STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL:
thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 39
SONGA NAYO............
“Mhhhhh ndo wewe mmoja wa miongoni mwa hao watano wanao daiwa kuwa wa siri sana?” kiongozi wa hao wanaume watano ambao walikuwa wametumwa na mkuu wa majeshi ndani ya chuo cha NIT aliongea kwa sauti yake nzito baada ya kumuona mwanaume huyo ambaye hata uso wake ulikuwa hauonekani kabisa, hiyo kauli ilimshtua sana japo hakutaka kuonyesha mshtuko wa moja kwa moja.
“Hii ni hatari sana kama tumesha anza kujulikana ni ishara mbaya mno” alijiongelesha mwenyewe kwenye nafasi yake akionyesha wasiwasi wa wazi baada ya kusikia hayo maneno hakujibu chochote alikuwa anawakadiria tu hao wanaume.
“Toa jibu la ninacho kuuliza kabla sijapata hatia ya kuua kiumbe kisichokuwa na hatia yoyote ile”
“Hahahahaha hahahah watu wa kawaida kama nyie ndiyo mnasema mnaogopa kuua kiumbe kisichokuwa na hatia? Ok ni nani aliyewapa taarifa kwamba mtanikuta hapa?” hakuwa na cha kuwaficha hao wanaume kwa sababu aliona ni kama walikuwa na taarifa za kutosha sana hivyo walikuwa wanajua kuna mtu hili eneo japo alijua kabisa kwamba walikuwa hawamjui sura yake.
“Acha kupoteza muda kuuliza maswali ya kijinga, jifunge mwenyewe pingu hizo kisha tuondoke hapa” jibu la mwanaume huyo lilimfanya achukie sana, yaani walikuwa wanamchukulia vipi mpaka wamrushie hizo pingu na kumwambia ajifunge?
“Una mtu yeyote kwenye familia yako ambaye anakutegemea na ukiondoka ataishi maisha magumu sana” alimuuliza mwanajeshi huyo kwa hasira sana huenda alitaka kufanya matukio ya kutisha sana kwenye hilo eneo
“Haahahahah hahaha wapo mahawala wengi sana ambao wanaishi hapa mjini kwa sababu ya kutegemea uwepo wangu, acha kupoteza muda usije ukafanya nikakuua badala ya kukupeleka unako hitajika” aliongea akiwa anawapa ishara vijana wakamchukue mwanaume huyo ambaye alionekana kwamba ni kijana mudogo sana
“Kuna wanazuoni wawili ambao huwa nazipenda sana kauli zao, wa kwanza aliwahi kusema kuna watu wapo hai kwa sababu tu ni kosa kisheria kuwaua alimaanisha kwamba kuna watu hawatakiwi kuwa hai basi tu kwa sababu sheria inasema kila mtu ana haki ya kuishi lakini mwingine alisema kwamba kuna watu huwa wanakufa wakiwa na miaka 25 ila huwa wanazikwa wakiwa na miaka 75 huyu wa pili alimaanisha kwa wale watu ambao hawana akili mmoja wao ni wewe hapo, unakuja kumtisha mtu ambaye humjui kwa sababu tu umeambiwa kamchukue bila kujiuliza kwa sababu ipi unamchukua unakazania tu, mimi huwa siongei sana leo nimeongea kwa sababu nipo eneo ambalo najua linahitaji amani na usalama wa wanafunzi hawatakiwi kuona mambo ya ajabu ndiyo maana nimekuwa mstaarabu sana vinginevyo mpaka wakati huu ungekuwa unahangaika kuitafuta pumzi yako ya mwisho. Mimi nimesha wajua kwa sura zenu na nitawatafuta nitakapokuwa na shida na nyie nendeni mkamwambie huyo ambaye amewatuma kama amefanikiwa kutambua uwepo wetu basi ni muda mfupi sana umebakia ili tumfikie hivyo mpatie taarifa kwamba ana miezi sita tu ya kuishi anavyotaka yeye baada ya hapo ataishi kwa namna tunavyotaka sisi” maneno ya busara pamoja na maelekezo yalimtoka kijana huyo huku akigeuka na kuanza kuondoka hilo eneo maana aliwasihi waweze kuondoka kwa amani kwa sababu eneo ambalo alikuwepo hakutakiwa kufanya mambo ya kutisha labda kama ingemlazimu kufanya hivyo basi asingekuwa na namna nyingine
Hakufika mbali sana alihisi hatua za mtu zinamjia pale alipo, aliyafumba macho yake, wakati anayafumbua yalikuwa ni mekundu sana, alikuwa anajitoa ule ufahamu wa kibinadamu na kuwa na haruma alihitaji kuingia kwenye ulimwengu wa uhalisia wake kama watu hao walishindwa kumuelewa kwa mdomo basi walitakiwa kujutia kufanya maamuzi ya kijinga na sasa dunia ingewapa namna sahihi na nzuri zaidi ya kuishi na wanadamu, aligeuka kwa kasi sana mwanaume ambaye alikuwa anakuja kwa nguvu kubwa alikuwa karibu kufika hilo eneo ila alipunguza spidi baada ya kuhisi kama anaona kivuli cha mtu kinakuja na sio mtu kamili alitoa macho ila alikuwa anjipotezea sana muda wa kuwa salama alipigwa na ngumi sita kwenye shingo yake, shingo ililainika kama mlenda hakuwa na uhai tena kwenye mwili wake kisha alipigwa na buti mbili za kifua baada ya mwanaume huyo kujirusha hewani na kutua akiwa amesimama, mwanajeshi huyo alienda kudondokea mbele ya miguu ya kiongozi wao huyo wa hao watano, aliinama na kumkagua mwenzake alikuwa amekufa miaka mingi sana, alishtuka sana inawezekana vipi mtu afe kirahisi sana namna hiyo?
Walipata hasira sana, wanajeshi wawili ambao walichomoa visu walikuwa wanamwendea huyo kijana baada ya kuona ameleta madhara kwa mwenzao, hawakutaka kutumia risasi kwa sababu zingeleta kelele na kuzua taharuki sana ndani ya eneo hilo, visu vyao ambavyo vilikuwa vinarushwa kwa nguvu vilizama kwenye gwanda la mwanaume huyo lakini hakuna hata mmoja ambaye alifanikiwa kuugusa mwili wake, mmoja alizungushiwa kiganja kwenye mbavu yake wakati anajinausa aliguswa na ngumi mithili ya tofali kwenye tumbo alihema kama vile kagongwa na nyundo hata kisu hakuwa na nguvu ya kukishika tena kilimponyoka na kutua kwenye mikono ya kijana huyo alikizamisha kwenye shingo ya mwanajeshi huyo na kuichana kama vile anachana karatasi mwanaume huyo aliachiwa na kudondoka chini akiwa anaruka ruka kama maji yanayo chemka mwenzake alikuwa anatetemeka alishangaa damu zinamtoka kwenye kifua chake upande wa moyo.
Alihisi kachomwa na kisu chake lakini alikuwa nacho mkononi, aliinua macho yake na kuona kuna nguo leusi ndilo nilikuwa limefika kwenye kifua chake hapo ndipo alipogundua kwamba ndani ya nguo hiyo nyeusi kulikuwa na upanga wa mwanaume huyo, alizungusha nguo hilo ambalo lilikuwa lipo ndani ya mwili wake huenda ndiyo maana alikuwa anavaa minguo mikubwa kumbe humo ndani alikuwa ana upanga mkubwa na mgumu sana sasa ulikuwa unaonekana vyema huo ndio ambao alimchoma nao mwanajeshi huyo, akiwa anatapa tapa upanga huo ulizamishwa zaidi kisha ukalazimishwa kushushwa chini ni kama alikuwa anafanyia oparesheni alitoa sana macho kuomba msaada ila hakuweza kutamka neno lolote alikufa hapo hapo. Wawili waliokuwa wamebaki walikuwa wameanza kuogopa sana hata yule kiongozi wa hao wanajeshi, aliona ule upanga ukiwa umerushwa lile eneo ambalo yeye alikuwepo alimvuta mwanajeshi mwenzake na kumtumia kama ngao upanga huo ulienda kunasa kwenye koromeo la kijana huyo ilibaki kidogo ufika mpaka kwake alibaki akiwa anatetemeka sana.
“Mimi ndiye huyo ambaye wewe umekuja hapa kumfuata ana kusema unamchukua kirahisi sana namna hiyo vipi unahitaji tuongozane wote?” Kijana huyo aliongea wakati amefika hapo na kuuchomoa upanga wake, alitoa mafuta kwenye kikopo akausafisha na kuurudishia kwenye nguo lake na kuuzamisha kwenye minguo yake hiyo mikubwa, alitoa bastola yake kiunoni ambayo ilikuwa na kizuia sauti alimmiminia risasi tano yule mwanajeshi ambaye kiongozi wao alimtumia kama ngao kwa sababu alikuwa bado anahema pale chini
“Hapana Hapana naomba unisamehe” alitamka wka wasiwasi sana akiwa anasogea nyuma
“Hii dunia sio salama sana kama unavyohisi ndiyo maana unajiamini na kuhisi kwamba unaweza kuingia sehemu yoyote ile bila wewe kuogopa chochote, leo nimekuonea huruma wewe kwa sababu huenda ulikuwa haufahamu chochote na pia nakuacha salama ili uirudushe miili ya hawa wenzako ikazikwe, nenda kamwambie huyo aliyekutuma ile kauli ambayo nimekwambia mwanzo, ataishi anavyotaka yeye kwa miezi sita ila baada ya hapo ataishi kwa namna tunavyotaka sisi” aliongea kwa msisitizo akiwa anamwangalia mwanaume huyo na kuanza kuondoka hilo eneo.
“Wewe unaitwa nani?” mwanajeshi huyo alijivika ujasiri na kuuliza, aligeuka na kumwangalia kwa umakini sana
“Hakikisha unasafisha hilo eneo pasibaki alama yoyote ile, “We are the five poisoned serial killers waweza kutuita THE TOXIC, sisi tutarudi uraiani baada ya miezi sita hivyo waambie hao watu wajiandae wamefanya kosa kubwa sana ambalo hatuwezi kuwasamehe mimi nakwenda nina imani mimi na wewe hatuta onana tena kama tutaonana uwe umeokoka vinginevyo nitakuua” alitamka huku akiwa ameanza kuondoka, alipotelea ndani ya mejengo na hakueleweka anaenda wapi ila aliahidi kwamba watarudi baada ya miezi sita maana yake ni kwamba kwa huo muda walikuwa wanapotea kwenye michanganyiko ya watu na kauli yake ya kusema kwamba hawataonana tena ilimaanisha kwamba hata wakirudi ndani ya hilo eneo basi wasingeweza kumpata tena maana yake baada ya kugundulika kwamba yupo eneo hilo alikuwa anapotea jumla.
Yule mwanajeshi aliichukua miili ya wenzake na kuipakiza kwenye gari moja akiwa ana wasiwasi mkubwa sana, aliwasha gari na kutoka nayo hilo eneo mwili wake ukiwa unatetemeka mno mambo ambayo alikuwa ameyaona mbele yake yalikuwa yanamnyima amani hali hiyo ilimpelekea yeye kuendesha gari mithili ya kichaa, alifika Kawe na kugonga geti kwa fujo sana mpaka walinzi wa kwenye hiyo nyumba walishangaa sana, baada ya kufungua kijana huyo alikimbilia mpaka ndani ambako alimkuta mheshimiwa akiwa amekaliwa na mrembo mmoja mpaka muda huo alikuwa anaendelea kupata buruani na kuzisulubu nyeti zake, mwanajeshi huyo akiwa kwenye suti yake akipiga magoti mbele ya mkuu wa majeshi.
“Nipe maelezo” aliongea kwa ukali huku akiwa anamtoa mwanamke huyo juu yake na kusimama, alisimama na Kwenda kwenye kabati alitoa pesa na kuwarushia wanawake hao akiwataka wavae haraka sana na kuondoka humo ndani kama ni nguo wakavalie huko nje, hali aliyokuwa ameiona kwa kijana wake alijua moja kwa moja huko alikotoka hakukuwa kwema sana kama siyo mambo kuharibika. Wanawake hao waliondoka humo ndani wakiwa uchi kila mtu akiwa ameshika nguo yake na pesa mkononi, kwao kutoka hivyo hakukuwa na shida kubwa sana, shida yao ilikuwa ni pesa na kila mtu alikuwa ameikunja milioni mbili tena kwa muda mfupi tu wa kumfurahisha tajiri huyo ambaye hawakujua kama ni mkuu wa majeshi wa nchi ya Tanzania, hiyo pesa ni mshahara wa mwezi wa mtu mwenye kazi ya maana sana lakini wao masaa kadhaa tu walikuwa nayo na muda huo huo walitarajia Kwenda kuendelea na hiyo biashara hayo ndiyo maisha halisi ya sasa kwenye huu ulimwengu.
“Mkuu naomba unisamehe sana, wale sio watu kama tulivyokuwa tunasema ni kama mashine ambazo zimetengenezwa tumafanikiwa kukutana naye muda sio mrefu”
“Yuko wapi mbona umekuja huku na nimekwambia mmpeleke dark house” CDF alitamka aki?wa anavaa nguo nzito ambayo iliufunika mwili wake vizuri
“Wenzanngu wote wamekufa”
“Whaaaaaat?” kauli hiyo ilimshtua sana CDF na kumfanya amsogelee kijana huyo na kumshika shingo yake kama mtu anaye hitaji kumnyonga
“Tumefika pale tumefanya kama ulivyo tuelekeza baadae akaja kujitokeza kweli amewaua wenzangu vifo vibaya sana nikiwa naona mbele ya macho yangu na amenipa maagizo ambayo alisema ni mhimu sana mimi kukufikishia” alikuwa anatamka kwa shida kwa namna alivyokuwa amekabwa, alikaziwa macho mpaka yeye mwenyewe akaamua kuendelea kutoa maelezo
“Amesema kwamba utaishi unavyotaka wewe kwa miezi sita tu lakini baada ya huo muda kuisha utaishi kwa namna wanavyo taka wao, nimemuuliza jina kake hajajitaja ila amesema wao wanaitwa The five poisoned serial killers au The TOXIC” CDF aliizungusha shingo ya kijana huyo na kuitupa chini baada ya kuyasikia hayo maelezo, aliipiga meza kwa hasira sana mpaka baadhi ya vijana wake waliokuwa nje wakaingia ndani kwa kuhisi kwamba huenda bosi wao alikuwa kwenye matatizo lakini walicho kutana nacho ni mwili wa mwenzao ukiwa chini waliuchukua na Kwenda kuupakiza kwenye gari ambayo alikuja nayo kukiwa na miili ya wenzake wanne kisha mmoja wa hao wanaume akaondoka na hilo gari kazi ilikuwa ni kwenda kuiteketeza miili hiyo. CDF alipandisha mpaka chumbani kwake aliichukua simu na kuipiga mahali.
“Hicho chuo cha NIT nahitaji kesho kiwe chini ya jeshi kuna kazi maalumu ya kuweza Kwenda kuifanya pale hakikisha kwa kesho hakuna shughuli ambayo inaendelea mpaka nitakapokupa ruhusa yangu mimi” aliongea kwa jazba na kukata simu yake akiwa na gadhabu mno, akiwa kwenye hayo mawazo simu yake iliianza kuita, aliangalia aliyekuwa anapiga alikuwa ni IGP
“Nakusikiliza” aliongea kwa sauti ambayo haikuwa ya kirafiki
“Ndugu yangu ebu nisikilize kwa umakini kwa mara ya mwisho tena, sikwambii haya kwa sababu nakufuatilia sana ila wewe kwangu ni kama kaka na nakuheshimu sana, tumetoka mbali mno mimi binafsi kwa yote ambayo nina uhakika umeyafanya nitakusamehe kwani najua binadamu tumezaliwa tukiwa watu wenye tamaa sana huenda uliteleza ila kuna mtu hatakuelewa siku utakapokuwa hauna namna zaidi ya kutegemea msamaha uendelee kuyalinda maisha yako hata mimi sina uwezo wa kumzuia wala kukulinda wewe ebu achana na haya mambo ndugu yangu, leo nimepata habari mchana uliagiza vijana wako waende pale ni kwa sababu tu bado huwajui hawa watoto ipo siku utanikumbuka sana na….” aliikata simu hiyo baada ya kuona kama mwenzake huyo alikuwa anampotezea muda kwanza alimuona kama mnafiki sana maana alionekana kuyajua mambo mengi mno lakini cha ajabu hakuwahi kumwambia chochote na hata juzi alitoka kumpa taarifa ambazo ndani yake zilikuwa zina ukakasi mwingi sana.
“Kwa sababu wameamua iwe hivi basi namimi nawasubiri kwa hiyo miezi sita ifike ili nijidhihirishe mimi ni nani, nadhani ni muda sahihi pia wa kuanza kuwaagiza vijana wangu kazini kwa yeyote atakaye jifanya kuingilia katika hili basi hatafanikiwa kuyamaliza masaa 24, nawasubiri wapuuzi nyie” alitamka kwa msisitizo sana huku akiipasua simu ambayo ilikuwa kwenye mkono wake na kutoka humo ndani.
Bado tupo taratibu na INNOCENT KILLER (THE REVENGE) sehemu ya 39 inafika mwisho tukutane ndani ya sehemu ijayo.
Wasalaam
Bux the storyteller.