Lukub
JF-Expert Member
- Feb 5, 2012
- 3,622
- 4,100
Hii zaidi ya kuangalia Hollywood standard
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii zaidi ya kuangalia Hollywood standard
Respect brother [emoji120]Hii zaidi ya kuangalia Hollywood standard
[emoji28][emoji28] twende taratibu mkuu
Shukrani chief. Mambo yanazidi kuwa makali
Tuendelee kuperuzi mdogo mdogo.Shukrani chief. Mambo yanazidi kuwa makali
Barikiwa sana chief
tupia basi mkuuHabari ya Jumapili? Ni matumaini yangu wote mpo salama.
Nilipotea siku mbili hizi, nilimuwa namalizana na simulizi hii, ambayo nimeandika mpaka mwisho. Ina kurasa 135.
Leo tunasoma kurasa mbili.
Wasalaam.
Naweka now.tupia basi mkuu
shukran Sana chief.STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 19
SONGA NAYO............
Siku ilikuwa ni ndefu sana lakini hatimaye ilikuwa imeisha, mazishi yalifanyika kwa amani sana, ndugu wa marehemu na wahusika wote walipewa maelekezo kwamba walikuwa wanahitajika Kwenda Ikulu baada ya hayo mazishi kuweza kufanyika ili wakapate pole za dhati kutoka kwa raisi mpya ambaye alikuwa ameapishwa siku hiyo ndani ya nchi ya Tanzania. Jason alikuwa kwenye suti moja nyeusi ambayo ilikuwa imempendeza sana lakini sura yake haikuwa kwenye furaha yoyote kwa siku hiyo ambayo ilikuwa ni ndefu sana kwa upande wake, baada ya kushuka ndani ya eneo hilo ambalo ni eneo la ndoto za kila mtu ndani ya nchi yoyote ile duniani kama sio kwa kuingia kwenye madaraka basi hata walau kupewa mwaliko wa kuweza kuingia ndani la hayo majengo ya ikulu, baada tu ya kushuka hapo alifuatwa moja kwa moja na watu ambo walimwambia kwamba mheshimiwa raisi alikuwa anahitaji kuongea naye basi wala hakuwa na shida ikabidi awafuate watu hao kuelekea hilo eneo ambalo alikuwa yupo mheshimiwa na muda huo alikuwa anajiandaa kuanza kuwapokea wageni ila kwake mtu wa mhimu zaidi kabla ya kuongea na wageni ambao walikuwa wengine ni maraisi na viongozi wakubwa kutoka nchi mbali mbali duniani wengine wakiwa wametuma wawakilishi wao hata hivyo Jason lilikuwa chaguo lake la kwanza.
“Jina lake anitwa Jason Japhary, ni mdogo wake wa damu na marehemu Markvelous Japhary ambaye alikuwa ni jaji mkuu wa nchi ya Tanzania. Ana umri wa miaka 28 kwa sasa akiwa ana shahada ya uzamili katika mambo ya uhandisi na kwa sasa anajiendeleza ili kuwa daktari wa falsafa kwenye uhandisi ambao ndio ameuishi tangu akiwa ni kijana mdogo. Elimu zake za awali nadhani inajulikana maeneo ambayo amesomea, elimu yake ya juu ameanzia hapo Kenya ambapo alisomea ndani ya chuo kikuu cha Kenyatta, baada ya hapo alienda kusomea udhamiri wa shahada yake ya kwanza ndani ya chuo cha Cambridge University kule nchini Uingereza na baada ya hapo ndipo alijiunga na chuo kikubwa zaidi duniani HAVARD UNIVERSITY ambako ndiko anasoma mpaka muda huu tunavyo zungumza.
Hajawahi kukatisha hata kidogo kwenye kusoma kwake na ni miongoni mwa wanafunzi walioweza kupokea tuzo nyingi sana za nidhamu na taaluma kwenye kila sehemu ambayo ameweza kupita, ni kijana ambaye hajawahi kukutwa na hatia yoyote au kosa lolote lile la kinidhamu iwe ni ndani au nje ya chuo hivyo ni moja kwa moja kwamba ni kijana mmoja msafi sana kwenye taarifa zake” ndani ya Ikulu katika chumba kimoja ambacho alikuwa amekaa mkuu wa majeshi na mwana historia mkuu wa Ikulu alikuwa anahitaji taarifa za kijana huyo kwa sababu mwana historia huyo alikuwa ni mtu ambaye alikuwa anaizitunza historia zote za nchi ya Tanzania pamoja na taarifa za viongozi ambao waliwahi kupita kwenye madaraka yao pamoja na familia zao kwa ujumla. Kwa tukio ambalo lilikuwa limetokea mkuu wa majeshi alimuomba mtu huyo ampe taarifa hizo ambazo alidai kwamba zitawasaidia sana kwenye kuweza kumtafuta mhusika wa mauaji ya mheshimiwa raisi lakini pia namna ya kuweza kuwalinda wana familia wa marehemu wa pande zote mbili hivyo alitaka jambo hilo mzee huyo kuliweka kuwa siri sana hakuhitaji hata raisi mpya aweze kuzipata kabisa taarifa hizo ndiyo maana aliiweka kama siri yao wenyewe.
Mkuu wa majeshi alilazimika kuzitafuta taarifa za kijana huyo ili kama kulikuwa kuna kitu ambacho hukukijua kuhusiana na kijana huyo aweze kukifahamu lakini hakukuwa na tatizo lolote lile juu ya Jason na kwa taarifa zake alikuwa ni kijana mmoja mlaini sana basi CDF aliamua kuamini kwamba huenda kijana huyo aliongea naye vile kwa sababu ya hasira na mawazo mazito ya msiba.
“Una uhakika hakuna taarifa yoyote nyingine ambayo inamhusu huyu kijana na haijulikani?” aliuliza akiwa anamwangalia mzee huyo ambaye alikuwa amefanya kazi ndani ya ikulu hiyo kwa muda mrefu sana.
“Nimekaa Ikulu kwa awamu nne tofauti tofauti najua mambo mengi pengine kuliko hata mtu ambaye anasimama kama raisi wa nchi, kama kungekuwa na taarifa za ziada kuhusu huyu kijana basi ningekuwa nimeshazipata muda mrefu sana kwani alikuwa ni mdogo wa mtu mkubwa sana ambaye pia ni familia ya mheshimiwa raisi hivyo taarifa zake haziwezi kujificha”
“Sawa kama kuna taarifa za mhimu zozote ambazo utazipata basi naomba usisite kunipa hiyo taarifa haraka sana maana saivi kuna taharuki kubwa sana hivyo inatakiwa tuhakikishe kwamba ulinzi na usalama vinaboreshwa ili kuhakikisha tunawalinda hawa watu lakini pia hata raia wa nje wasije wakapata matatizo na sisi tupo kama tulivyoweza kushindwa kuwalinda ndugu zetu”
“Sawa mkuu” CDF alitabasamu baada ya mzee huyo kutamka hivyo kisha akatoka ndani ya chumba hicho. Baada ya yeye kutoka mzee huyo alifunga mlango na kuchukua simu yake kisha akaipiga mahali, iliita kwa muda mfupi tu na kupokelewa.
“Nina wageni wengi sana hivyo nikiwa na muda nitakutafuta mwenyewe kama kuna jambo la mhimu la kuongea nawewe” ilisikika sauti upande wa pili baada ya simu hiyo kuweza kupokelewa.
“Mheshimiwa amekuja kumuulizia Jason” aliongea kwa sauti ndogo sana ambayo hakutaka kusikika na mtu yeyote yule.
“Whaaaaat” Upande wa pili wa simu ulionekana kushtuka sana
“Yes, alikuwa anazihitaji taarifa za historia ya Jason tangu azaliwe?”
“Ni nani ambaye amefanya hicho kitu?”
“Mkuu wa majeshi”
“Umemwambiaje?”
“Nimempa zile taarifa za siku zote”
“Safi, kakwambiaje baada ya wewe kumwambia hivyo?”
“Amesema kwa taharuki ambayo imezuka kwa sasa wanahitaji kufanya uchunguzi mkubwa sana juu ya tukio lililo tokea hivyo alikuwa anahitaji taarifa za Jason ili aweze kumlinda maana mpaka sasa hawana imani na usalama wake ndiyo maana wanataka kuwa na taarifa zake zote ili waweze kumlinda na lisitokee kosa lingine kama lile ambalo limefanyika kwa kaka yake”
“Ni bora ufe ila hizo taarifa hazitakiwi kumfikia mtu yeyote yule, kwa watu ambao tupo hai, tulikuwa wawili tu mpaka pale ambapo niliamua kukushirikisha wewe hapo tumekuwa jumla watatu ndio ambao tuna taarifa za huyo mtoto hivyo kama ikivuja hata sentensi moja basi hakutakuwa na mwingine zaidi ya sisi watatu ambaye ndiye atakuwa amevujisha hizi habari hivyo hicho kitu hakikisha unakufa nacho kwenye kifua chako yule ndiye future ya nchi na mambo mengi yanamtegemea yeye ili hii nchi iwe sawa nadhani unanielewa”
“Ndiyo mheshimiwa nakuelewa vizuri”
“Nikimaliza vikao nitakutana na wewe baadaye”
“Sawa mheshimiwa” alionekana kwamba alikuwa anaongea na mtu ambaye yeye binafsi alikuwa akimheshimu sana kwa jinsi alivyokuwa mnyenyekevu mbele ya mtu huyo, alihema baada ya kukata simu yake na kuchora ishara ya kutoa shukrani kwa muumba wake.
Ndani ya chumba ambacho alikuwa amekaa mheshimiwa raisi, mlango ulifunguliwa aliingia mwanaume ambaye uso wake ulikuwa na ndevu nyingi ambazo zilichongwa vyema, baada ya kuufunga mlango huo mwanaume huyo alizibandua ndevu zake hizo usoni kwake, Jason ndiye ambaye alikuwa ameingia humo ndani, tangu asubuhi ya siku hiyo alikuwa ndani ya hizo ndevu ilikuwa sio rahisi kuweza kumtambua kama ni yeye ndiye ambaye alikuwa kwenye hiyo hali, mheshimiwa alinyanyuka kutoka kwenye kiti chake na Kwenda kumkumbatia kijana huyo akiwa anampiga piga mgongoni mwake.
“Pole sana pole sana mwanangu, nisamehe mno tangu umefika sijapata hata bahati ya kuweza kukutana na kuongea nawewe najua ni maumivu makali sana ambayo unayapitia mpaka wakati huu ila kwa mimi nipo bega kwa bega na wewe”
“Asante sana mzee”
“Kwanini leo umeamua kuwa kwenye mwonekano wa hivyo?”
“Unayajua maisha yangu vizuri kwamba mimi ni mtu ambaye sitakiwi kujulikana sana hivyo sina namna nyingine ndiyo maisha ambayo mmesha nichagulia, leo vyombo vya habari vilizagaa sana sura yangu ingetambulika kiwepesi kila sehemu”
“Daaah pole sana, unajua kuna muda inaniuma sana kuona unaishi hivi ila hakuna namna kwa ajili ya usalama wa hili taifa inakulazimu kuwa hivyo tu, siku ya kwanza ya kukujua kwamba wewe ni nani nilikuonea huuruma sana kwa sababu ulikuwa umepewa majukumu mazito sana ungali bado kijana mdogo tu ambaye ulitakiwa kuendelea kuzipambania ndoto zako na sijajua kwanini ulikubali kufanya kazi za kutisha kama hizo na umri wako huo” mheshimiwa raisi aliongea hayo maneno akiwa anamimina wine kwenye bilauri mbili zilizokuwa juu ya meza ghali ya vioo hiyo huku akiendelea kuongea na kijana wake.
“Na ndiyo maana hata baada ya kukubali sikuwahi kuruhusu kaka yangu aweze kuyajua haya mambo maana angechukia sana na asidhani kama angemsamehe mheshimiwa raisi au baba mkubwa ambaye ni mmoja kati ya wale ndugu zake ndiye mwenye taarifa zangu zote. Mimi nilichagua kazi hii kwa sababu napenda ninacho kifanya na hata kama kufa nipo tayari muda wowote ule, kilicho nifanya nikawa na moyo wote wa kuifanya hii kazi ni pale ambapo raisi alikuwa tayari kunipa kazi kubwa kama ile wakati sikuwa na taaluma yoyote ile na baada ya kunieleza kwamba wananihitaji mimi sikuwaza mara mbili japo kwa wakati ule nilikuwa bado mdogo ila niliamua kuikubali na kufa na ile siri kwenye kifua changu hata kaka yangu amekufa akiwa hamjui mdogo wake ambaye amemlea yeye mwenyewe kwa mikono yake” Jason alijibu huku akiwa anashushia bilauri yake hiyo ya wine.
“Na hilo ndilo jambo ambalo nilikuwa naliogopa mpaka leo kwamba vipi kama Mark angejua angetuchukia sana kukuingiza kwnye hatari kubwa kama hiyo mtu ambaye akili yake ilikuwa inatumika kuliongoza taifa, niseme tu MUNGU amlaze mahala pema huko aliko”
“Sina imani kama kaka yangu anaweza kupumzika kwa amani kama hawa watu wanaendelea kuishi”
“Mhhhh nalielewa hilo lakini si unajua kwamba watu wa namna hii lazima watakuwa na nguvu na kila kitu ndiyo maana kirahisi tu wamepata mpaka kiburi cha kuweza kumuua mkuu wa nchi, hili ni jambo la kutisha sana saivi nchi nyingi duniani zinahoji sana kuhusu hilo na hata umoja wa mataifa wanahoji kwamba nchi itachukua uamuzi gani ili kama tuna uhitaji na msaada wao basi watusaidie”
“Kuhusu hilo jambo la kuwatafuta hawa watu niachie mimi mwenyewe nitaifanya hiyo kazi na hao wanao hoji waambie kama taifa tunawatafuta hao watu na muda wowote kuanzia sasa watapatikana”
“Sasa wasipo patikana?”
“Mhhhh hakuna mtu anayeweza kupona katika hili kama tu aliingiza mkono wake na akaonyesha uhusika wake iwe moja kwa moja u hata kwa kugusia tu”
“Unataka kufanya nini?”
“Nikitoka hapa kuna mtu nitawasiliana naye yupo CANADA kwa sasa kesho ataingia nchini, baada ya hapo nitataka anihakikishie kitu fulani kama ni cha kweli basi nitatoa muda kwa hao watu ambao wamehusika waje wenyewe mbele ya vyombo vya habari, kwa atakaye jitokeza basi atahukumiwa kwa sheria ila kwa wale ambao watapuuza basi hii nchi itakuwa sehemu mbaya sana kwao kwa ajili ya maisha yao”
“Una uhakika gani kama watu hao watajitokeza?”
“Ndiyo maana nimesema wasipo jitokeza basi mimi nitafanya maamuzi yangu mwenyewe”
“Mhhhh unataka kuanza kuua tena”
“Yes”
“Hapana hapana, hawa watu naomba tuwakamate tu wateswe vikali na kufungwa au kunyongwa kwa sheria, kama utaua mtu hata mmoja basi utawafanya wananchi waishi maisha ya hofu sana maana kile kiwango cha mauaji kama kuna mwananchi akiona au marehemu akipigwa picha kuna mtu atatamani kuishi nchi hii kweli? Hapana Hapana huko ni mbali mno” mheshimiwa raisi aliyapinga sana mawazo ya Jason ambaye haikueleweka huwa anauaje mpaka mheshimiwa anaogopa sana kuweza kumruhusu kufanya hayo maamuzi yake.
“Ndiyo maana nimesema nitatoa muda, miezi sita inatosha sana kwa watu hao kujifikiria na kujitokeza na kwa huo muda hawatakuja kunisikia kabisa ila kama utapita huo muda wakadharau na wakagoma kujisalimisha kwenye vyomba vya habari basi itabidi niwatafute mimi mwenyewe”
“Mhhhhhh mimi biafsi huwa sitaki hata kuona mwili wa mtu ambaye umempiga inanitisha sana sasa ukirudi kwenye uuaji hii nchi haitakuwa sehemu salama kwa kuishi”
“Nimefanya uzembe raisi wa nchi amekufa, kama ningebaki hapa hapa nchini hakuna mtu ambaye angekuwa na jeuri ya kufanya hayo yote lakini kuondoka kwangu tu sijajua imekuwaje mpaka uzembe mdogo sana namna hiyo unafanyika, hao wajinga hawajaishia hapo wameenda na kuigusa familia yangu sasa hapo nitawaachaje mheshimiwa? Huruma yangu ni kwa huo muda ambao nitautoa ila baada ya hapo itabidi watu waijue sehemu yangu ambayo inaishi gizani ninapokuwa nashika kalamu ya wino pamoja na hizi nguo nzuri ambazo nakuwa nazivaa”
“Mkuu wa majeshi amekuja kuzitafuta taarifa zako”
“Huyo usijali kuhusu yeye nitamalizana naye mimi mwenyewe”
“Una uhakika na usalama wako? kama inawezekana uwe unatembea na vijana?”
“Hao watoto ndo wanilinde mimi hapa?”
“Nadhani itafaa zaidi kule kuna watu wana uwezo sana”
“Hao nitawapa tu majukumu ya kuweza kuendelea kukusanya taarifa za wahusika”
“Ni lini utaruhusu wakujue?”
“Kama nikiondoka kwa huo muda ambao nitawapa nafasi watu hao kujitokeza kama hawatajitokeza basi nikirudi vijana watanifahamu” Jason alijibu huku akiwa anasimama ili kuweza kutoka humo ndani.
“Kuwa makini sana” Mheshimiwa raisi aliongea huku akiwa anamtazama kijana huyo ambaye alikuwa anaishia mlangoni. Jason baada ya kutoka hapo aliichukua simu yake na kupiga mahali.
“Alphonce, i need you by tomorrow, location Dar es salaam” aliongea kifupi tu na kukata simu hiyo kisha akatoka na kuondoka kabisa ndani ya Ikulu.
Huyu Jason ni nani? ni mtu wa aina gani?
19 nafika tamati sehemu inayofuata inaweza kutupatia majibu ya maswali yetu.
Wasalaam
Bux the storyteller.