria sana ilikuwa wapi mpaka akamuona kijana huyo, siku ambayo alikuwa amealikwa Ikulu kwa ajili ya kupongezwa kwa kazi nzuri sana ya uchungaji ambayo imetukuka kwa namna alivyokuwa amesaidia sana kuweza kutokomeza tabia za ajabu mtaani kwani watu walimwamini sana kiasi kwamba kuna watu walikuwa wapo tayari kuacha mambo ya ajabu na kuanza kusali kwenye kanisa lake.

Hiyo ndiyo siku ambayo alipishana na Jason akiwa anatoka ndani ya chumba cha mkutano ambacho mheshimiwa raisi alikuwa anaongea na kijana huyo, hapo sasa kumbukumbu zake aliamini kwamba hicho kitu kilikuwa sawa sawa na alivyokuwa anhisi japo kuhusu kijana huyo kuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa hio nalo lilikuwa geni sana kwa upande wake.

“Hata mimi nilikuwa najiuliza swali hilo hilo kama wewe kwa sababu mimi nilikuwa rafiki mkubwa sana wa Mark, raisi, IGP pamoja na mwenzetu mmoja ambaye alikuwa ameshakufa tayari sasa kutokuwa na taarifa za haya mambo zinaanza kunipa taarifa kwamba huenda hawa watu walisha nijua kama sio kutujua mapema sana na huenda wanatuwekea mtego ili tuzame moja kwa moja kisha ndipo waje wajitokeze hadharani”

“Achana na hayo mambo nipe taarifa za huyo kijana pamoja na kile kilichofanya mpaka leo ukataka kukutana namimi hapa” aliongea kwa sauti yake nzito ambayo ilimfanya mkuu wa majeshi aiweke sauti yake sawa ili amuelekeze alicho jia ikiwa ni pamoja na kumpa taarifa chache za Jason.

“IGP moja kwa moja amefanikiwa kujua kwamba mimi sipo upande wao yaani ni kwamba nawasaliti, siku ile nilituma meseji kumsisitiza Mark asifanye kile kitu ile simu IGP aliipata mapema na zile meseji zangu akazifuta kama kujaribu kunisaidia lakini hata hivyo inasemekana kwamba Jason anajua kwamba kuna meseji zilifutwa kwa sababu hata mimi alinitafuta na kunisihi kama nahusika basi niseme mapema ila mimi niligoma kabisa kuhusiana na tuhuma hizo”

“Yule bwana mdogo amekua na kuishi nikiwa namuona kuambiwa kwamba ni usalama wa taifa kwangu haikuniingia akilini ila baada ya kuona IGP anasisitiza sana niliamua kulichukulia hili jambo kwenye uzito wa hali ya juu sana”
“Kitu cha kwanza ambacho niliambiwa na sikutaka kukichukuliwa poa japo IGP kuna namna alinipa stori za uongo ni baada ya kuambiwa kwamba huyo bwana mdogo ana kundi lake moja la watu watano la hatari sana na mmoja wao alikuwa yupo pale NIT. Niliamua kulichukulia uzito na kuwatuma watu pale mchana wake walimkosa ila majira ya usiku walienda na kuuawa vibaya sana alipona mmoja ambaye alileta miili ya wenzake naye sikuona umuhimu wake wa kuendelea kuishi hivyo nikamuua”

“Kuja kwako leo naona kabisa mambo yameanza kuharibika nadhani kuna umuhimu kwanza wa kumjua huyu bwana mdogo ni nani kwenye upande wake wa pili ndipo tuweze kuangalia namna ya kuweza kumkamata, kwa sababu hatuwezi kumfuata mtu bila kujua kwamba yupoje na ni mtu gani ambaye anampa kiburi nyuma yake” alitulia na kuhema kwa nguvu sana baada ya kutoa hayo maelezo mbele ya John Mwituka.

“Mhhhhhh kwahiyo unataka nini kifanyike?”
“Najua mheshimiwa raisi wa sasa na IGP wana taarifa za yule mtu na wanaonekana wazi kwamba kuna mambo mengi sana ambayo wananificha, hivyo nahitaji kwanza tumpate IGP huyu lazima atatupatia taarifa zote ambazo zipo nyuma ya huyu mtoto” aliongea akiwa anasubiri mchungaji huyo aweze kuchangia chochote kuhusu hicho alichokuwa amekiongea.

“Huyo ni rafiki yako wewe kwanini unakuja kuniambia kwamba nimkamate wakati majibu ya nini kinatakiwa kufanyika unayo? kwanini usilifanye wewe mwenyewe hilo jukumu?” mkuu wa majeshi aliulizwa swali ambalo alikuwa na majibu yake kabisa.
“Mimi sitakiwi kabisa kujulikana kama nahusika na hayo mambo mapema sana namna hii, mimi nahitaji kwanza kuwa karibu na wale watu ili niendelee kujua kile ambacho kimepangwa ni kipi, kwahiyo nahitaji nyie ndo mmkamate huyu mtu kisha mmhoji”

“Utakuwa tayari kwa madhara ambayo yatatokea?”
“Ndiyo”
“Nipe kete ya mkono wake wa kulia”
“Ana watoto wawili ila ana binti yake mdogo huyu ndiye udhaifu wake mkubwa, anampenda sana huyu mtoto na yupo tayari kufanya chochote kwa ajili yake. Anasoma pale St Joseph hivyo mkimpata huyu basi mtu huyu atakuwa tayari kuwasikiliza kwa lolote lile na huyu ndiye ambaye anatakiwa kuja kuelezea historia nzima ya huyu kijana ili tujue kwamba tunadili na mtu wa aina gani”
Maelezo yake yalikuwa yamekamilisha mazungumzo yao
“Usinisumbue tena nitakutafuta mwenyewe nitakapo maliza kazi, unaweza Kwenda” John Mwituka alimjibu mtu huyo na kumhitaji aondoke maana hakutakiwa kukaa sana hilo eneo kitu ambacho kingeleta taharuki sana kama watu wangemuona.

Cosmas Laurien ndilo lilikuwa jina la mwanaume mmoja ambaye naye alizua taharuki kubwa sana ndani ya jiji la Dar es salaam. Huyu alikuwa ni miongoni mwa watu ambao walikuwa na biashara kubwa sana ndani ya jiji la Dar na utajiri wake ulikuwa umewafikia karibia watu wengi sana ndani ya hili jiji maana yake alikuwa akifahamika sana kwa biashara zake ambazo alikuwa anaziendesha ndani ya jiji hili. Kilichokuwa kimeleta taharuki kubwa sana siku hiyo majira ya jioni ikiwa ni siku moja tu tangu yasambazwe matangazo ya kuwapa wahusika wa mauaji ya jaji mkuu na raisi muda wa kuweza kujitokeza hadharani na kuomba msamaha, tajiri huyo alionekana akikimbilia kwenye midia moja kubwa sana kwa ajili ya kuomba msaada.

Midia hiyo ilikuwa inaendelea na matangazo yake ya moja kwa moja ndipo walipovamiwa na ugeni wa tajiri huyo ambaye getini alidai kwamba alikuwa amealikwa humo ndani na kwa vile walinzi walikuwa wakimjua vizuri hawakuwa na shaka naye sana walimruhusu japokuwa walikuwa na walakini sana kutokana na hali yake ilivyokuwa. Alikuwa amechakaa sana siku hiyo, nguo zake zilionekana kuu kuu sana huku akiwa amelowa damu kwenye maeneo ya mwili wake na miguuni akiwa peku anaendelea kutoa damu. Alikimbilia humo ndani na Kwenda kukaa kwenye sakafu akiwa anawaomba watu hao wasikatishe matangazo kwani alihitaji kuomba msaada na msamaha kwa ujumla maisha yake yalikuwa kwenye hatari kubwa sana hata kufika tu hapo ilikuwa ni bahati kubwa sana yeye kupona.

Watu wote ambao walikuwa wanaendesha matukio ya kipindi cha muda huo ambacho kilikuwa moja ya vipindi pendwa na vikubwa sana nchini kwa kutoa taarifa za uhakika walibaki wanamshangaa sana ikiwa ni pamoja na watazamaji ambao walikuwa wanatazama tukio hilo moja kwa moja.

“Mr Laurien umeingia hapa kwa namna ambayo siyo yenyewe na hata sisi huwa hatuingii tukiwa namna hiyo, kuna tatizo gani mpaka umesema kwamba unataka kuomba msamaha pamoja na kuomba msaada?" aliongea mama mmoja ambaye alikuwa ndiye kiongozi wa kipindi hicho huku akiwa anampatia mtu huyo maji ya baridi hapo chini ya sakafu alipokuwa amekaa. Aliyapokea maji hayo na kuyabugia kwa nguvu kiasi kwamba alikuwa na siku kadhaa ndani ya jangwa na alikuwa hajui kama atatoka salama kwenye hilo eneo.

“Ananiua,ananiua” aliongea na kuachia kikombe hicho huku akitazama nyuma yake sehemu ambayo ilikuwa na mlango.
“Nani anakuua?” mama huyo alitamka huku akiwa anawaangalia wenzake kwa mshangao na wote walikuwa kwenye mshangao mkubwa hivyo walibaki wanatazamana tu kila mtu akitamani kutoa neno lakini hawakujua ni neno gani sahihi la kulitoa kwa muda huo.

“Funga mlango, funga mlango tafadhali” alitamka akiwa ananyanyuka na kusogea mbele zaidi ambako kulikuwa ni mbali na mlango, hapo ndipo walipo shuhudia damu ya kutosha kwenye lile eneo ambalo alikuwa amekaa, walimtazama kwenye mwili wake na kugundua kwamba kwenye miguu yake yote vidole vyake vilikuwa vimekatwa kabisa na hakubahatika kubakishwa na kidole hata kimoja. Kila mmoja humo ndani alishtushwa sana na jambo hilo kwa sababu lilikuwa ni jambo la usalama hali ya mtu huyo haikuonekana kuwa nzuri ila alisisitiza sana wasiufungue mlango huo na mwisho akaangua kilio kikali sana.

“Kaka yangu naomba unisamehe sana, nimekukosea sana wewe na familia yako. Ni tamaa za mali zimeniponza ndugu yangu ila mimi sikuwahi kuwaza kuwa hivi, nipo tayari kurudisha kila kitu naomba uruhusu niishi kaka yule mtu ataniua kama nikiendelea kushikilia hizi mali zako kwa nguvu” aliongea akiwa analia sana huku wasiwasi mkali ukiwa ni sehemu ya mwili wake. Kwa maelezo yake huyu alikuwa ni moja kati ya ndugu wa baba yake na Nayrah au waweza kumwita Nurryat Hashim na hawa ndio wale ambao waliweza kumtapeli baba yake mali zake zote bila kujali kwamba mzee huyo aliwatoa mbali sana na kujitolea kuwasaidia kwa kila hali na kila alichokuwa nacho hakuwa mchoyo kuwachotea kiasi kikubwa ndugu zake lakini ndio hao hao ambao walikuwa wamemfanya kuwa na ulemavu wa akili mwanaume huyo, msaada wake mwenyewe ulimponza.

Kuna kipi kimemkuta mpaka anakuja yeye mwenyewe kuomba msaada kwenye vyombo vya habari na kumfanya aombe msamaha hadharani kwa kudai kwamba alihusika moja kwa moja kuwatapeli mali familia hiyo? Hata mimi sijui sana mgoja tuendelee kugusa taratibu.

49 naachia kalamu hapa tukutane wakati ujao.

Wasalaam

Bux the storyteller.View attachment 2696703

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Duh Jason keshaanza timbwili zake[emoji23][emoji23] mkuu FEBIANI BABUYA tuletee uhondo tena kwa heshima ya vyura na MAKOLO [emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari, natumai mpo salama kabisa.

Simulizi yetu ya MUUAJI ASIYE NA HATIA (KISASI) au waweza kuiita INNOCENT KILLER (THE REVENGE). Licha ya kuwa na ubora wa hali ya juu kwenye matukio yake na mpangilio wake lakini pia ni moja ya simulizi zenye urefu wa kujitosheleza.

Ina kurasa 135. Hivyo wakati unasubiria baadae kidogo nishushe ukurasa wa 50, kwa sasa unaweza kuisoma yote kuanzia ulipo ishia ukurasa wa 49 mpaka ukurasa wa mwisho kabisa wa 135 kwa shilingi 3000 tu.

Ukilipia 3000 unachagua kama unataka kumalizia kuanzia ulipo ishia au kama unata pdf yenye simulizi nzima basi nakupatia unabaki nayo kama kumbukumbu kwenye maisha yako.

Namba za kulipia

0621567672 (WhatsApp)........HALOTEL

0745982347 ......... MPESA

Zote jina ni FEBIANI BABUYA.

Kwa pamoja tuendelee kuburudika na kuyafurahia maandishi [emoji996].

FEBIANI BABUYA.
1690259235063.jpg

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
STORY: DOCUMENT namba 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 1.

Chumba kilichokuwa na mwanga hafifu, kikitawaliwa na kiza kinene ndipo ilipokuwa hofu ya moyo wake.

Hakuwa akiogopa kuhusu kufa kwake au kupoteza kwake maisha, lahasha! bali alikuwa anaogopa kushuhudia yale matukio ambayo yalikuwa yamatokea ndani ya hicho chumba.

Mwanga wa blue ambao ulikuwa unamulika kwa mbali, ulimfanya asitamani muda mwingi kuweza kuyafungua macho yake, kwa maana yalikuwa yanamuuma. Chumba hakikuwa rafiki sana kwa mwanadamu kuishi na huenda haikutakiwa kabisa kukaliwa na mtu kwa muda mrefu kwa namna kilivyokuwa kimechakaa. Huenda kwa mtu mwenye maisha ya chini angekitumia kama nyumbani kwake ila kwa mtu mwenye maisha yake hakikustahili kuishi kabisa.

Kwenye kiti kimoja ambacho kilikuwa kimekunjwa lakini kuna muda kilikuwa kinaweza kukunjuliwa na kikalazwa kama kitanda na mtu akapumzika hapo, alikuwa amefungwa mtu mmoja ambaye bila shaka licha ya kile kiza lakini alionekana kuwa ni mwanamke ambaye usoni kwake nywele zilikuwa zimejaa sana. Ilionyesha kwamba ni muda mrefu kidogo tangu kichwa chake hicho kiweze kufanyiwa usafi kama sio nywele kuoshwa vizuri.

Pembeni kidogo ya ile sehemu ambayo mwanamke huyo alikuwa amefungwa kwenye kiti, palikuwa na kitanda ambacho kilikuwa ni kisafi mno na kilionekana kwa mbali kwa jinsi mashuka yake yalivyokuwa yaking'aa kwa ule mwanga hafifu wa blue ambao ulikuwa unamulika humo ndani. Sehemu ya mbele yake kwa juu, sehemu ambayo ilikuwa na TV ndogo ya zamani, maana ilikuwa na tumbo kwa nyuma, palionekana kuwa na mpauko mkubwa sana isivyokuwa kawaida, rangi kuu kuu iliyo banduka banduka ukutani ilionekana kwa mbali.

Tv hiyo ilikuwa inaendelea kupiga kelele lakini mwanamke huyo ambaye alikuwa humo ndani, alikuwa ameinamisha kichwa chake chini. TV hiyo haikuwa na faraja yoyote mwake zaidi ya kumuongezea maumivu makali kwenye nafsi yake, kilichokuwa kinasikika kwenye TV hiyo ni miguno tu ya watu wakiwa wanafanya mapenzi, ilizidi kumpa hasira sana kwenye moyo wake akajikuta anadondosha chozi lisilokuwa na thamani gizani.

Hicho chumba kwake hakikuwa kigeni kabisa kwani alikuwa ana muda mrefu sana tangu aanze kuishi humo ndani hivyo hata bila kiza mazingira hayo alikuwa anayajua vizuri sana. Chozi lake lilikuwa linamshuka kwa sababu alikuwa anajua kile ambacho kilikuwa kinaenda kumkuta kwa muda mchache ujao. Mlio wa TV hiyo na miguno ya mahaba ilikuwa inawekwa kwa sababu maalumu ambayo ilikuwa inamuuma sana kwenye nafsi yake huku ikimpelekea majuto makubwa sana ya yeye kuingia kwenye mikono ya hao watu ambao walimfanya aishie ndani ya hicho chumba alicho kuwepo kwa wakati huo.

Alikuwa anatamani ni bora hata angejiua au angeuliwa lakini sio kwa unyama ambao alikuwa anakutana nao hapo ndani, hivyo hakuwa na namna ya kulizuia chozi lisilo na mkingaji wa kulipooza kwa wakati huo ambapo hakujua kama nje ni usiku au mchana japo kwa ndani kulikuwa na kiza totoro.

Hakupewa nafasi ya kuweza kujidhuru ama kutoka kwenye mikono ya watu hao ambao walikuwa wamemuhifadhi hiyo sehemu. Akiwa anatoa chozi la uchungu, mlango wa hiyo sehemu ulifunguliwa na taa nyeupe zikawashwa, alichukua dakika nzima mpaka kufungua macho yake ili kuangalia nani aliyekuwa ameingia.

Aliye ingia humo ndani, alikuwa ni mwanamke mmoja ambaye asili yake ilikuwa ni ya Rwanda, alikuwa ni mwanmke mrembo sana. Alionekana kuwa mwenyeji wa hilo eneo ndiyo maana hakusita hata kufanya shughuli ambazo zilimleta hapo baada tu ya kuingia. Mwanga uliowashwa ulisaidia kuweza kukimulika vyema chumba hicho ambacho hakikuwa na ubora wowote ule.

Chumba cha zamani sana ambacho kilichoka, rangi ilikuwa imechubuka mno kiasi kwamba kikapoteza mvuto wa mtu mwenye afya salama kuishi, kilionekana vyema. Upande wa kushoto kulikuwa na mlango ambao bila shaka ulikuwa wa uani japo ulifungwa kwa komeo iliyo choka, licha ya kuwa na ubaya ulio kithiri lakini, chumba hicho kilikuwa kimepambwa na kitanda cha gharama isivyokuwa kawaida.
Kitanda kilicho nakshiwa na mashuka ya gharama bila kusahau friji la bei ghali ambalo liliwekwa mkabala na pembe moja ya kitanda lilileta maswali mengi sana juu ya siri iliyopo kwenye hicho chumba. Mwanamke ambaye alikuwa ameingia wakati huo, mkononi mwake alikuwa ana vifaa vya kuogea, vipodozi kiasi pamoja na beseni kubwa lenye maji huku akiwa amevaa bikini tu pekee kwenye mwili wake.

Alimwangalia mwanamke mwenzake kwa umakini sana, hakueleweka kama alikuwa anamuonea huruma au alikuwa anamsanifu. Aliinama na kulowanisha taulo dogo kwenye maji na wakati huo yule mwanamke ambaye alikuwa amefungwa pale kwenye kitu aliinua uso wake na kumtazama mwenzake ambaye alikuwa hapo chumbani kwa ajili yake, huku naye kwenye mwili wake akiwa na bikini tu pekee ila kuinua kwake sura alionyesha moja kwa moja kwamba ni mtanzania.
"Sorry do you speak swahili? ( samahani unaongea kiswahili?" yule mwanamke ambaye alikuwa kwenye kiti alimuuliza mrembo huyo ambaye alikuwa na taulo mkononi huku akiwa ameanza kumfuta kwenye uso wake. Alimwangalia sana kabla ya kumjibu.
"Yes, I'm not native but somehow i try cuz i once lived in Tanzania back in days (ndiyo mimi sio mzawa ila naongea kwa kiasi chake maana niliwahi kuishi Tanzania huko nyuma)" jibu lake lilionyesha kwamba anajua kuongea japo sio sana maana aliwahi kuishi Tanzania kwa miaka kadhaa huko nyuma.
"Unaweza kuniambia lolote kuhusu Tanzania?" Alimuuliza kwa kiswahili baada ya kuonekana kwamba anakiweza.
"Unajua nyi watu mko na janja janja sana ndicho nilicho jifunza about Tanzania" alijibu kuonyesha kwamba hakuwa anakijua sana kila neno kuongea japo alikuwa anaelewa kila kitu. Mwanamke huyo ambaye alifungwa kwenye kiti alitoa tabasamu hafifu kwani kilichokuwa kimezungumzwa, ni ukweli mtupu. Watanzania wanaogopeka kwa maneno maneno na ujanja mwingi sana mdomoni.

"Hii sehemu mimi ndiye wa kwanza kufanyiwa hivi na kuletwa?"
"Hapana, watu mingi sana waliwahi kuletwa kama wewe ila janja zao zinawafanya kufa haraka"
"Wanaweza kuwa wangapi ambao waliwahi kuletwa hapa?"
"Sijui, tangu anze mimi kuja, watu mingi kama kumi meona wakikuja kwa hapa"
"Huwa huwaonei huruma wanawake wenzako kifanyiwa huu ukatili?"
"Onea wapi huruma watu wengine? Wewe lini onea huruma mimi navyofanywa mbele yako? Ishi maisha ya wewe, acha kufuatilia yangu mimi" alijibu kwa hasira sana akiona kama mwenzake anataka mazoea ambayo yeye hakuyapenda kabisa. Alimkanda kanda na kumfuta uchafu ambao ilikuwa kwenye mwili wake na kumpaka vipodozi.
Baada ya kumaliza,alisogea na kuufungua ule mlango wa uani na kwenda kumwaga maji aliyokuwa akimsafishia mwenzake. Alirudi na kwenda kujilaza kitandani huku akivua nguo zote, dakika kama tatu zilipita akaingia mwanaume mmoja mwenye kitambi akiwa kifua wazi na kipensi kifupi, mkononi mwake alikuwa ameshika sigara yake akiivuta taratibu. Ni bwana mmoja mfupi lakini kibonge, hakuwa na wasiwasi, utulivu na nuru ilikuwa sawa machoni pake, huenda ni kwa sababu ya maisha kama siyo mamlaka aliyokuwa nayo juu ya hiyo sehemu ambayo alikuwepo kwa wakati huo.

Alisogea mpaka pale kwenye kiti na kumbusu yule mwanamke ambaye alikuwa amefungwa kisha akaenda mpaka kitandani na kuvua kipensi chake, akaanza kufanya mapenzi kwa fujo sana na yule dada wa kinyarwanda mpaka alipo fika safari yake. Mwanamke yule wa kinyarwanda aliinuka na kuanza kumnyonya sehemu za siri tena mwanaume huyo ambaye baada ya dakika tano alimvamia yule mwanamke wa kwenye kiti ambaye mpaka wakati huo alikuwa akitoa machozi.

Aliichana ile bikini na kukilaza kile kiti kisha akawa anambaka kwa nguvu bila huruma mpaka pale alipo tosheka akasimama, yule dada wa kinyarwanda alimsogelea mwanaume yule na kuanza kunyonyana naye midomo yake mpaka walipo tosheka, bwana yule mfupi akavaa kipensi chake na kumsogelea yule mwanamke wa kwenye kiti baada ya kukiinua akiwa bado yupo uchi.

"Tina" mwaaume huyo aliita kwa dharau huku akicheka.
"Mara ya kwanza tu nakuona, nilijua kuna kitu hakipo sawa, mwanamke mrembo kama wewe huwezi kumpenda mwaaume mfupi kama mimi, huo ni uongo na najua hilo. Nilishangaa siku ile ukisema kwamba unanipenda sana mimi na unataka nikuoe niwe na wewe kama mke wangu, nilishangaa sana kwa maana nilijua mrembo kama wewe kuna wanaume wengi sana wenye maisha yao mazuri hata zaidi yangu wangetamani wakuite mke"
"Kwanini mimi? Hahahahah kumbe ulikuwa na malengo yako kuniweka kwenye mtego? Bibie umefanya moja kati ya kosa ambalo litayagharimu maisha yako na mwili wako kwa ujumla mpaka akili yako. Umejiingiza kwenye upelelezi wa vitu ambavyo haujui hata madhara yake wala kujua historia yake ya kweli ipoje"

"Ulitakiwa kwanza kujua kwamba;.. kwanini haya mambo yanatokea! Kwanini hawa watu waaishi hivi na ni nani ambaye yupo nyuma ya maisha haya ambayo sisi tunayaishi?. Unajua kwanini nilikimbia Tanzania? Unajua maisha yamekuwaje mpaka nipo hapa na haya maisha mazuri ambayo unaniona nayo?"

"Pengine kiongozi wako alikutuma bila kukwambia yaliyopo nyuma ya makaratasi au alikutuma makusudi ili ufe, na kitu kibaya na cha kushangaza wanakutumaje mtoto mzuri kama wewe? Umeletwa ili ufe? Sasa mimi nataka nikuhakikishie kwamba wewe hautakufa kirahisi sana namna hii kama unavyo dhani, nitahakikisha kwamba unakufa huku ukijuta na ukitamani hata kujiua mwenyewe ila hautakuja kupata hiyo nafasi kabisa hususani ya kuishi kwa furaha tena" Bwana huyo aliongea kwa msisitizo akihitaji kueleweka kwa mwanamke huyo ambaye hakujulikana amemkosea nini.

"Kesho ratiba inaendelea kama kawaida ila mimi sina ratiba na mwili wako, nikijisikia tu nakuja, ndiyo maana hata kondomu situmii ila hao wanaokuja kesho lazima watumie kondomu maana vinginevyo nawaua mwenyewe kwa mkono wangu"
"This is Rwanda not beautiful Tanzania. Hahahahah" Mwanaume huyo alicheka sana huku akiwa anatoka ndani ya hicho chumba akiongozana na yule dada wa kirwanda huku mlango ukifungwa na rangi zikibadilishwa na kubakia kama zile za mwanzo.

Kuna kipi kimemkuta mwanamke huyu Tina? Yeye ni nani na alikuwa akiwapeleleza hao wanaume kwa sababu zipi? Na ni kiongozi wake yupi huyo aliye mtuma huko? Huyo mwanaume anadai alikimbia Tanzania kwa kipi?....nini sababu ya wao kuwepo Rwanda?

Maswali ni mengi sana ila ndiyo kwanza tunaufungua ukurasa wa kwanza kabisa wa simulizi yetu safi ya DOCUMENT namba 72. Twende pamoja tuweze kujibiwa maswali yetu.

Hii ni moja kati ya simulizi bora sana ya kipelelezi utakayo isoma kwenye maisha yako.

Kalamu ni yangu mwenyewe,

FEBIANI BABUYA.
JamiiForums-351824967.jpg

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom