Innocent Killer (The Revenge)

STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 23

SONGA NAYO............

“Niseme kwamba nashukuru sana wazazi wangu kunilea kwenye maadili yaliyokuwa bora na ndiyo yamenifanya mpaka nikakamilisha ndoto yangu ya kuweza kuusomea udaktrai ambao niliuota nikiwa tangu mdogo sana na nilitamani kuweza kuiishi ndoto hiyo siku zote. Pale tunapo ishi kwa pembeni kidogo kuna nyumba moja hivi ambayo yenyewe ni nzuri kiasi kuizidi nyumba yetu, kwenye ile nyumba alikuwa anaishi bibi mmoja ambaye alikuwa mara nyingi sana anakaa nje ya geti kwa sababu palikuwa na mti mkubwa na hapo alipenda kakaa kupumzika akiwa anawasimulia hadithi watoto wachache ambao walikuwa wamemzoea sana wakiwemo na wadogo zangu wote wawili walikuwa wakimpenda sana.

Yule bibi alinizoea sana kwa sababu mara nyingi sana mimi nilikuwa nikimsaidia baadhi ya kazi kama Kwenda sokoni au kwa chochote ambacho yeye alikuwa anakihitaji hivyo ilifanya kwa kiasi kikubwa yeye kuweza kuyajua maisha ya familia yangu hivyo akawa kama mtu wa kunipa ushauri sana ikiwa pomoja na kuwa makini sana na hii dunia hususani wanaume ambao alisema kwamba hawana huruma kabisa na mtoto wa kike hasa yule ambaye wanajua hana msaada kabisa. Baada ya kukata tamaa ya kusoma kabisa nilianza kulipambania lile genge ili familia yangu iweze kuishi angalau kwa kupata uhakika wa chakula, kuna siku akawa ananiuliza maswali mengi sana kuhusu elimu yangu kwani aliona nikiwa kama binti mdogo ambaye nilikuwa na majukumu mazito sana lakini hata hivyo nilitakiwa kuwa shule kwa ule wakati basi sikuwa na namna zaidi ya kumpa maelezo yote pamoja namaamuzi ambayo mimi nilikuwa nimeyachukua baada ya kuona kwamba sina namna nyingine ya kuweza kugharamikia kusoma.

Baada ya maelezo yangu aliniuliza swali moja tu ambalo nadhani lilienda kuikamilisha ndoto yangu hiyo

“Unapenda kusoma?”

“Ndiyo tena sana natamani sana niwe kwenye orodha ya watu wasomi nchini”

“Unataka kusoma nini na wapi?”
“Kwa sasa siwezi tena ili nilitamani sana nisomee udakitari Mhimbili”
“Masomo yao ya mhula huu yanaanza lini?”

“Walianza juzi jumatatu kwa sababu ndio muda ambao ilitakiwa nifanyiwe usahili lakini sina pesa”

“Jiandae kesho tunaenda na mimi”
“Wapi?”
“Wewe si umesema unataka kusoma?”
“Ndiyo bibi ila mimi sina pesa ya kufanyia hivyo” aliijua hofu yangu alitabasamu na kuitoa simu yake kwenye kimkoba chake kidogo kisha akavaa miwani, alikuwa ni bibi lakini cha ajabu alikuwa na simu ya kisasa kabisa, aliipiga mahali ambapo sikujua kwamba ni wapi

“Joseph kesho nakuja na mwanangu hapo hospitalini anakuja kuanza masomo, sio muda sana nakutumia taarifa zake zote hakikisha unaandaa kila kitu pesa nakuingizia baadae ya ada na kingine sitaki kuja kusikia huyu binti anasumbuliwa mchukulie kama mdogo wako na hakikisha unampa kila anacho kitaka anapokuwa anasoma na nisije nikasikia kitu chochote cha kijinga kimempata utajuta” alitoa maelezo ambayo mimi yaliniacha mdomo wazi kwa sababu sikuwahi kufikiria kama bibi huyo ana mamlaka sehemu yoyote ile kwa namna alivyokuwa akiishi maisha ya kawaida sana, baada ya kukata simu yeye ndiye aliye nishtua kwenye mshangao ambao mimi nilikuwa nimemezwa nao mpaka wakati huo, kwangu kila kitu kilikuwa kama ndoto ambayo haikuwa ya kweli.

“Haya jiandae mjukuu wangu uyaanze maisha ya ndoto zako na hakikisha ukienda huko haufanyi ujinga wowote ule, naona kwa siku zangu chache ambazo nimebakisha naweza nikakusaidia ukatimiza ndoto zako nahisi nitafurahia sana kama hilo litatimia kabla ya mimi kufa” alitamka huku akiwa ananishika kichwani kama kunipa baraka, wakati wote huo nilikuwa nimepiga magoti nikiwa nalia sikuamini kama naweza kupata neema kubwa sana kama hiyo kwenye maisha yangu ambayo sikuitegemea kabisa kutoka sehemu yoyote ile

“Bibi hivi unacho kiongea kina ukweli wowote ule?” niliuliza nikiwa nina hamu kubwa sana isiwe alikuwa ananitania maana kwa namna nilivyokuwa ninamuona sikudhani kama angeweza kunilipia ada ya kusoma sehemu kama mhimbili, kwa mwaka ada tu ilikuwa ni kama milioni tano za kitanzania ukitoa na vitu vingine kama usafiri na chakula.

“Nilipokuwa binti mdogo kama wewe niliyaishi maisha ambayo yalinipa somo kubwa sana kwenye maisha yangu, wanaume walinitumia watakavyo wao kwa sababu sikuwa na chochote kitu, kwa sababu waliamua kunifanya mimi sehemu ya kupumzikia hivyo namimi niliamua kuwatumia wao ili nifanikiwe, nilichagua wanaume wenye pesa tu ndio ambao nilikuwa tayari kufanya kila ambacho walikuwa wakihitaji kunifanyia, sio kwamba nilipenda hapana bali kwa maisha ambayo nilikuwa naishi yalikuwa yamejaa dharau, dhihaka, kuonewa na kudhalilishwa hivyo niliamua kuutafuta utajiri kwa namna yoyote ile huku nikiwa na hasira sana na maisha haya ya kudhalilishwa kila siku. Hiyo ilinifanya nitumike sana unaweza ukahisi kwamba nilikuwa pekeyangu ila nilikuwa na ndugu wa kutosha tu na wengine walikuwa nauwezo hata wa kunisaidia lakini hawakufanya hivyo walinifungia vioo vyao kwamba hawaniju namimi niliamua kuishi kama vile nipo mwenyewe hapa duniani”
“Kwenye shughuli zangu za kuutafuta utajiri nilifanikiwa kukutana na mwanaume mmoja ambaye alikuwa tajiri mkubwa sana, huyo mwanaume alinipenda sana, alinifanyia kila kitu na kunifanya nijutie kuyaishi maisha yale ya nyuma na huyo ndiye ambaye alikuja kuwa mume wangu wa ndoa kabisa na tulibahatika kupata watoto wawili wa kike mmoja na wa kiume mmoja, huwa sipendi sana kukumbuka kuhusu wanangu ila wote wametangulia mbele za haki pamoja na mume wangu hivyo kwa sasa nipo mimi na wajukuu zangu watatu ambapo wawili ni wa kike na mmoja ni wa kiume na wote wapo nje ya nchi wanasoma huko nadhani baada ya miaka miwili watakuwa wamemaliza hivyo watarudi tena kuungana na mimi. Mume wangu wakati anakufa aliniacha na utajiri mkubwa sana ambao mpaka hivi sasa ninavyo ongea na wewe upo wa kutosha ila nimewaandalia wajukuu zangu ndio maana nimewasomesha kwa nguvu sana ili kila mtu awe na uwezo mkubwa wa kuuendesha utajiri wake nikifa”

“Wewe hapo siyo mjukuu wangu ila nikikuona hauna tofauti sana na wajukuu zangu hivyo kwa mazingira ambayo umeyapitia imeniuma sana ndiyo maana nimetamani sana nikusaidie utimize walau ndoto zako za kuwa msomi mkubwa na kama nipo hai hata baada ya kumaliza masomo yako basi utasema unataka kuajiriwa wapi na siku hiyo hiyo utapata kazi ila zingatia sana masomo na tabia njema kwa sababu tabia yako nzuri ndiyo iliyo nivutia sana kuweza kukusaidia, wewe ni binti mwenye moyo wa pekee sana upo tayari ukose ili wenzako wapate umenivutia sana nadhani kwa sasa nitakuweka kwenye orodha ya wajukuu zangu na siku moja wakirudi muonane wakutambue kama ni moja ya ndugu yao ili hata nikiondoka utakuwa mikono salama maana watakusaidia kwa vitu vingi sana, haya nimechoka mimi njoo ndani huku uchukue kiasi ambacho kitawasaidia wazazi wako pindi utakapokuwa shule huko na ukirudi kama siku ukiwa na muda ndipo utakuwa unaenda kufanya hiyo biashara yako ya genge” aliongea na kuanza kuondoka pale alipokuwa amekaa, kiukweli nilibaki pale nimeduwaa sana kwanza sikuwahi kuamini kwamba bibi kama huyo angekuwa mtu tajiri kama yeye alivyokuwa anasema, nilimfuata ndani nikiwa na furaha kubwa sana na hiyo ndiyo ilikuwa siku yangu ya kwanza kuweza kuingia ndani ya nyumba yake hiyo, ilikuwa ni ya kawaida sana kwa nje ila kwa ndani ilikuwa imepambwa kwa thamani za gharama sana, kuna swali ambalo nilitamani sana nilipatie majibu kwa wakati ule hivyo ilinilazimu kumuuliza

"Bibi sasa kwanini umechagua kuja kuishi sehemu ya kawaida kama hii” baada ya lile swali alitabasamu sana huku akiwa ananikabidhi bahasha yenye pesa

“Mjukuu wangu kwenye haya maisha kabla mimi sina pesa niliwahi kuamini pesa ndiyo kila kitu, ni kweli kama una maisha ,magumu pesa ni kila kitu kwako kwa sababu unaihitaji kuliko hata unavyo uhitaji uhai wako lakini siku ukiwa una pesa ndiyo unakuja kujua kwamba pesa siyo kila kitu kwa sababu furaha ndiyo inakamilisha sehemu ya maisha yote ya mwanadamu, baada ya kuwa na pesa za kutosha na kuanza kuyaishi maisha ya kitajiri hususani baada ya mume wangu kufa niligundua kwamba pesa haikuwa sehemu ya furaha kubwa kwenye maisha japo kama nisingekuwa na pesa bado nisingeishi kwa furaha hivyo hiyo inakuhakikishia kwamba hakikisha una pesa kwanza ndipo mengine yafuate. Hiyo ndiyo sababu niliwalea wajukuu wangu kwenye maisha mazuri sana na ndio waliokuwa wananifanya nakuwa na furaha muda wote wakiwa karibu yangu, walivyokuwa wanaenda shule niliona kabisa maisha yangu yatakuwa magumu sana kwa sababu niliona nitakosa mtu wa kuwa naye karibu ndiyo maana niliamua kuitafuta furaha yangu mwenyewe sehemu ambayo naweza nikapata nafasi ya kukutana na watu kirahisi sana hususani watoto wadogo”

“Maisha yangu ya kuishi masaki yalinifanya muda mwingi sana niwe nashinda ndani tu au Kwenda hotelini au kufurahi mara moja moja lakini licha ya pesa zote hizo bado nilikuwa nipo mpweke sana muda mwingi ndipo nilipo amua kuhamia eneo kama hili ambalo nimefanikiwa mpaka kukutana na nyie” maelezo yake yalinipa funzo kubwa sana na huo ndio ulikuwa mwanzo wangu wa kuipata elimu ambayo mpaka sasa ninayo. Yule bibi alinisomesha kwa miaka mitano yote na sikutoa kitu chochote kile kwenye kuipata ile elimu kwangu alikuwa ni mtetezi na mkombozi wa maisha yangu.

Nilifanikiwa kumaliza masomo yangu kwa hiyo miaka mitano huku nikiwa nasaidiwa kila kitu na yule bibi hata pale kwenye familia yetu yeye ndiye aliyekuwa anatusaidia sana, aliwaanzisha mpaka shule wadogo zangu, shule ambazo kidogo zilikuwa na unafuu na kwa miaka yote ile mitano pale nyumbani kidogo palikuwa na unafuu mkubwa sana kwa sababu yake na hiyo kiasi fulani ilirejesha tumaini jipya la maisha, alifanikiwa kunikutanisha na hao wajukuu zake ambao kiukweli hawakuwa wema sana kwa sababu nadhani kwa sababu ya ubinafsi wao na kwakweli sijawahi kuwalaumu kwa sababu zilikuwa ni mali zao. Nilivyo maliza masomo yangu hali yake haikuwa nzuri sana kiafya na alikuwa amerudi Masaki ambako ndiko walikokuwa wanaishi wajukuu zake, akiwa huko niliwasiliana naye mara moja tu ambapo kwa mwezi unao kuja alinihakikishia kwamba nilitakiwa kuanza kazi pale pale mhimbili kuna vijana wake wengi sana hivyo akiwa sawa basi atawasiliana nao nikaanze kazi, nilikuwa namuombea sana nadhani kuliko hata ndugu zake na nilikuwa naenda kuikamilisha ndoto yangu na kuisaidia familia yangu kutoka kwenye yale maisha ya taabu ambayo tuliyapitia kwa miaka kadhaa baada ya kuchukuliwa kila kilichokuwa cha kwetu.

Bahati mbaya sana ilikuwa upande wangu, ikiwa imebakia wiki moja ili ufike muda ambao aliniambia atawasiliana na vijana wake nianze kazi pale mhimbili ambao kiuhalisia zaidi ya yule Joseph ambaye alinitambulisha kama kijana ambaye aliwasaidia sana wazazi wake kufanikiwa kwenye maisha yao ndiyo maana yule kijana alikuwa anamheshimu sana hata mimi kwenda kusoma pale ilikuwa ni kwa sababu huyo kijana alikuwa anamheshimu sana yule bibi, kijana ambaye alibahatika kupata ajira pale akiwa bado ni kijana mdogo sana, ilikuwa ni usiku was aa 7 ambao nilipokea sms kutoka kwa moja ya wajukuu zake ambaye alinipa taarifa kwamba bibi yao alikuwa amekufa ila alinionya kwamba nisije nikasogea kwenye familia yao maana zile mali hazinihusu kabisa ilikuwa ni haki yao, nilimuomba nihudhurie tu msiba ya yule bibi lakini ilishindikana ilifika mahali nilitishiwa mpaka kuuliwa na sikuwa nikijua msiba ungefanyikia wapi kwa sababu hata Masaki ambapo nilipajua kwamba ni nyumbani kwake ukiacha pale Mbagala sikuweza kumkuta mtu yeyote hivyo mimi na ile familia tukawa tumeishia pale kufanya mawasiliano kwani hata ile nyumba ya Mbagala waliiuza baada ya wiki moja na sikuwahi kuwaona tena licha ya kuwatafuta sana.

Ndoto zangu za kupata kazi zilianza kuyeyuka sana na hata maisha ya nyumbani yalianza kuwa magumu kama mwanzo baada ya yule bibi kufariki, nilijaribu sana Kwenda pale mhimbili kukutana na Joseph cha ajabu naye alinikataa kama hanijui kabisa vinginevyo alidai kwamba nikae kwake kwa wiki moja nimpe mwili wangu ili nipate kazi, hiyo kwangu ilikuwa ni zaidi ya udhalilishaji nilimkataa kabisa na hapo ni kama niliharibu sana maana alienda kunichafulia jina langu kwenye hospitali nzima maana hata wale watu ambao nilijuana nao kipindi nasoma walinikataa kabisa. Wadogo zangu waliacha shule kwanza ili nipambane na maisha ya mtaani kama ninaweza kupata ada zao na tegemeo langu kubwa ilikuwa ni kupata kazi kwanza hiyo ingenifanya niwe na uhakika wa kuwasomesha lakini ilishindikana, nimezunguka kwenye taasisi nyingi sana kwa mwaka mzima lakini kote nimeishia kuona unyanyasaji mkubwa kwa sababu wanahitaji kwanza hongo ya penzi ndipo kaz itolewe cha ajabu hata wanawake wenzangu nao wananibania mpaka imefika hatua nimeamua kukata tamaa ya kazi. Nilirudi kwenye lile genge la mama la zamani lakini kwa wakati huu hakuna biashara ambayo inaenda hivyo imefanya maisha kuwa magumu sana kwa upande wetu kwa sasa hata wadogo zangu hawasomi tena juzi ulipo nipatia ile pesa nimeenda kuliboresha genge pamoja na kununua mahitaji mengine ya mhimu ya nyumbani kidogo hali imekuwa angalau niombe nikushukuru tena kwa hilo.

Mimi sijawahi kuwa jasiri sana mpaka kumwambia mwanaume maneno kama niliyo kwambia siku ile ila nilivutiwa sana na upole wako machoni na usoni ndiyo maana nilikuja kukuongelesha vile nikihisi huenda ulikuwa upo pale kuwaangalia wanawake hata hivyo sikuwa na maana kwamba ungefanya mapenzi na mimi ila nilitaka nifanye namna yoyote ile ili nipate pesa japo sikuwa tayari kuutoa mwili wangu maana siku ile mdogo wangu alikuwa anaumwa sana na sikuwa na chochote mfukoni hivyo nilitaka nitumie akili ili kuzipata pesa naomba unisamehe sana na namshukuru sana MUNGU kwa kukuleta kwenye maisha yangu” hadithi ndefu yenye kusikitisha sana ya maisha ya Nairah waweza kumuita Nurryat aliihitimisha na kilio kizito sana ambacho kilimfanya ampe kazi Jason ya kuanza kumbembeleza mwanamke huyo.

Vipi kuna tukio gani baya au hali gani ya kusikitisha ya maisha ambayo umewahi kuipitia hata iweje hauji kuisahau kabisa kwenye maisha yako yote mpaka unakufa?

Sehemu ya 23 sina la ziada tena tukutane wakati ujao ndani ya INNOCENT KILLER (THE REVENGE)

Wasalaam

Bux the storyteller.
 
STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 24

SONGA NAYO............
“Unahitaji nini kutoka kwangu” swali la kistaarabu sana kutoka kwa Jason lilimuingia vyema mrembo Nayrah kutoka kwenye majonzi ambayo alikuwa nayo baada ya kumsimulia mwanaume huyo historia nzima ya maisha yake, sasa alikuwa akimjua mwanamke huyo kinaga ubaga, licha ya kumsikiliza kwa umakini sana lakini hiyo ndiyo ilikuwa kauli yake ya kwanza kumtoka kwenye mdomo wake wala hakuhangaika sana kutoa pole kwa mwanamke huyo. Nadhani hata yeye alitegemea kupewa pole za kutosha hivyo swali hilo kiasi chake ni kama lilimshangaza, kutokana na matatizo ambayo alikuwa ameyapitia kwenye maisha yake ukizingatia yeye ni mtoto wa kike ilikuwa ni lazima mwanaume ambembeleze kidogo lakini cha ajabu alikutana na swali ambalo alielewa kwamba lilihitaji maarifa sana kulijibu kuliko kutumia maarifa huenda ulikuwa ni mtego.

“Natakiwa kuchagua kitu kimoja tu au naweza kuchagua zaidi ya kimoja?” alijibu huku akijifuta vizuri machozi na kuvuta pumzi kwa nguvu ili awe sawa wakati anaongea.

“Ndiyo maana binadamu wengi huwa wanafeli kwenye maisha yao wanapopewa nafasi ya kuwa na machaguo mengi, hata wewe leo tukikupeleka sokoni ukakutana na mafungu mengi ya nyanya nzuri utachanganyikiwa kwa sababu utakuwa unahitaji kila fungu ulibebe wewe mpaka hapo unakuwa ushapoteza umakini wako unaweza ukachagua hata bovu kuliko yote ila ukiwa una chaguo moja tu basi inakulazimu tu uchague hilo hilo maana unakuwa hauna namna, nilikuwa nakukumbusha tu kwamba kwenye maisha hakuna machaguo mawili, chaguo huwa ni moja tu yakiwa mengi hizo zinakuwa ni tamaa” alimjibu binti huyo kumwelewesha kwamba hakuwa na machaguo mengi kama akili yake ilivyokuwa inamdanganya alitakiwa kuchagua kitu kimoja tu pekee kilikuwa kinatosha.

“Naomba niwe sehemu ya maisha yako” aliongea kwa kutetemeka lakini kwa msisitizo huku akiwa ameinamisha kichwa chake chini kwa aibu, Jason wala hakushtuka ni kama vile hicho kitu alikuwa anakitegemea tangu mwanzo, aliangalia mbele ambako kulikuwa na uwanja ambao alikuwa anapita mtu mmoja mmoja kwa mbali muda ulikuwa unazidi kusogea, alivuta kumbu kumbu zake mpaka nchini Marekani ambako alikuwa na moja ya mwanamke ambaye alikuwa akimpenda sana kenye maisha yake, alihema kwa nguvu sana na kumgeukia Nayrah.

“Unaweza kuwa miongoni mwa watu ambao wana moyo wa kuyapigania mapenzi kwenye maisha yao?” alimuuliza swali bila kupepesa macho, Nayrah hata hakujipa muda kujibu, aliitikia kwa kichwa kuonyesha kwamba alikuwa amekubali hicho kitu Jason alisikitika sana, alikuwa anamuonea sana huruma huyo mwanamke ambaye alionekana kumpenda ghafla sana mtu ambaye alikuwa hata hamjui uhalisia wake yeye ni nani, anatoka wapi? huenda kumuona anaenda kwa afisa wa polisi kulimpa moyo kwamba mtu huyo hakuwa na ubaya wowote ule.

“Unamwamini vipi mwanadamu ambaye hata majina yake matatu haumjui, haujui anatokea wapi? anaishije? Ameoa au hajaoa? Hauogopi kucheza hiyo kamali na moyo wako pamoja na maisha yako kwa ujumla?” alimuongezea swali hilo mwanadada huyo ambaye alionekana kwamba alikuwa amesha yafanya maamuzi yake tayari na hakuwa tayari kuanza kurudi nyuma tena.

“Hakuna mtu ambaye aliwahi kunipa nafasi ya kunisikiliza kwenye maisha yangu kujua nina shida kiasi gani wala maumivu ambayo ninayapitia ukiacha yule bibi, hakuna mtu alikuwa tayari kunisaidia kwa lolote lile lakini wewe umekuja kitofauti sana kwenye maisha yangu, haunijui lakini ulikuwa tayari kunisaidia, umekubali kupoteza muda wako kwa ajili yangu, naomba unisamehe sana ila mimi nimekupenda sana” alitamka akiwa anamuangalia mwanaume usoni kwa huruma sana, ni kama alikuwa anampa ishara kwamba asije akagoma kulipokea ombi lake kwani angemfanya kuyajutia sana maamuzi yake, Jason alitabasamu na kumpiga busu zito eneo la mdomo, Nayra alitabasamu sana na kumkumbatia mwanaume huyo, kwa mara ya kwanza kwenye maisha yake alikuwa amekubali kuukabidhi moyo wake kwa mwanaume ubaya ni kwamba mtu mwenyewe alikuwa hata hamjui ila alikubali kucheza kamali ya pata potea madhara ambayo angeyapata baadae ilikuwa ni juu yake yeye na aliulizwa kama anaweza kuwa tayari kuyapigania mapenzi akakubali mwenyewe japo huenda hakuielewa hiyo kauli ilikuwa inamaanisha nini Jason aliamua kutoendelea kuleta maumivu mengine kwenye moyo wa mwanamke huyo hivyo alikubali japo ukweli alikuwa akiujua yeye na kile ambacho kilihifadhiwa moyoni mwake ambako alidai kwamba Monalisa alikuwa tayari ameshawahi mwanamke ambaye naye hakujulikana sana ana nini mpaka akawa anafurahia sana kifo cha raisi wa Tanzania.


“Nina dakika arobaini za kukaa huku, naomba nipeleke huko nyumbani nikawaone wazazi na wadogo zako kabla sijaondoka” aliongea huku akiwa anasimama baada ya kuiangalia saa yake, alikuwa na majukumu mazito sana ambayo yalitakiwa kuanza kesho yake hakutaka waendelee kupoteza muda hilo eneo ambalo mrembo huyo alionekana kunogewa sana. kauli yake ilizalisha furaha nyingine kwa mwanamke huyo alinyanyuka kwa pupa na kuanza kuongoza njia, njia haikuwa nzuri sana ila walifika salama mwanaume alikaribishwa ndani.

Ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na vitu vya kawaida tu ambavyo huwa vinapatikana kwenye nyumba za kawaida.
“Shikamoo mama” alisalimu kwa adabu
“Marahaba mwanangu karibu” mama alijibu kwa wasiwasi salamu hiyo ya Jason huku akiwa ana wasiwasi mgeni wa usiku usiku huyo tena kaletwa na mtoto wake ilikuwa inamtishia amani kutokana na mazingira yenyewe yalivyokuwa

“Asante” alijibu Jason na kutulia kama hakuwepo kwa sababu kazi ya kuongea Nayrah ndo alitakiwa kuifanya.

“Mama huyo ndiye mtu ambaye alinipa msaada wa zile pesa siku ile” aliongea kiufupi sana na kumfanya mama huyo ageuke tena kumwangalia Jason kwenye kichwa chake alikuwa amezidiwa sana na maswali mengi lakini alijibiwa kiwepesi mno, Jason alivaa nguo za kumfanya kuonekana kama kijana wa kisasa wa kawaida tu lakini sura yake ilionyesha ni mtu ambaye hakuwa na dhiki kwenye maisha yake.

“Nashukuru sana baba yangu kwa msaada wako, mimi sina cha kukulipa ila MUNGU atanilipia, umetenda msaada mkubwa sana kwenye familia nakuomba uendelee kuwa na moyo huo huo pale unapo hisi una uwezo wa kusaidia wale ambao wana uhitaji” mama aliongea kwa uchungu sana machozi yakimlenga lenga, chembe chembe za shida ya maisha yake zilikuwa zinampa kumbukumbu kwenye kichwa chake kila akikumbuka maisha ambayo walikuwa wanayaishi mwanzo mpaka sasa walipo fikia ilikuwa inatisha sana. Jason alimuangalia mama huyo anavyotoa machozi alijikuta hata yeye machozi yanamtoka kwenye macho yake ni kitu ambacho hata Nayrah kilimshangaza sana, mbele yake hakuwa akimuona mwanamke tu bali alihisi kama anamtazama mama yake mzazi ambaye hakuwahi kumuona wala kumfahamu kabisa tangu azaliwe na wala hakuwahi kuita mama, tangu siku ya kwanza anaanza kujielewa alikuwa kwenye mikono ya kaka yake na ndiye huyo ambaye siku hiyo hiyo alitoka kumpoteza na kumzika aliumia sana.

“Usinishukuru mama, naumia sana napo ona mwanamke wa aina yako anateseka sana namna hii natamani ungekuwa mama yangu nikapata bahati ya kuwa na mama namimi kwenye haya maisha, tangu nizaliwe sijawahi hata siku moja kutamka neno mama, simjui mama yangu hata kutamka tu neno mama nikiwa namuita mtu mbele yangu sijawahi leo ndiyo kwa mara ya kwanza nashukuru sana wewe kunikamilishia hilo sitasahau” aliongea kwa uchungu sana, mama ni zawadi bora sana kwa mtoto yeyote yule duniani, mama ni neno lenye thamani kuliko hata utajiri ulimwenguni, mtoto yeyote yule mdomo wake ukikosa kulitamka hilo neno huwa anajisikia vibaya sana ndicho kilichokuwa kinampata Jason kitendo cha kumuona mwanamke huyo anamshukuru mpaka anatoa machozi ilimuuma sana na kumfanya ajisikie vibaya kwa sababu hakutakiwa kumshukuru sana namna hiyo huyo kwake alikuwa kama mama tu japo hata iweje asingekuja kuwa mama yake mzazi, mama huyo alinyanyuka na kwenda kukaa mahali alipokuwepo Jason akamkumbatia alijihisi amani sana alitamani naye angekuwa na mama siku moja moja awe anadeka kama hivyo au pale anapo jihisi kwamba ana dukuduku lake moyoni basi kupitia amani ya mama angekuwa anairejesha furaha yake na amani yake.

“Pole sana mwanangu unaweza ukaniita mama tu wala haina shida, muda wowote ukijisikia wewe niite” mama huyo aliongea kwa utulivu sana kitu ambacho kilimzindua Jason akarudi kwenye hali yake ya kawaida.

“Mwanao ameniambia kila kitu kuhusu nyinyi na mambo magumu ambayo mumeweza kuyapitia kwenye maisha yenu sasa kuna mambo matatu nataka niyafanye kwenu kama mpo tayari” aliongea kwa msisitizo sana akiwa yupo makini na saa yake ya mkononi, hapo sebuleni walikuwa watatu tu basi hivyo Nayrah na mama yake waliyatega masikio yao vizuri kuwa tayari kusikiliza kitu ambayo mtu huyo alidai kwamba anataka kuyasema, aliujua wasiwasi wao hivyo alitabasamu kidogo ili kuwatoa huo wasiwasi ambao ulikuwa umewajaa.

“Jambo la kwanza nataka wewe na mumeo mtibiwe mpaka mpone kwa sababu nimeambiwa kila kitu kuhusu nyie, kama itashindikana kwa hapa Tanzania basi mtapelekwa India, wewe tatizo laki linapona kabisa lakini hata mzee tatizo ambalo nimeambiwa kwamba analo la kuchizika kwa sababu ya kupoteza vitu vyake na mali zake hayo ni matatizo ya saikolojia na yanatibika vizuri sana hivyo atarudi kwenye hali yake na akirudi kwenye hali yake jambo la msingi ambalo anatakiwa kukutana nalo ndilo jambo la pili ambalo huenda kwenu ni kubwa naenda kulifanya” mioyo yao ilikuwa inawaenda mbio sana hivyo walizidisha umakini sana kulisikiliza hilo jambo lingine la pili ambalo lilifanya mama na mwana waangaliane kwa macho ya kuulizana ni nini hiki kinaendelea?

“Jambo la pili nataka niwarudishie mali zenu zote ambazo nimeambiwa kwamba hao watu walisha zichukua kwenye mikono yenu inatakiwa wazirudishe wao wenyewe kisha wewe ndiye utakaye amua kama utataka wahukumiwe kwa sheria, wauawe au chochote kile ambacho wewe kama mama wa familia utapendezwa nacho hivyo hiyo itasaidia mumeo siku anapona akute mali zake zote zipo hiyo itamfanya kuweza kutengamaa kwa muda mfupi sana” wote wawili walibaki wameduwaa wakiwa wanaangaliana tu mambo ambayo alikuwa anayaongea yalikuwa yanachekesha kama sio kufurahisha sana na ni mambo ambayo walihisi huenda mtu huyo amechizika kwa sababu walikuwa hawana kitu cha kukifanya kwa watu hao walikuwa wamesha jimilikisha kila kitu tayari juu ya mali zile

“Baba nashukuru sana kwa moyo wako lakini nadhani hata unacho kiongea haukijui vizuri naomba haya mambo achana nayo” mama huyo hakuhitaji hiyo maada iwe ndefu sana maana alihisi kama kijana huyo hakuwa ana uelewa na anacho kisema.

“Mhhh mama ninacho kiongea namaanisha kuliko unavyo kifikiria wewe, kwani unanifahamu mama yangu?” swali lake lilifuatiwa na mama huyo kuikunja shingo yake kuonyesha kwamba anapinga kitu hicho cha kumjua mwanaume huyo.

“Ninavyo ondoka hapa naomba majina yote ya hao watu ambao walihusika na hilo tukio na baada ya muda mfupi kuna watu wanakuja hapa kuwachukua na kuwahamishia eneo ambalo mnastahili kuyaanza maisha yenu mapya, msiwe na wasiwasi sana kwa sababu huyo askari Asp Zalimo naye atakuwepo pamoja na IGP hivyo mtakuwa mikono salama ila mimi sitakuwepo na huenda msinione kwa zaidi ya miezi sita kuanzia muda huu, mkitolewa hapa kuanzia keshokutwa wewe na mzee mtaanza kupewa matibabu, Nayrah anaanza kazi mhimbili na hao wanao wengine kesho wanatafutiwa moja ya shule za gharama sana hapa mjini, kuhusu majina ya hao watu naombeni myaandike hapa muda huu ndani ya hiyo miezi ambayo sitakuwepo nitakapo rudi basi nitarudi nao watakuja kukupigia magoti na kuomba msamaha wakiwa na hizo mali zote ambazo walizichukukua kutoka kwenu. Jambo la tatu ambalo nimeshalizungumza ni kuhusu hao watoto wako ambao kuanzia saivi suala la wao kusoma linabaki kwenye mkono wangu” mama huyo alikuwa anamsikiliza kwa umakini mkubwa sana kijana huyo ambaye alikuwa hammalizi mpaka muda huo wakati huo Jason alimsogezea mama huyo kalamu na kipande cha ganda gumu jeupe hapo ndipo walitakiwa kuandikwa hao wanandugu wa mumewe ambao walihusika kupotea na hizo mali, ilikuwa ni tofauti sana na kwa Nayrah yeye licha ya mambo yote ya kushangaza humo ndani bado alikuwa ameganda tu akiwa haamini macho yake muda mfupi ambao ulikuwa umepita alitoka kuukabidhi moyo kwa mwanaume huyo lakini muda mfupi baadae alidai kwamba anaenda kupotea kwa zaidi ya miezi sita, alihisi huenda kwamba mtu huyo alikuwa anamkataa kwa kumfariji.

Hili saga litaishia wapi? je ni muda mwafaka wa kuenda kuufunua ukurasa wa maisha halisi ya Jason ili kumjua yeye ni nani mpaka wanamuogopa sana kiasi hiki?

24 nafika tamati niseme tu tukutane wakati ujao.

Wasalaam

Bux the storyteller
 
STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 25

SONGA NAYO............
Saa 6 kamili usiku ndio muda ambao Jason alikuwa anatoka kwenye nyumba ya akina Nayrah, alitumia muda mrefu sana kumwelewesha binti huyo mpaka kumuelewa kile ambacho alikuwa amekifanya kitu kikubwa ambacho alimsisitiza sana binti huyo ni kwamba hakutakiwa kabisa kukatika hewani kwenye simu yake ahakikishe muda wote inakuwa hewani kwa gharama yoyote ile na alihitaji usiku huo huo akitoka tu hapo basi wafunge milango yote kuna watu watakuja sio muda sana na asimfungulie mtu yeyote yule mpaka yeye mwenyewe ampigie simu kumruhusu afungue, hiyo ndiyo sababu mwanaume aliweza kuondoka akiwa pekeake kabisa hiyo sehemu hakuhitaji watu hao wamsindikize hata hivyo hakufanikiwa kumuona baba yake pamoja na wadogo zake ila aliahidi kwamba kuanzia siku hiyo hawatabahatika kumuona tena mpaka pale itakapo isha miezi sita.

Aliinyanyua simu yake na kuiweka sikioni, iliita kwa muda kidogo kisha ikawa imepokelewa upande wa pili.

“Umeiona hiyo namba ambayo nimekutumia” aliongea kwa sauti nzito sana baada ya kuhakikisha upande wa pili simu imepokelewa

“Ndiyo bosi”
“Nendeni mpaka namba hiyo inapo onyesha ipo, mkifika hapo kuna familia inatakiwa muichukue na kuondoka nayo na kuipeleka Kigamboni kwenye nyumba ya baharini kule, mtakuja na IGP na kujifanya nyie ni miongoni mwa maaskari na kuna askari nitampa maagizo mtaungana naye yeye yupo Mbagala ila baada ya nyie kufika hapo na hiyo familia ikimuona yeye atabaki na nyie mkiondoka hapo IGP atawaacha wenyewe mkiondoka, mimi sitakuwepo kwa miezi sita hivyo jukumu la kuilea hiyo familia nakukabidhi wewe hapo na wenzako hakikisheni hiyo familia inakuwa salama kwa gharama yoyote ile, kuna watoto wawili wa kiume hakikisha unawatafutia moja ya shule bora na za gharama sana hapa mjini wasome kwa amani na walindwe sana. lakini pia kuna mama ana matatizo ya moyo atibiwe kama mama yangu mzazi na kwa gharama yoyote ile mpaka apone na kuna mzee ni mgonjwa wa akili ambaye ni mume wa huyo mama atibiwe kama ni Tanzania au nje IGP atakupa maelekezo zaidi kama atahitajika kupelekwa nje ya nchi ila hakikisha ninavyorudi awe amepona” aliongea kwa msisitizo na kuweka kituo baada ya mwili wake kumsisimka sana alihisi hilo eneo lilikuwa na usalama mdogo sana mpaka wakati huo, alisikitika kisha akaendelea kuongea.

“Halafu kuna huyo mwanamke ambaye utamkuta hapo ni mtoto mkubwa wa huyo mzee na huyo mama huyo keshokutwa anatakiwa kuanza kazi mhimbili pale hilo atalimaliza IGP kwamba anaendaje pale ila wewe hapo nakupa kazi ya kumlinda wewe mwenyewe hakikisha hakuna binadamu anamgusa hata kidole chake wala sehemu yoyote ya mwili na kama nikija kupata hizo taarifa basi mimi nitakuua wewe hapo, nina imani hivi ninavyo ongea nawewe nadhani sio zaidi ya dakika kumi utakuwa hapa na wenzako” aliongea kwa msisitizo sana tena kwa sauti nzito na kukata simu akiwa anatembea haraka haraka, hakusimama tena bali alibonyeza tarakimu kadhaa kwenye simu yake na kupiga Kwenda namba ya IGP


“Mhhhh kuna nini kijana wangu mpaka unanipigia na usiku wote huu?” IGP aliipokea hiyo simu akiwa anaonekana kama alitoka kuamka mida hiyo ni wazi alikuwa amepitiwa na usingizi.

“Nisikilize kwa umakini hivi ninavyo ongea nawewe nipo mbagala, kuna namba nakutumia hapo sasa hivi itrack kwenye simu yako na sehemu ilipo ndipo wewe unatakiwa kuwepo ndani ya muda mfupi ujao ila kabla ya wewe kufika mpigie simu yule ASP mwambie awahi kwa akina Nayrah akae nje kuwasubiri vijana wangu yeye ataelewa nadhani nawewe ukifika nitamruhusu huyo binti kuufungua mlango wa kwao, familia yake itatolewa na yeye mwenyewe Kwenda Kigamboni muda huu eneo ambalo ni salama zaidi na wewe kazi yako hapo ni kuhakikisha wameondoka salama kisha huyo binti ambaye anaitwa Nayrah hakikisha kesho unafanya lolote pale mhimbili anapata kazi na keshokutwa anaingia kazini kwa sababu amesomea udaktari hayo mengine tutaongea tukikutana mimi na wewe wakati mwingine” aliongea akiwa anajiandaa kukata simu hiyo lakini IGP alimuwahi kabla hajafanya hivyo.

“Hey mbona unanichanganya umesema Mbagala kuna familia? wewe Mbagala una ndugu gani na umefika saa ngapi huko wakati ulipaswa kuwa Ikulu?”

“Mzee sio muda wa kuanza kuulizana maswali saivi fanya hicho nilicho kwambia halafu hayo mengine tutayaongea mimi nawewe tukionana, hiyo ni familia yangu mpya hivyo hawa watu wasiguswe na mtu yeyote ambaye anaishi kwa kuutegemea moyo wake ili awe hai wapewe kila kitu maelekezo utayapata kwa vijana wangu kwamba ni kitu gani kinahitajika nimesha waambia nadhani sina muda sana”aliongea akionyesha wazi kwamba alikereka sana na kilicho kuwa kinaulizwa hakuhitaji maswali mengi sana yalikuwa yanamboa mno.

“Mhhhh sawa ndani ya dakika ishirini nitakuwa hapo lakini umeona tukio linalo endelea saivi kwenye vyombo vya habari?” hilo swali lilimshtua sana Jason licha ya hivyo aliikata simu hiyo na kuingia kwenye mtandao wa kijamii ili kuweza kujua kwamba ni nini hicho ambacho alikuwa ameambiwa na kilikuwa kinaendelea, alijua fika kwamba hayo maeneo kulikuwa na watu hata hivyo hakujali sana hilo alikuwa anatembea kwa mwendo wa haraka sana mpaka pale alipokaribia kufika kwenye kona moja ya uwanja wa ile sehemu ambayo alikutana kwa mara ya kwanza na Nayrah alisimama.

Kwenye mitandao ya kijamii kulikuwa na taarifa ya kushtua sana kuhusu mdada mmoja ambaye alikuwa mwanasheria alijirekodi video kwa kudai kwamba kesi ya mauaji ya mheshimiwa raisi pamoja na jaji mkuu wa nchi ya Tanzania yeye alikuwa ana ushahidi wa kutosha juu ya hicho kitu ambacho kilikuwa kinaendelea na aliweka wazi kwamba hao ambao walikuwa wamehusika na hilo jambo kuna uzembe mkubwa sana waliufanya ambao ulimsaidia yeye kuupata huo ushahidi hivyo alitaka kuutumia ushahidi huo kuweka wazi mambo yote mbele ya mahakama na kila aliye husika kutenda hilo jambo akutane na mkono wa sheria na kuadhibiwa kama inavyo stahili. Hiyo video ndani ya saa moja tu tangu iachiwe ilikuwa imetazamwa na watu milioni kumi na kuvunja rekodi ya nchi kwa kuwa video ambayo ilikuwa imetazamwa na watu wengi zaidi kwa muda mfupi kwenye historia ya nchi ya Tanzania, watanzania wengi sana walikuwa wanatoa maoni kwamba kama mwanasheria huyo alikuwa ana ushahidi basi serikali ilitakiwa kumlinda kwa gharama yoyote ile ili kuhakikisha kwamba anawaumbua watu wote ambao walikuwa wanahusika kuutenda huo unyama ndani ya nchi yao huku wengine walikuwa wakikomenti kumuonea huruma mwanamke huyo kwa kudai kwamba anaweza kuwa na maisha mafupi sana kwani huenda watu ambao alikuwa anaenda kuwaripoti ndio hao hao viongozi wakubwa wa nchi hivyo wasingekuwa tayari kuweza kuruhusu afichue maovu yao mbele ya jamii lazima wangemuua tu, Jason akiwa anaendelea kuirudia video hiyo alihisi mvumo wa kitu ukiwa unakuja upande ambao alikuwepo alibinya batani ya kuiweka simu off kuupoteza mwanga kwenye skirini ghafla sana na kuinama kidogo tu, ilipita shoka moja ambayo ilikuwa inang’aa sana kwa taa ambazo zilikuwa zinamlika kwa mbali sana na kwenye kukita kwenye mti mmoja ambao ulikuwa upo mbele, alisimama vizuri na kugeukia upande ambao ilitokea shoka hiyo walikuwa wanaume watano ambao wote walikuwa wameziba sura zao kwa vitambaa vyeusi huku vichwa vyao vikiwa wazi, mmoja alipita karibu yake na kupitiliza mpaka kwenye ule mti na Kwenda kuichomoa shoka kwenye ule mti kisha akawa anarudi taratibu mwanaume hakuwa ametikisika wala kuongea chochote alikuwa anasubiri wageni wake hao waongee chochote.

“Mchukueni tuondoke naye” mmoja wao aliongea kwa sauti ambayo ilikuwa kavu kana kwamba hakuwa mtu ambaye maji yalikuwa sehemu ya maisha yake zaidi ya sigara ambayo mpaka wakati huo ilikuwa ipo kwenye mdomo wake kitambaa yeye akiwa amekishusha kidogo.

“Mtu dhaifu kama wewe hapo ndo unawaambia wenzako wanichukue mimi?” Jason aliuliza akiwa anawasogelea pale walipokuwepo mpaka wenyewe wakabaki wametaharuki mtu gani huyo ambaye alikuwa anajiamini sana kiasi cha kuwa na ujasiri huo wa kuwafuata mpaka hapo walipokuwa wamesimama? Hakuna ambaye alikuwa ana jibu la hilo swali lao.

“Mhhhhh kijana mdogo kama wewe na udhaifu wote huo unajiaminia nini mpaka huogopi hata kutusogelea watu kama sisi?" aliongea kwa msisitizo sana mwanaume huyo ambaye paji lake la uso lilikomaa sana kuonyesha hata umri haukuwa rafiki sana kwake tofauti na wenzake, Jason alitabasamu mara moja tu kwenye uso wake

“Mimi huwa nacheka mara chache sana ninapokuwa mbele ya wanaume wenzangu, ok tuachane na hayo mna muda gani mnanifuatilia na huyo ambaye amewatuma watu walaini kama nyie kuja kunifuata hapa ni nani na mnahitaji mnichukue ili twende wapi?”

“Mchukueni mbwa huy……..” kauli yake ilikatishwa na ngumi ya moyo, alipigwa ngumi nzito sana mithili ya jiwe kwa namna mkono huo ulivyokuwa umekomaa alibaki amesimama hivyo hivyo na sigara yake mdomoni, iliongezwa ngumi nyingine pale pale kwenye moyo alishuka chini kama anahitaji kukaa chini ila safari yake ndiyo ilikuwa imetimia ya Kwenda kujitetetea mbele ya muumba kwa madhambi ambayo alikuwa ameyafanya, vijana watatu ambao walikuwa wapo mbele yake walikuwa bado wameduwaa sana ni jambo ambalo lilitendeka kwa muda mfupi mno tena na mwanaume ambaye wao walidai kwamba alikuwa ni mlaini sana, aliyekuwa nyuma na shoka alizinduka kutoka kwenye hiyo simanzi alirusha shoka lake tena kwa nguvu huku akiwa anasogea kwa kasi, shoka Jason aliipisha kidogo ikampita kisha aliuchomoa mkono wake kwa nguvu sana akalidaka hilo shoka, yule kijana wakati anakaribia pale shoka lilirudishwa nyuma na kutua kwenye kifua chake, ilisikika sauti ndogo tu

“Mhhhhhhhh” hiyo ndiyo sauti pekee ambayo ilisikika kutoka kwenye kinywa chake, kifua kilipasuliwa kama mtu ananapasua kuni na shoka namna kuni inavyo chakazwa na ule uzito wa shoka ndicho kilichokuwa kimemkuta mtu huyo, damu ilikuwa inamtoka mdomoni kwake pamoja na kifuani huku hata kuhema kwake kukiwa kwa shida sana alishuka shini na shoka lake likiwa kifuani mwake lilikuwa ni miongoni mwa matukio ya mauaji ya kutisha sana miongoni mwa wanadamu ambao waliwahi kutokea kuishi ulimwenguni. Waliokuwa wapo mbele yake alikuwa amewakazia macho sana licha ya kiza totoro ambacho kilikuwa kimetawala ila walimuona vyema, mikononi mwao wote walikuwa na vishoka vidogo tofauti na yule ambaye alikuwa amepasuliwa na shoka lake mwenyewe yeye shoka lake lilikuwa ni kubwa kiasi walianza kusogea nyuma taratibu mwanaume aliitoa bastola kwenye kiuno chake na kuvichakaza vichwa viwili vya miongoni mwa hao vijana ambao walikuwa mbele yake na ubaya risasi hizo zilitolewa kwenye bastola ambayo haikuwa hata na kiwambo cha kuzuia sauti za risasi hizo hivyo hiyo sauti ilisikika mbali sana kitu kilicho pelekea ndani ya sekunde za kuhesabu mtaa kubaki kimya sana kana kwamba hakukuwa na watu ambao walikuwa wanaishi.

“Hautakiwi kubahatika kukutana namimi nikiwa namna hii utakufa kifo kibaya sana ambacho utatamani hata ni heri ungejiua mwenyewe, kwanini unaacha kutafuta mwanamke mrembo majira haya ya usiku akakupa burudani unahangaika kuwinda roho za watu ambao hata hauwajui?” alikuwa anaongea na huyo kijana mmoja ambaye ndiye pekee alikuwa amebaki hapo, alikuwa akisogea nyuma akitetemeka huku kishoka chake akiwa amekiweka kwa juu kama ishara ya kujitetea.

“Hapana Hapana naomba usiniue”

“Ok kawatuma nani kuja kunifuatilia mpaka huku?”
“Hapana Hapana mimi simju….” Alipigwa risasi mbili za mguu alianza kulia sana akiwa amedondoka chini

“Kwahiyo unaona hapa unaongea na mtoto mdogo sio, ok kama hilo ni tatizo kubwa sana kwako basi ngoja nikupunguze viungo kadhaa kwenye mwili wako” Jason aliongea huku akiichomoa lile shoka kubwa kwa yule mwanaume ambaye alimpasua nalo kwa mara ya kwanza kifuani.

“Nasema nasema usinifanyie hivyo tafadhali”

“Tumetumwa na Oden”

“Oden ni nani?”

“Mtoto wa CDF”
“Amewatuma ili mfanye nini na mimi?”
“Alikuwa anakuhitaji kwa gharama yoyote ile uwe hai au umekufa, maelekezo yake alikuwa anatamani ufike kwake ukiwa hai ila kama ingeshindikana basi alitupa maagizo kwamba tukuue”

“Waambie na wenzako walio tangulia huko wasilete mazoea na binadamu wasio wajua” alimaliza kuongea hivyo huku akishusha shoka hilo kwenye shingo ya kijana huyo kisha akalitupa hilo shoka pembeni na kutoweka hilo eneo haraka sana baada ya kusikia muungurumo wa magari yakiwa yanafika eneo la kwenye huo uwanja, waliokuwa wamefika alikuwa anajua ni akina nani ila hakutaka kabisa wamkute hilo eneo ndiyo maana alipotea kwa kasi sana kuelekea kwenye vichochoro ambavyo vilikuwa mtaani hapo.

Tumeanza kumfunua taratibu huyu mwanaume ili tumjue kwamba yeye ni nani hasa kwenye maisha yake mpaka baadhi ya watu wanamuogopa sana, kwa haya mauaji unahisi jamaa kweli ni mlaini kama baadhi ya watu walivyokuwa wanasema au ni maneno tu ya wale ambao hawaijui hata ncha ya maisha yake ya kweli?

25 sina la ziada niseme tu kwanza inafika tamati.

Wasalaam

Bux the storyteller.
 
STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 26

SONGA NAYO............
Saa 6 kamili usiku ndio muda ambao
Sinza mori
Karibu na moja ya hoteli nzuri sana ya Manyama hotel ndilo eneo ambalo ilikuwa inapatikana nyumba moja ambayo ilikuwa na ubora ambao haukuwa wa kutisha sana wala wa kuboa sana ishara ya kuonyesha kwamba mtu aliyekuwa akiishi hapo alikuwa ni mtu ambaye alikuwa anaishi maisha ya mazuri ya kuweza kujikidhi yeye kama yeye hakuwa na chembe chembe ya njaa kwenye tumbo lake mlo mzuri ilikuwa sehemu ya maisha yake hakuwa na wasiwasi sana juu ya jambo hilo. Ndani ya nyumba hiyo majira ya usiku wa saa nne kulikuwa na mwanga ambao kama mtu angeuona basi angekuwa na uhakika kwamba ndani ya chumba hicho wenyeji au mwenyeji alikuwa bado hajalala japo hakukuwa na nafsi yoyote ya mtu yeyote ambaye alikuwa nje ya nyumba hiyo kuwa na upenyo wa kumuwezesha yeye kuona chochote ambacho kilikuwa kinaendelea ndani ya nyumba hiyo.

Ndani ya hiyo nyumba alionekana mwanamke mrembo ambaye kwa umri wake alikuwa bado ni binti mbichi kabisa miaka kuanzia 24 na isiyozidi 28, alichokuwa anakifanya majira hayo ya usiku alikuwa ameandaa stick ya kuwekea simu na kuisimamisha mbele ya sehemu ambayo alikuwa amekaa ikawa inamtazama, alibonyeza batani ya kuruhusu baada ya sekunde thelathini ianze kurekodi kila ambacho yeye alihitaji kukisema mbele ya kamera yake hiyo ya simu. Yasinta Kobe ndilo lilikuwa jina lake huyu mwanamke, alikuwa ni mhitimu wa chuo cha sheria na kupata alama za juu sana japo mpaka muda huo hakuwa amepata ajira sehemu yoyote ile tangu amalize kusomea mambo hayo ya sheria, alikuwa ni mwanasheria wa kujitegemea na alikuwa na ofisi yake maeneo ya hapo hapo Sinza Mori, licha ya kutokuwa kwenye ajira rasmi ya kiserikali au shirika lolote lile la mtu binafsi bado alikuwa anajulikana sana umahiri wake anapo simama mbele ya mahakama kwa ajili ya kumtetea mtuhumiwa wake hususani kwa wale ambao hawakuwa na hatia yoyote ile hivyo hiyo ilimfanya kuwa mtu maarufu sana licha ya umri wake kuwa mdogo mno kwenye tasnia hiyo ya sheria.

Alikuwa amesimamia kesi zaidi ya nne tangu aweze kuhitimu masomo yake na hakuna kesi hata moja ambayo iliweza kumshinda, kwenye hiyo video ambayo alikuwa anajirekodi yeye ndiye aliyeweza kuishtua mitandao ya kijamii sana pamoja na taifa zima la Tanzania hususani kwa wale watu ambao wanapenda sana kufuatilia na ni wapenzi wakubwa sana wa mitandao ya kijamii, alitoa taarifa kwamba alikuwa ana ushahidi wote kuhusu wale watu ambao walikuwa wamehusika na mauaji ya mheshimiwa raisi wa nchi pamoja na jaji mkuu Markvelous Japhary, hilo ni jambo ambalo liliishtua nchi pakubwa sana na kuwafanya raia wajae taharuki juu ya ukakasi wa mauaji ya viongozi hao wakubwa wa nchi. Licha ya kwamba hukumu ilitolewa kwa mtu ambaye alidaiwa kuwa mhusika wa hilo jambo bado wananchi walikuwa wanaendelea na minong’ono yao na kudai kwamba haiwezekani mauaji ya mheshimiwa raisi yaweze kupangwa na mtu mmoja tu pekee lazima kulikuwa na kundi kubwa sana la watu nyuma ya huyo mtu na huyo huenda aliwekwa kama chambo tu ila wenye ndoano wenyewe walikuwa wapo mahali kuweza kutazama kila ambacho kilikuwa kinaendelea kutokea.

Hivyo hiyo taarifa yake iliwashtua sana watu wengi ambao walikuwa wapo macho muda huo, habari hiyo ilisambaa kwa kasi sana kiasi kwamba iliweza kuvifikia mpaka vyombo vya dola,IGP aliipata taarifa hiyo aliwapigia vijana wake waende sehemu hiyo kwa ajili ya kuweka ulinzi kwa mwanamke huyo kwani aliyaweka hatarini sana maisha yake bila kujua hatari ambayo inaweza kuwa mbele yake. Baada ya kuwasiliana na vijana wake na ndio muda ambao yeye aliamua kujipumzisha ili kesho yake asubuhi aweze kuwahi hilo eneo ili kama inawezekana waweze kumhamisha mwanamke huyo na kumpeleka eneo lenye usalama zaidi kwani alikuwa tayari ameingia kwenye mstari wa watu ambao hata walikuwa hawajulikani kwamba hiyo ramani yao walikuwa wanaichora wakiwa wapi. Muda ambao IGP alihitaji kupumzika ndio muda ambao Jason alimpigia simu na kumtaka kwamba aweze kufika maeneo ya Mbagala Kwenda kuichukua familia yake mpya ni jambo ambalo lilizidi kumchanganya sana kwa sababu matukio ya ajabu ajabu yalikuwa yanafuatana sana na hakutambua kabisa kwamba mwafaka wake ungekuwa ni upi.

Mwanamke huyo baada ya kumaliza kujirekodi video hiyo aliiaplodi moja kwa moja kwenye mtandao kisha akaiweka simu pembeni na Kwenda kwenye laptop yake, kuna video aliifungua na kuinyonya na kuiweka kwenye flasha ndogo ambayo aliienda kuipenyeza kwenye tobo dogo la sofa ambalo lilikuwa kama fasheni tu lakini hata hivyo hakuishia hapo alienda kuinyonya tena na kuiweka kwenye mamorycard ndogo ambayo yenyewe aliweka kwenye kidani kidogo na kuirushia chini ya kitanda chake cha kulalia upande wa konani kabisa ilihitaji mtu ambaye alikuwa zaidi ya makini kuweza kukiona kidani hicho na mwonekano wake ulivyokuwa hakuna mtu angeweza kuhisi kwamba kidani hicho kilikuwa kinaweza kufunguka katikati. Baada ya hilo zoezi lake kukamilika alirudi kwenye meza yake ya kazi akiwa anaangalia video hiyo huku akiendelea kutafakari sana yeye mwenyewe hakuelewa hatima ya hilo jambo ambalo alikuwa amelianzisha.

Kumbu kumbu zake zilirudi nyuma kidogo, siku hiyo majira ya mchana akiwa ofisini kwake kuna simu aliipokea kutoka kwa mtu ambaye hakuwa akimtambua hata namba ambayo ilikuwa imepigwa kwenye simu yake ilikuwa ni kutoka kwenye kibanda cha njiani cha simu, sauti hiyo ambayo ilikuwa ni ya kiume ilimpa taarifa kwamba mtu huyo alikuwa ana taarifa za mhimu sana za kumpa mwanamke huyo na hawakutakiwa kuzungumza kwa simu bali walitakiwa kukutana moja kwa moja ili siri hiyo isije ikavuja, mwanamke huyo aligoma kabisa kwa kusema kama mtu huyo ana taarifa za mhimu basi aende ofisini kwake vinginevyo hawezi kutoka Kwenda mahali popote pale kutokana na mambo ya kutisha ambayo yalikuwa yanaendelea kutokea ndani ya jiji la Dar es salaam hususani utekaji wa watu na kupotelea kusiko julikana lakini hata hivyo mwanaume huyo aligoma kabisa kwa kudai kwamba hawezi kufika ofisini hapo kwani anaweza kuonekana au kuingia kwenye matatizo kabla hata hajamkabidhi mwanamke huyo huo ushahidi ambao ulikuwa ni wa mhimu sana na alimchagua mwanamke huyo kwa sababu aliona ndiye mtu ambaye alionekana kuitendea sheria haki bila kuonea upande wowote ule.

Yasinta aligoma kabisa na kuhitaji kuikata simu hiyo moja kwa moja kwenye kichwa chake alipata jawabu kwamba mtu huyo moja kwa moja alikuwa ni tapeli na wala hakuwa na habari za maana kama alivyokuwa akijinadi lakini alisita kuikata simu huyo na kujikuta anapata hamu kubwa ya kuendelea kumsikiliza huyo mwanaume kitu alicho kisikia kilikuwa ni mhimu sana kuweza kukipata na kwake ingekuwa moja ya hatua kubwa sana kwenye kufanikisha malengo yake ya kuitendea haki sheria ili azidi kuwa kwenye mstari ambao ungemfanya afurahie sana kuifanya kazi yake.

“It’s about the president and the Chief Justice” alishtuka sana baada ya kusikia kwamba mtu huyo kitu ambacho alihitaji kumpatia yeye kilikuwa kinawahusu viongozi hao wakubwa wa nchi ya Tanzania mheshimiwa raisi pamoja na jaji mkuu.

“Whaaaaaat do you mean?” aliuliza kwa mshangao mkubwa mpaka mkono mmoja aliuweka kwenye mdomo wake, nafsi yake ilishtuka sana kusikia hilo jambo.

“Nina taarifa kuhusu vifo vya hao watu wawili na ushahidi wa wahusika wa hilo jambo, ni ushahidi wa video ambao upo kwenye frash bahati mbaya sana mimi sina uwezo wa kusimama mahakamani na kuweza kutolea ufafanuzi wa hili jambo hapa penyewe nipo hatarini maisha yangu yapo kwenye mstari mdogo sana wa kuendelea kuwa hai ndio maana nahitaji sana nikupatie wewe kwa sababu ni miongoni mwa wanasheria ambao mnatenda haki sana kwa watu hivyo wewe una uwezo wa kulisimamia hili mbele ya mahakama na haki ikaweza kutendeka” aliongea kwa msisitizo sana mwanaume huyo huku akionekana kuwa kama mtu mwenye mashaka sana maana hata sauti yake ilikuwa haijatulia kabisa wakati anayatoa maelezo hayo.

“Unataka nije wapi?” mwanamke huyo aliuliza moja kwa moja sawali hilo kumaanisha kwamba alikuwa amemuelewa mtu huyo na alikuwa tayari kumsikiliza kwa kila ambacho yeye alikuwa anakihitaji kwa wakati huo.

“Saa moja kamili ya jioni njoo Makumbusho stendi pale, kwa pembeni kuna ghorofa ambalo ndani yake kuna mafundi nguo wengi sana, mimi nitakuwa pale nakusubiri ukifika tu nitakuona wewe njoo ile sehemu ambayo wanashonea sana nguo na usionyeshe mashaka yoyote kana kwamba kuna mtu unamtafuta wewe utaendelea na safari zako mimi nitapita pale ulipo usoni nitavaa hood hivyo ukiona mtu mwenye hood nyeusi kote bila baka lolote kuwa makini kwa sababu sitakiwi kusimama nawewe nitapita tu na kukuachia frash hiyo kwenye mkono wako wewe mimi nitaendelea na safari yangu hata wewe utaendelea na safari yako usionyeshe mshtuko wowote ule wala kuhamaki kiasi kwamba mtu ahisi kuna jambo linaendelea fanya kama nawewe ni miongoni mwa wateja kule, kama nikija kupata nafasi siku nyingine nitakutembelea tena tutakuja kuonana kwa wakati mwingine ila kama nitakufa basi hakikisha hilo jambo linajulikana kwa gharama yoyote ile, zingatia sana usije ukachelewa hata kwa dakika moja tu hautanikuta pale” sauti kavu iliyo nyooka ilisikika vyema kwenye masikio ya mwanadada huyo Yasinta Kobe, kabla hajajibu jambo lolote lile simu hiyo ilikatwa kitu kilicho mfanya aanze kuongea kwenye simu pekeyake lakini hakuna mtu ambaye angemsikia tena simu hiyo ilikuwa haipo hewani tena.

Alichanganyikiwa kama sio kutahamaki hilo jambo halikuwa na kawaida hata kidogo kwa upande wake yeye lilikuwa ni moja ya jambo la kutisha na kuogofya sana na sasa hapo ndipo alipo anza kuona ugumu wa kazi ya kuwa mwanasheria, hata hivyo hakujali sana alitamani mno kuweza kuupata ushahidi huo hapo ndipo angeweza kujua kwamba ni kitu gani ambacho kilipaswa kufuata baada ya hilo jambo kuwa kwenye mkono wake. Kwake muda ulikuwa unaenda taratibu sana majira hayo ya mchana alitamani muda uende haraka aweze kuwahi hilo eneo, hakuwa na uwezo wa kufanya kazi nyingine tena moyo wake ulikuwa unaenda mbio sana hata hamu ya kula tena hakuwa nayo muda wote mtu huyo alimtawala kwenye kichwa chake.

Muda huwa hausimani ndiyo kauli kubwa ya wanazuoni kuhusu muda, majira ya saa kumi na moja na nusu alikuwa kwenye gari yake ndogo akiwa anawahi ndani ya eneo hilo, hapakuwa mbali sana kwa gari hivyo ilimfanya kuendesha taratibu ili aweze Kwenda sawa na muda maana hata kama angewahi huko basi hakuwa na jambo la kufanya ambalo lingemfanya aweze kuuvuta muda mpaka majira hayo. Alifika nusu saa kabla ya muda kutimia ilimlazimu kuingia kwenye duka moja na kumpa simu yake bwana mmoja ambaye alikuwa ni fundi humo ndani na kumwambia alihitaji aweze kuikagua simu yake hiyo kwenye mashine kwa muda wa dakika 20 ili aweze kujua kama ipo salama au ilikuwa na tatizo gani lakini kiuhalisia simu yake haikuwa na tatizo lolote alikuwa anaununua ni muda tu ili hata kama kutakuwa kuna mtu anamtupia macho asije akahisi kwamba mwanadada huyo alikuwa hapo kwa ajili ya mambo yatakayo leta wasiwasi.

Baada ya muda kufika wa hiyo simu kama alivyokuwa ameagiza basi alikabidhi simu yake na kumlipa mtu huyo ujira wake ambaye hakufanya kazi yoyote kwa sababu simu ilikuwa nzima lakini kuifungua, kutumia mashine yake pamoja na umeme ilikuwa ni lazima kuacha pesa, Yasinta aliongoza mpaka kwenye hilo jengo kubwa la ghorofa na kuanza kutembea taratibu kupandisha eneo ambalo walikuwa wamejaa mafundi nguo kila mtu akiwa anaendelea na mambo yake nao wateja wakiwa wanapishana kwa wingi akitoka huyu anaingia huyu na akiingia huyu basi anatoka huyu, saa yake ilikuwa inasoma saa moja kasoro dakika moja alikuwa kila akitazama sehemu yoyote ile haoni hata dalili ya mtu kuwa na ule mwonekano ambao yeye aliambiwa kwenye simu. Muda ulikuwa umeisha na ilikuwa ni saa moja kamili na hakuona mtu mawazo yake yalianza kumpa hisia za kusema kwamba itakuwa alikuwa ni mtu alikuwa anamchezea tu akili kuweza kumzubaisha namna hiyo lakini kabla hajazama zaidi katika mawazo hayo katika moja ya duka ambalo lilikuwa lipo mbele ya macho yake humo ndani alitoka mwanaume mmona akiwa na mfuko ambao bila shaka ulikuwa una nguo na alikuwa amevaa kama vile alivyokuwa ameelekezwa yeye.

Mwanaume huyo alivyo ikaribia hiyo sehemu alijiweka kama vile anatembea kwa kutanua mikono yake na Yasinta alielewa aliusogeza mkono wake mithili ya mtu anaye hitaji kuutoa mkoba wake kutoka mkono mmoja Kwenda mwingine na mikono ikakutana ambapo aliachiwa kitu kigumu kwenye mkono wake hakugeuka wala kushtuka aliingia kwenye duka moja ambapo alilipia kitambaa na kudai kwamba angekifuata kisha akaondoka hilo eneo, baada ya kufika nje ya jengo hilo alitupia macho kila sehemu kuona kama atamuona mtu huyo lakini hakuna chochote hivyo aliamua kuondoka.

Alishtuka kutoka kwenye hizo kumbukumbu na namna alivyofanikiwa kuupata ushahidi huo, aliivuta simu yake na kuiangalia ile video yake ambayo alikuwa ameitupia muda siyo mrefu sana, alitabasamu baada ya kuona kila sekunde ilivyokuwa inaenda na idadi ya watu ambao walikuwa wameitazama walikuwa wanazidi kuongezeka hata vyombo vikubwa vya habari vilikuwa vimeanza kuisambaza habari hiyo kwa ukubwa sana. Akiwa kwenye hiyo taharuki ya kuangalia namna video yake inavyozidi Kwenda mbali namna hiyo alishtuka kusikia sauti kama kitu kinapasuka nje, akahitaji Kwenda dirishani ili achungulie kwamba kuna nini? ila ghafla sana umeme ulizima nyumba nzima na huko nje alisikia sauti moja tu ya kilio ambayo bila shaka alikuwa ni mlinzi wake wa getini.

Madamu kayabananga au kayakanyaga? Na walio mfikia hapa kwake ni akina nani ambao wanaonekana kabisa kwamba hawakufika kwa wema ndani ya hilo eneo?

26 sina la kuongezea tena tukutane ndani ya sehemu ambayo inafuatia.

Wasalaam

Bux the storyteller.
 
STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 27

SONGA NAYO............
Saa 6 kamili usiku ndio muda ambao
Alikuwa akitetemeka sana madam Yasinta kama alivyokuwa akipenda sana kujiita yeye lakini watu walikuwa wakimtambua kama peoples’ lawyer kutokana na tabia yake nzuri ya kupenda kusimama katika haki hususani kutetea haki za wale ambao walikuwa ni wanyonge sana, aliifunika laptop na kuizima simu yake haraka huku akiwa anatetemeka sana hakuelewa kwamba hatima ya maisha yake ingekuwaje mpaka wakati huo, alisogea kwenye dirisha na kufungua kidogo dirisha ili aweze kuona kama kulikuwa kuna nini nje alihisi kama kuna kivuli cha mtu kimepita mbele yake haraka sana alitamani kuweza kumuona mtu huyo ila hakuwa na huo uwezo kwani dirisha hilo lilikuwa limefungwa na hata kama lingekuwa limefunguliwa asingeweza kuona chochote kutokana na kwamba lilikuwa na nondo za kutosha sana ndani ya eneo hilo ambazo zisingemuwezesha yeye kutoa kichwa chake.

Akiwa kwenye huo mshangao mkubwa moyo wake ulipiga paaaa baada ya eneo la getini kuona mwili ukiwa umelala chini, kulikuwa na kiza kutokana na taa zote humo ndani kuzima bila kuelewa kwamba ni kitu gani ambacho kilikuwa kimezima taa hizo lakini bila shaka alijua yule lazima alikuwa ni mlinzi wake na hapo ndipo alipojipa uhakika kwamba nyumba hiyo ilikuw aimezungukwa na watu, alikimbilia pale mezani ili aweze kuwasha simu yake na kupiga polisi aweze kupata msaada wa haraka ila ni kama alichelewa kwani muda huo huo akiwa tu ndiyo ameshika simu hiyo mlango ulifunguliwa ghafla sana na taa zikawaka, aliogopa mno mpaka ile simu yenyewe kwenye mkono wake iliweza kumponyoka na kudondoka kabisa chini, alijiuliza watu hao wamewezaje kuingia kwenye mlango wenye kitasa kigumu kama hicho na hata funguo ilikuwamo kwenye hicho kitasa? Jibu lake lilikuwa ni rahisi sana baada ya kuona mlangoni hapo pamepasuliwa alielewa kwamba hiyo itakuwa ni risasi tu lazima na kwa ishara hiyo watu hao walikuwa wametumia silaha ambazo zilikuwa zimewekwa viwambo vya kuweza kuzuia sauti kutoka kwani kama wangetumia sauti basi moja kwa moja angewasikia.

Mbele yake walikuwa wamesimama wanaume wawili ambao wote sura zao zilikuwa hazionekani kabisa mpaka nywele zao, mmoja ambaye alikuwa mbele zaidi alikuwa na bastola kwenye mkono wake huku mwenzake akiwa hajashika kitu chochote alikuwa yupo pembeni akizungusha macho kwenye kila pembe ya nyumba hiyo.

“Nyie ni akina nani na mnataka nini kwangu” aliuliza swali ambalo lilitoka kwenye mdomo ambao ulikuwa ukitetemeka isivyo kawaida lakini hakupata jibu lolote lile hali hiyo iliwafanya watu hao ambao kwa mwonekano wao alijua wazi kwamba lazima walikuwa ni wanaume wamkazie sana macho mpaka yeye mwenyewe alijishtukia.

“Kwanini mmemuua mlinzi wangu? Mnajua mtu ambaye mmekuja kwake kienyeji sana namna hiyo na kuleta matatizo kama haya? Nawaahidi kati yenu nyote wawili mtaishia gerezani” alikuwa kama chura ndani ya maji kuhitaji kukoroma ili kumzuia tembo kunywa maji, kwa hapo yeye ndiye ambaye alitakiwa kuomba MUNGU na sio kuanza kuwatisha watu ambao walikuwa hawana hata muda na hicho kitisho chake, na ndiyo kwanza walianza kumsogelea ile sehemu ambayo yeye alikuwepo, alijitahidi sana kusogea nyuma lakini hakuwa na kwa kwenda zaidi meza ilikuwa imegota kwenye ukuta alijikuta hana pakwenda zaidi ya kuiegamia meza hiyo, zikiwa zimebakia hatu chache sana watu hao kuweza kumfikia alipokuwa alisikia sauti moja ambayo ilimfanya mpaka aogope sana, hakuwa na uhakika kama aliyekuwa anaiongea alikuwa ni mwanadamu wa kawaida tu.

“Hiyo video iko wapi?” ni swali moja kutoka kwa watu ambao walikuwa wapo siriasi sana

“Video ipi?” alijibu akiwa anatetemeka sana alihitaji kuficha kwa njia hiyio ila huenda na usomi wake wote wa sheria hakujua kama njia ambayo alikuwa ameamua kuichagua hapo ilikuwa ni ya kitoto sana, hakujibiwa chochote tena aliona mwanaume mmoja akiwa anaanza kujifungua kwenye eneo lake la kiuno kilichokuwa kinaenda kutokea hapo alikuwa anakielewa vizuri sana.

“Tafadhali naombeni msinifanyie hivyo nawaombeni sana kama mnaihitaji ni video hii hapa kwenye frashi na kwenye laptop” baada ya kuongea hivyo mwanaume mmoja ambaye alikuwa yupo mbele na bastola kwenye mkono wake alinyoosha mkono kumaanisha kwamba mwanamke huyo ampatie hivyo vitu,

“Mamaa nakufaa………” alipiga kelele ambayo ilizimishwa na kiganja Kizito cha mwanaume huyo ambacho kilitua kwenye shingo yake, alizimia hapo hapo, mwanaume huyo alisogea kwenye hiyo meza na kuichukua laptop ambayo kwa pembeni ilikuwa na frashi, akiwa anahitaji kuifungua alishtuka kama kuna kitu alihisi

"Mbebe huyo mwanamke tuondoke naye haraka sana inaonekana sio salama sana haya maeneo” alitamka akiwa anafanya haraka sana Kwenda mlangoni, mwenzake ambaye alikuwa naye alimbeba haraka sana Yasinta mgongoni kana kwamba anabeba ni kipande cha nguo tu, walitoka nje na kuruka fensi wakatokomea kusiko julikana ila kwa bahati mbaya sana yule ambaye alikuwa amembeba Yasinta wakati anaruka huo ukuta akiwa na mwanamke huyo alidondosha kipande kidogo cha kikadi kutoka kwenye mfuko wake na hakuona hilo jambo kabisa wakawa wamepotea.


Baada ya Jason kuweza kutoweka kule Mbagala alichukua boda boda alivyofika barabarani, kupitia ile video ambayo alikuwa ameiona ya huyo mwanamke aliingia kwenye mtandao huo na kuweza kugundua kwamba mwanamke huyo alikuwa ni maarufu sana na hata ofisi yake ilikuwa maeneo ya Sinza mori ambapo hapakuwa mbali sana na kwake lilikuwa ni suala la dakika chache sana kutoka ofisini kwake kufika mpaka nyumbani kwake, kilicho mshangaza Jason ni namna mwanamke huyo alivyokuwa akijulikana sana huku watu wakiwa wanajua mpaka hata sehemu ambayo alikuwa anakaa halafu anaenda kufanya jambo la hatari kama hilo kwenye midia, alitikisa kichwa kuonyesha masikitiko na ndipo alipo amua kufungua taarifa za mwanamke huyo ilia pate kumsoma kwamba alikuwa ni mwanamke wa aina gani.

Taarifa za mwanamke huyo zilimvutia sana kiasi kwamba alijikuta anatamani sana kuonana naye na alijua kwa huo muda hakuwa kwenye usalama sana baada ya kutoa taarifa kama hizo, ilimlazimu kumwambia derva boda boda kwamba waende mpaka Sinza Mori eneo ambalo ramani ya mwanamke huyo kuweza kuwepo ilipokuwa inasomea, alimsihi dereva huyo kujitahidi kwa namna yoyote ile ili waweze kuwahi hilo eneo angemlipa mara tatu ya pesa ambayo alikuwa amemtajia. Dereva hakufanya ajizi alikuwa kwa ajili ya abiria wake na ilikuwa ni lazima atimize kile ambacho abiria wake alikuwa akikihitaji, majira ya saa saba walikuwa wameingia ndani ya Sinza hakulaza damu alilipa pesa kwa boda boda huyo na kuondoka kwa kasi sana kutaka kuwahi kwenye nyumba ya mwanasheria huyo.

Nje aliona kuna taa ya getini ikiwa imepasuka na baadhi ya vioo vimepasukia nje ya geti alijua wazi hilo eneo halikuwa salama tena, alijigeuza kwa sarakasi ya haraka sana akatua ndani, chini alipotua kwa pembeni kidogo kulikuwa na mwili wa mwanaume ambaye alikuwa amelala hapo, alimgusa bado alikuwa wa moto japo alikuwa ameshakufa ilimpa ishara kwamba hayo mauaji yamefanyika kwa muda mfupi sana uliopita, aliitoa bastola kwenye mfuko wake na kunyata mpaka dirishani, alikuwa makini sana kwa sababu hata taa za ndani bado zilikuwa zinawaka. Kilicho mshangaza mlango ulikuwa upo wazi kabisa basi alijivuta mpaka hapo kitasa chake kilikuwa kimetobolewa kwa risasi, alijibinua kwa sarakasi na kutua ndani akiwa ameinyoosha bastola yake kwa umakini sana lakini hapo ndani hakukuwa na chochote kile, aliangaza na kwa umakini na kuona ukimya mkubwa hakuona hata haja ya kuendelea kuangaza kitu chochote kile alikuwa ameshachelewa sana.

“Shiiiiiiiit” alitamka kwa ghadhabu sana kwani ule muda ambao alikuwa amekaa kwa akina Nayrah kama angewahi hata dakika thelathini basi angemkuta mwanmke huyo ambaye angekuwa ni mhimu sana kwa upande wake yeye, basi alitoka nje na kuangalia mazingira hayo kwa umakini sana alizunguka kidogo ndani ya hiyo fensi ambayo haikuwa kubwa sana kulingana na udogo wa nyumba hiyo, chini ya ukuta upande ambao kwa nje kulikuwa na mti aliona kitambulisho kidogo sana, alikifuata na kuchuchumaa kukiokota

“DH Triple not X no 0012” ndivyo hicho kitambulisho hicho kilivyokuwa kimeandikwa, alikiangalia sana lakini ghafla alisikia sauti ya ving’ora vya polisi, aliangalia kule getini na kuhisi watu hao walikuwa wapo karibu kabisa na hilo eneo, alidunda kwenye ukuta huo na kutua juu kisha akajigeuza kwa sarakasi mara moja tu alikuwa nje naye alipotelea kule alikokuwa anakujua yeye mwenyewe. Askari zaidi ya kumi walikuwa wamefika ndani ya nyumba hiyo wakiwa na silaha zao mikononi, waliizunguka nyumba hiyo na kugonga geti ambalo lilikuwa limefungwa, waligonga kwa zaidi ya dakika tano lakini hakukuwa na dalilili zozote za geti hilo kuweza kufunguliwa

“Nina uhakika nyumba kama hii haiwezi kuwa bila mlinzi sasa kwanini hafungui?”
“Mimi nadhani tuvunje tu mkuu tunaendelea kupoteza muda na tumeambiwa ni jambo la dharura hatujui ni kitu gani ambacho kitakuwa kimetokea huko ndani tunavyo endelea kupoteza muda hapa tunachelewa”

“Yes kweli halafu tumeambiwa muda mrefu sana na tumechelewa mno kufika sijui tutajibu nini kwa wakubwa hizi tabia zetu za kujivuta vuta sana tunapokuwa tunasikia kwamba kuna hatari sehemu fulani zitakuja kututokea puani siku moja” aliongea kiongozi wa kundi hilo ambaye alikiri wazi kwamba taarifa hiyo walikuwa wamepewa muda mrefu sana lakini walikuwa wakijivuta vuta sana kuja mpaka kufika hapo hivyo kama kuna tatizo lolote ambalo litakuwa limetokea hapo basi watakuwa na cha kujibu mbele ya wakubwa hapo, aliongea huku akiwapisha vijana wake waweze kuvunja geti hilo.

Baada ya kufanikiwa kuingia ndani ya nyumba hiyo hawakuambulia kitu chochote kile, waliingia mpaka ndani kwa mazingira tu yalivyo onekana walikuwa wamechelewa sana.

“Daah ndo yale yale ambayo nimeyasema nadhani tumesha chelewa sana kufika hapa na kwa aina ya mazingira kuanzia mlinzi alivyoweza kuuawa mpaka mlango wa ndani ulivyo funguliwa moja kwa moja ni tukio la utekaji limetokea. Sasa mnisikilize mimi kwa umakini sana ripoti iandikwe kwamba tumefika hapa kwa muda mwafaka kabisa lakini ndiyo hivyo tumekuta tukio limeshafanyika ambapo inatakiwa ionekane kwamba huenda mtekaji alikuwa eneo la karibu zaidi ya nyumbani kwa huyu mwanasheria” aliongea akiwa anampa taarifa hizi kijana wake ambaye alikuwa na daftari kwenye mkono wake ka ajili ya kuweza kuchukua taarifa za matukio yote ambayo yameweza kutokea hapo ndani.

“Sawa mkuu ila mbona inanishangaza sana hivi inawezekanaje mwanasheria kama yule anaishi kwenye nyumba ambayo hata kamera haina kabisa?” alimuuliza mkubwa wake swali hilo ambalo lilimfanya atabasamu sana

“Huwa naongea kila siku naonekana nawaonea siku zote wanawake huwa wanajua kuwajali watu wengine tu ila wao hawajijali kabisa sasa wewe angalia kama huyu anapigania haki za wanyonge kibao ila hata yeye mwenyewe namna tu ya kujilinda hajui” aliongea huku akisogea kwenye mwili wa yule mlinzi.

“Hivi Jacob yupo hapa?”
“Ndiyo nipo mkuu”

“Hebu tupe taarifa za hii risasi ambayo imetumika kumuulia mlinzi huyu”

“Mhhhhhhh hizi risasi huwa zinatumika na bunduki zinazo milikiwa na makomando tu”

“Nini?”
“Namaanisha kwamba kwa namna ya huu uchimbaji wa hili eneo ambalo hii risasi imepita ni kwamba haiwezi kuwa inatumiwa na mtu wa kawaida kwa sababu hizi zinapatikana kwa makomando pekee ndani ya nchi hii na mtu mwingine ukikutwa nayo ni kosa la jinai, bastola zinazotumia hizi risasi hapa nchini ni chache sana ndiyo maana wamepewa watu hao tu na kwenye soko la silaha ni moja ya silaha za bei ghali mno” askari huyo ambaye alionekana kwamba alikuwa mtaalamu sana wa mambo ya silaha alitoa takwimu zake hizo za kitaalamu ambazo alionekana kuwa anazijua vizuri sana na walikuwa wakimtegemea kwenye hayo mambo ya silaha.

“Mhhhhhh mhhh hii ni hatari sana kwahiyo unataka kuniambia kwamba haya mauaji ameyafanya komando wa nchi?”

“Hapana mkuu mimi sina uhakika wa moja kwa moja ila ninacho kijua ni kwamba hizi silaha hazitumiwi na mtu au mwanajeshi wa kawaida, na huyu mtu alivyopigwa inaonyesha wazi kwamba mtu ambaye amefanya haya mauaji ni mtu ambaye ni imara sana kuanzia nguvu zake za mikono na namna ya uachiaji wa risasi hivyo kama siyo komando basi ni mtu mwenye mafunzo makali sana na atakuwa ni mtu mwenye pesa sana kwa sababu hii hawezi kuimiliki mtu ambaye kuishi kwake ni kwa kubangaiza maana bei ya hizo risasi tu ni bajeti ya mtu ya miaka kadhaa” maelezo hayo yaliwatosheleza kujua kwamba mauaji hayo hayakufanywa kwa bahati mbaya bali yalifanywa na mtu ambaye alikuwa moja kwa moja anajua kile ambacho alikuwa anakifanya.

Nje ya fensi ya nyumba hiyo Jason likuwa hajaondoka, alikuwa amejibana kwenye kuta hizo akiwa anasikiliza kwa umakini sana maelezo ya maaskari hao, baada ya kuzipata hizo taarifa ambazo kwa wakati huo zilikuwa ni za mhimu sana kwake basi aliondoka hilo eneo akiwa hajulikani anaelekea wapi majira hayo ya usiku wa manane.

Unadhani hao wauaji ni akina nani na ni sababu ipi ambayo imewafanya wao kuichukua video hiyo pamoja na kuweza kuondoka na huyo mwanasheria?

Sehemu ya 27 sina la ziada tena inafika mwisho panapo majaaliwa tukutane katika sehemu zingine ambazo zinafuata ili tuweze kujua nini hatima ya haya yote ambayo yanazidi kujitokeza kadri muda unavozidi Kwenda.

Wasalaam

Bux the storyteller.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…