Innocent Killer (The Revenge)

Innocent Killer (The Revenge)

Mpangilio wa matukio, wahusika upo vizuri.. Hongera kwako mtunzi.
 
STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 35

SONGA NAYO............
“Elimu ndiyo msingi wa maisha ya mwanadamu hata kabla ya kuletewa hii elimu ya kisasa ya kwenye nadharia na kujaza madaftari kwenye vichwa vyetu lakini bado tulikuwa na elimu yetu ya vitendo hata kabla ya ujio wa hawa wakoloni hivyo hakuna ulazima wa kuipata tu elimu ya darasani ili useme umeelimika unaweza kuipata elimu tu ambayo inaendana na mazingira uliyopo ili uweze kustaarabika, bahati iliyokuwa njema mimi nimezipata elimu zote ndiyo maana sihangaiki sana na elimu dunia wala elimu ya darasani hivyo mpaka mimi nakaa kuzungumza nawewe jambo huwa ni mtu ambaye ninaweza kufikiria mara tano mbele madhara ya kile ambacho ninakiongea na athari zake zitakuwaje na mpaka mheshimiwa kakuagiza uje hapa ina maana mpaka yeye ananiamini sana juu ya hilo sasa kama mkuu wa nchi ananiamini kiasi hicho yanini mimi nianze kukaa na kukutungia hadithi za kukupa ili zikusaidie nini wewe hapo? Nikikudanganya nitafaidika na kipi labda cha kusema niseme sasa hapa namdanganya ndugu yangu wa damu? Mimi nimekujibu kile ambacho wewe umeniuliza na majibu yake ndiyo hayo” IGP alijibu kwa upole lakini uliokuwa unamaanisha sana na ndiyo illikuwa haiba yake hakuwa mtu wa kukurupuka kabisa kwenye maisha yake alikuwa ni mtu ambaye ilikuwa ni lazima ajiridhishe kwanza kitu ndipo akifanyie maamuzi ndiyo sababu hata jeshi la polisi ambalo lilikuwa chini yake lilipata mafanikio makubwa licha ya kuwepo kwa baadhi ya mambo ambayo yalikuwa hayaridhishi sana lakini kwa namna yake alijitahidi sana, alimpa jibu hilo ndugu yake huyo na kutulia kumsikiliza mwenzake kama alikuwa anahitaji aendee kupewa taarifa au aendelee kuwa mjuaji azikose taarifa.

“Sawa ndugu yangu mimi nakuamini sana tena sana na nakujua tangu wakati ule tukiwa vijana wadogo baada ya Mark wewe ndiye tulikuwa tunakutegemea sana kwenye maamuzi ya busara lakini hilo jambo linanipa ukakasi sana kwa sababu nina maswali hata miambili kidogo na ningependa sana kama maswali yote haya nitayapatia ufumbuzi wake, ilikuwaje mpaka huyu mtoto akapewa nafasi kubwa sana namna hii? Na hicho unachokisema ni kikundi chake kilikuwa na sababu gani kuanzishwa na kwanini hata yeye mwenyewe taarifa zake ni za siri sana namna hii?” swali lake lilimfanya aongeze umakini sana maana huko mbele aliamini kutakuwa na taarifa zingine nyeti sana.

“Mhhhhh mimi nitakujibu kwa yale ninayo yajua tu maana hizi taarifa hata mimi nimeletewa usiku wa leo na….”
“Whaaaaaat?” CDF alishangaa sana kusikia hivyo
“Usiku wa leo? Inawezekana vipi?”
“Kwani juzi hapo si uliniuliza kuhusu haya mambo?”
“Ndiyo na ulisema hujui”
“Sasa kama juzi nilikuwa sijui unashangaa nini ninavyo kwambia kwamba nimezipata leo usiku?”
“Enhe nambie imekuwaje”

“Jana nilikuwa nimekaa hapa majira ya usiku wa manane sana nikiwa napunga upepo baada ya kuchoka kukaa sana ndani, nilitamani nipigwe na upepo huku nikiwa nayatafakari sana mambo mengi sana ambayo yametokea ikiwemo kuweza kuwapoteza ndugu zetu wapendwa, nikiwa nimezama kwenye mawazo hayo nilifumba macho ila baada ya muda kidogo niliona uzito wa hili eneo baada ya kuhisi kwamba kutakuwa kuna mtu ameongezeka, kwa haraka haraka nilihisi ni mke wangu lakini mke wangu manukato yake nayajua kuliko mtu yeyote yule hivyo nilijua siye na mtu huyo alionekana kuwa mgeni kabisa ndani ya hili eneo ndipo nilipo yafumbua macho yangu na kushangaa kukutana na ninja akiwa mbele yangu, sijui kama ni ninja kweli au ni watu wanao vaa nguo za kininja ila pia alikuwa na upanga wake mgongoni uso wake ukiwa umezibwa ila juu ya kichwa kulikuwa wazi anaonekana kama ni kijana wa Kihindi hivi japo anaongea Kiswahili ambacho kimenyooka sana, niliogopa mno nikaangaza huku na huko nikihisi huenda alishafanya mauaji kwa walinzi wangu au mtu mwingine yeyote yule amedhulika lakini ni kama alinisoma nilichokuwa nakiwaza

“Usiogope mimi sijaua mtu yeyote yule kwenye hii nyumba kuwa na amani nilitaka kuzungumza nawewe ndiyo maana nimekuja hapa usiku huu sehemu ambayo imetulia sana hii” aliongea kwa kujiamini sana huku akiwa anakitoa kitambaa chake kabisa usoni na kuketi pembeni yangu na hapo ndipo nilipoweza kuthibitisha yale mawazo yangu kwamba huyo ni mhindi kabisa kwa asili ila anaonekana kaishi Tanzania kwa miaka mingi sana

"Unataka kuzungumza nini na mimi mpaka univamie nyumbani? Kwanini usingesubiri kesho nije ofisini?"
"Ofisini kusingekuwa na uhuru kama ambao tunao hapa sasa hivi ndiyo maana nimeona hapa ni salama zaidi”
“Huoni kama unajihararishia maisha yako kunivamia kiongozi mkubwa kama mimi, naweza nikawaita walinzi sasa hivi”
“Mhhhhh usifike huko mzee wangu mimi sijaja kuwaua hao walinzi wako hapa nimekuja kwa kuagizwa”
“Umeagizwa na nani?
“Hakuna umuhimu sana wa kumjua ni nani kaniagiza ila nimekuja hapa kwa ajili ya huyo kijana wako”
“Nani?”
“Jason”
“Kafanyaje”

“Mwambie kwamba aache kile ambacho anataka kukifanya, mkalishe chini muonye na umhamishe kwenye hii nchi vinginevyo ndani ya muda mfupi tu mtatangaziwa msiba wake”
“Mbona sikuelewi unamaanisha nini?”

“Hizi taarifa hazijafika ndani sana ila tunazo watu wachache mno, mimi najua kwamba yule ndiye mkurugenzi wa usalama wa taifa, yule najua kwamba anamiliki kikundi cha watu watano ambao wanajulikana kama FIVE POISONED SERIAL KILLERS ambacho ni cha siri kubwa sana na huwa hawatumii jina hilo wao wanatumia jina la TOXIC, ukiangalia neno TOXIC lina herufi tano sawa sawa na idadi yao kama ambavyo wapo watano, kati ya hao wote tunamjua yeye tu na hao vijana wake hatuna taarifa nao sana zaidi ya wawili ambao tuna taarifa zao kwa uchache mno, hiyo T inasimama kwa niaba yake yeye Jason ikiwa na maana ya Team Leader, ila hiyo O na I mpaka sasa hatujajua maana yake ni nini na ni watu gani hao japo nasikia wanajulikana kwa baadhi ya watu wa siri, hiyo C inasimama badala ya Communication Director na huyu ndiye anayewapa kiburi sana hawa watu maana nasikia anaujua mtandao kuliko hata idadi ya herufi za jina lake, anaweza kuingia popote na kufanya anachotaka yeye huku akiwa amejifungia chumbani, hajulikani ni nani na anaishi wapi huyu mtu ila ndiye mzizi wa hili kundi kwa sababu anaweza kuwapa taarifa yoyote ya kitu chochote kile kinacho endelea popote pale lakini kwa sasa nilisikia alipewa mapumziko ila kwa muda ambao inasemekana Jason amepanga kupotea akirudi basi huyo naye atarudi na hapo ndipo ataanza mipango yake kama anavyo enda kuahidi kwenye vyombo vya habari”

“Na hiyo X ya katikati ambayo inabaki hiyo inabaki kama ilivyo kwa sababu huyo ni mtu ambaye hajulikani kabisa ni nani na hakuna hata dalili zozote za kujulikana kwake, anajihusisha na nini na yupo hapo kwa sababu ipi hakuna anaye jua kabisa hivyo huwa wanamchukulia kama X ambaye anatakiwa kutumika ili kutafuta thamani za wenzake wote kwenye kundi lao maana yake huyo ni moja ya mtu wa mhimu zaidi ukimtoa Jason ndani ya hilo kundi, huyo inasemekana anaye mjua ni Jason pekeyake hata wenzake hao watatu hawamjui na hata sisi bado hatujamjua ila kama hatafuata maagizo yetu ya kuacha kila kitu na kuondoka nchini basi tutawatafuta kwa nguvu na tutawamaliza wote bila huruma yoyote kama kilicho muua kaka yake kwa sababu ya ubishi” nilibaki natetemeka sana kwa maelezo ambayo yule Ninja alikuwa ananipa pale nilipatwa na uoga pamoja na hasira kali sana, kwanza walionekana kuwa ni watu ambao walikuwa wamejipanga pakubwa mno kwa sababu taarifa ambazo walikuwa nazo zilikuwa zinatisha sana lakini baadae niligundua kwamba hawa ndio waliokuwa wamemuua Mark na bila shaka hata raisi walimuua wao, nilipatwa na ghadhabu sana nilitaka kumkaba yule kijana mdogo lakini alinionya na ilinilazimu kuwa mpole

“Kumbuka hapa una familia yako mzee, hivyo jiangalie sana usije ukawapoteza wote usiku huu huu ukapata msiba mwingine kabla hujamaliza msiba wa marafiki zako, mimi mpaka nakuja hapa sijakurupuka najua muda unao lala, muda unao amka, mkeo anapenda nini, unapenda kufanya nini ndiyo maana hata muda huu nilijua lazima nitakukuta hapa” aliongea kwa kujiamini sana akiwa anageuka kuangalia kule ndani ambako alikuwa anajua familia yangu ipo kule

“Hizi taarifa wewe umezipatia wapi?” hakunipa jibu lolote lile zaidi ya kunitolea simu na kunionyesha hizo taarifa, alinionyesha na video moja ya Jason kwa sura yake akiwa anafanya mauaji ya kutisha mno mpaka mimi mwenyewe nilifumba macho yangu nilishindwa kuweza kuendelea kuangalia yale ambayo yanafanyika,nilihitaji sana anipe taarifa zaidi ya ukweli wa haya mambo lakini aliniambia kwamba tukikutana siku nyingine huenda nitayajua na mengine ambayo sina taarifa nayo ila kwa taarifa ambazo alikuwa amenionyesha na kuniambia zilikuwa zinatisha sana.

“Sasa hao vijana wake wako wapi?”
“Mimi simjui hata mmoja wao na hata ambao wana hizi taarifa hakuna ambaye anawajua zaidi ya huyo Jason ambaye naye wengi hawana siri za uhalisia wake japo nasikia kijana wake mmoja ni mlinzi pale ndani ya chuo cha NIT tunaendelea kuchunguza kwa umakini sana siku tukimjua basi tutaondoka naye na hiyo inaonyesha kwamba tunaweza kuwapata muda wowote ule, ni vjana wadogo tu na pale anapewa mshahara wa chini sana sasa sisi tunahitaji kuwapata wote ikiwemo huyo kiongozi wao ila kama tu atapingana na hili agizo kwani mpaka sasa viongozi wangu wa juu hawajui haya kwahiyo mwambie aondoke ikiwezekana ahame kabisa nchi hii asije kuonekana tena na haya mambo ayaache kama yalivyo ila kama akiwa mbishi sana basi kutakuwa hakuna namna zaidi ya kumuua tu” aliongea kwa ujasiri sana wakati ananionyesha baadhi ya taarifa za kijana huyo ambaye alidai kwamba ni mlinzi wa NIT pale nilitamani sana kujua mengi lakini aliondoka kwa kasi sana na kupotea ukutani baada ya kudunda mara moja tu na kuruka juu nadhani alitua ni nje ila sikumuona tena

Hivyo baada ya mimi kupata taarifa hizo nililazimika usiku ule ule kumpigia simu mheshimiwa raisi na kumuuliza kama alikuwa anajua jambo hilo lakini hata yeye alikuwa amegoma kabisa na kusema kwamba ni kweli Jason ndiye mkurugenzi wa usalama wa taifa baada ya kuirithi nafasi hiyo kutoka kwa mtu ambaye alikuwa kabla na kupotelea kusiko julikana, hata yeye amesema kwamba hajui sababu ya Jason kuwekwa hapo na ilikuwa imepangwa tangu mwanzo kabla hata raisi hajafa kwamba huyo ndiye mrithi wa hiyo nafasi hata yeye hana jibu kamili sasa nadhani hata kabla sijakutana nawewe ndipo ukawa umekutana naye ndiyo maana nimekwambia mimi mwenyewe hizi taarifa nimezipata usiku wa leo ila kwa niliyo yashuhudia kama kweli Jason yupo vile basi siyo binadamu yule ambaye sisi tunamjua kile kitakuwa ni kifaa ambacho kilitengenezwa kwa kazi maalumu nimeogopa sana hata kukutana na huyo mtoto kwa sasa sitaki tena kujiamini" IGP maelezo yake yalionekana kuwa na ukweli ndani yake kwamba alitembelewa na mwanaume huyo lakini maneno ambayo aliyatoa hapo hayakuwa ya ukweli kwamba ndiyo ambayo aliambiwa na huyo mtu ambaye alimjia, ni presha za mkuu wa majeshi zilimfanya ashinndwe kung’amua uongo wa kitoto aliokuwa ameambiwa hapo.

“Mhhhh nimeshindwa kuelewa kama nikuamini au nisikuamini maana maelezo yako yana maswali mengi sana ndani yake ila kwa sasa tuishie hapa japo najua unanidanganya sana tu tena sana na kuna maelezo mengi sana umeyatunga wewe mwenyewe kwa sababu zako ila kumbuka unaongea na mkuu wa majeshi wa nchi ya Tanzania sidhani kama utoto kama huo mimi naweza nikaukubali, hili jambo kwa sasa nataka nilifuatilie mwenyewe na mwambie huyo mtoto kwamba nataka kukutana naye mimi mwenyewe tuongee tukiwa wawili” mkuu wa majeshi alihisi mwenzake huyo kwenye maelezo yake kuna taarifa za uongo alikuwa amemjazia haikumpa ugumu kuweza kujua hilo kwa sababu ndugu yake huyo hakuwa mtu wa uongo sana hivyo hata kudanganya alikuwa hajui ndiyo maana kwenye maelezo yake alijikanyaga sana yeye mwenyewe, alinyanyuka bila hata kuaga na kuanza kuondoka akiwa ana hasira sana

“By the way mbona una wasiwasi sana juu ya hili jambo kuna nini umekifanya?” IGP alimtolea uvivu mwenzake huyo baada ya kugundua kwamba alikuwa amemsoma kwamba kuna vitu anamdanganya, CDF alisimama akiwa hajageuka na kuangalia saa yake

“Muda utakuja kukuelezea vizuri kuhusu mimi” alijibu kwa nyodo sana na kumfanya IGP ajikohoze vizuri ili kumpa neno ndugu yake huyo wa muda mrefu sana

“Siku ile nilikuja kwako nikakushauri kwamba kama kuna jambo baya umelifanya niweke wazi mimi kama ndugu yako nikusaidie uligoma kabisa, huenda ingekuokoa sana ila unaona kama mimi nakufuatilia sana ila kwa sasa nakuacha kama ulivyo na hayo ambayo unayaficha nyuma yako, mimi najua kwamba wewe umehusika kwa namna moja ama nyingine kumuua raisi na Mark japo mpaka sasa sijui sababu ni nini, zile sms nina uhakika haukutuma kwa bahati mbaya zilikusudiwa ila nataka nikushauri ndugu yangu sehemu ambayo umeingia kwa sasa siyo kabisa na usitegemee kwamba nitakuja kukusaidia kwa hilo kwa sababu ulikataa kunisikiliza, ila kama ungekuwa unajua kuhusu uzito wake ungeamua kujisafisha na kumuomba msamaha yule kijana pamoja na familia ya raisi waone kama watakusamehe ila ni muda mchache sana utaingia kwenye vitabu vya watu ambao watakuwa na mwisho mbaya sana kwenye maisha yao” IGP aliongea akiwa ananyanyuka, CDF aliyasikia maneno hayo vizuri sana, alisimama na kugeuka alipokuwa IGP alimtazama kwa jicho moja baya sana, hakuongea neno lolote aliingia kwenye gari yake na kutoka kwa vurugu sana ndugu yake alibaki anasikitika sana mwenzake aliamua kuanza kujionyesha makucha yake ikiwa ni mapema sana.

Ndugu hawa wawili wameanza kupishana na kuwekeana visasi moyoni kwa mambo ambayo mmoja wapo anaonekana kuhusika nayo, je kuna ukweli wowote au hatima yao ni ipi?

35 natia nukta hapa tukutane tena sehemu inayo fuata

Wasalaam

Bux the storyteller.
 
STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 36

SONGA NAYO............
JNIA
Mafahari wawili hawawezi kukaa ndani ya zizi moja na kama ikitokea wakawekwa pamoja basi madhara yatakayo tokea ni matatizo makubwa sana na hiki ndicho kilichokuwa kinatokea ndani ya huo uwanja wa ndege, wanawake wawili ambao walikuwa ni warembo kupita kiasi walikuwa wanashuka kutoka ndani ya ndege moja mchana wa siku hiyo, walikuwa ni wazuri tena wazuri kulipita hata hilo neno na hicho ndicho kilichoweza kuzalisha ufahari baina yao hao warembo, kila aliyekuwa karibu nao basi hakuisha hamu ya kuendelea kuwaangalia wote wakiwa wanaonekana kabisa kuelekea sehemu ya mapokezi ambako walikuwa wanatoka kabisa nje ya uwanja huo wa ndege. Wakiwa wanaelekea pale mapokezi waligongana mlangoni na kila mtu akaivua miwani yake walitazamana kwa umakini sana mrembo mmoja kati yao akiwa ameshika eneo la bega lake kuonyesha kwamba alikuwa amepata maumivu na huenda alishangaa sana inakuwaje mwanamke mwenzake ana mwili ambao umekomaa sana kiasi hicho wakati kwa nje ni mrembo sana na ana ngozi laini kupitiliza.

Dakika nzima iliisha wakiwa wanatazamana kwa umakini mkubwa kisha yule mrembo ambaye alionekana kukomaa mwili wake akatabasamu na kuanza kupiga hatua za kuelekea nje mwenzake akiwa anamtazama bado kisha naye akaanza kuondoka, hicho kitendo kilikuwa kama filamu moja fupi ya taharuki kwenye uwanja huo kwani kila aliyekuwa hapo alisimamisha shughuli zake ili kuwaangalia mafahari hao hatima yao ingekuwa ni nini, huyo mwanamke ambaye alikuwa anaonekana kama vile amakomaa mwili wake alikuwa ni Monalisa kutoka ndani ya nchi ya Marekani alikuwa amekuja Tanzania kama alivyokuwa ameahidi na huyo mrembo mwingine ambaye alionekana kuwa laini sana alikuwa ni Asharose Jaiwelo Mkupi Makubilo binti wa damu kabisa wa mheshimiwa mkuu wa majeshi naye alikuwa amekanyaga ndani ya ardhi ya nchi yake ambapo aliondoka kwa muda mrefu sana kwenda kukamilisha masomo ya sheria na sasa alikuwa amerudi akiwa kama mwanasheria kamili na aliahidi kuanza kuifanya kazi yake pindi atakapokuwa amefika tu ndani ya nchi yake.

Kila mtu alikuta kuna watu wanamsubiri wa kumpokea na msafara wa magari na watu hao magari ambayo yalikuwa yakiwasubiri hayakuwa mbali sana, kila mmoja kabla ya kuingia ndani ya gari ambalo alitakiwa kupanda alimtazama sana mwenzake kwa umakini sana bila hata kujua kama kulikuwa na kitu chochote kati yao ila walijikuta tu kila mtu akiwa anamuwekea mwenzake umakini mkubwa sana wa kumtafakari mwenzake huenda ilikuwa ni kwa sababu ya uzuri wao ambao ulikuwa umepitiliza lakini kila mtu majibu yake alikuwa nayo yeye mwenyewe kwenye kichwa chake, kila mmoja aliingia kwenye gari yake na misafara yao ikatawanyika hapo.

“Kazi yangu ya kwanza itakuwa ni kumtafuta Jason kwanza” Monalisa aliongea kwa ujasiri huku akiwa amesonona kwenye uso wake, kwa uchovu aliokuwa nao alijiegesha kwenye kiti alichokuwa amekalia akiwa ana uhakika kwamba atakapo amka hapo atakuwa mbele ya baba yake.


Upande wa pili kulikuwa na taarifa ya kushtua sana kwenye upande wa vyombo vya habari, ilikuwa ni ghafla sana mheshimiwa raisi alitangaza kwamba muda mchache ujao angekuwa na mkutano na vyombo vya habari ambao ungekuwa unarushwa kwa matangazo ya moja kwa moja na mtu yeyote angekuwa na uwezo wa kumuona au kumsikia mchana huo hivyo wananchi wa Tanzania wajiandae kuanzia wakati huo, ilikuwa ni taarifa ya ghafla sana ambayo iliibua minong’ono kila sehemu ilikuwa imezoeleka taarifa huwa inatolewa mapema lakini hii ilikuwa ni ya ghafla sana kiasi kwamba ilipelekea wananchi kutamani sana kumsikia huyo kiongozi wao labda huenda angetolea ufafanuzi wa kile ambacho kilikuwa kimetoka kutokea na jana yake tu kuna mwanasheria mkubwa sana aitwaye Yasinta Kobe ambaye alidai kwamba alikuwa ana ushahidi wa kutosha wa mauaji ya mheshimiwa raisi aliyekuwa amefia madarakani alitoka kutekwa japo jambo hilo lilifichwa fichwa lakini lilifika kwenye vyombo vya habari na kuweza kuzua upya taharuki kwa wananchi hivyo taarifa hiyo licha ya kuwa ya ghafla sana kwao ilikuwa ni kama neema kwa sababu walikuwa wanaenda kuyapata majibu yao.

Jason na Alphonce walikuwa wapo ndani bado mpaka mchana huo nao pia walikuwa wapo mbele ya runinga kutazama tukio hilo ambalo raisi huyo alikuwa anaenda kuliwasilisha mbele ya watu wake

“Nawasalimieni nyote kwa jina la Jamhuri tukufu ya muungano wa Tanzania, ni matumaini yangu wengi mu wazima wa afya kabisa na kwa wale ambao wana matatizo ya hapa na pale basi MUNGU akawaponye na kuwapa nguvu mpya ya kuweza kuinuka tena ili tuendelee kulinda na kuipigania nchi yetu pendwa ya Tanzania. Wengi mtakuwa mna hamu kubwa sana ya kuweza kusikia tamko la serikali kutokana na mambo yote magumu ambayo tumeyapitia hizi siku kadhaa ikiwemo kuwapoteza wapendwa wetu wawili na jana yake tu kumpoteza mwanasheria mmoja ambaye alionekana akisema kwenye mtandao kwamba alikuwa anao ushahidi wa kuwahusu wauaji na wahusika wa tukio lile la mheshimiwa kupigwa risasi ndani ya mipaka ya nchi yetu, naomba kwanza niwatoe wasiwasi wananchi wangu kwamba mwanasheria atapatikana mapema sana kwa sababu tangu jana usiku swala hilo limeanza kushughulikiwa na huyo kipenzi chenu mapema sana atarudi halafu aje atusaidie kutupatia huo ushahidi kama kweli anao ili na sisi tuufanyie uchunguzi wa kina kuweza kujiridhisha kama kuna ukweli wowote ule” mheshimiwa alipumzika kidogo na kuendelea

“Lengo la kuja mbele yenu siku ya leo ni kuhusiana na mambo makubwa matatu na la kwanza nimesha ligusia kuhusu mwanasheria huyo atapatikana mapema tu wala msijali kuhusu hilo kabisa, lakini jambo la pili nilitaka kuwatoa hofu wananchi wangu na kuwahakikishia kwamba nchi haipo kwenye machafuko kama baadhi ya watu wanavyo sambaza huko mitandaoni na kuzua taharuki kubwa sana miongoni mwenu hivyo puuzieni hizo taarifa ulinzi upo imara kwa masaa 24 na hakuna mwananchi atakaye pata tatizo lolote lile la namna hiyo. Lakini jambo kubwa sana la tatu ni kwamba rasmi natoa tamko kwa yote yaliyo tokea kwa mheshimiwa raisi pamoja na jaji mkuu kuuawa na baadhi ya watu kukamatwa mpaka sasa wanaendelea kutoa ushahidi na mwingine alinyongwa mbele ya mahakama hadharani lakini majibu kamili na kila kitu kitawekwa wazi baada ya miezi sita kupita, siku ambayo utakuwa unatimia mwezi wa sita kuanzia hii leo ninavyo zungumza hapa basi mimi nitakuja tena hadharani kutoa ukweli wa wahusika na kuwatoa kwenye hiyo taharuki kubwa ambayo mlikuwa mpo nayo hivyo puuzeni hizo propaganda ambazo zimelenga kuweza kuichafua taswira ya nchi yetu pendwa tusaidiane kuitunza nchi yetu, huo muda ni kwa ajili ya kupisha uchunguzi mkali na wa kina kwa vitengo vya kipelelezi ambavyo nimeviteua hivyo ndani ya miezi sita wahusika watawekwa wazi na watapata adhabu kali sana ambazo zitakuwa ni funzo kubwa sana kwa wengine. Ahsanteni sana ndugu watanzania MUNGU awabariki sana, MUNGu aibariki Tanzania, MUNGU aibariki Afrika” mheshimiwa raisi alimaliza hotuba yake na kuondoka hiyo sehemu ya mikutano, watu wengi walionekana wakimpongeza mheshimiwa kwa kuanza vizuri japo wengine walikuwa wanadai kwamba alikuwa anaficha ficha mambo maana lazima alikuwa anaujua ukweli wote hiyo miezi sita ilikuwa ni upotezaji wa muda tu na kupoteza rasilimali za nchi ila wengi walimpongeza sana.

“Hili jambo naona ni zito sana kuliko hata ninavyo lichukulia”Alphonce alitamka akiwa anaizima runinga hiyo

“Huku kuliko baki niachie mimi, leo naondoka na tutakutana baada ya miezi sita, kama kutakuwa na shida au nitahitaji msaada wako nitakutafuta mwenyewe kwani kwa sasa hautanipata kabisa hewani” Jason aliongea huku akiwa ananyanyuka hapo alipokuwa anakaa na Kwenda kwenye kabati ambalo lilikuwa hapo sebuleni aliitoa Diary kutoka ndani ya kabati hilo na kuishika kwenye mkono wake, Alphonce alikuwa anamwangalia tu rafiki yake huyo

“Unaenda wapi?”
“Nitakwambia siku nyingine, shika hii kadi ya benki humo ndani kuna bilioni tano, tumia mpaka utakapo fikia kwa muda ambao utakuwa hapa Tanzania mimi nikirudi utanikabidhi kadi yangu, shika na hiyo funguo ya nyumba kwenye hiyo kadi yake kuna sehemu ambayo nyumba hiyo ipo hiyo ni nyumba yangu andika namba 5 zijirusie rudie mpaka ziwe kumi hiyo ni nywila ya kadi ya benki ambayo yenyewe utaziweka nne pamoja na hiyo nyumba ndo unatumia kumi, ni moja ya nyumba zangu ipo Magomeni huko, ishi unavyotaka, fanya unacho jisikia ila tu usijulikane kabisa nitakaporudi utaelewa kwanini niliondoka” alimaliza kuongea na kutoka ndani ya nyumba hiyo ambayo ilikuwa ya kaka yake na alicho kibeba humo ilikuwa ni Diary tu tena hakutoka na gari hata moja alitoka kwa mguu, Alphonce alibaki anamshangaa rafiki yake huyo kwenye mkono wake kwenye funguo ya nyumba kulikuwa na funguo mbili, alitoka nje na kubonyeza funguo moja aliona kuna gari moja sana ya kifahari inapiga alamu hiyo ni gari ambayo alikuwa ameachiwa kwa ajili ya safari zake za hapa mjini alifurahi sana nae hakukaa kabisa alipanda na kuondoka.


KEKO
Ni eneo ambalo kwa kiasi chake linasifika sana kuwa na vibaka wengi sana hususani maeneo ya usiku na kwa mtu ambaye ni mgeni basi anaweza akajikuta yupo kwenye wakati mgumu sana akiwa ndani ya hayo maeneo, nyuma ya godauni moja ambalo lilikuwa limetelekezwa na watu wengi walikuwa wakilitumia kama danguro majira ya usiku wa manane kulikuwa na watu wengi sana wengine walikuwa wanacheza kamali haswa, na kuna sehemu ambayo ilikuwa na makelele sana hapo kulikuwa kunakuwa na mapigano ya mtaani kila siku ya MUNGU pembeni kidogo na hapo pia walikuwepo madada poa ambao wao walikuwa wanafanya biashara ya kuuza miili yao hususani kwa wale wanaume ambao wangeshinda kwenye kamali zao au kwenye mapigano basi walikuwa wanapata pesa za kuchagua warembo wawatakao wao na kuingia nao ndani ya danguro hilo kuufaudi ufundi wa uumbaji. Pembeni kidogo kutoka ilipokuwa hiyo sehemu kulikuwa na matairi ambayo yalisimikwa hapo mengi sana na kuna watu walikuwa wanatulia hapo kupunga upepo na kutazama namna wanaume walivyokuwa wanachakalika kwenye kamali pamoja na mapigano ili kuukimbia umaskini na hapo ndipo alikuwa amekaa ASP Bakari Zalimo kwa majira yake ambaye kwake kulikuwa ni Mbagala.

“Nadhani huwa unajihisi amani zaidi na furaha unapokuwa kwenye hili eneo” alishtushwa na sauti ya mtu ambaye naye alikuwa anajiandaa kukaa pembeni yake maana tairi hilo lilikuwa kubwa sana huku mkononi kwake akiwa anamkabidhi ASP huyo karanga mbichi huku naye akiwa anaendelea kuzitafuna taratibu, ASP Bakari Zalimo alitabasamu kwa wasiwasi sana baada ya kumuona Jason ila alilazimika kutulia tu maana kwa mauaji ambayo aliyashuhudia siku ile yakiwa yamefanywa kwa wale watu mbagala na kuambiwa akaitupe ile miili na IGP huku mhusika mwenyewe akiwa pembeni yake muda huu ilimtisha kidogo japo aliamua kutulia kwani kama mtu huyo angekuwa na nia mbaya naye basi angekuwa amesha mdhuru muda mrefu sana na hakuwa na kosa lolote la kumfanya kuingia kwenye ugomvi mkali na huyo bwana.

“Yes, huwa najiona nimefika sehemu ya mbali sana ya dunia ninapokuwa hapa, nimekulia kwenye hii mitaa na mimi nikaja kuwa mpiganaji maarufu sana hapa mpaka nilipopata nafasi ya kujiunga na jeshi la polisi baada ya kuchukuliwa na IGP, hapa licha ya kuwa na mambo machafu ambayo kiuhalisia kisheria ni kosa kubwa lakini ndilo eneo ambalo huwa linanipa amani kila ninapo litazama, nishawahi kumpiga mtu kwenye lile eneo mpaka akapoteza kumbukumbu zake mpaka hii leo ninavyo ongea hivyo nina historia kubwa sana hapa na ndiyo sababu hata atokee nani hawezi kunipa kazi ya kumkamata mtu hata mmoja hapa nikakubali kwa sababu ndipo pamenilea na kama kuna mtu anataka kumgusa mtu yeyote pale basi ahakikishe nipo mbali maana vinginevyo naweza kumuua” aliongea huku akitafuna karanga alizokuwa amepewa akiwa anaendelea kuangalia ile sehemu ambayo watu walikuwa wanapigana haswa, zilikuwa ni ngumi za mtaani lakini zilikuwa zinawahusisha wanaume haswa ambao walikuwa wanajua ni nini walikuwa wanakifanya.

“Unahisi kwanini unafanya hivyo?”
“Wazungu wanasema “GO EAST, GO WEST, HOME IS ALWAYS THE BEST (nenda mashariki, nenda magharibi ila siku zote nyumbani ndiko bora zaidi)” yaani hata uende wapi nyumbani ni nyumbani tu, mimi nimelelewa hapa na mwanamke ambaye aliniokota tu na hizi shughuli haramu ambazo alikuwa anazifanya ndizo zimenilea na hao ambao wanadai wanafanya shughuli halali walinitupa sasa unahisi nitamjali nani kama sio hawa watu wangu ambao nimekua nao na kujifunza kwamba hawaishi haya maisha kwa kupenda bali kwa sababu ndiyo njia pekee ya kuwafanya waishi, serikali ni kama imewatelekeza, hakuna haki popote ni rushwa tu, tupo ndani ya jeshi la polisi ila hakuna cha sheria wala nani kila kitu kinaongozwa na pesa, vipi wewe kama gongo ndiyo imekufanya ukasoma ukapata kazi na kuwa na maisha mazuri labda ukawa mwanasheria au mwanajeshi au polisi unaweza ukamkamata muuza gongo baadae kwa sababu ni haramu wakati ndiyo imekuweka pale? jibu ni hapana na hiyo ndiyo sababu inanifanya mimi nimeamua kuishi hivi” Bakari Zalimo aliongea kitu ambacho kilimgusa sana Jason.

“Tutaongea siku nyingine nimekuja hapa kukupa kazi ya kuifanya usiku wa leo mpaka kunavyokucha asubuhi basi hizi taarifa zinatakiwa kuwa zimetapakaa kila mahali, hii karatasi inatakiwa kwenda kuchapiswa zitoke kopi nyingi sana kisha zibandikwe kile mahali na kila sehemu ndani ya jiji la Dar tafuta vijana hata 1000 muda huu najua utawapata tu mimi nakuachia pesa ya kutosha hakikisha vinasambaa kila sehemu nadhani milioni hamsini inatosha kukamilisha hili ila hakikisha haujulikani kama ni wewe ndiye uliye ifanya hii kazi” mwanaume hakuja hapo kupiga stori alikuwa amekuja kumpa ASP huyo kazi tena ilitakiwa kufanyika usiku huo huo, alitoa mabunda ya pesa kwenye mfuko wake wa koti ambalo alilivaa usiku huo na kumwachia ASP huyo ambaye hakupata nafasi ya kuhoji sana alijua mtu huyo hawezi kumpa majibu hivyo sehemu yake ya kupatia majibu ilikuwa ni kwa IGP.

“Ulijuaje kama nipo hapa?” aliuliza na kumfanya Jason ageuke
“Simu yako ipo on hivyo ninaweza kukupata popote pale ila zingatia sana naomba hizo karatasi kufikia saa 11 asubuhi ziwe zimetapakaa kila sehemu usije ukaharibu hicho kitu nakuomba kistaarabu sana kama ukiifanya hiyo basi tutaonana baada ya miezi sita ila kama ukikaidi basi tutakutana kwako kesho” alimaliza na kuondoka akapotelea kizani kwenye nyumba ambazo zilikuwa pembeni mwa hilo eneo huku akiwa amemuacha ASP huyo na mawazo mengi sana kichwani.

Hizo karatasi zina nini mpaka anahitaji zibandikwe? Zina ujumbe gani na unaenda kwa nani? na ndani ya hiyo miezi sita anaenda wapi Jason? 36 sina la ziada tukutane ndani ya sehemu inayo fuata.

Wasalaam

Bux the storyteller.
 
Hii ni simulizi ya kijasusi.....ambayo inamhusu kijana mmoja aliyepatwa kuitwa Jason.

Kijana huyu alikuwa ni mdogo wa jaji mkuu wa nchi ya Tanzania. Ambaye alikuwa akisoma ndani ya nchi ya Marekani.

Alikuwa kijana wa kawaida sana kwenye macho ya watu, ambapo alikuwa na mpenzi wake waliyekuwa wakisoma wote.

Mpenzi wake huyo alikuwa ni Agenti wa CIA bila kijana huyo kujua.

Kisa kinaanzia wapi?

Raisi wa nchi ya Tanzania anapigwa risasi tano za kichwa akiwa Tiptop darajani kwenye msafara wake usiku. Kesi hiyo inaangukia kwenye mkono wa jaji mkuu, ambaye alikuwa ni rafiki wa karibu wa raisi, anaapa kumuua aliye husika mbele ya mahakama.

Jaji huyo usiku mmoja kabla ya hukumu anapewa onyo kwenye simu kwamba aupindishe ukweli siku ya hukumu....

Siku ya HUKUMU.
Anamsomea hukumu ya kunyongwa mhusika ambaye ananyongwa mbele ya mahakama. Baada ya kutekeleza hilo anapokea simu ya kumpa dakika 15 tu za kuiokoa familia yake.

Anakimbia na kufika nyumbani anakuta mkewe amechomwa kisu cha tumbo akiwa mjamzito huku mwanae wa kike akiwa ameuliwa.

Anpiga simu kwa mdogo wake kumpa taarifa lakini naye anatokewa na mtu na kuuliwa huku akiwa amefanikiwa kumtamkia mdogo wake kwamba....."THEY HAVE KILLED YOUR BROTHER" (Wamemuua kaka yako).

Mauaji anayofanyiwa yanafanana na namna raisi alivyo uliwa, sasa kama mtuhumiwa alinyongwa vipi mauaji yawe yale yale kama ya raisi? maana yake muuaji hakufa? INAZALIWA SINTOFAHAMU.

Kijana huyo kwa uchungu anarudi kumzika kaka yake na mheshimiwa raisi wa nchi yake ambaye walijuana vyema kwa mengi yaliyokuwa yamejificha nyuma.

Siku kadhaa baada ya msiba, watu wanakutana na tangazo ambalo linawataka wahusika wa mauaji ya jaji mkuu na raisi wajitokeze ndani ya miezi sita, kisha waombe msamaha kwa jamii atawaacha hai..kama muda huo utaisha bila wao kufanya hivyo basi huyo mtu atafanya anavyotaka yeye..

Hapo ndipo tunaenda kumfunua huyo Jason na kumjua yeye ni nani baada ya kuanza kufanya mauaji ya kutisha.

Inaitwa: MUUAJI ASIYE NA HATIA (KISASI)

Softcopy yake inapatikana kwa shilingi 4000 tu.

0621567672 (WhatsApp)
FB_IMG_1686457206350.jpg
 
STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 37

SONGA NAYO............
Jaiwelo Mkupi Makubilo alirudi nyumbani kwake akiwa mwenye hasira sana hakwenda makongo juu ambako ndiko alikuw anaishi, alienda na gari yake mpaka maeneo ya Ununio ambako kulikuwa na nyumba yake huko ambayo alikuwa anaenda kupumzika pale anapokuwa hayupo sawa au hataki usumbufu wowote kutoka kwa mtu yeyote yule, alipitiliza mpaka ndani na Kwenda kwenye kioo kikubwa sana alivua nguo zote na kujiangalia mbele ya kioo hicho alijiona kama vile ni mtoto mdogo baada ya kuona kwamba ni kama kuna michezo ya kitoto alikuwa anachezewa yeye bila kujua hali ilivyokuwa inaenda alipiga ngumi yake kwenye kioo chake kwa hasira sana na kufanya kioo kicho cha gharama kupata mipasuko mingi sana kikawa kinaonyesha watu kumi kumi pale mtu anapokuwa anajiangalia. Aliinama pale chini ambapo alizirusha nguo zake na kuingiza mfukoni, alitoa simu ndogo haikuchukua hata sekunde kumi simu ilikuwa sikioni kwake.

“Nawahitaji hapa Ununio ndani ya dakika thelathini zijazo muwe sita” aliongea kwa jaziba na kukata simu yake alienda hivyo hivyo sebuleni akiwa uchi, alitoa chupa ya pombe kali kwenye friji lake na kuibugia mdomoni alipiga funda kadhaa huku akiwa anahema sana kama mwanaume ambaye alikuwa ametoka kifuani kwa mwanamke mrembo baada ya kufika safari zake kadhaa. Baada ya muda kidogo kupita alisikia geti likifunguliwa bila shaka walikuwa ni walinzi wanalifungua na alijua kabisa kwamba ni watu wake wamefika hapo, waliingia wanaume sita ambao walikuwa na miili mikubwa sana ya mazoezi iliyotuna haswa ila baada ya wote kuingia humo ndani waliinamisha vichwa vyao baada ya kumuona mtu ambaye bila shaka alikuwa kiongozi wao akiwa yupo uchi bila nguo.

“Hapa kuna kazi mbili za kuzifanya haraka sana” aliongea kwa msisitizo huku akibugia chupa hiyo ya pombe kali na kuimaliza yote kisha akasimama akiwa hana nguo hata moja kwenye mwili wake.

“Mmoja wenu aondoke muda huu akanitafutie wanawake warembo sana ndani ya hili jiji, nitawalipa pesa yoyote ile wawe ni wanawake ambao wamekamilika kila idara yaani kuanzia usoni, shingoni, vifuani, miguuni na nyuma kuwe na milima inayo eleweka, nahitaji wanawake kumi ndani ya nusu saa ijayo tu wawe hapa na muda huo nitakuwa nimesha vaa sura bandia hawatakiwi kunijua mimi ni nani hivyo mmoja akafanye hiyo kazi haraka sana” aliongea akiwa anamsogelea mwanaume mmoja kati yao, hakuchelewa tena alitoka humo ndani kama mshale maana yake yeye ndiye aliyekuwa amechaguliwa kufanya kazi ya kuwatafuta hao warembo

“Nyie watano muda huu nahitaji muende ndani ya chuo cha NIT, sina uhakika sana na mnacho enda kukifanya kwa sababu ni kama kubahatisha tu ila inatakiwa iwe hivyo, kuna kijana mmoja nasikia kwamba ni muaji wa hatari sana yupo pale na anafanya kazi kama mlinzi wa kawaida tu, hajulikani jina wala hakuna ambaye ana picha yake wale dalili yoyote ya kitu chochote ambacho kinaweza kumtambulisha na huyu kijana anatakiwa kupatikana haraka sana iwezekanavyo kuanzia hivi ninavyo ongea. Namna ya kumjua mtu ambaye ni tofauti na walinzi wa kawaida nadhani mnajua hivyo kwa mtu ambaye mtamuona hafananii kabisa na ile kazi au ataonekana kuwa mtu wa mazoezi sana basi naombeni muondoke naye kama mkiulizwa onyesheni vitambulisho vya jeshi na kusema kwamba ni mambo ya kiusalama mtu huyo mkiondoka naye mtamrudisha baada ya uchunguzi kuisha kutokana na hilo ambalo limetokea kwa mheshimiwa raisi, jaji mkuu kufa pamoja na mwanasheria huyo wa kike kupotea, mna masaa mawili tu nahitaji mrudi na huyo mtu na mkimpata mpelekeni kwenye Dark house halafu mtanipigia simu” alikuwa amemaliza kutoa maelezo waliondoka humo na kupanda kwenye magari yao kuelekea ndani ya chuo cha Taifa cha Usafirishaji kwa ajili ya Kwenda kumchukua mtu wao ambaye walikuwa hawamjui jina wala sura yake hata mfanano wake.

Dakika arobaini zilipita geti la nyumba hiyo lilifunguliwa, mkuu wa majeshi alikuwa bado yupo uchi kama alivyokuwa ameachwa mwanzo, waliingia wanawake kumi na huyo kijana wake baada ya kuhakikisha wote wameingia ndani alienda kukaa mlangoni na kuufunga mlango huo, mheshimiwa usoni kwake alikuwa amevaa sura ya bandia ili kutojulikana uhalisia wake asije akajiharibia baadae, kwa ishara tu aliwapa maelezo wanawake hao wavue nguo zao wote wakati huo walikuwa wameanza kumshika shika alihitaji mechi iwe ya wazi zaidi kwani yeye alikuwa uchi tayari, wanawake wote kumi walikuwa ni wazuri mno nyuma walibeba mizigo ya kutosha na hayo ndiyo mambo ambayo yeye alikuwa anayataka.

“Mpaka asubuhi wote ni shilingi ngapi?” aliuliza kwa sauti yake nzito huku akiwa anatoa vinywaji vikali sana kwenye friji lake pamoja na kikopo kidogo ambacho haikujulikana kina nini ndani yake, alitua vinywaji vyake kwenye meza huku wanawake hao wakiwa wananong’onezana ili kukubaliana bei

“Milioni mbili” mmoja aliropoka baada ya kuona wenzake wana sita sita
“Mkinifurahisha nawapa milioni kumi kesho asubuhi baada ya kuamka, vyakula vitakuja mtakula, mtakunywa ila hakikisheni mnanifurahisha vilivyo nimewaita nyie kumi mlio nona sana kwa sababu nataka kuwafaidi haswa siku ya leo mpaka asubuhi hatulali kabisa labda mpaka mimi nichoke” aliongea tena kwa msisitizo huku akiwa anajipaka yale mafuta ya kwenye kikopo na kufanya mhogo wake mkubwa kuendelea kuumuka na kutanuka sana, mwili wake ulikuwa unaonekana kabisa alikuwa ni mtu wa mazoezi haswa ndiyo maana alijiamini kuwaambia kwamba alitaka kuwafaidi.

Mwanamke aliyekuwa karibu yake alimuinamisha pale pale kwenye meza shughuli ilianzia hapo wengine wakiwa wanaendelea kumshika sehemu zingine za mwili, mwanamke aliyekuwa ameinamishwa hapo hakuwa nyuma kwenye kuzungusha kiuno chake, alijitahidi sana, aliachiwa akavutwa mwingine ambaye yeye alilazwa kwenye kochi huku akiwa anapata juisi ya miwa kwa mwanamke mwingine, mzee huyu ambaye alikuwa ni kiongozi mkubwa alikuwa akiufanya ushenzi mkubwa sana kwa siri huku mbele ya jamii akionekana kuwa mtu safi na baba bora sana kwenye familia yake tena nyumbani kwake akiwa na mwanamke mwingine ambaye alikuwa akiishia naye.

Yalipita masaa mawili akiwa bado anawasulubu wanawake hao maana mhogo wake haukuwa hata na dalili za kusinyaa kwa yale madawa ya kuongeza nguvu za kiume aliyokuwa ameyapaka muda huo bado kichwani alikuwa ana hasira zake ndiyo maana alikuwa anafanya kwa hasira sana, alisikia miungurumo ya gari aliuchomoa mhogo wake kwa mwanamke ambaye alikuwa amekolea sana na alikuwa akipiga kelele kwa kutoa sauti za mahaba kudhihirisha kwamba alifikishwa kunako, mwanaume huyo alifungua mlango na kutoka nje ambako alikutana na kiongozi wa wale wanaume watano aliokuwa amewatuma ndani ya chuo cha NIT, mtu huyo alianza kutoa maelezo kwa kumsimula kilichokuwa kimetokea huko.

Baada ya wao kufika ndani ya chuo cha NIT walipitiliza mpaka kwenye uongozi wa chuo ambapo walienda pale na vitambulisho vyao vya jeshi, walidai kwamba kuna mtu wao wana mtafuta na wamepata taarifa kwamba yupo pale na anafanya kazi ya ulinzi hivyo wanataka wafanye ukaguzi kama wakimpata mtu wao waondoke naye hivyo walihitaji walinzi wote waitwe kitu ambacho kilikuwa ni cha muda mfupi sana majira hayo ya mchana.

Kulikuwa na wanaume sita na wanawake saba ndio listi ya walinzi ambao walikuwa wapo hapo mchana huo, walinzi hao walipanga foleni na kuanza kukaguliwa na mtu huyo, alimkagua mlinzi mmoja mmoja kwa kumpa mkono ili apime uzito wa mikono yao huku akiwa anawaangalia sana machoni kuweza kumsoma mtu ambaye ndiye, kuna kijana mmoja alikuwa wa wastani tu mwili mzuri wa kuvalia nguo ulimkubali na uso wake wa rangi nyeusi ya kung’aa sana kwa wanawake wangeita chokoleti alivyo mgusa mkono tu kwa nguvu kijana huyo alitaka mpaka kutoa machozi kwa maumivu ambayo aliyapata mikono yake ilikuwa ni laini sana kama mtoto wa mama, mwanaume huyo alimpiga piga mgongoni kama ishara ya kumwambia ajikaze yeye alikuwa ni mwanaume na siyo mtoto wa kike mpaka walipo maliza ukaguzi wao huo na kujiridhisha kwamba hakuwepo mtu hata mmoja wa aina hiyo wakashukuru na kuondoka.

“Mhhhhh kwahiyo hamjapata chochote kile?”
“Ndiyo mkuu na wamesema walinzi ni wale wale wa siku zote wapo vile vile 13 wengine mchana huwa wanapumzika wanaingia usiku na wote walikuwa pale kwa sababu wengine wakiona uvivu kurudi huwa wanapumzika karibu na mazingira ya pale na wakati tumeenda wote waliitwa pale hivyo hakuna ambaye hakuwepo pale wote walikuwepo”

“Yule rafiki yangu namjua vizuri sana tena zaidi ya sana hawezi kunidanganya mimi kuhusu hizi habari kama kaniambia hilo jambo basi lazima lina ukweli, nina uhakika miongoni mwa hao watu mlio wakagua kuna mmoja ndiye, hawa watu wanaonekana kwamba wana mafunzo ya hatari sana na huwa wanafundishwa kuishi kulingana na mazingira husika ambayo wao huwa wanaenda kuishi, kwa mfano akitaka kuigiza kama kichaa anakuwa kichaa kweli na ambaye humjui unaamini kwa asilimia miamoja hivyo lazima alikuwepo. Kama kweli yupo pale lazima huwa anahakikisha pia na kuwalinda wanafunzi na watumishi wa pale kwahiyo hawezi kuona mtu anateswa akawa kimya tu cha kukifanya leo majira ya usiku nendeni pale halafu mchukueni mwanafunzi mmoja kwa nguvu na kuanza kumtesa huku mkiondoka naye hamtafika mbali kama kweli yupo lazima atajitokeza kumsaidia mwanafunzi huyo na hapo ndipo mtakapo mpata” mzee huyu huenda alikuwa ana akili nyingi sana bado hakuamini kwamba eti hizo zilikuwa ni hadithi tu alitaka kujihakikishia yeye mwenyewe juu ya hayo mambo ambayo alikuwa ameambiwa ndiyo maana aliwahimiza vijana wake ho kuweza kurudi tena ndani ya lile eneo huku yeye akirudi ndani kuendelea na shughuli yake.


Majira ya saa sita za usiku chuoni palitulia sana huku akiwa anaonekana mwanafunzi mmoja mmoja akiwa anapita pita ndio muda ambao wanaume hao walifika hapo na gari zao ambapo wakati wanapita getini palikuwa na walinzi wawili, mlinzi mmoja aliwaangalia kwa umakini mkubwa sana mpaka gari zao zilipo ishia sehemu ambayo walienda kuzipaki, tangu mchana walikuwa wamejulikana ni akina nani na wapo hapo kwa sababu ipi ndiyo sababu hakukuwa na mtu ambaye alikuwa na jeuri ya kuweza kuwasimamisha watu hao. walijongea mpaka ndani ya darasa moja mmoja kati yao akiwa na silaha yake mkononi, wanafunzi walikuwa wanasoma kwa amani sana ndani yake ila baada ya kuona watu hao tena mmoja akiwa na silaha mkononi walipiga sana makelele lakini walitulizwa na kuambiwa kama kuna ambaye angeendelea kupiga makelele basi alikuwa na dakika chache sana za kuwa salama.

Alichukuliwa mwanafunzi mmoja na wanaume hao watano kisha wakatoka naye, walianza kumtesa kwa kumtaka awe anagalagala chini huku akiwa anaimba wimbo wa taifa, walitembea naye akiwa anagala gala mpaka karibu na eneo ambalo walipaki gari zao, mmoja kati yao alimpiga buti la tumbo kijana huyo hali ambayo ilimfanya apige sana kelele za maumivu lakini hakukuwa na mtu yeyote ambaye alikuwa anasogelea eneo hilo

“Mhhhhh nadhani mlitakiwa kutangaza moja kwa moja kwamba mnanihitaji mimi na sio kuanza kumpiga bila sababu za msingi kijana wa watu ambaye hajui chochote kwenye hii dunia kama huyu” ni sauti liyo komaa ambayo iliwashtua wote watano hapo, waligeuka kwa sababu mtu huyo alitokea upande wa pili wa sehemu ambayo walikuwa wamepaki magari yao, alitokezea mbele yao na kumpa ishara mwanafunzi huyo aondoke hilo eneo haraka sana maana hata wenzake walitoka mle darasani kwa kukimbia sana kila mtu akiwa anayaokoa maisha yake. Kwenye mwili wake alivaa manguo makubwa sana ambayo yalikuwa hayaonyeshi uhalisia wa mwili wake upoje, chini alivaa mabuti makubwa sana ambayo yalimfanya aonekane kama mtu mrefu huku uso wake ukiwa umefungwa kwa vitambaa kuanzia usoni na kichwani yakiachwa macho tu pekee ndiyo yalikuwa yapo wazi.

Je ndiye huyu ambaye wao wanamtafuta kati ya wale watano? Kama ndiye mchana alikuwa wapi wakati wanamtafuta na yupo hapa kwa sababu ipi? 37 naweka nukta tukutane ndani ya sehemu ambayo inafuata.

Wasalaam
Bux the sroryteller.
 
STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 38

SONGA NAYO............
Monalisa akiwa ndani ya gari mawazo yake yalikuwa mbali sana wakati amejiegesha kwenye ile siti, alikumbuka akiwa ndani ya nchi ya Marekani baada ya kutoka John F Kenedy street kwenye ile club kukutana na mwanaume ambaye alikuwa ni moja ya viongozi wake wa CIA (Central Intelligence Agency) aliivaa mask usoni baada ya kupanda kwenye pikipiki yake. Safari yake ilikuwa ni kuelekea sehemu ambayo aliifuatilia kwa muda mrefu sana na kugundua kwamba ndipo kulikuwa nyumbani kwa professor Michael, mzee huyo alikuwa moja kati ya wahadhiri ndani ya chuo kikuu cha Havard. Lengo la Kwenda kumtafuta mzee huyo kimya kimya bila kujulikana lilikuwa ni kutaka kumbana ili aseme Jason alipoteleaje mle ndani maana hicho kitu kilianza kumtisha sana na kumfanya kichwa chake kijaze vitu viwili vya haraka haraka.

Kwanza alihisi huenda Jason alipata tatizo kubwa ndiyo maana hakutoka tena mle ndani lakini jambo la pili kama alifanikiwa kutoka mle ndani ina maana alitokea wapi? inaonyesha kulikuwa na mambo ya siri ambayo yalikuwa yakiendelea alihitaji sana kuyafahamu pamoja na kumfahamu professor Michael alikuwa ni nani hasa, hakutaka kabisa kujulikana ndiyo maana usoni kwake aliweka mask nyeusi huku sikioni kwake akiweka kifaa ambacho kilikuwa na waya mrefu ambao ulipitishwa mpaka karibu na mdomo ambacho kazi yake kubwa ilikuwa ni kubadilisha sauti ili asiweze kujulikana. Aliendesha gari yake mpaka eneo moja ambalo walikuwa wanaishi watu wenye maisha mazuri kiasi hawakuwa juu sana wala hawakuwa chini sana na hapo ndipo ambapo yeye alikuwa amejihakikishia kwamba palikuwa ni nyumbani kwa professor Michael. Aliiacha pikipiki yake mbali sana na pale ili hata likitokea lolote aone ni namna gani anaweza kujilinda na hatari yoyote kama inaweza kujitokeza, alitembea taratibu mpaka nyuma ya nyumba hicho, alitoa tablet yake kwenye mfuko wa koti na kuibonyeza mara tano tu alihitaji kuzima kamera za hiyo nyumba ili isije ikabaki hata alama ya uwepo wake hapo ingekuja kuleta shida baadae.

Alidunda mara mbili tu na kutua ndani mithili ya paka ambaye alikuwa ndani ya mawindo na hakuwa tayari kupoteza windo lake, aligeuka huku na huku hakuona mtu akaanza kusogelea eneo ambalo lilikuwa na dirisha ili aweze kulifungua apenye ndani.

“Koh koh koh, usijisumbue kuingia ndani mimi nipo huku halafu sio vizuri kuingia namna hiyo kwenye nyumba za watu ni kosa kubwa sana naweza hata kukushtaki ila kwa leo nitafanya kama hakuna kilicho tokea kama una maongezi na mimi njoo tuongee haraka niende nikapumzike” ilisikika sauti nyuma yake kutoka mbali kidogo ambayo ilimfanya moyo wake udunde kwa haraka sana, hakuelewa mtu huyo alijuaje kama yeye atakuja ndani ya hiyo nyumba. Aligeuka nyuma ili amuone huyo mtu alimuona mzee wa makamo kidogo akiwa kwenye koti lake huku akipata kahawa, sehemu ambayo alikuwa amekaa kulikuwa na maua mengi sana marefu hivyo ingekuwa ni ngumu sana kumuona na sehemu hiyo ilionekana kuwa na viti vya kukalia. Monalisa aliangaza huku na huko hakuona mtu mwingine alisogea lile eneo akiwa anaitoa bastola kwenye kiuno chake na kumsogelea mtu huyo, mawazo yake yote alijua ni professor Michael cha ajabu kufika pale alikutana na mzee mwingine tofauti kabisa tena ambaye alikuwa ni mzungu.

“Professor Michael yuko wapi?” aliuliza kwa ghadhabu kwa lugha ya kiingereza sauti ikiwa inatoka kama ya kiume akiwa anainyoosha bastola yake kwa huyo mzee ambaye alikuwa hana wasiwasi anaendelea kupata kahawa yake.
“Haipendezi kijana mdogo kama wewe kukutana na mtu mzima kama mimi halafu unashindwa kunipa hata salamu unaanza kuniuliza kwa jazba namna hiyo, hiyo ni hatari sana kwa kizazi ambacho unaenda kuwa nacho, halafu ongea sauti yako ya kike usinipotezee muda nataka nikalale nilivyo ona kuna ugeni niliamua kusubiri nimjue huyo mgeni wangu ni nani” mzee huyo aliongea huku akiwa anatua hiyo kahawa yake chini, aliongea mambo ambayo Monalisa yalianza kama kumtisha kiasi chake akasahau hata swali ambalo alikuwa ameuliza yeye mwenyewe.

“Umejuaje kama utakuwa na mgeni?”
“Hapa ni kwangu na huu ni mtaa wangu ambao nimeishi kwa muda mrefu sana, huwa najua kila nyumba wanalala saa ngapi, huwa najua muda ambao hili eneo linakuwa kimya sana, huwa najua watu wanaamka saa ngapi na mtaa unachangamka saa ngapi, majirani zangu wote nawajua na ndugu zao wote nawajua, najua huwa wanatembelewa muda gani na hao ndugu huwa wanaondoka saa ngapi hivyo baada ya kuona kuna pikipiki imeingia hapa mtaani nikajua moja kwa moja huyu mgeni atakuwa ni mgeni wangu ndiyo maana nikaamua kukusubiri ili nikusikilize” alijibu kwa kujiamini mno kwamba alikuwa anajua amepata mgeni ndiyo maana aliamua kumsubiri mgeni wake ili amsikilize, Monalisa alichoka sana alikuja hapo kwa siri kubwa lakini kumbe alikuwa anajulikana kwamba anakuja bila shaka alielewa huo mtaa lazima kuna mtu au watu ambao huwa wapo macho muda wote wanaulinda kama sio kumlinda mzee huyo hivyo huwa wanafuatilia kila hatua ya mtaa huo na kujua nini kinaendelea.

“Ok naomba uniambie haraka professor Michael yuko wapi kabla sijaingia kwenye dhambi ya kuweza kumuua mzee kama wewe maana unajifanya kunijua sana na unahisi wewe ndiye mtu makini sana”

“Mhhhh binti mdogo sana namna hiyo unaanza kunitishia mtu ambaye ninaweza kumzaa baba yako kweli, huna uoga japo kidogo binti yangu, ok tufanye ndiyo maisha ambayo vijana mmeamua kuyachagua ya kutokuwa na heshima huyo professor Michel ndo nani na unataka nini kwake? Mimi naitwa Doctor Morgan” kauli za mzee huyu zilimfanya azime hicho kifaa cha kubadilishia sauti kwa sababu aliona hakina umuhimu sana, majibu ambayo aliyapata yalimuongezea maswali mengine kwenye ubongo wake inawezekanaje huyu mzee akakana kuto kumjua professor Michael wakati yeye alihakikisha kabisa na kujipa uhakika kwamba hapo ni nyumbani kwa professor Michael? Lakini pia huyo mzee aliweza kutambua vipi kwamba yeye ni mwanamke na anaigiza sauti? Bila shaka huenda aliingia kwa mtu ambaye alikuwa mwepesi sana kwenye macho yake lakini hakuwa kama yeye alivyokuwa anamdhania kwenye uhalisia wa mzee huyo.

“Hhahahaha we mzee unanifanyia mzaha sio sasa ngoja nikuguse kidogo ili upunguze huo uswahili wa kunijibu unavyo jisikia” alitamka kwa hasira baada ya kuona mzee huyo ni kama alikuwa anamchangaya tu huku akiikoki bastola hiyo na kuhitaji kumpiga na kitako cha bastola mzee huyo, kitu kilicho mshangaza alijishtukia yupo chini umbali kadhaa kutoka pale alipokuwa amesimama mwanzo, bastola yake hakuwa nayo kwenye mikono yake tena ilidondokea mbali sana, mbavu yake ya upande wa kulia ilikuwa inauma sana na kumfanya aume meno yake kwa maumivu ambayo yalichanganyikana na hasira, alituliza akili ili aelewe alifanywa nini, alisimama na kumuona mtu amesimama mbele ya mzee huyo huku huyo mzee akiwa anaendelea kupata kahawa yake bila wasiwasi.

Wakati yeye anajiandaa kushusha bastola hiyo ili ampige nayo mzee huyo ambaye alijitambulisha kama Dr Morgan ambaye alihisi kama anampotezea muda mkono wake ulidakwa kwa nguvu na kuvutwa kwa kasi kisha alipigwa ngumi mbili kwenye mbavu yake na kushindiliwa teke zito kifuani ambalo lilimrusha mbali na bastola yenyewe ilimponyoka kwenye mkono wake na kudondokea mbali, alitikisa kichwa chake baada ya akili yake kukumbuka hilo tukio maana lilifanyika kwa muda mfupi sana ambao hata yeye ulimshangaza mno. Alimkadiria mtu huyo ambaye alikuwa na mavazi meusi kama yake lakini yeye hakuvaa mask bali alivaa barakoa pamoja na kitamba ambacho alikipitisha juu ya paji la uso wake na kuzipanga vizuri nywele zake sura ilikuwa haionekani kabisa, alijikusanya na kuruka sarakasi mbili za mwendokasi akiwa anachomoa kisu kwenye buti lake, alirusha kisu hicho kwa nguvu mwanaume huyo aliinama na kumsukuma huyo mwanamke, wakati anatua chini alijigeuza kwa teke zito ambalo lilimpata mwanaume huyo kwenye shingo mpaka akakunja sura yake japo hakurudi nyuma hilo teke lilionekana kumuingia vizuri, mwanamke huyo hakuonekana kuwa mtu wa kawaida mapigo yake yalionekana kuwa ni aina ya watu ambao huwa wanafanya kazi za mauaji na anajua ni wapi akupige na wapi akuguse ili ufe haraka sana.

Monalisa alitabasamu kidogo ndani ya mask yake na kuja kwa mfumo wa kuzunguka huku akiwa anakizungusha kisu chake kwa kasi sana alihitaki kutoka na shingo ya mtu huyo ambaye hakuwa amemjua ni nani mpaka muda huo wakati huo Dr Morgan alikuwa anapitia pitia magazeti sehemu ambayo alikuwa amekaa huku watu hao wawili wakiwa wanaipasha miili yao, Monalisa alivyosogea kwa mtu huyo alishangaa amekata hewa alihisi mtu huyo yupo pembeni maana kilikuwa ni kitendo cha haraka sana aligeuka kwa wepesi na kutaka kuchoma sehemu ya moyo ya mtu huyo, mtu huyo alirudi nyuma kidogo kisha akamjia Monalisa kwa nguvu ni kama mara ya kwanza alikuwa anamuonea huruma kwa sasa aliamua kuuvaa uhalisia wake, Monalisa alipigwa ngumi ya kifua mpaka alikohoa, kabla hajavuta pumzi aliguswa kwenye bega na kiganja cha mkono kisha akatishiwa ngumi ya uso ambayo ilikuja kama machine mpaka alifumba macho hakuwa na namna ya kuikwepa lakini mtu huyo hakuifikisha bali aliishusha na kumpiga nayo kifuani, ilimpeleka mwanamke huyo mbali sana, mwanaume huyo alienda kuiokota bastola ya Monalisa alivyo sogeleana naye wakati anamkabidhi mwanamke huyo bastola yake ndipo Monalisa aligundua kwamba huyo ni kijana wa kiume tena mdogo tu.

“Nisingekuwa nakujua basi leo ningekuua, mwanamke mrembo kama wewe hautakiwa kupigwa vibaya sana namna hii ndiyo maana sijataka kukupiga usoni maana hakuna daktari ambaye angeweza kuirudisha hiyo sura yako nzuri uliyo nayo, bado mwili wako ni mlaini sana ambao hauwezi kuhimili hata pigo moja bila kutetereka hivyo hakikisha hapa hauji kurudi tena” kijana huyo aliongea bila kuwa na wasiwasi wakati akimkabidhi bibie bastola yake ambayo alikuwa ameidondosha kisha yeye akawa anaondoka hilo eneo, Monalisa alibaki anawashangaa hao watu kwa sababu walionekana wanamjua sana tena zaidi ya sana, alikuwa kwenye mask walijuaje kama yeye ana sura nzuri na mtu huyo kusema kwamba kama asingekuwa anamjua basi angemuua, anamjua vipi na anahusiana naye vipi mpaka amsamehe? Alijikuta akiwa mwingi wa wasiwasi sana na alijuta kuja hilo eneo.

“Una bahati sana mpaka amekuacha hai basi ujue kuna sababu kubwa sana, hakuna mtu anaweza kuja kunitishia mimi maisha halafu akaendelea kuishi tena, jina langu kama mimi nilivyoweza kukwambia naitwa Dr Morgan nimekushangaa sana unasema professor Michael kwani ni nani huyo na anahusiana nini na wewe?” mzee huyo alikuwa amesogea hilo eneo na kumkabidhi Monalisa kikombe cha kahawa, alivamia hilo eneo lakini alijikuta yeye ndiye anakuwa kama mgeni mualikwa kabisa, hakuwa na cha kujificha ficha aliamua kutoa mask yake na kunywa hiyo kahawa.

“Hivi kwani nyie ni akina nani?” aliuliza wakiwa wanaelekea kukaa kwenye viti
“Sisi ni watu wa kawaida tu kama wewe hapo mimi ni Dr nina mali nyingi sana hivyo kuna watu wengi huwa wanahitaji kunipata ili wajichukulie mali zangu ndiyo maana nina ulinzi binafsi lakini pia wewe nakujua ni moja ya wanafunzi wa pale chuo kikuu cha Havard kwa sababu huwa nafundisha pale mara moja moja na kwenye mifumo ya chuo mimi nina kila picha ya mwanafunzi wa pale maana huwa napima sana DNA zenu ndiyo maana mimi nakujua vizuri sana hata kijana wangu anakujua kupitia hilo kwani huwa ananisaidia baadhi ya kazi hicho ndo kimekufanya ukabaki salama, tuachane na hayo kwani huyo unaye mtafuta ni nani?” mzee huyo alitoa maelezo ya kujibu swali la Monalisa huku naye akimuuliza swali Monalisa

“Ni professor ndani ya chuo cha Havard, kuna siku niliwahi kumuona akiingia hapa hivyo nikajua ni kwake naomba unisamehe sana kwa usumbufu nilio uleta kwako”
“Sasa ndo uje na bastola vipi kakufanya nini?”
“Amna ni mambo binafsi tu” Monalisa alijibu huku akiwa amenyanyuka na kuanza kuondoka hakutaka kumpa ukweli mzee huyo, alikuwa anelekea nyuma ya ukuta ili aruke tena lakini mzee huyo alimpa ishara apitie mlangoni naye akafanya hivyo, baada ya kufika nje aligeuka kuiangalia nyumba hiyo akiwa na maumivu kwenye mbavu yake, aliwaza sana na alikuwa ana uhakika hapo ndipo alipo muona mtu huyo sasa nini kilifanyika mpaka awe amekosea akili yake iligoma kabisa kuamini akaamua kuondoka. Dr Morgan aliingia ndani kwake haraka sana na kupitiliza mpaka kwenye chumba chake, aliingia kwenye machine moja ambamo alikaa kwa dakika 10 baada ya kutoka kwenye machine hiyo alikuwa amebadilika kabisa na sura yake ilirudi kwenye uhalisia huyu alikuwa ni professor Michael mwenyewe, alichukua kinywaji chake na kuanza kunywa taratibu.

Monalisa baada ya kuondoka lile eneo hakuamini kabisa, alipiga simu mahali na kuutaka upande wa pili kwenye simu hiyo uende na watu wa kutosha kwenye nyumba ambayo yeye alielekeza sehemu hiyo watamkuta mzee mmoja wahakikishe wanaondoka naye, alisubiri kwa masaa mawili jibu alilopewa lilimchosha sana, watu aliokuwa amewaagiza walimrudishia majibu kwamba kwenye hiyo nyumba hakuna mzee yeyote yule bali ilikuwa ni familia ya baba mmoja mwenye mke na mtoto mmoja tena ni askari, hakuamini mpaka alipotumiwa video na nyumba ilikuwa ni ile ile. Kumbukumbu zake ziliishia hapo wakati akiwa ameshtuka kwenye gari alikuwa ameefika na dereva ndiye aliyekuwa amemuamsha na rasmi alikuwa ametua kwenye viunga vya nchi ya amani kukamilisha kazi ambayo alisema anakuja kuifanya pamoja na kumtafuta mwanaume wake.

Huyu professor Michael ni nani mpaka anaicheza hii michezo ya hatari sana namna hii? huko Marekani anatafuta nini, na ni mtu wa aina gani mpaka anaonekana kumiliki watu hatari sana namna hii ingali wanamjua kama professor ndani ya chuo kikuu cha Havard?....38 inafika tamati tukutane wakati ujao.

Wasalaam

Bux the storyteller.
JamiiForums1586263124.jpg
 
STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 39

SONGA NAYO............
“Mhhhhh ndo wewe mmoja wa miongoni mwa hao watano wanao daiwa kuwa wa siri sana?” kiongozi wa hao wanaume watano ambao walikuwa wametumwa na mkuu wa majeshi ndani ya chuo cha NIT aliongea kwa sauti yake nzito baada ya kumuona mwanaume huyo ambaye hata uso wake ulikuwa hauonekani kabisa, hiyo kauli ilimshtua sana japo hakutaka kuonyesha mshtuko wa moja kwa moja.

“Hii ni hatari sana kama tumesha anza kujulikana ni ishara mbaya mno” alijiongelesha mwenyewe kwenye nafasi yake akionyesha wasiwasi wa wazi baada ya kusikia hayo maneno hakujibu chochote alikuwa anawakadiria tu hao wanaume.

“Toa jibu la ninacho kuuliza kabla sijapata hatia ya kuua kiumbe kisichokuwa na hatia yoyote ile”
“Hahahahaha hahahah watu wa kawaida kama nyie ndiyo mnasema mnaogopa kuua kiumbe kisichokuwa na hatia? Ok ni nani aliyewapa taarifa kwamba mtanikuta hapa?” hakuwa na cha kuwaficha hao wanaume kwa sababu aliona ni kama walikuwa na taarifa za kutosha sana hivyo walikuwa wanajua kuna mtu hili eneo japo alijua kabisa kwamba walikuwa hawamjui sura yake.

“Acha kupoteza muda kuuliza maswali ya kijinga, jifunge mwenyewe pingu hizo kisha tuondoke hapa” jibu la mwanaume huyo lilimfanya achukie sana, yaani walikuwa wanamchukulia vipi mpaka wamrushie hizo pingu na kumwambia ajifunge?
“Una mtu yeyote kwenye familia yako ambaye anakutegemea na ukiondoka ataishi maisha magumu sana” alimuuliza mwanajeshi huyo kwa hasira sana huenda alitaka kufanya matukio ya kutisha sana kwenye hilo eneo
“Haahahahah hahaha wapo mahawala wengi sana ambao wanaishi hapa mjini kwa sababu ya kutegemea uwepo wangu, acha kupoteza muda usije ukafanya nikakuua badala ya kukupeleka unako hitajika” aliongea akiwa anawapa ishara vijana wakamchukue mwanaume huyo ambaye alionekana kwamba ni kijana mudogo sana

“Kuna wanazuoni wawili ambao huwa nazipenda sana kauli zao, wa kwanza aliwahi kusema kuna watu wapo hai kwa sababu tu ni kosa kisheria kuwaua alimaanisha kwamba kuna watu hawatakiwi kuwa hai basi tu kwa sababu sheria inasema kila mtu ana haki ya kuishi lakini mwingine alisema kwamba kuna watu huwa wanakufa wakiwa na miaka 25 ila huwa wanazikwa wakiwa na miaka 75 huyu wa pili alimaanisha kwa wale watu ambao hawana akili mmoja wao ni wewe hapo, unakuja kumtisha mtu ambaye humjui kwa sababu tu umeambiwa kamchukue bila kujiuliza kwa sababu ipi unamchukua unakazania tu, mimi huwa siongei sana leo nimeongea kwa sababu nipo eneo ambalo najua linahitaji amani na usalama wa wanafunzi hawatakiwi kuona mambo ya ajabu ndiyo maana nimekuwa mstaarabu sana vinginevyo mpaka wakati huu ungekuwa unahangaika kuitafuta pumzi yako ya mwisho. Mimi nimesha wajua kwa sura zenu na nitawatafuta nitakapokuwa na shida na nyie nendeni mkamwambie huyo ambaye amewatuma kama amefanikiwa kutambua uwepo wetu basi ni muda mfupi sana umebakia ili tumfikie hivyo mpatie taarifa kwamba ana miezi sita tu ya kuishi anavyotaka yeye baada ya hapo ataishi kwa namna tunavyotaka sisi” maneno ya busara pamoja na maelekezo yalimtoka kijana huyo huku akigeuka na kuanza kuondoka hilo eneo maana aliwasihi waweze kuondoka kwa amani kwa sababu eneo ambalo alikuwepo hakutakiwa kufanya mambo ya kutisha labda kama ingemlazimu kufanya hivyo basi asingekuwa na namna nyingine

Hakufika mbali sana alihisi hatua za mtu zinamjia pale alipo, aliyafumba macho yake, wakati anayafumbua yalikuwa ni mekundu sana, alikuwa anajitoa ule ufahamu wa kibinadamu na kuwa na haruma alihitaji kuingia kwenye ulimwengu wa uhalisia wake kama watu hao walishindwa kumuelewa kwa mdomo basi walitakiwa kujutia kufanya maamuzi ya kijinga na sasa dunia ingewapa namna sahihi na nzuri zaidi ya kuishi na wanadamu, aligeuka kwa kasi sana mwanaume ambaye alikuwa anakuja kwa nguvu kubwa alikuwa karibu kufika hilo eneo ila alipunguza spidi baada ya kuhisi kama anaona kivuli cha mtu kinakuja na sio mtu kamili alitoa macho ila alikuwa anjipotezea sana muda wa kuwa salama alipigwa na ngumi sita kwenye shingo yake, shingo ililainika kama mlenda hakuwa na uhai tena kwenye mwili wake kisha alipigwa na buti mbili za kifua baada ya mwanaume huyo kujirusha hewani na kutua akiwa amesimama, mwanajeshi huyo alienda kudondokea mbele ya miguu ya kiongozi wao huyo wa hao watano, aliinama na kumkagua mwenzake alikuwa amekufa miaka mingi sana, alishtuka sana inawezekana vipi mtu afe kirahisi sana namna hiyo?

Walipata hasira sana, wanajeshi wawili ambao walichomoa visu walikuwa wanamwendea huyo kijana baada ya kuona ameleta madhara kwa mwenzao, hawakutaka kutumia risasi kwa sababu zingeleta kelele na kuzua taharuki sana ndani ya eneo hilo, visu vyao ambavyo vilikuwa vinarushwa kwa nguvu vilizama kwenye gwanda la mwanaume huyo lakini hakuna hata mmoja ambaye alifanikiwa kuugusa mwili wake, mmoja alizungushiwa kiganja kwenye mbavu yake wakati anajinausa aliguswa na ngumi mithili ya tofali kwenye tumbo alihema kama vile kagongwa na nyundo hata kisu hakuwa na nguvu ya kukishika tena kilimponyoka na kutua kwenye mikono ya kijana huyo alikizamisha kwenye shingo ya mwanajeshi huyo na kuichana kama vile anachana karatasi mwanaume huyo aliachiwa na kudondoka chini akiwa anaruka ruka kama maji yanayo chemka mwenzake alikuwa anatetemeka alishangaa damu zinamtoka kwenye kifua chake upande wa moyo.

Alihisi kachomwa na kisu chake lakini alikuwa nacho mkononi, aliinua macho yake na kuona kuna nguo leusi ndilo nilikuwa limefika kwenye kifua chake hapo ndipo alipogundua kwamba ndani ya nguo hiyo nyeusi kulikuwa na upanga wa mwanaume huyo, alizungusha nguo hilo ambalo lilikuwa lipo ndani ya mwili wake huenda ndiyo maana alikuwa anavaa minguo mikubwa kumbe humo ndani alikuwa ana upanga mkubwa na mgumu sana sasa ulikuwa unaonekana vyema huo ndio ambao alimchoma nao mwanajeshi huyo, akiwa anatapa tapa upanga huo ulizamishwa zaidi kisha ukalazimishwa kushushwa chini ni kama alikuwa anafanyia oparesheni alitoa sana macho kuomba msaada ila hakuweza kutamka neno lolote alikufa hapo hapo. Wawili waliokuwa wamebaki walikuwa wameanza kuogopa sana hata yule kiongozi wa hao wanajeshi, aliona ule upanga ukiwa umerushwa lile eneo ambalo yeye alikuwepo alimvuta mwanajeshi mwenzake na kumtumia kama ngao upanga huo ulienda kunasa kwenye koromeo la kijana huyo ilibaki kidogo ufika mpaka kwake alibaki akiwa anatetemeka sana.

“Mimi ndiye huyo ambaye wewe umekuja hapa kumfuata ana kusema unamchukua kirahisi sana namna hiyo vipi unahitaji tuongozane wote?” Kijana huyo aliongea wakati amefika hapo na kuuchomoa upanga wake, alitoa mafuta kwenye kikopo akausafisha na kuurudishia kwenye nguo lake na kuuzamisha kwenye minguo yake hiyo mikubwa, alitoa bastola yake kiunoni ambayo ilikuwa na kizuia sauti alimmiminia risasi tano yule mwanajeshi ambaye kiongozi wao alimtumia kama ngao kwa sababu alikuwa bado anahema pale chini

“Hapana Hapana naomba unisamehe” alitamka wka wasiwasi sana akiwa anasogea nyuma
“Hii dunia sio salama sana kama unavyohisi ndiyo maana unajiamini na kuhisi kwamba unaweza kuingia sehemu yoyote ile bila wewe kuogopa chochote, leo nimekuonea huruma wewe kwa sababu huenda ulikuwa haufahamu chochote na pia nakuacha salama ili uirudushe miili ya hawa wenzako ikazikwe, nenda kamwambie huyo aliyekutuma ile kauli ambayo nimekwambia mwanzo, ataishi anavyotaka yeye kwa miezi sita ila baada ya hapo ataishi kwa namna tunavyotaka sisi” aliongea kwa msisitizo akiwa anamwangalia mwanaume huyo na kuanza kuondoka hilo eneo.

“Wewe unaitwa nani?” mwanajeshi huyo alijivika ujasiri na kuuliza, aligeuka na kumwangalia kwa umakini sana
“Hakikisha unasafisha hilo eneo pasibaki alama yoyote ile, “We are the five poisoned serial killers waweza kutuita THE TOXIC, sisi tutarudi uraiani baada ya miezi sita hivyo waambie hao watu wajiandae wamefanya kosa kubwa sana ambalo hatuwezi kuwasamehe mimi nakwenda nina imani mimi na wewe hatuta onana tena kama tutaonana uwe umeokoka vinginevyo nitakuua” alitamka huku akiwa ameanza kuondoka, alipotelea ndani ya mejengo na hakueleweka anaenda wapi ila aliahidi kwamba watarudi baada ya miezi sita maana yake ni kwamba kwa huo muda walikuwa wanapotea kwenye michanganyiko ya watu na kauli yake ya kusema kwamba hawataonana tena ilimaanisha kwamba hata wakirudi ndani ya hilo eneo basi wasingeweza kumpata tena maana yake baada ya kugundulika kwamba yupo eneo hilo alikuwa anapotea jumla.

Yule mwanajeshi aliichukua miili ya wenzake na kuipakiza kwenye gari moja akiwa ana wasiwasi mkubwa sana, aliwasha gari na kutoka nayo hilo eneo mwili wake ukiwa unatetemeka mno mambo ambayo alikuwa ameyaona mbele yake yalikuwa yanamnyima amani hali hiyo ilimpelekea yeye kuendesha gari mithili ya kichaa, alifika Kawe na kugonga geti kwa fujo sana mpaka walinzi wa kwenye hiyo nyumba walishangaa sana, baada ya kufungua kijana huyo alikimbilia mpaka ndani ambako alimkuta mheshimiwa akiwa amekaliwa na mrembo mmoja mpaka muda huo alikuwa anaendelea kupata buruani na kuzisulubu nyeti zake, mwanajeshi huyo akiwa kwenye suti yake akipiga magoti mbele ya mkuu wa majeshi.

“Nipe maelezo” aliongea kwa ukali huku akiwa anamtoa mwanamke huyo juu yake na kusimama, alisimama na Kwenda kwenye kabati alitoa pesa na kuwarushia wanawake hao akiwataka wavae haraka sana na kuondoka humo ndani kama ni nguo wakavalie huko nje, hali aliyokuwa ameiona kwa kijana wake alijua moja kwa moja huko alikotoka hakukuwa kwema sana kama siyo mambo kuharibika. Wanawake hao waliondoka humo ndani wakiwa uchi kila mtu akiwa ameshika nguo yake na pesa mkononi, kwao kutoka hivyo hakukuwa na shida kubwa sana, shida yao ilikuwa ni pesa na kila mtu alikuwa ameikunja milioni mbili tena kwa muda mfupi tu wa kumfurahisha tajiri huyo ambaye hawakujua kama ni mkuu wa majeshi wa nchi ya Tanzania, hiyo pesa ni mshahara wa mwezi wa mtu mwenye kazi ya maana sana lakini wao masaa kadhaa tu walikuwa nayo na muda huo huo walitarajia Kwenda kuendelea na hiyo biashara hayo ndiyo maisha halisi ya sasa kwenye huu ulimwengu.

“Mkuu naomba unisamehe sana, wale sio watu kama tulivyokuwa tunasema ni kama mashine ambazo zimetengenezwa tumafanikiwa kukutana naye muda sio mrefu”

“Yuko wapi mbona umekuja huku na nimekwambia mmpeleke dark house” CDF alitamka aki?wa anavaa nguo nzito ambayo iliufunika mwili wake vizuri
“Wenzanngu wote wamekufa”
“Whaaaaaat?” kauli hiyo ilimshtua sana CDF na kumfanya amsogelee kijana huyo na kumshika shingo yake kama mtu anaye hitaji kumnyonga

“Tumefika pale tumefanya kama ulivyo tuelekeza baadae akaja kujitokeza kweli amewaua wenzangu vifo vibaya sana nikiwa naona mbele ya macho yangu na amenipa maagizo ambayo alisema ni mhimu sana mimi kukufikishia” alikuwa anatamka kwa shida kwa namna alivyokuwa amekabwa, alikaziwa macho mpaka yeye mwenyewe akaamua kuendelea kutoa maelezo

“Amesema kwamba utaishi unavyotaka wewe kwa miezi sita tu lakini baada ya huo muda kuisha utaishi kwa namna wanavyo taka wao, nimemuuliza jina kake hajajitaja ila amesema wao wanaitwa The five poisoned serial killers au The TOXIC” CDF aliizungusha shingo ya kijana huyo na kuitupa chini baada ya kuyasikia hayo maelezo, aliipiga meza kwa hasira sana mpaka baadhi ya vijana wake waliokuwa nje wakaingia ndani kwa kuhisi kwamba huenda bosi wao alikuwa kwenye matatizo lakini walicho kutana nacho ni mwili wa mwenzao ukiwa chini waliuchukua na Kwenda kuupakiza kwenye gari ambayo alikuja nayo kukiwa na miili ya wenzake wanne kisha mmoja wa hao wanaume akaondoka na hilo gari kazi ilikuwa ni kwenda kuiteketeza miili hiyo. CDF alipandisha mpaka chumbani kwake aliichukua simu na kuipiga mahali.

“Hicho chuo cha NIT nahitaji kesho kiwe chini ya jeshi kuna kazi maalumu ya kuweza Kwenda kuifanya pale hakikisha kwa kesho hakuna shughuli ambayo inaendelea mpaka nitakapokupa ruhusa yangu mimi” aliongea kwa jazba na kukata simu yake akiwa na gadhabu mno, akiwa kwenye hayo mawazo simu yake iliianza kuita, aliangalia aliyekuwa anapiga alikuwa ni IGP

“Nakusikiliza” aliongea kwa sauti ambayo haikuwa ya kirafiki
“Ndugu yangu ebu nisikilize kwa umakini kwa mara ya mwisho tena, sikwambii haya kwa sababu nakufuatilia sana ila wewe kwangu ni kama kaka na nakuheshimu sana, tumetoka mbali mno mimi binafsi kwa yote ambayo nina uhakika umeyafanya nitakusamehe kwani najua binadamu tumezaliwa tukiwa watu wenye tamaa sana huenda uliteleza ila kuna mtu hatakuelewa siku utakapokuwa hauna namna zaidi ya kutegemea msamaha uendelee kuyalinda maisha yako hata mimi sina uwezo wa kumzuia wala kukulinda wewe ebu achana na haya mambo ndugu yangu, leo nimepata habari mchana uliagiza vijana wako waende pale ni kwa sababu tu bado huwajui hawa watoto ipo siku utanikumbuka sana na….” aliikata simu hiyo baada ya kuona kama mwenzake huyo alikuwa anampotezea muda kwanza alimuona kama mnafiki sana maana alionekana kuyajua mambo mengi mno lakini cha ajabu hakuwahi kumwambia chochote na hata juzi alitoka kumpa taarifa ambazo ndani yake zilikuwa zina ukakasi mwingi sana.

“Kwa sababu wameamua iwe hivi basi namimi nawasubiri kwa hiyo miezi sita ifike ili nijidhihirishe mimi ni nani, nadhani ni muda sahihi pia wa kuanza kuwaagiza vijana wangu kazini kwa yeyote atakaye jifanya kuingilia katika hili basi hatafanikiwa kuyamaliza masaa 24, nawasubiri wapuuzi nyie” alitamka kwa msisitizo sana huku akiipasua simu ambayo ilikuwa kwenye mkono wake na kutoka humo ndani.

Bado tupo taratibu na INNOCENT KILLER (THE REVENGE) sehemu ya 39 inafika mwisho tukutane ndani ya sehemu ijayo.

Wasalaam

Bux the storyteller.
FB_IMG_1686457206350.jpg
 
Back
Top Bottom